caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Ash-Shu'araa الشعراء

Aya 227 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 47

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ طسٓمٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTw'a Siin Miim.[1]

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تِلْكَ ءَايَٰتُ ٱلْكِتَٰبِ ٱلْمُبِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHizi ni Aya za Kitabu kinachobainisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَعَلَّكَ بَٰخِعٌ نَّفْسَكَ أَلَّا يَكُونُوا۟ مُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuenda ukaihiliki nafsi yako kwa kuwa hawawi Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِن نَّشَأْ نُنَزِّلْ عَلَيْهِم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ ءَايَةً فَظَلَّتْ أَعْنَٰقُهُمْ لَهَا خَٰضِعِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTungependa, tungeliwateremshia kutoka mbinguni Ishara zikashinda zimezinyenyekea shingo zao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّنَ ٱلرَّحْمَٰنِ مُحْدَثٍ إِلَّا كَانُوا۟ عَنْهُ مُعْرِضِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahman (Mwingi wa rehema), isipokuwa wao huupa mgongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَقَدْ كَذَّبُوا۟ فَسَيَأْتِيهِمْ أَنۢبَٰٓؤُا۟ مَا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa yakini wamekwishakanusha; kwa hivyo zitakuja wafikia habari za yale waliyokuwa wakiyafanyia stihizai.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوَلَمْ يَرَوْا۟ إِلَى ٱلْأَرْضِ كَمْ أَنۢبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawakuiona ardhi, ni mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika katika haya zipo Ishara. Lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذْ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰٓ أَنِ ٱئْتِ ٱلْقَوْمَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mola wako Mlezi, alipomwita Musa, akamwambia: Nenda kwa kaumu madhalimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَوْمَ فِرْعَوْنَ أَلَا يَتَّقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKaumu wa Firauni. Kwani hawamchi Mwenyezi Mungu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبِّ إِنِّىٓ أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Mola wangu Mlezi, hakika mimi ninachelea kwamba watanikadhibisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَضِيقُ صَدْرِى وَلَا يَنطَلِقُ لِسَانِى فَأَرْسِلْ إِلَىٰ هَٰرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kifua changu kina dhiki, na ulimi wangu haukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَهُمْ عَلَىَّ ذَنۢبٌ فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wao wana dhambi niliyowafanyia, kwa hivyo ninahofu wanaweza kuniua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ كَلَّا فَٱذْهَبَا بِـَٔايَٰتِنَآ إِنَّا مَعَكُم مُّسْتَمِعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Sivyo hivyo kabisa! Nendeni na miujiza yetu. Hakika Sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأْتِيَا فِرْعَوْنَ فَقُولَآ إِنَّا رَسُولُ رَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi nendeni kwa Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَنْ أَرْسِلْ مَعَنَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwamba: Waachilie Wana wa Israili waende pamoja nasi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ أَلَمْ نُرَبِّكَ فِينَا وَلِيدًا وَلَبِثْتَ فِينَا مِنْ عُمُرِكَ سِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Firauni) akasema: Je, sisi hatukukulea wewe utotoni, na ukakaa miongoni mwetu katika umri wako miaka mingi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَفَعَلْتَ فَعْلَتَكَ ٱلَّتِى فَعَلْتَ وَأَنتَ مِنَ ٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ukatenda kitendo chako ulichotenda, nawe ukawa miongoni mwa wenye kukufuru?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ فَعَلْتُهَآ إِذًا وَأَنَا۠ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipokuwa miongoni mwa wale waliopotea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَفَرَرْتُ مِنكُمْ لَمَّا خِفْتُكُمْ فَوَهَبَ لِى رَبِّى حُكْمًا وَجَعَلَنِى مِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi nikawakimbia nilipowahofu, tena Mola wangu Mlezi akanitunukia hukumu, na akanijaalia niwe miongoni mwa Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتِلْكَ نِعْمَةٌ تَمُنُّهَا عَلَىَّ أَنْ عَبَّدتَّ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hiyo ndiyo neema ya kunisimbulia, na wewe umewatia utumwani Wana wa Israili?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ فِرْعَوْنُ وَمَا رَبُّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterFirauni akasema: Na ni nani huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَآ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na vilivyo baina yake, ikiwa nyinyi ni wenye yakini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ لِمَنْ حَوْلَهُۥٓ أَلَا تَسْتَمِعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Firauni) akawaambia waliomzunguka: Kwani hamsikilizi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبُّكُمْ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba zenu wa kwanza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ ٱلَّذِىٓ أُرْسِلَ إِلَيْكُمْ لَمَجْنُونٌ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliyetumwa kwenu ni mwendawazimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبُّ ٱلْمَشْرِقِ وَٱلْمَغْرِبِ وَمَا بَيْنَهُمَآ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na vilivyo baina yake, ikiwa nyinyi mnatia akilini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ لَئِنِ ٱتَّخَذْتَ إِلَٰهًا غَيْرِى لَأَجْعَلَنَّكَ مِنَ ٱلْمَسْجُونِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Firauni) akasema: Ukijifanyia mungu mwingine asiyekuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga gerezani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكَ بِشَىْءٍ مُّبِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Je, hata kama nitakuletea kitu cha kubainisha wazi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ فَأْتِ بِهِۦٓ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Kilete basi, kama wewe ni katika wakweli.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wa kuonekana dhahiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنَزَعَ يَدَهُۥ فَإِذَا هِىَ بَيْضَآءُ لِلنَّٰظِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akautoa nje mkono wake, mara ukawa mweupe kwa watazamao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ لِلْمَلَإِ حَوْلَهُۥٓ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٌ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Firauni) akawaambia waheshimiwa waliomzunguka: Hakika huyu ni mchawi mtaalamu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُم بِسِحْرِهِۦ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnataka kuwatoa katika nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna shauri gani?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوٓا۟ أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَٱبْعَثْ فِى ٱلْمَدَآئِنِ حَٰشِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Mpe muda yeye na kakaye na uwatume mijini wakusanyao watu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَحَّارٍ عَلِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakuletee kila mchawi bingwa mtaalamu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَجُمِعَ ٱلسَّحَرَةُ لِمِيقَٰتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakakusanywa wachawi kwa ajili ya miadi ya siku maalumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقِيلَ لِلنَّاسِ هَلْ أَنتُم مُّجْتَمِعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watu wakaambiwa: Je, mtakusanyika?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَعَلَّنَا نَتَّبِعُ ٱلسَّحَرَةَ إِن كَانُوا۟ هُمُ ٱلْغَٰلِبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuenda tutawafuata wachawi ikiwa wao ndio watakaoshinda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّا جَآءَ ٱلسَّحَرَةُ قَالُوا۟ لِفِرْعَوْنَ أَئِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ ٱلْغَٰلِبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi walipokuja wachawi, wakamwambia Firauni: Je, tutapata ujira ikiwa sisi ndio tutakaoshinda?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ إِذًا لَّمِنَ ٱلْمُقَرَّبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Ndiyo! Na hakika mtakuwa katika watu wa mbele.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ لَهُم مُّوسَىٰٓ أَلْقُوا۟ مَآ أَنتُم مُّلْقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMusa akawaambia: Tupeni mnavyotaka kutupa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَلْقَوْا۟ حِبَالَهُمْ وَعِصِيَّهُمْ وَقَالُوا۟ بِعِزَّةِ فِرْعَوْنَ إِنَّا لَنَحْنُ ٱلْغَٰلِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakatupa kamba zao na fimbo zao, na wakasema: Kwa nguvu za Firauni hakika sisi hapana shaka ni wenye kushinda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَلْقَىٰ مُوسَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Musa akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza vile walivyovizua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأُلْقِىَ ٱلسَّحَرَةُ سَٰجِدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHapo wachawi hao walipinduka wakasujudu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا بِرَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

رَبِّ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMola Mlezi wa Musa na Harun.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ ءَامَنتُمْ لَهُۥ قَبْلَ أَنْ ءَاذَنَ لَكُمْ إِنَّهُۥ لَكَبِيرُكُمُ ٱلَّذِى عَلَّمَكُمُ ٱلسِّحْرَ فَلَسَوْفَ تَعْلَمُونَ لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَٰفٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Firauni) akasema: Je, mmemuamini kabla ya kuwaruhusu? Bila ya shaka yeye basi ndiye mkubwa wenu aliyewafunza uchawi. Basi mtakuja jua! Nitakatakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha. Na nitawasulubisha misalabani nyote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ لَا ضَيْرَ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا نَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لَنَا رَبُّنَا خَطَٰيَٰنَآ أَن كُنَّآ أَوَّلَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika sisi tunatumai kwamba Mola wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu, kwa kuwa tumekuwa wa kwanza wa Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنْ أَسْرِ بِعِبَادِىٓ إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tulimuamrisha Musa kwa ufunuo: Nenda na waja wangu wakati wa usiku. Kwa hakika mtafuatwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَرْسَلَ فِرْعَوْنُ فِى ٱلْمَدَآئِنِ حَٰشِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Firauni akawatuma mijini wakusanyaji.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَشِرْذِمَةٌ قَلِيلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Wakieneza): Hakika hawa ni kikundi kidogo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّهُمْ لَنَا لَغَآئِظُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNao kwa hakika wanatuudhi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّا لَجَمِيعٌ حَٰذِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa sisi ni wengi, wenye kuchukua hadhari.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَخْرَجْنَٰهُم مِّن جَنَّٰتٍ وَعُيُونٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukawatoa katika mabustani na chemchemi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكُنُوزٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mahazina, na vyeo vya heshima,

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَٰلِكَ وَأَوْرَثْنَٰهَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterVivyo hivyo, na tukawarithisha hayo Wana wa Israili.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَتْبَعُوهُم مُّشْرِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakawafuata lilipochomoza jua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّا تَرَٰٓءَا ٱلْجَمْعَانِ قَالَ أَصْحَٰبُ مُوسَىٰٓ إِنَّا لَمُدْرَكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa yalipoonana majeshi mawili haya, watu wa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumekutwa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ كَلَّآ إِنَّ مَعِىَ رَبِّى سَيَهْدِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنِ ٱضْرِب بِّعَصَاكَ ٱلْبَحْرَ فَٱنفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍ كَٱلطَّوْدِ ٱلْعَظِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tulimletea Musa ufunuo tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَزْلَفْنَا ثَمَّ ٱلْـَٔاخَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawasongesha hapo karibu wale wengine.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنجَيْنَا مُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُۥٓ أَجْمَعِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTukawaokoa Musa na wale waliokuwa pamoja naye wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ أَغْرَقْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukawazamisha hao wengine.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si wenye kuamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ إِبْرَٰهِيمَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wasomee habari za Ibrahim.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِۦ مَا تَعْبُدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlipomwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ نَعْبُدُ أَصْنَامًا فَنَظَلُّ لَهَا عَٰكِفِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Tunaabudu masanamu, daima tunayanyenyekea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ هَلْ يَسْمَعُونَكُمْ إِذْ تَدْعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Je, yanawasikia mnapoyaita?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوْ يَنفَعُونَكُمْ أَوْ يَضُرُّونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu yanawafaa, au yanawadhuru?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ بَلْ وَجَدْنَآ ءَابَآءَنَا كَذَٰلِكَ يَفْعَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Bali tuliwakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ أَفَرَءَيْتُم مَّا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: "Je, mmewaona hawa mnaowaabudu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَنتُمْ وَءَابَآؤُكُمُ ٱلْأَقْدَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNyinyi na baba zenu wa zamani?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِنَّهُمْ عَدُوٌّ لِّىٓ إِلَّا رَبَّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani hakika hao ni adui zangu, isipokuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِى خَلَقَنِى فَهُوَ يَهْدِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbaye ndiye aliyeniumba, na Yeye ndiye ananiongoa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِى هُوَ يُطْعِمُنِى وَيَسْقِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا مَرِضْتُ فَهُوَ يَشْفِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ninapougua, ni Yeye ndiye anayeniponesha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِى يُمِيتُنِى ثُمَّ يُحْيِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِىٓ أَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لِى خَطِيٓـَٔتِى يَوْمَ ٱلدِّينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ambaye ndiye ninayemtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

رَبِّ هَبْ لِى حُكْمًا وَأَلْحِقْنِى بِٱلصَّٰلِحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na walio wema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱجْعَل لِّى لِسَانَ صِدْقٍ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa unijalie nitajwe kwa wema na watu watakaokuja baadaye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱجْعَلْنِى مِن وَرَثَةِ جَنَّةِ ٱلنَّعِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa unijalie katika warithi wa Bustani za neema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱغْفِرْ لِأَبِىٓ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تُخْزِنِى يَوْمَ يُبْعَثُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala usinihizi Siku watakapofufuliwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌ وَلَا بَنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku ambayo kwamba mali haitafaa kitu wala wana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا مَنْ أَتَى ٱللَّهَ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأُزْلِفَتِ ٱلْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Bustani ya mbiguni itasogezwa kwa wacha Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَبُرِّزَتِ ٱلْجَحِيمُ لِلْغَاوِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Jahannamu itadhihirishwa kwa wapotovu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقِيلَ لَهُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wataambiwa: Wako wapi mliokuwa mkiwaabudu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مِن دُونِ ٱللَّهِ هَلْ يَنصُرُونَكُمْ أَوْ يَنتَصِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBadala ya Mwenyezi Mungu? Je, wanawasaidia, au wanajisaidia wenyewe?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكُبْكِبُوا۟ فِيهَا هُمْ وَٱلْغَاوُۥنَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجُنُودُ إِبْلِيسَ أَجْمَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa majeshi ya Ibilisi yote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ وَهُمْ فِيهَا يَخْتَصِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema, na hali ya kuwa wanazozana humo:

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تَٱللَّهِ إِن كُنَّا لَفِى ضَلَٰلٍ مُّبِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation Center"Tallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhahiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ نُسَوِّيكُم بِرَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTulipowafanya nyinyi ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَضَلَّنَآ إِلَّا ٱلْمُجْرِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hawakutupoteza isipokuwa wale wakosefu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَمَا لَنَا مِن شَٰفِعِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi hatuna waombezi wowote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا صَدِيقٍ حَمِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala rafiki wa dhati.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَكُونَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLaiti tungelipata kurejea tena, tungelikuwa katika Waumini."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَّبَتْ قَوْمُ نُوحٍ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ نُوحٌ أَلَا تَتَّقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlipowaambia ndugu yao, Nuhu: Je, hamumchi Mwenyezi Mungu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mcheni Mwenyezi Mungu, na nitiini mimi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siwaulizi juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko isipokuwa kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mcheni Mwenyezi Mungu, na nitiini mimi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوٓا۟ أَنُؤْمِنُ لَكَ وَٱتَّبَعَكَ ٱلْأَرْذَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Je, tukuamini wewe, ilhali wanaokufuata ni watu duni?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ وَمَا عِلْمِى بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Ninayajuaje waliyokuwa wakiyafanya?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنْ حِسَابُهُمْ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّى لَوْ تَشْعُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHesabu yao haiko isipokuwa kwa Mola wao Mlezi, laiti mngelitambua!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala mimi si wa kuwafukuza Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنْ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMimi si chochote isipokuwa ni Mwonyaji wa dhahiri shahiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ يَٰنُوحُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمَرْجُومِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبِّ إِنَّ قَوْمِى كَذَّبُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikadhibisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱفْتَحْ بَيْنِى وَبَيْنَهُمْ فَتْحًا وَنَجِّنِى وَمَن مَّعِىَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami miongoni mwa Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَنجَيْنَٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِى ٱلْفُلْكِ ٱلْمَشْحُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hivyo tukamwokoa yeye na waliokuwa pamoja naye katika marikebu iliyosheheni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ أَغْرَقْنَا بَعْدُ ٱلْبَاقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukawazamisha baadaye waliobakia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika katika haya ipo Ishara, lakini si wengi wao waliokuwa Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَّبَتْ عَادٌ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKina 'Aad waliwakanusha Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ هُودٌ أَلَا تَتَّقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlipowaambia ndugu yao, Hud: Je, hamumchi Mungu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mcheni Mwenyezi Mungu, na nitiini mimi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala siwaulizi juu yake ujira wowote, kwani ujira wangu hauko isipokuwa kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَتَبْنُونَ بِكُلِّ رِيعٍ ءَايَةً تَعْبَثُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَتَّخِذُونَ مَصَانِعَ لَعَلَّكُمْ تَخْلُدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mnajenga majengo ya kifahari kama kwamba mtaishi milele!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا بَطَشْتُم بَطَشْتُمْ جَبَّارِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mnapotumia nguvu, mnatumia nguvu kwa ujabari.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mcheni Mwenyezi Mungu, na nitiini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱتَّقُوا۟ ٱلَّذِىٓ أَمَدَّكُم بِمَا تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mcheni aliyewapa haya mnayoyajua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمَدَّكُم بِأَنْعَٰمٍ وَبَنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAliwapa wanyama wa kufuga na wana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَنَّٰتٍ وَعُيُونٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mabustani na chemchemi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika mimi ninawahofia adhabu ya Siku Kubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ سَوَآءٌ عَلَيْنَآ أَوَعَظْتَ أَمْ لَمْ تَكُن مِّنَ ٱلْوَٰعِظِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni mwa watoao mawaidha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنْ هَٰذَآ إِلَّا خُلُقُ ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHaya si chochote isipokuwa ni mtindo wa watu wa tokea zamani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala sisi hatutaadhibiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكَذَّبُوهُ فَأَهْلَكْنَٰهُمْ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakamkadhibisha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila ya shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَّبَتْ ثَمُودُ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKina Thamud waliwakadhibisha Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ صَٰلِحٌ أَلَا تَتَّقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlipowaambia ndugu yao Saleh: Je, hamumchi Mungu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mcheni Mwenyezi Mungu, na nitiini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala siwaulizi ujira wowote juu yake. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَتُتْرَكُونَ فِى مَا هَٰهُنَآ ءَامِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, mtaachwa salama salimini katika haya yaliyopo hapa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فِى جَنَّٰتٍ وَعُيُونٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKatika mabustani, na chemchemi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَزُرُوعٍ وَنَخْلٍ طَلْعُهَا هَضِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa konde na mitende yenye makole yaliyowiva.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَنْحِتُونَ مِنَ ٱلْجِبَالِ بُيُوتًا فَٰرِهِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mnachonga milimani majumba kwa ustadi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mcheni Mwenyezi Mungu, na nitiini mimi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تُطِيعُوٓا۟ أَمْرَ ٱلْمُسْرِفِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msitii amri za waliopitiliza mipaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ يُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَا يُصْلِحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbao wanafanya uharibifu katika nchi, wala hawatengenezi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوٓا۟ إِنَّمَآ أَنتَ مِنَ ٱلْمُسَحَّرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَآ أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا فَأْتِ بِـَٔايَةٍ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWewe si chochote isipokuwa ni mtu kama sisi. Basi leta Ishara ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ هَٰذِهِۦ نَاقَةٌ لَّهَا شِرْبٌ وَلَكُمْ شِرْبُ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابُ يَوْمٍ عَظِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msimguse kwa wovu, ikawashika adhabu ya Siku Kubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَعَقَرُوهَا فَأَصْبَحُوا۟ نَٰدِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini wakamuua, na wakawa wenye kujuta.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَخَذَهُمُ ٱلْعَذَابُ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَّبَتْ قَوْمُ لُوطٍ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatu wa Luti waliwakadhibisha Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ لُوطٌ أَلَا تَتَّقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlipowaambia ndugu yao, Luti: Je, hamumchi Mungu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mcheni Mwenyezi Mungu na nitiini mimi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala mimi sikuwauliza ujira wowote juu yake; ujira wangu hauko isipokuwa kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَتَأْتُونَ ٱلذُّكْرَانَ مِنَ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَذَرُونَ مَا خَلَقَ لَكُمْ رَبُّكُم مِّنْ أَزْوَٰجِكُم بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ عَادُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mnaacha alichowaumbia Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnaoruka mipaka!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ يَٰلُوطُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُخْرَجِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Ewe Luti! Usipoacha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanaotolewa mji!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ إِنِّى لِعَمَلِكُم مِّنَ ٱلْقَالِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Hakika mimi ni katika wanaokichukia hiki kitendo chenu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

رَبِّ نَجِّنِى وَأَهْلِى مِمَّا يَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَنَجَّيْنَٰهُ وَأَهْلَهُۥٓ أَجْمَعِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukamwokoa yeye na ahali zake wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا عَجُوزًا فِى ٱلْغَٰبِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa kikongwe katika waliokaa nyuma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ دَمَّرْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukawaangamiza wale wengine.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا فَسَآءَ مَطَرُ ٱلْمُنذَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawanyeshea mvua, basi ni ovu mno mvua ya waliyoonywa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَّبَ أَصْحَٰبُ لْـَٔيْكَةِ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatu wa Machakani waliwakanusha Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ قَالَ لَهُمْ شُعَيْبٌ أَلَا تَتَّقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterShuaibu alipowaambia: Je, hamumchi Mungu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mcheni Mwenyezi Mungu, na nitiini mimi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala siwaulizi ujira wowote juu yake. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوْفُوا۟ ٱلْكَيْلَ وَلَا تَكُونُوا۟ مِنَ ٱلْمُخْسِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTimizeni kipimo sawasawa, wala msiwe katika wanaopunja.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَزِنُوا۟ بِٱلْقِسْطَاسِ ٱلْمُسْتَقِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pimeni kwa haki iliyonyooka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تَبْخَسُوا۟ ٱلنَّاسَ أَشْيَآءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا۟ فِى ٱلْأَرْضِ مُفْسِدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri katika ardhi kwa kufanya uharibifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱتَّقُوا۟ ٱلَّذِى خَلَقَكُمْ وَٱلْجِبِلَّةَ ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mcheni aliyewaumba nyinyi na vizazi vilivyotangulia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوٓا۟ إِنَّمَآ أَنتَ مِنَ ٱلْمُسَحَّرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Hakika wewe ni katika waliorogwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا وَإِن نَّظُنُّكَ لَمِنَ ٱلْكَٰذِبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wewe si chochote isipokuwa ni mtu tu kama sisi, na kwa yakini tunakuona wewe ni katika waongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَسْقِطْ عَلَيْنَا كِسَفًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبِّىٓ أَعْلَمُ بِمَا تَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Mola wangu Mlezi anajua zaidi mnayoyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمْ عَذَابُ يَوْمِ ٱلظُّلَّةِ إِنَّهُۥ كَانَ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya Siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya Siku kubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika katika hayo ipo Ishara, lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّهُۥ لَتَنزِيلُ رَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

نَزَلَ بِهِ ٱلرُّوحُ ٱلْأَمِينُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmeuteremsha Roho muaminifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

عَلَىٰ قَلْبِكَ لِتَكُونَ مِنَ ٱلْمُنذِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJuu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بِلِسَانٍ عَرَبِىٍّ مُّبِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّهُۥ لَفِى زُبُرِ ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوَلَمْ يَكُن لَّهُمْ ءَايَةً أَن يَعْلَمَهُۥ عُلَمَٰٓؤُا۟ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanachuoni wa Wana wa Israili?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْ نَزَّلْنَٰهُ عَلَىٰ بَعْضِ ٱلْأَعْجَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa tungeliiteremsha juu ya mmoja wa wasiokuwa Waarabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَقَرَأَهُۥ عَلَيْهِم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ مُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akawasomea, wasingelikuwa wenye kuamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَٰلِكَ سَلَكْنَٰهُ فِى قُلُوبِ ٱلْمُجْرِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNamna hivi tunaingiza katika nyoyo za wahalifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا يُؤْمِنُونَ بِهِۦ حَتَّىٰ يَرَوُا۟ ٱلْعَذَابَ ٱلْأَلِيمَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHawataiamini mpaka waione adhabu chungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَيَأْتِيَهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi itawafikia kwa ghafla, na hali hawana habari.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَيَقُولُوا۟ هَلْ نَحْنُ مُنظَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watasema: "Je, tutapewa muhula?"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi je, wanaihimiza adhabu yetu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَرَءَيْتَ إِن مَّتَّعْنَٰهُمْ سِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ جَآءَهُم مَّا كَانُوا۟ يُوعَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha yakawafikia waliyokuwa wakiahidiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَآ أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يُمَتَّعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYatawafaa nini yale waliyostareheshewa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلَّا لَهَا مُنذِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala hatukuangamiza mji wowote isipokuwa ulikuwa na waonyaji.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذِكْرَىٰ وَمَا كُنَّا ظَٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ ٱلشَّيَٰطِينُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala Mashetani hawakuteremka nayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا يَنۢبَغِى لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala haitakiwi kwao, na wala hawawezi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّهُمْ عَنِ ٱلسَّمْعِ لَمَعْزُولُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika hao wametengwa na kusikia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَا تَدْعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ فَتَكُونَ مِنَ ٱلْمُعَذَّبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa miongoni mwa watakaoadhibiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ ٱلْأَقْرَبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱخْفِضْ جَنَاحَكَ لِمَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watwae kwa upole wanaokufuata miongoni mwa Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِنْ عَصَوْكَ فَقُلْ إِنِّى بَرِىٓءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ikiwa watakuasi, basi sema: Mimi ninajitenga mbali na hayo mnayoyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَوَكَّلْ عَلَى ٱلْعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِى يَرَىٰكَ حِينَ تَقُومُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbaye anakuona unaposimama.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَقَلُّبَكَ فِى ٱلسَّٰجِدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mageuko yako katika wanaosujudu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Yeye ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua zaidi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَلْ أُنَبِّئُكُمْ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ ٱلشَّيَٰطِينُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, niwaambieni nani wanawashukia Mashetani?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يُلْقُونَ ٱلسَّمْعَ وَأَكْثَرُهُمْ كَٰذِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanawapelekea yale wanayoyasikia; na wengi wao ni waongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلشُّعَرَآءُ يَتَّبِعُهُمُ ٱلْغَاوُۥنَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watungaji mashairi ni wapotovu ndio wanawafuata.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ تَرَ أَنَّهُمْ فِى كُلِّ وَادٍ يَهِيمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنَّهُمْ يَقُولُونَ مَا لَا يَفْعَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwamba wao husema wasiyoyatenda?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَذَكَرُوا۟ ٱللَّهَ كَثِيرًا وَٱنتَصَرُوا۟ مِنۢ بَعْدِ مَا ظُلِمُوا۟ وَسَيَعْلَمُ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓا۟ أَىَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa wale walioamini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapodhulumiwa. Na wanaodhulumu watakuja jua mgeuko gani watakaogeuka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70