Swahili Translation - Rowad Translation Center(Kumbuka) Musa alipowaambia ahali zake: Hakika nimeona moto, nitakwenda niwaletee habari kutoka huko, au nitawaletea kijinga kinacho waka ili mpate kuota moto.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini aliyedhulumu, kisha akabadilisha wema baada ya ubaya, basi Mimi hakika ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ingiza mkono wako katika mfuko wako, utatoka mweupe bila ya maradhi. Ni katika Ishara tisa za kumpelekea Firauni na kaumu yake. Hakika hao walikuwa kaumu waovu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakazikataa kwa dhuluma na kujivuna, na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo. Basi angalia ulikuwaje mwisho wa waharibifu!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tuliwapa Daudi na Suleiman elimu, na wakasema: Alhamdu Lillahi (Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu) aliyetufadhilisha kuliko wengi katika waja wake Waumini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Suleiman alimrithi Daudi, na akasema: Enyi watu! Tumefunzwa usemi wa ndege, na tumepewa katika kila kitu. Hakika hii ni fadhila iliyo dhahiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMpaka walipofika kwenye bonde la wadudu chungu, alisema mdudu chungu mmoja: Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu, asiwapondeni Suleiman na majeshi yake bila ya wao kutambua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi (Hud-hud) akakaa si mbali na akasema: Nimegundua usilogundua wewe, na ninakujia hivi kutoka nchi ya Sabai, na nakuletea habari za yakini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu; na Shetani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia Njia. Kwa hivyo hawakuongoka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hawamsujudii Mwenyezi Mungu ambaye huyatoa yaliyofichikana katika mbingu na ardhi, na anayajua mnayoyaficha na mnayoyadhihirisha.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika, imetoka kwa Suleiman nayo hakika ni: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwingi wa kurehemu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Hakika wafalme wanapouingia mji, wanauharibu, na wanawafanya wale watukufu wake kuwa wanyonge. Na hivyo ndivyo watendavyo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi alipofika (mjumbe) kwa Suleiman, alisema (Suleiman): Hivyo ndivyo nyinyi mnanisaidia kwa mali? Aliyonipa Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko aliyowapa nyinyi. Lakini nyinyi mnafurahia hii zawadi yenu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterRejea kwao! Kwa yakini sisi tutawajia kwa majeshi wasioyaweza kuyakabili. Na hakika tutawatoa humo na hali wao wamekuwa madhalili na wanyonge.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Enyi waheshimiwa! Ni nani kati yenu atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajanijia, nao wamekwisha salimu amri?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema Afriti mmoja katika majini: Mimi nitakuletea kabla hujainuka pahala pako hapo. Na mimi kwa hakika katika hilo nina nguvu na muaminifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema mwenye elimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako. Basi alipokiona kimewekwa kimetulia mbele yake, akasema: Haya ni katika fadhila zake Mola wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa hakika, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake. Na anayekufuru, kwa hakika Mola wangu Mlezi ni Mkwasi na Mkarimu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi (Malkia) alipofika akaambiwa: Je, kiti chako cha enzi ni kama hiki? Akasema: Kama kwamba ndicho hiki. (Suleiman na watu wake wakasema): Na sisi tumepewa elimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa yale aliyokuwa akiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yalimzuilia. Hakika yeye (Malkia) alikuwa katika kaumu ya makafiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipoliona, alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Suleiman) akasema: Hakika hilo ni behewa lililofanyiwa sakafu ya vioo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimejidhulumu, na sasa ninanyenyekea pamoja na Suleiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Enyi kaumu yangu! Kwa nini mnauhimiza wovu kabla ya wema? Kwa nini hamuombi msamaha kwa Mwenyezi Mungu ili mrehemewe?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Tuna kisirani nawe na wale walio pamoja nawe. Yeye akasema: Uaguzi wa ukorofi wenu uko kwa Mwenyezi Mungu; lakini nyinyi ni watu mnaojaribiwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Apishaneni kwa Mwenyezi Mungu tutamshambulia usiku yeye na ahali zake; kisha tutamwambia mrithi wake: Sisi hatukuona maangamizo ya watu wake, na sisi bila ya shaka tunasema ukweli.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi hizo nyumba zao ni tupu kwa sababu ya walivyodhulumu. Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara kwa watu wanaojua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi haikuwa jawabu ya kaumu yake isipokuwa ni walisema, "Wafukuzeni wafwasi wa Luti kutoka katika mji wenu. Hakika wao ni watu wanaojitia usafi."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Alhamdu Lillahi (Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu!) Na amani ishuke juu ya waja wake aliowateua. Je, Mwenyezi Mungu ndiye bora, au wale wanaowashirikisha naye?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu ni nani yule aliyeziumba mbingu na ardhi, na akawateremshia maji kutoka mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamkuwa na uwezo wa kuiotesha miti yake. Je, yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni kaumu waliopotoka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu nani yule aliyeifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito, na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kizuizi? Je, yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu ni nani yule anayemjibu mwenye shida kubwa pale anapomwomba, na akaiondoa dhiki, na akawafanya warithi wa ardhi? Je, yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni machache mnayoyazingatia.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu ni nani yule anayewaongoa katika giza la bara na bahari, na akazipeleka pepo kuleta bishara kabla ya rehema zake? Je, yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ametukuka Mwenyezi Mungu juu ya hao wanaomshirikisha nao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu ni nani anayeuanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je, yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wakweli.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani huo ujuzi wao umefikilia kuijua Akhera? Bali wao wamo katika shaka nayo tu, bali wao ni vipofu nayo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika ni haya haya tu tuliahidiwa sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya isipokuwa ni hadithi za uongo za watu wa kale.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa itakapowaangukia kauli juu yao, tutawatolea mnyama katika ardhi atakayewasemesha, ya kuwa watu walikuwa hawana yakini na Ishara zetu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Siku tutakapokusanya kutoka katika kila umma kundi miongoni mwa wale wanaokadhibisha Ishara zetu, nao watagawanywa mafungu mafungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawaoni kwamba sisi tumeufanya usiku ili watulie, na mchana wa kuonea. Hakika katika hayo, zipo Ishara kwa watu wanaoamini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Siku litakapopulizwa baragumu, watahangaika waliomo mbinguni na katika ardhi, isipokuwa amtakaye Mwenyezi Mungu. Na wote watamfikia huku ni wanyonge.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa utaiona milima utaidhania imetulia; ilhali inakwenda kama mwendo wa mawingu. Huo ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu aliyetengeneza sawasawa vilivyo kila kitu. Hakika Yeye anazo habari za yote myatendayo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa atakayekuja na ubaya, basi zitasunukishwa nyuso zao Motoni. Je, kwani mnalipwa isipokuwa mliyokuwa mkiyatenda?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAma mimi, nimeamrishwa nimuabudu Mola Mlezi wa mji huu aliyeufanya ni mtakatifu; na ni vyake Yeye tu vitu vyote. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu (wenye kunyenyekea).
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa niisome Qur-ani. Na mwenye kuongoka, basi ameongoka kwa faida ya nafsi yake. Na mwenye kupotea, basi sema, "Hakika mimi ni miongoni mwa waonyaji."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa sema: Alhamdu lillaahi (Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu). Yeye atawaonyesha Ishara zake, na mtazijua. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika mbali na hayo myatendayo.