Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, wala hakuwa na mwana, wala hakuwa na mshirika katika ufalme, na akaumba kila kitu na akakikadiria kwa kipimo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wamesema waliokufuru: "Haya si chochote ila ni uzushi aliouzua, na wamemsaidia kwa haya watu wengine!" Hakika hawa wamekuja na dhuluma na uongo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ameyateremsha haya ajuaye siri za katika mbingu na ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu akaangushiwa hazina juu yake, au akawa na bustani ale katika hiyo? Wakasema madhalimu: Nyinyi hamumfuati ila mtu aliyerogwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmetukuka ambaye akitaka atakujalia yaliyo bora kuliko hayo, nayo ni mabustani yapitayo mito kati yake, na atakujaalia majumba ya fahari.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku atakapowakusanya wao na hao wanaowaabudu, na akasema: Je, ni nyinyi mliowapoteza waja wangu hawa, au wao wenyewe walipotea njia?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema: Subhanaka! (Umetakasika na upungufu!) Haikutupasia sisi kuchukulia walinzi badala yako, lakini Wewe uliwastarehesha wao na baba zao hata wakasahau kukumbuka, na wakawa watu walioangamia.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hatukuwatuma kabla yako Mitume wowote ila kwa hakika na yakini walikuwa wakila chakula, na wakienda masokoni. Na tumewajaalia baadhi yenu wawe ni majaribio kwa wengine. Je, mtasubiri? Na Mola wako Mlezi ni Mwenye kuona.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku watakapowaona Malaika, hakutakuwa na furaha yoyote siku hiyo kwa wahalifu. Na watasema, "Mwenyezi Mungu apishe mbali!"
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake, na huku anasema: Laiti ningelishika njia pamoja na Mtume!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika alinipoteza, nikaacha Ukumbusho, baada ya kwisha nijia, na kweli Shetani ni haini mkubwa kwa mwanadamu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa vivyo hivyo tumemfanyia kila Nabii adui miongoni mwa wahalifu, na Mola wako Mlezi anatosha kuwa Mwenye kuongoa na Mwenye kunusuru.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakasema wale waliokufuru: Kwa nini hakuteremshiwa Qur-ani yote mara moja tu? Hayo ni hivyo ili tuuimarishe kwayo (ufahamu wa) moyo wako, na ndiyo tumeisoma kwa mafungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala hawatakuletea mfano wowote, isipokuwa na Sisi tutakuletea (jawabu) kwa haki, na tafsiri iliyo bora zaidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale ambao watakusanywa kwa nyuso zao hadi katika Jahannamu, hao watakuwa na mahali pabaya mno, nao ndio wenye kuipotea zaidi njia.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kaumu ya Nuhu, walipowakanusha Mitume, tuliwazamisha, na tukawafanya ni Ishara kwa watu. Na tumewaandalia madhalimu adhabu chungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa yakini wao walikwisha ujia mji ulioteremshiwa mvua mbaya. Basi, je, hawakuwa wakiuona? Bali walikuwa hawataraji kufufuliwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanapokuona, hawakuchukulii isipokuwa ni mzaha tu, na (wanasema): Ati huyu ndiye Mwenyezi Mungu alimtuma kuwa Mtume?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika alikuwa karibu zaidi kutupoteza tuiache miungu yetu, lau kuwa hatukushikamana nayo kwa kuvumilia. Bado watakuja jua, watakapoiona adhabu, ni nani aliyepotea zaidi njia.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia au wanaelewa? Hao sio isipokuwa ni kama wanyama tu, bali wao wamepotea zaidi njia.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, huoni jinsi Mola wako Mlezi anavyokitandaza kivuli. Na angelitaka, angelikifanya kikatulia tu. Kisha tumelifanya jua kuwa ni kiongozi wake.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye ndiye aliyewafanyia usiku kuwa ni vazi, na usingizi kuwa mapumziko, na akawafanyia mchana ni kufufuka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye ndiye anayezituma pepo kuwa bishara njema kabla ya rehema yake, na tunayateremsha kutoka mbinguni maji safi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa yakini tumeibadilibadili kati yao wapate kukumbuka. Lakini wengi wa watu wanakataa isipokuwa kukufuru tu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye ndiye aliyezipeleka bahari mbili, hii ni tamu mno, na hii ni ya chumvi chungu. Na akaweka baina yake kinga na kizuizi kizuiacho.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye ndiye aliyemuumba mwanadamu kutokana na maji, akamjaalia kuwa na nasaba na ushemeji. Na Mola wako Mlezi ni Muweza mno.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanayaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yasiyowafaa wala yasiyowadhuru. Na kafiri daima ni msaidizi wa kumpinga Mola wake Mlezi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mtegemee aliye Hai, ambaye hafi. Na umtakase kwa sifa zake. Naye anatosha kuwa ndiye Mwenye habari zote za dhambi za waja wake.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbaye aliziumba mbingu na ardhi, na vilivyo kati yake kwa siku sita. Kisha akainuka akawa juu ya Kiti cha Enzi. Mwingi wa rehema (Arrahman)! Uliza habari zake kwa amjuaye.[1]
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanapoambiwa: Msujudieni Arrahman (Mwingi wa rehema!) Wao husema: Ni nani Arrahman (Mwingi wa rehema)? Je, tumsujudie unayetuamrisha wewe tu? Na huwazidishia kujitenga mbali.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waja wa Arrahman (Mwingi wa rehema) ni wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza, hujibu: Salama!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale ambao wanapotoa matumizi, hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubahili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale wasiomuomba mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyoiharimisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki, wala hawazini. Na atakayefanya hayo, atapata madhara.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa atakayetubu, na akaamini, na akatenda matendo mema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale wanaosema: "Mola wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu na wana wetu yaburudishayo macho, na utujalie tuwe waongozi kwa wacha Mungu."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mola wangu Mlezi asingewajali lau kuwa si kuomba kwenu. Lakini nyinyi mmemkadhibisha. Basi adhabu lazima iwe.