Swahili Translation - Rowad Translation CenterKitabu kilichoteremshwa kwako, basi isiwe dhiki yoyote katika kifua chako kwa sababu yake, ili uonye kwacho, na kiwe ni ukumbusho kwa Waumini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kipimo Siku hiyo kitakuwa kwa haki. Kwa hivyo, yule ambaye vipimo vyake vitakuwa vizito, basi hao ndio waliofaulu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa yule ambaye vipimo vyake vitakuwa hafifu, basi hao ndio waliozihasirisha nafsi zao kwa sababu ya vile walivyokuwa wakizifanyia Ishara zetu udhalimu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tumewaimarisha katika dunia, na tukawajalia humo njia za kupata maisha. Ni kidogo tu mnavyoshukuru.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema, "Basi teremka kutoka humo! Haikufalii kufanya kiburi humo. Basi toka! Hakika wewe ni miongoni mwa walio duni."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha nitawajia kwa mbele yao na kwa nyuma yao na kuliani kwao kwote na kushotoni kwao kwote. Wala hutawakuta wengi wao ni wenye shukrani.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Shetani akawatia wasiwasi ili awafichulie tupu zao walizofichwa, na akasema: Hakuwakataza Mola wenu Mlezi mti huu isipokuwa mkaja kuwa Malaika, au mkawa katika wanaoishi milele.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi akawatumbukiza kwa hadaa. Na walipouonja ule mti, tupu zao zikawafichukia na wakaanza kujibandikia katika majani ya Bustani hiyo. Na Mola wao Mlezi akawaita, "Je, sikuwakataza mti huo, na kuwaambia ya kwamba hakika Shetani kwenu ni adui wa dhahiri?"
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Teremkeni! Nyinyi kwa nyinyi ni maadui. Nanyi katika ardhi mtakuwa na makao na starehe mpaka ufike muda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi wanadamu! Hakika tumewateremshia vazi la kuficha tupu zenu na vazi la pambo. Na vazi la ucha Mungu, hilo ndilo bora zaidi. Hilo ni katika Ishara za Mwenyezi Mungu ili mpate kukumbuka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi wanadamu! Kamwe Shetani asiwafitini kama alivyowatoa wazazi wenu katika Bustani ile, akawavua vazi lao ili awaonyeshe tupu zao. Hakika yeye anawaona yeye na kabila yake kwa namna ambayo nyinyi hamuwaoni. Hakika Sisi tumewafanya Mashetani kuwa ni marafiki wasaidizi wa wale wasioamini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanapofanya uchafu, husema: Tuliwakuta baba zetu juu yake, na Mwenyezi Mungu ndiye aliyetuamrisha hayo. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi uchafu. Je, mnasema juu ya Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mola wangu Mlezi ameamrisha uadilifu, na zielekezeni nyuso zenu kila mnaposujudu, na muombeni Yeye kwa kumfanyia yeye tu Dini. Kama alivyowaanzisha, ndivyo mtakavyorudi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKundi moja ameliongoa, na kundi jingine limethibitikiwa na upotovu. Kwa hakika hao waliwafanya mashetani kuwa ndio marafiki walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, na wanadhani kuwa wao wameongoka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi wanadamu! Chukueni pambo lenu mnapokwenda kwenye kila mahali pa kusudjudu (kama vile msikiti), na kuleni, na kunyweni, wala msipitilize. Kwa hakika Yeye hapendi wanaopitiliza.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ni nani aliyeharamisha pambo la Mwenyezi Mungu alilowatolea waja wake, na vile vilivyo vizuri katika riziki? Sema: Hivyo ni kwa wale walioamini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivyo ndivyo tunavyowaelezea Ishara kaumu wanaojua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Hakika Mola wangu Mlezi ameharamisha machafu, yaliyodhihiri yake na ya siri, na dhambi, na kuvuka mipaka bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na ambacho hakukiteremshia uthibitisho wowote, na kusema juu ya Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliozikadhibisha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi, hao ndio watu wa Motoni, wao humo watadumu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo, au akazikadhibisha Ishara zake? Hao litawafikia fungu lao waliloandikiwa, mpaka watakapowajia wajumbe wetu kuwafisha, watawaambia: Wako wapi wale mliokuwa mkiwaomba badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema: 'Wametupotea!' Na watashuhudia dhidi yao wenyewe kwamba walikuwa makafiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu atasema: Ingieni (Motoni) pamoja na umma zilizopita kabla yenu miongoni mwa majini na watu. Kila utakapoingia umma, utalaani dada yake. Mpaka watakapokusanyika wote humo, wa mwisho wao atasema juu ya wa mwanzo wao: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio waliotupoteza. Basi wape adhabu ya Motoni maradufu. Atasema: Kila mmoja ana maradufu, lakini nyinyi hamjui tu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wa mwanzo wao atamwambia wa mwisho wao: Basi nyinyi pia hamkuwa na ubora wowote kuliko sisi. Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyachuma.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale waliozikadhibisha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi, hawatafunguliwa milango ya mbingu, wala hawataingia Bustanini mle mpaka aingie ngamia katika tundu ya sindano. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa wahalifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWana kitanda chao katika Jahannamu, na juu yao nguo za moto za kujifunika. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa madhalimu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale walioamini na wakatenda mema, hatuitwiki nafsi yoyote isipokuwa kwa kiasi cha uwezo wake. Hao ndio watu wa Bustanini. Wao watadumu humo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tutaondoa kilicho katika vifua vyao cha chuki, na chini yao itapita mito. Na watasema: Alhamdulillah (sifa njema ni za Mwenyezi Mungu), ambaye alituongoa kuyafikia haya. Wala hatukuwa wenye kuongoka wenyewe lau kuwa Mwenyezi Mungu hakutuongoa. Hakika Mitume wa Mola wetu Mlezi walikuja na haki. Na watanadiwa kwamba: Hiyo ndiyo Bustani mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watu wa Bustanini watawanadi watu wa Motoni, "Sisi tumeshakuta yale aliyotuahidi Mola wetu Mlezi kuwa ni kweli. Na je, nyinyi pia mmekuta yale aliyowaahidi Mola wenu Mlezi kuwa ni kweli?" Watasema: "Ndiyo!" Basi mtangazaji atatangaza kati yao kwamba, "Laana ya Mwenyezi Mungu iko juu ya madhalimu."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa baina yao (makundi mawili hayo) patakuwapo pazia. Na juu ya Minyanyuko patakuwa watu watakaomjua kila mmoja kwa alama zao, na wao watawaita watu wa Peponi: Salamu Alaykum (amani iwe juu yenu)! Wao bado hawajaingia humo, lakini wanatumai.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa yanapogeuzwa macho yao kuelekea watu wa Motoni, watasema: Mola wetu Mlezi! Usitujaalie kuwa pamoja na kaaumu madhalimu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watu wa Motoni watawaita watu wa Bustanini: Tumiminieni maji, au chochote alichowaruzuku Mwenyezi Mungu. Nao watasema: Hakika Mwenyezi Mungu ameviharamisha hivyo kwa makafiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbao waliifanya dini yao kuwa ni pumbao na mchezo, na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi leo sisi tunawasahau kama walivyousahau mkutano wa Siku yao hii, na kwa sababu ya kule kuzikataa Ishara zetu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, lipo wanalolingojea isipokuwa matokeo yake? Siku yatatapofika matokeo yake watasema wale waliokisahau: Kweli Mitume wa Mola Mlezi wetu walileta Haki! Je, tunao waombezi ili watuombee? Au turudishwe ili tufanye yasiyokuwa yale tuliyokuwa tukiyafanya? Bila ya shaka wamejihasiri nafsi zao, na yamewapotea waliyokuwa wakiyazua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu ambaye aliziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Kisha akainuka akawa juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana, ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazotumika kwa amri yake. Fahamuni! Ni kwake kuumba na amri. Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa baraka, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msifanye uharibifu katika dunia baada ya kutengenea kwake. Na mwombeni kwa hofu na kutumai. Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu iko karibu na wafanyao uzuri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Yeye ndiye anayetuma pepo (za kuvuma) kuwa ni bishara kabla ya kufika rehema yake. Hata hizo pepo zinapobeba mawingu mazito, tunayapeleka kwenye nchi iliyokufa. Kisha tunateremsha kwayo maji, na tukatoa kwayo kila aina ya matunda. Basi namna hiyo ndivyo tunavyowafufua wafu, ili mkumbuke.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ardhi nzuri mimea hutoka yake kwa idhini ya Mola Mlezi wake. Nayo ardhi ambayo ni mbaya haitoki isipokuwa mimea michache, isiyokuwa na faida, tena kwa shida. Na hivyo ndivyo tunavyozipambanua Ishara (Aya) kwa kaumu wanaoshukuru.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Enyi watu wangu! Mimi siko katika upotovu, lakini mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNawafikishia Ujumbe wa Mola Mlezi wangu, na ninawanasihi; na ninayajua kwa Mwenyezi Mungu msiyoyajua nyinyi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, mnastaajabu kukujieni mawaidha yanayotoka kwa Mola Mlezi wenu kwa njia ya mtu ambaye ni mmoja wenu, ili akuonyeni na ili mumche Mungu, na ili mpate kurehemewa?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi walimkanusha. Nasi tukamwokoa yeye na waliokuwa pamoja naye katika jahazi. Na tukawazamisha wale waliozikanusha Ishara zetu. Hakika hao walikuwa watu vipofu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa 'Aadi tulimpeleka ndugu yao, Huud. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu ila Yeye. Basi je, hamumchi?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema watukufu wa wale waliokufuru katika kaumu yake: Sisi tunakuona uko katika upumbavu, na hakika sisi tunakufikiria kuwa wewe ni katika waongo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Enyi watu wangu! Mimi sina upumbavu. Lakini mimi ni Mtume niliyetoka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMnaona ajabu kukufikieni mawaidha yanayotoka kwa Mola wenu Mlezi kwa mtu aliye mmoja wenu nyinyi ili awaonye? Na kumbukeni alivyokufanyeni mshike mahali pa kaumu ya Nuhu, na akawazidishia katika umbo. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Je, umetujia ili tumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na tuyaache waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu? Basi tuletee hayo unayotuahidi, ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Bila ya shaka adhabu na ghadhabu zimekwishakuwaangukia kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Mnabishana nami kwa sababu ya majina tu mliyoyaita nyinyi na baba zenu ambayo kwayo Mwenyezi Mungu hakuteremsha uthibitisho? Basi ngojeni, mimi pia ni pamoja nanyi katika wanaongoja.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukamwokoa yeye na waliokuwa pamoja naye kwa rehema zetu, na tukaikata mizizi ya wale waliozikanusha Ishara zetu, na hawakuwa wenye kuamini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa Thamud tulimpeleka ndugu yao, Swaleh. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika imekwishawafikia Ishara iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Huyu ni ngamia jike wa Mwenyezi Mungu aliye Ishara kwenu. Basi mwacheni ale kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala msimdhuru, isije kukushukieni adhabu chungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kumbukeni alivyowafanya wafuatizi (makhalifa) wa A’adi na akawaweka vizuri katika nchi, mnajenga majumba ya fakhari katika nyanda zake, na mnachonga majumba katika milima. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu wala msienee katika nchi kwa kufanya uharibifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaheshimiwa wa kaumu yake wanaojivuna waliwaambia wanaoonewa wenye kuamini miongoni mwao: Je, mnaitakidi ya kwamba Swaleh ametumwa na Mola wake Mlezi? Wakasema: Hakika sisi tunayaamini yale aliyotumwa nayo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakamuua yule ngamia, na wakaiasi amri ya Mola Mlezi wao, na wakasema: Ewe Saleh! Tuletee unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa Mitume.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Swaleh akawaacha na akasema: Enyi watu wangu! Niliwafikishia Ujumbe wa Mola wangu Mlezi, na nikawanasihi, lakini nyinyi hamuwapendi wanaonasihi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Lut alipowaambia kaumu yake, "Je, mnafanya uchafu ambao hajawatangulia kwa huo yeyote katika walimwengu?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa halikuwa jibu la kaumu yake isipokuwa walisema, "Watoeni kutoka katika mji wenu. Maana wao hakika ni watu wanaojitakasa."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa (watu wa) Madyana tulimtuma ndugu yao Shu'aib. Akasema, "Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Hamna mungu yeyote isipokuwa Yeye. Hakika imekwishawajia hoja wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi timizeni sawasawa vipimo na mizani, wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye uharibifu katika ardhi baada ya kutengenea kwake. Hayo ndiyo bora kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msikae katika kila njia mkitishia, na mkiizuia njia ya Mwenyezi Mungu wale waliomuamini, na mkiitaka ipotoke. Na kumbukeni mlipokuwa wachache, naye akawafanya kuwa wengi. Na tazameni jinsi ulivyokuwa mwisho wa waharibifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kama liko kundi miongoni mwenu lililoamini haya niliyotumwa nayo, na kundi lingine halikuamini, basi subirini mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu baina yetu. Naye ndiye Mbora zaidi wa wenye kuhukumu."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema waheshimiwa waliotakabari katika kaumu yake, "Lazima tutakutoa ewe Shu'aib na wale walioamini pamoja nawe katika mji wetu, au lazima mtarejea katika mila yetu." Akasema, "Je, hata kama tunachukia?"
Swahili Translation - Rowad Translation Center"Bila ya shaka tutakuwa tumemzulia uongo Mwenyezi Mungu ikiwa tutarudi katika mila yenu baada ya Mwenyezi Mungu kwishatuokoa kutokana nayo. Wala haiwi kwetu sisi kuirejea mila hiyo, isipokuwa akitaka Mwenyezi Mungu, Mola wetu Mlezi. Mola wetu Mlezi umekienea kila kitu kwa elimu. Kwa Mwenyezi Mungu tumetegemea. Mola wetu Mlezi, hukumu baina yetu na kaumu yetu kwa haki, nawe ndiwe Mbora zaidi wa wanaohukumu."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale waliomkadhibisha Shu'aib ni kama kwamba hawakuishi humo. Wale waliomkadhibisha Shu'aib walikuwa ndio waliohasiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hatukumtuma katika mji wowote Nabii yeyote isipokuwa tuliwachukua wakazi wake kwa umaskini na maradhi ili wanyenyekee.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukabadilisha pahali pa ubaya kwa wema, mpaka wakazidi, na wakasema, "Hakika ziliwafikia baba zetu taabu na raha." Basi tukawachukua kwa ghafla hali ya kuwa hawatambui.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa watu wa miji wangeliamini na wakamcha Mungu, basi hakika tungeliwafungulia baraka za kutoka mbinguni na ardhini. Lakini walikadhibisha, basi tukawachukua kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, wana amani dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu? Kwani hawawi na amani dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kaumu waliohasiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani haijawabainikia wale wanaoirithi ardhi baada ya waliokuwa wenyewe kwamba tukitaka tunawasibu kwa madhambi yao, na tukaziba nyoyo zao, kwa hivyo hawatasikia?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMiji hiyo, tunakusimulia katika habari zake. Na hakika waliwajia Mitume wao na hoja zilizo waziwazi. Lakini hawakuwa wenye kuamini yale waliyoyakadhibisha zamani. Namna hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoziba nyoyo za makafiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala hatukuwapata wengi wao wakiwa ni wenye kushika agano lolote, bali kwa hakika tuliwapata wengi wao ni wavukao mno mipaka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukamtuma baada yao Musa na Ishara zetu kwa Firauni na waheshimiwa wake. Nao wakazifanyia dhuluma. Basi tazama namna ulivyokuwa mwisho wa waharibifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterInastahiki zaidi juu yangu kwamba nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa haki tu. Hakika nimewajia na Ishara za waziwazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi waachilie pamoja nami Wana wa Israili."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Tupeni! Basi walipotupa, waliyafanyia uchawi macho ya watu na wakawatia hofu, na wakaleta uchawi mkubwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema Firauni: Mmemuamini kabla mimi kuwapa idhini? Hakika, hii ni njama mliyoipangia huko mjini ili muwatoe humo wenyewe. Basi karibu mtajua!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNawe hutushutumu kwa chuki isipokuwa kwa kuwa tumeziamini Ishara za Mola wetu Mlezi pindi zilipotujia. Ewe Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira na utufishe hali ya kuwa ni Waislamu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakasema waheshimiwa kutoka kwa kaumu ya Firauni: Je, unamuacha Musa na kaumu yake ili wafanye uharibifu katika ardhi na akuache wewe na miungu yako? Akasema: Tutawaua sana wavulana wao, na tuwaache hai wanawake wao. Na bila ya shaka sisi ni wenye nguvu juu yao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMusa akawaambia kaumu yake: Ombeni msaada kwa Mwenyezi Mungu, na subirini. Hakika ardhi ni ya Mwenyezi Mungu, anairithisha amtakaye katika waja wake. Na mwisho mwema ni wa wacha Mungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Tumeudhiwa kabla wewe kutujia, na baada ya wewe kutujia! Musa akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamuangamiza adui wenu, na akawafanya nyinyi ndio wa kufuatia kushika ardhi, ili atazame mtakavyokujatenda nyinyi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tuliwachukua watu wa Firauni kwa miaka (ya ukame), na kwa upungufu katika mazao, huenda wakakumbuka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakijiwa na zuri, wanasema, "Ni haki yetu hii." Na likiwasibu ovu, wanaona mkosi kwa Musa na wale walio pamoja naye. Tazama! Hakika mkosi wao huo unatoka kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wao hawajui.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukawatumia tufani, na nzige, na chawa, na vyura, na damu, ziwe ni Ishara za kina. Lakini wakatakabari, na wakawa kaumu wahalifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukawaadhibu, tukawazamisha katika bahari kwa sababu walizikadhibisha Ishara zetu, na wakawa wanaghafilika mbali nazo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawarithisha kaumu wale waliokuwa wakidhoofishwa, mashariki ya ardhi na magharibi yake ambayo tulibariki ndani yake. Na likatimia neno jema la Mola wako Mlezi juu ya Wana wa Israili, kwa vile walivyosubiri. Na tukayaangamiza yale aliyokuwa akiyafanya Firauni na kaumu yake, na yale waliyokuwa wakiyajenga.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawavusha bahari Wana wa Israili, kisha wakajia kaumu waliokuwa wanayaabudu masanamu yao. Wakasema, "Ewe Musa! Tufanyie mungu kama hawa walivyo na miungu." Musa akasema: Hakika nyinyi ni kaumu msiojua kitu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pale tulipowaokoa kutoka kwa watu wa Firauni waliowatia adhabu mbaya zaidi. Wakiwaua wavulana wenu, na wakiwaacha hai wanawake wenu. Na katika hayo yalikuwa majaribio makubwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tulimuahidi Musa usiku thelathini na tukazitimiza kwa kumi; basi ikatimia miadi ya Mola wake Mlezi usiku arobaini. Na Musa akamwambia kaka yake, Harun: Shika pahali pangu katika kaumu yangu na utengeneze, wala usifuate njia ya waharibifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa alipokuja Musa kwenye miadi yetu, na Mola wake Mlezi akamuongelesha, alisema: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe nikutazame. Mwenyezi Mungu akasema: Hutaniona. Lakini utazame huo mlima. Ikiwa utabaki mahali pake, basi utaniona. Basi alipojionyesha Mola wake Mlezi kwa mlima huo, akaufanya upasukepasuke, na Musa akaanguka chini akazimia. Basi alipozindukana, akasema: Subhanaka (Umetakasika)! Nimetubia kwako, na mimi ni wa kwanza wa Waumini.
Swahili Translation - Rowad Translation Center(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Musa! Hakika Mimi nilikuteua uende kwa watu na jumbe zangu na maneno yangu. Basi chukua hayo niliyokupa na kuwa katika wanaoshukuru.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukamuandikia kwenye mbao zile katika kila kitu, mawaidha na maelezo ya kina ya kila kitu. (Tukamwambia): Basi yachukue kwa nguvu na uwaamrishe kaumu yako wayachukue kwa ubora wake. Nami nitawaonyesha makazi ya wale waliovuka mipaka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNitawaepusha na Ishara zangu wale wanaotakabari katika ardhi bila ya haki. Na wao wakiona kila Ishara, hawaiamini. Wakiiona njia ya uwongofu, hawaichukui kuwa ndiyo njia. Lakini wakiiona njia ya ukengeufu, wanaichukua kuwa ndiyo njia. Hayo ni kwa sababu walizikadhibisha Ishara zetu, na walikuwa wakighafilika mbali nazo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kaumu ya Musa wakamfanya baada yake kutoka katika mapambo yao ndama mwenye kiwiliwili, mwenye kutoa mlio wa ng'ombe. Kwani hawakuona kuwa hawasemeshi wala hawaongoi njia yoyote? Walimchukua (kumuabudu), na wakawa madhalimu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakati mambo yalipoangushwa katika mikono yao, na wakaona ya kwamba wamekwishapotea, wakasema: Ikiwa Mola wetu Mlezi hataturehemu na akatufutia dhambi, basi bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa waliohasiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakati aliporudi Musa kwa kaumu yake hali ya kuwa ameghadhibika na kuhuzunika, akasema: Ni mabaya mno mliyonifanyia nyuma yangu! Je, mmeiharakisha amri ya Mola wenu Mlezi? Na akazitupa chini mbao zile, na akamkamata kaka yake kichwa akimvuta kwake. (Harun) akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Hakika kaumu hawa waliniona kuwa mimi ni dhaifu, na walikaribia kuniua. Basi usiwafurahishe maadui zangu, wala usiniweke pamoja na kaumu madhalimu.
Swahili Translation - Rowad Translation Center(Musa) akasema: Mola wangu Mlezi! Nifutie dhambi mimi na kaka yangu, na utuingize katika rehema yako. Nawe ni Mwenye kurehemu zaidi kuliko wote wenye kurehemu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale waliojifanyia (na kumuabudu) ndama, itawapata ghadhabu kutoka kwa Mola wao Mlezi, na udhalilifu katika maisha ya dunia. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa wazuao uongo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliotenda mabaya, kisha wakatubia baada yake na wakaamini, hakika Mola wako Mlezi baada ya hayo ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakati ghadhabu ilipomtulia Musa, akazichukua mbao zile. Na katika maandiko yake kuna uongofu na rehema kwa wale ambao wanamhofu Mola wao Mlezi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Musa akawateua kaumu wake wanaume sabini kwa ajili ya miadi yetu. Na ulipowachukua mtetemeko mkubwa, akasema: Mola wangu Mlezi! Ungelitaka, ungeliwaangamiza wao hapo kabla na hata mimi. Unatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wapumbavu katika sisi? Haya si chochote isipokuwa ni majaribio yako, unampoteza kwayo umtakaye, na unamuongoa umtakaye. Wewe ndiye rafiki mlinzi wetu. Basi tusitiri dhambi na uturehemu. Na Wewe ndiwe Mbora zaidi wa wasitirio dhambi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tuandikie mazuri katika dunia hii na katika Akhera. Hakika sisi tumerejea kwako. (Mwenyezi Mungu) akasema: Adhabu yangu nitamsibu kwayo nimtakaye. Na rehema yangu imeenea kila kitu. Basi nitaiandika hii hasa kwa wale wanaomcha Mungu, na wanaotoa Zaka, na wale ambao wanaziamini Ishara zetu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale ambao wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiyesoma wala kuandika, ambaye wanamkuta ameandikwa kwao katika Taurati na Injili, anayewaamrisha mema na anawakataza maovu, na anawahalalishia vizuri, na anawaharamishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo ambayo ilikuwa juu yao. Basi wale waliomwamini yeye, na wakampa taadhima, na wakamnusuru, na wakaifuata nuru ambayo iliteremshwa pamoja naye, hao ndio waliofaulu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Enyi watu! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi nyote, Yeye ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi. Hakuna mungu isipokuwa Yeye. anahuisha na anafisha. Basi mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Nabii asiyejua kusoma na kuandika, ambaye anamwamini Mwenyezi Mungu na maneno yake. Na mfuateni yeye ili muongoke.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawakatakata makabila kumi na mawili, mataifa mbali mbali. Na tulimfunulia Musa wakati kaumu yake walipomwomba maji kwamba: 'Lipige hilo jiwe kwa fimbo yako.' Mara zikabubujika kutoka humo chemchemi kumi na mbili, na kila watu wakajua pahali pao pa kunywea. Na tukawafunikia kivuli kwa mawingu, na tukawateremshia Manna na Salwa. 'Kuleni katika vizuri hivi tulivyowaruzuku.' Na hawakutudhulumu Sisi, bali walikuwa wakijidhulumu wenyewe.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pale walipoambiwa: Ukaeni mji huu, na mle humo popote mpendapo, na semeni: 'Tufutie dhambi zetu.' Na uingieni mlango wake kwa kusujudu, tutawasitiria makosa yenu. Walio wema tutawazidishia.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini wakabadilisha wale waliodhulumu miongoni mwao kauli isiyo ile waliyoambiwa. Basi tukawatumia adhabu kutoka mbinguni kwa vile walivyokuwa wakidhulumu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waulize kuhusu kijiji kilichokuwa kando ya bahari, walipokuwa wakiivunja Sabato (Jumaamosi ya mapumziko). Walipokuwa samaki wakiwajia juu juu siku ya Sabato, na siku isiyokuwa ya Sabato hawawajii. Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakivuka mipaka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kikundi miongoni mwao walisema: Kwa nini mnawawaidhi watu ambao tangu hapo Mwenyezi Mungu atawaangamiza au atawaadhibu adhabu kali? Wakasema: Ili uwe ni udhuru kwa Mola wenu Mlezi, na huenda nao wakamcha Mungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pale alipotangaza Mola wako Mlezi kwamba hakuna shaka atawaletea watu ambao watawaadhibu kwa adhabu mbaya mpaka Siku ya Kiyama. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuadhibu, na bila ya shaka ni Mwenye maghfira, na Mwenye kurehemu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawagawanya katika ardhi umma mbalimbali. Miongoni mwao kuna wale walio wema, na miongoni mwao kuna walio kinyume cha hivyo. Na tukawajaribu kwa mazuri na mabaya huenda wakarejea.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakafuatia baada yao wafuatizi waliokirithi Kitabu. Wanachukua anasa za haya maisha duni, na wanasema, "Tutasitiriwa dhambi!" Na ikiwajia tena anasa mfano wake, wanaichukua pia. Je, halikuchukuliwa juu yao agano la Kitabu kuwa wasiseme juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa haki tu? Nao wamekwishasoma yale yaliyo humo. Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wachao. Basi je, hamtii akilini?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pale tulipounyanyua mlima juu yao ukawa kama kwamba ni kiwingu kilichowafunika, na wakadhani kuwa utawaangukia, (tukawaambia): Chukueni yale tuliyowapa kwa nguvu, na yakumbukeni yaliyo ndani yake ili mche.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pale Mola wako Mlezi alipochukua kutoka kwa wanadamu kutoka katika migongo yao dhuria zao na akawashuhudisha juu ya nafsi zao (na kuwaambia), "Je, mimi si Mola wenu Mlezi?" Wakasema, "Ndiyo, tumeshuhudia." Mje mkasema Siku ya Kiyama, "Hakika sisi tulikuwa tumeghafilika mbali na haya."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu mkasema: Hakika baba zetu ndio walioshirikisha kabla yetu, na sisi ni dhuriya zao tu baada yao. Basi utatuangamiza kwa sababu ya waliyoyafanya wapotovu?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wasomee habari za yule ambaye tulimpa Ishara zetu, naye akajivua kutoka kwazo, basi Shetani akamfuata. Kwa hivyo, akawa miongoni mwa waliopotea.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa tungelitaka, tungelimwinua kwazo, lakini yeye alizama katika ulimwengu na akafuata matamanio yake. Basi mfano wake ni kama mfano wa mbwa. Ukimhujumu hupumua na kutoa ulimi nje, na ukimwacha, pia hupumua na kutoa ulimi nje. Huo ni mfano wa kaumu ambao walizikadhibisha Ishara zetu. Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYule ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoa, basi huyo ndiye mwongofu. Na yule aliyempoteza, basi hao ndio waliohasiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tumeiumbia Jahannamu wengi katika majini na watu. Wana nyoyo wasizofahamu kwazo. Na wana macho wasiyoona kwayo. Na wana masikio wasiyosikia kwayo. Hao ni kama wanyama wa mifugo, bali wao ni wapotovu zaidi. Hao ndio walioghafilika.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanaopindukia mipaka katika majina yake. Watakujalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawatazami ufalme wa mbingu na ardhi, na vile vyote alivyoviumba Mwenyezi Mungu katika vitu, na kwamba huenda muda wao umekwishakaribia? Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYule Mwenyezi Mungu alimpoteza, basi hana wa kumwongoa. Na atawaacha hao katika upotovu wao wakitangatanga.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanakuuliza kuhusu hiyo Saa (ya Kiyama) kusimama kwake ni lini? Sema: Elimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake isipokuwa Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haitawajia isipokuwa kwa ghafla tu. Wanakuuliza kama kwamba wewe una pupa ya kuijua. Sema: Elimu yake iko tu kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wa watu hawajui.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Siimilikii nafsi yangu manufaa wala madhara, isipokuwa apendavyo Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa ninayajua ya ghaibu, ningalitenda mema sana, wala ubaya usingenigusa. Mimi si chochote ila ni mwonyaji na mbashiri kwa kaumu wanaoamini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye aliyewaumba kutoka katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili ajitulize kwake. Na alipomuingilia, akabeba mimba nyepesi, akitembea nao. Anapokuwa mjamzito, wote wawili humwomba Mwenyezi Mungu, Mola wao Mlezi: Kama ukitupa mwana mwema hakika tutakuwa katika wanaoshukuru.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi alipowapa mwana mwema, wakamfanyia washirikina Mwenyezi Mungu katika kile kile alichowapa. Basi Mwenyezi Mungu ametukuka na huko kushirikisha kwao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu ni waja mfano wenu nyinyi. Basi waombeni, nao wawaitikie ikiwa nyinyi ni wakweli.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kama uchochezi kutoka kwa Shetani utakuchochea, basi tafuta ulinzi wa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Msikizi mzuri, Mwenye kujua vyema.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale wamchao Mungu, zinapowagusa pepesi kutoka kwa Shetani, mara huzindukana na hapo huwa wenye kuiona haki.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa usipowajia na Ishara, wanasema: Kwa nini hukuibuni? Sema: hakika mimi ninafuata tu yale yanayofunuliwa kwangu kutoka kwa Mola wangu Mlezi. Hii (Qur'ani) ni hoja zinazotoka kwa Mola wenu Mlezi, na uongofu, na rehema kwa kaumu wanaoamini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mkumbuke Mola wako Mlezi katika nafsi yako kwa unyenyekevu na hofu, na bila ya kuinua sauti juu kwa kauli, asubuhi na jioni, wala usiwe miongoni wa walioghafilika.