وَقَطَّعْنَٰهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ أُمَمًا مِّنْهُمُ ٱلصَّٰلِحُونَ وَمِنْهُمْ دُونَ ذَٰلِكَ وَبَلَوْنَٰهُم بِٱلْحَسَنَٰتِ وَٱلسَّيِّـَٔاتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawagawanya katika ardhi umma mbalimbali. Miongoni mwao kuna wale walio wema, na miongoni mwao kuna walio kinyume cha hivyo. Na tukawajaribu kwa mazuri na mabaya huenda wakarejea.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa tuliwafarikisha katika ardhi makundi makundi. Wako kati yao walio wema, na wengine kinyume cha hivyo. Na tukawajaribu kwa mema na mabaya ili wapate kurejea.