وَٱلْبَلَدُ ٱلطَّيِّبُ يَخْرُجُ نَبَاتُهُۥ بِإِذْنِ رَبِّهِۦ وَٱلَّذِى خَبُثَ لَا يَخْرُجُ إِلَّا نَكِدًا كَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ ٱلْـَٔايَٰتِ لِقَوْمٍ يَشْكُرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ardhi nzuri mimea hutoka yake kwa idhini ya Mola Mlezi wake. Nayo ardhi ambayo ni mbaya haitoki isipokuwa mimea michache, isiyokuwa na faida, tena kwa shida. Na hivyo ndivyo tunavyozipambanua Ishara (Aya) kwa kaumu wanaoshukuru.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa ardhi njema, yenye udongo wa rutba, hutoa mimea yenye kukua vizuri yenye uhai, kwa idhini ya Mola Mlezi wake. Na ardhi mbaya haitoi ila mimea michache, isiyo na faida, tena kwa shida. Na hivyo ndivyo tunavyo zipambanua Ishara (Aya) kwa watu wanao shukuru.