caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-A'raaf, Aya 37

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 39 · 7:37

فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِهِۦٓ أُو۟لَٰٓئِكَ يَنَالُهُمْ نَصِيبُهُم مِّنَ ٱلْكِتَٰبِ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَتْهُمْ رُسُلُنَا يَتَوَفَّوْنَهُمْ قَالُوٓا۟ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ قَالُوا۟ ضَلُّوا۟ عَنَّا وَشَهِدُوا۟ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا۟ كَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo, au akazikadhibisha Ishara zake? Hao litawafikia fungu lao waliloandikiwa, mpaka watakapowajia wajumbe wetu kuwafisha, watawaambia: Wako wapi wale mliokuwa mkiwaomba badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema: 'Wametupotea!' Na watashuhudia dhidi yao wenyewe kwamba walikuwa makafiri.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniBasi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, au anaye zikanusha Ishara zake? Hao itawafikia sehemu yao waliyo andikiwa, mpaka watakapo wafikia wajumbe wetu kuwafisha, watawaambia: Wako wapi mlio kuwa mkiwaomba badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Wametupotea! Na watajishuhudia wenyewe kwamba walikuwa makafiri.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70