وَبَيْنَهُمَا حِجَابٌ وَعَلَى ٱلْأَعْرَافِ رِجَالٌ يَعْرِفُونَ كُلًّۢا بِسِيمَىٰهُمْ وَنَادَوْا۟ أَصْحَٰبَ ٱلْجَنَّةِ أَن سَلَٰمٌ عَلَيْكُمْ لَمْ يَدْخُلُوهَا وَهُمْ يَطْمَعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa baina yao (makundi mawili hayo) patakuwapo pazia. Na juu ya Minyanyuko patakuwa watu watakaomjua kila mmoja kwa alama zao, na wao watawaita watu wa Peponi: Salamu Alaykum (amani iwe juu yenu)! Wao bado hawajaingia humo, lakini wanatumai.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa baina ya makundi mawili hayo patakuwapo pazia. Na juu ya Mnyanyuko patakuwa watu watakao wajua wote kwa alama zao, na wao watawaita watu wa Peponi: Assalamu Alaykum, Amani juu yenu! Wao bado hawajaingia humo, lakini wanatumai.