فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَٰقَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَٰلَٰتِ رَبِّى وَنَصَحْتُ لَكُمْ فَكَيْفَ ءَاسَىٰ عَلَىٰ قَوْمٍ كَٰفِرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi akawaachilia mbali na akasema, "Enyi kaumu yangu! Hakika nimewafikishia jumbe za Mola wangu Mlezi, na nimewanasihi. Basi vipi niwahuzunikie kaumu makafiri?"
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniBasi akawaachilia mbali na akasema: Enyi kaumu yangu! Nimekufikishieni Ujumbe wa Mola Mlezi wangu, na nimekunasihini; basi vipi niwahuzunikie watu makafiri?