caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-A'raaf, Aya 137

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 39 · 7:137

وَأَوْرَثْنَا ٱلْقَوْمَ ٱلَّذِينَ كَانُوا۟ يُسْتَضْعَفُونَ مَشَٰرِقَ ٱلْأَرْضِ وَمَغَٰرِبَهَا ٱلَّتِى بَٰرَكْنَا فِيهَا وَتَمَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ ٱلْحُسْنَىٰ عَلَىٰ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ بِمَا صَبَرُوا۟ وَدَمَّرْنَا مَا كَانَ يَصْنَعُ فِرْعَوْنُ وَقَوْمُهُۥ وَمَا كَانُوا۟ يَعْرِشُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawarithisha kaumu wale waliokuwa wakidhoofishwa, mashariki ya ardhi na magharibi yake ambayo tulibariki ndani yake. Na likatimia neno jema la Mola wako Mlezi juu ya Wana wa Israili, kwa vile walivyosubiri. Na tukayaangamiza yale aliyokuwa akiyafanya Firauni na kaumu yake, na yale waliyokuwa wakiyajenga.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa tukawarithisha watu walio kuwa wanadharauliwa mashariki na magharibi ya ardhi tuliyo ibariki. Na likatimia neno jema la Mola Mlezi wako juu ya Wana wa Israili, kwa vile walivyo subiri. Na tukayaangamiza aliyo kuwa akiyafanya Firauni na kaumu yake, na waliyo kuwa wakiyajenga.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70