وَلَمَّا وَقَعَ عَلَيْهِمُ ٱلرِّجْزُ قَالُوا۟ يَٰمُوسَى ٱدْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ لَئِن كَشَفْتَ عَنَّا ٱلرِّجْزَ لَنُؤْمِنَنَّ لَكَ وَلَنُرْسِلَنَّ مَعَكَ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ilipowaangukia adhabu, wakasema, "Ewe Musa! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa yale aliyokuahidi. Ukituondolea adhabu hii, hakuna shaka tutakuamini, na tutawaachilia Wana wa Israili waende pamoja nawe."
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa ilipo waangukia adhabu wakasema: Ewe Musa! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa aliyo kuahidi. Ukituondolea adhabu hii hapana shaka tutakuamini, na tutawaachilia Wana wa Israili wende nawe.