caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-A'raaf, Aya 169

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 39 · 7:169

فَخَلَفَ مِنۢ بَعْدِهِمْ خَلْفٌ وَرِثُوا۟ ٱلْكِتَٰبَ يَأْخُذُونَ عَرَضَ هَٰذَا ٱلْأَدْنَىٰ وَيَقُولُونَ سَيُغْفَرُ لَنَا وَإِن يَأْتِهِمْ عَرَضٌ مِّثْلُهُۥ يَأْخُذُوهُ أَلَمْ يُؤْخَذْ عَلَيْهِم مِّيثَٰقُ ٱلْكِتَٰبِ أَن لَّا يَقُولُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلْحَقَّ وَدَرَسُوا۟ مَا فِيهِ وَٱلدَّارُ ٱلْـَٔاخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ أَفَلَا تَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakafuatia baada yao wafuatizi waliokirithi Kitabu. Wanachukua anasa za haya maisha duni, na wanasema, "Tutasitiriwa dhambi!" Na ikiwajia tena anasa mfano wake, wanaichukua pia. Je, halikuchukuliwa juu yao agano la Kitabu kuwa wasiseme juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa haki tu? Nao wamekwishasoma yale yaliyo humo. Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wachao. Basi je, hamtii akilini?
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wakafuatia baada yao kizazi kibaya walio rithi Kitabu. Wakashika anasa za haya maisha duni, na wakasema: Tutasamehewa! Na ikiwajia tena anasa kama hiyo wataishika pia. Je, hawakufanyiwa agano la Kitabu kuwa wasiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila Haki tu? Nao wamekwisha soma yaliomo humo. Na nyumba ya Akhera ni bora kwa wanao jikinga na maasi. Basi je, hamtii akilini?
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70