caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-A'raaf, Aya 150

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 39 · 7:150

وَلَمَّا رَجَعَ مُوسَىٰٓ إِلَىٰ قَوْمِهِۦ غَضْبَٰنَ أَسِفًا قَالَ بِئْسَمَا خَلَفْتُمُونِى مِنۢ بَعْدِىٓ أَعَجِلْتُمْ أَمْرَ رَبِّكُمْ وَأَلْقَى ٱلْأَلْوَاحَ وَأَخَذَ بِرَأْسِ أَخِيهِ يَجُرُّهُۥٓ إِلَيْهِ قَالَ ٱبْنَ أُمَّ إِنَّ ٱلْقَوْمَ ٱسْتَضْعَفُونِى وَكَادُوا۟ يَقْتُلُونَنِى فَلَا تُشْمِتْ بِىَ ٱلْأَعْدَآءَ وَلَا تَجْعَلْنِى مَعَ ٱلْقَوْمِ ٱلظَّٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakati aliporudi Musa kwa kaumu yake hali ya kuwa ameghadhibika na kuhuzunika, akasema: Ni mabaya mno mliyonifanyia nyuma yangu! Je, mmeiharakisha amri ya Mola wenu Mlezi? Na akazitupa chini mbao zile, na akamkamata kaka yake kichwa akimvuta kwake. (Harun) akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Hakika kaumu hawa waliniona kuwa mimi ni dhaifu, na walikaribia kuniua. Basi usiwafurahishe maadui zangu, wala usiniweke pamoja na kaumu madhalimu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa alipo rudi Musa kwa watu wake, naye amekasirika na kuhuzunika, alisema: Ni maovu yalioje mlio nifanyia nyuma yangu! Je, mmeitangulia amri ya Mola wenu Mlezi? Na akaziweka chini zile mbao, na akamkamata kichwa ndugu yake akimvutia kwake. (Haarun) akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Hakika hawa watu wamenidharau, na wakakaribia kuniuwa. Basi usiwafurahishe maadui juu yangu, wala usinifanye pamoja na watu madhaalimu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70