وَقَالَ ٱلْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوْمَهُۥ لِيُفْسِدُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ وَيَذَرَكَ وَءَالِهَتَكَ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبْنَآءَهُمْ وَنَسْتَحْىِۦ نِسَآءَهُمْ وَإِنَّا فَوْقَهُمْ قَٰهِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakasema waheshimiwa kutoka kwa kaumu ya Firauni: Je, unamuacha Musa na kaumu yake ili wafanye uharibifu katika ardhi na akuache wewe na miungu yako? Akasema: Tutawaua sana wavulana wao, na tuwaache hai wanawake wao. Na bila ya shaka sisi ni wenye nguvu juu yao.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWakasema waheshimiwa wa kaumu ya Firauni: Unamuacha Musa na watu wake walete uharibifu katika nchi na wakuache wewe na miungu yako? Akasema: Tutawauwa wavulana wao, na tutawaacha hai wanawake wao. Na bila ya shaka sisi ni wenye nguvu juu yao.