قَالَ يَٰمُوسَىٰٓ إِنِّى ٱصْطَفَيْتُكَ عَلَى ٱلنَّاسِ بِرِسَٰلَٰتِى وَبِكَلَٰمِى فَخُذْ مَآ ءَاتَيْتُكَ وَكُن مِّنَ ٱلشَّٰكِرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Musa! Hakika Mimi nilikuteua uende kwa watu na jumbe zangu na maneno yangu. Basi chukua hayo niliyokupa na kuwa katika wanaoshukuru.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Musa! Mimi nimekuteuwa wende kwa watu na Ujumbe wangu na maneno yangu. Basi chukua niliyo kupa na uwe katika wanao shukuru.