سَأَصْرِفُ عَنْ ءَايَٰتِىَ ٱلَّذِينَ يَتَكَبَّرُونَ فِى ٱلْأَرْضِ بِغَيْرِ ٱلْحَقِّ وَإِن يَرَوْا۟ كُلَّ ءَايَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا۟ بِهَا وَإِن يَرَوْا۟ سَبِيلَ ٱلرُّشْدِ لَا يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا وَإِن يَرَوْا۟ سَبِيلَ ٱلْغَىِّ يَتَّخِذُوهُ سَبِيلًا ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَٰتِنَا وَكَانُوا۟ عَنْهَا غَٰفِلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNitawaepusha na Ishara zangu wale wanaotakabari katika ardhi bila ya haki. Na wao wakiona kila Ishara, hawaiamini. Wakiiona njia ya uwongofu, hawaichukui kuwa ndiyo njia. Lakini wakiiona njia ya ukengeufu, wanaichukua kuwa ndiyo njia. Hayo ni kwa sababu walizikadhibisha Ishara zetu, na walikuwa wakighafilika mbali nazo.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNitawatenga na Ishara zangu wale wanao fanya kiburi katika nchi bila ya haki. Na wao wakiona kila Ishara hawaiamini. Wakiiona njia ya uwongofu hawaishiki kuwa ndiyo njia; lakini wakiiona njia ya upotofu wanaishika kuwa ndiyo njia. Hayo ni kwa sababu wamezikanusha Ishara zetu, na wameghafilika nazo.