وَلَوْ شِئْنَا لَرَفَعْنَٰهُ بِهَا وَلَٰكِنَّهُۥٓ أَخْلَدَ إِلَى ٱلْأَرْضِ وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ فَمَثَلُهُۥ كَمَثَلِ ٱلْكَلْبِ إِن تَحْمِلْ عَلَيْهِ يَلْهَثْ أَوْ تَتْرُكْهُ يَلْهَث ذَّٰلِكَ مَثَلُ ٱلْقَوْمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَٰتِنَا فَٱقْصُصِ ٱلْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa tungelitaka, tungelimwinua kwazo, lakini yeye alizama katika ulimwengu na akafuata matamanio yake. Basi mfano wake ni kama mfano wa mbwa. Ukimhujumu hupumua na kutoa ulimi nje, na ukimwacha, pia hupumua na kutoa ulimi nje. Huo ni mfano wa kaumu ambao walizikadhibisha Ishara zetu. Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa tungelitaka tungeli mtukuza kwa hizo Ishara, lakini yeye aliushikilia ulimwengu na akafuata pumbao lake. Basi mfano wake ni mfano wa mbwa. Ukimhujumu hupumua na kutoa ulimi na ukimwacha pia hupumua na kutoa ulimi. Huo ni mfano wa kaumu wanao zikanusha Ishara zetu. Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari.