وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِنۢ بَنِىٓ ءَادَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ قَالُوا۟ بَلَىٰ شَهِدْنَآ أَن تَقُولُوا۟ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَٰذَا غَٰفِلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pale Mola wako Mlezi alipochukua kutoka kwa wanadamu kutoka katika migongo yao dhuria zao na akawashuhudisha juu ya nafsi zao (na kuwaambia), "Je, mimi si Mola wenu Mlezi?" Wakasema, "Ndiyo, tumeshuhudia." Mje mkasema Siku ya Kiyama, "Hakika sisi tulikuwa tumeghafilika mbali na haya."
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa pale Mola wako Mlezi alipo waleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Wakasema: Kwani! Tumeshuhudia. Msije mkasema Siku ya Kiyama sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo.