caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-A'raaf, Aya 145

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 39 · 7:145

وَكَتَبْنَا لَهُۥ فِى ٱلْأَلْوَاحِ مِن كُلِّ شَىْءٍ مَّوْعِظَةً وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَىْءٍ فَخُذْهَا بِقُوَّةٍ وَأْمُرْ قَوْمَكَ يَأْخُذُوا۟ بِأَحْسَنِهَا سَأُو۟رِيكُمْ دَارَ ٱلْفَٰسِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukamuandikia kwenye mbao zile katika kila kitu, mawaidha na maelezo ya kina ya kila kitu. (Tukamwambia): Basi yachukue kwa nguvu na uwaamrishe kaumu yako wayachukue kwa ubora wake. Nami nitawaonyesha makazi ya wale waliovuka mipaka.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa tukamuandikia katika mbao kila kitu, mawaidha na maelezo ya mambo yote. (Tukamwambia): Basi yashike kwa nguvu na uwaamrishe watu wako wayashike kwa ubora wake. Nami nitakuonyesheni makaazi ya wapotofu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70