ثُمَّ بَدَّلْنَا مَكَانَ ٱلسَّيِّئَةِ ٱلْحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَوا۟ وَّقَالُوا۟ قَدْ مَسَّ ءَابَآءَنَا ٱلضَّرَّآءُ وَٱلسَّرَّآءُ فَأَخَذْنَٰهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukabadilisha pahali pa ubaya kwa wema, mpaka wakazidi, na wakasema, "Hakika ziliwafikia baba zetu taabu na raha." Basi tukawachukua kwa ghafla hali ya kuwa hawatambui.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniKisha Sisi hubadilisha mahala pa ubaya kwa wema, hata wakazidi, na wakasema: Taabu na raha ziliwafikia baba zetu. Basi kwa ghafla tukawashika, hali ya kuwa hawajatambua.