وَإِذْ قِيلَ لَهُمُ ٱسْكُنُوا۟ هَٰذِهِ ٱلْقَرْيَةَ وَكُلُوا۟ مِنْهَا حَيْثُ شِئْتُمْ وَقُولُوا۟ حِطَّةٌ وَٱدْخُلُوا۟ ٱلْبَابَ سُجَّدًا نَّغْفِرْ لَكُمْ خَطِيٓـَٰٔتِكُمْ سَنَزِيدُ ٱلْمُحْسِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pale walipoambiwa: Ukaeni mji huu, na mle humo popote mpendapo, na semeni: 'Tufutie dhambi zetu.' Na uingieni mlango wake kwa kusujudu, tutawasitiria makosa yenu. Walio wema tutawazidishia.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa pale walipo ambiwa: Kaeni katika mji huu, na mle humo mpendapo, na semeni: Tufutie dhambi zetu. Na ingieni katika mlango wake kwa unyenyekevu, tupate kukusameheni makosa yenu. Walio wema tutawazidishia.