caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-A'raaf, Aya 155

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 39 · 7:155

وَٱخْتَارَ مُوسَىٰ قَوْمَهُۥ سَبْعِينَ رَجُلًا لِّمِيقَٰتِنَا فَلَمَّآ أَخَذَتْهُمُ ٱلرَّجْفَةُ قَالَ رَبِّ لَوْ شِئْتَ أَهْلَكْتَهُم مِّن قَبْلُ وَإِيَّٰىَ أَتُهْلِكُنَا بِمَا فَعَلَ ٱلسُّفَهَآءُ مِنَّآ إِنْ هِىَ إِلَّا فِتْنَتُكَ تُضِلُّ بِهَا مَن تَشَآءُ وَتَهْدِى مَن تَشَآءُ أَنتَ وَلِيُّنَا فَٱغْفِرْ لَنَا وَٱرْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ ٱلْغَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Musa akawateua kaumu wake wanaume sabini kwa ajili ya miadi yetu. Na ulipowachukua mtetemeko mkubwa, akasema: Mola wangu Mlezi! Ungelitaka, ungeliwaangamiza wao hapo kabla na hata mimi. Unatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wapumbavu katika sisi? Haya si chochote isipokuwa ni majaribio yako, unampoteza kwayo umtakaye, na unamuongoa umtakaye. Wewe ndiye rafiki mlinzi wetu. Basi tusitiri dhambi na uturehemu. Na Wewe ndiwe Mbora zaidi wa wasitirio dhambi.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa Musa akawateuwa watu sabiini katika kaumu yake kwa miadi yetu. Na ulipo fika mtetemeko mkubwa alisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Ungeli taka ungeli wahiliki wao na mimi zamani! Unatuhiliki kwa waliyo yafanya wajinga katika sisi? Haya si chochote ila ni mtihani wako, umpoteze umtakaye na umhidi umtakaye. Wewe ndiye Rafiki Mlinzi wetu. Basi tughufirie na uturehemu. Na Wewe ndiye mbora wa kughufiria.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70