caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-A'raaf, Aya 163

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 39 · 7:163

وَسْـَٔلْهُمْ عَنِ ٱلْقَرْيَةِ ٱلَّتِى كَانَتْ حَاضِرَةَ ٱلْبَحْرِ إِذْ يَعْدُونَ فِى ٱلسَّبْتِ إِذْ تَأْتِيهِمْ حِيتَانُهُمْ يَوْمَ سَبْتِهِمْ شُرَّعًا وَيَوْمَ لَا يَسْبِتُونَ لَا تَأْتِيهِمْ كَذَٰلِكَ نَبْلُوهُم بِمَا كَانُوا۟ يَفْسُقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waulize kuhusu kijiji kilichokuwa kando ya bahari, walipokuwa wakiivunja Sabato (Jumaamosi ya mapumziko). Walipokuwa samaki wakiwajia juu juu siku ya Sabato, na siku isiyokuwa ya Sabato hawawajii. Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakivuka mipaka.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa waulize khabari za mji ulio kuwa kando ya bahari, wakiivunja Sabato (Jumaamosi ya mapumziko). Samaki walikuwa wakiwajia juu juu siku ya mapumziko yao, na siku zisio kuwa za kupumzika hawakuwa wakiwajia. Kwa namna hiyo tuliwajaribu kwa sababu walikuwa wakifanya upotovu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70