Swahili Translation - Rowad Translation CenterSifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye aliumba mbingu na ardhi, na akafanya giza mbalimbali na nuru. Kisha wale waliokufuru wanawafanya wengine kuwa sawa na Mola wao Mlezi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye aliyewaumba kutokana na udongo, kisha akawahukumia muda, na muda maalumu uko kwake tu. Kisha nyinyi mnatia shaka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Yeye ndiye Mwenyezi Mungu katika mbingu na katika ardhi. Anajua ya siri yenu na ya dhahiri yenu. Na anajua mnayoyachuma.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi hakika walikwishaikadhibisha haki ilipowajia. Kwa hivyo, zitawajia habari za yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawakuona ni vizazi vingapi tulivyoviangamiza kabla yao? Tuliwaimarisha katika dunia namna ambavyo hatukuwaimarisha nyinyi; na tukawatumia mvua nyingi na tukaifanya mito inapita kwa chini yao. Mwishowe tukawaangamiza kwa madhambi yao; na tukaanzisha baada yao kizazi kingine.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau tungelikuteremshia kitabu cha karatasi, wakakigusa kwa mikono yao, wangelisema wale waliokufuru: Haya si chochote isipokuwa ni uchawi ulio wazi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walisema, "Mbona hakuteremshiwa Malaika?" Na kama tungelimteremsha Malaika, basi bila ya shaka ingeshahukumiwa amri, kisha wasingelipewa muhula.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kama tungelimfanya Malaika, bila ya shaka tungelimfanya kuwa mwanamume, na tungeliwatilia matatizo yale wanayoyatatiza wao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ni vya nani vilivyo katika mbingu na katika ardhi? Sema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Yeye ameiandika rehema juu ya nafsi yake. Hakika atawakusanya hadi Siku ya Kiyama isiyokuwa na shaka. Wale waliojihasiri nafsi zao, wao hawaamini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Je, nimfanye rafiki mwandani asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mwanzilishi wa mbingu na ardhi, naye ndiye anayelisha wala halishwi? Sema: Hakika Mimi nimeamrishwa kwamba niwe wa kwanza wa wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ikiwa Mwenyezi Mungu atakugusa kwa madhara, basi hapana wa kuyaondoa isipokuwa Yeye. Na ikiwa atakugusa kwa heri, basi Yeye ndiye Muweza wa kila kitu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ni kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa kabisa? Sema: Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye shahidi baina yangu na nyinyi. Na imefunuliwa kwangu Qur-ani hii ili kwayo niwaonye nyinyi na kila inayemfikia. Ati kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu wapo miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii hayo. Sema: Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu, nami hakika niko mbali na mnaowashirikisha.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale tuliowapa Kitabu wanakijua kama wanavyowajua watoto wao. Wale waliozihasiri nafsi zao, basi wao hawaamini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa miongoni mwao kuna wale wanaokusikiliza; na tumezitia pazia kwenye nyoyo zao wasije kuyafahamu. Na upo uziwi katika masikio yao, na wakiona kila Ishara, hawaiamini. Mpaka wakikujia kwa kujadiliana nawe, wanasema wale waliokufuru: Hizi si chochote isipokuwa hadithi za watu wa kale.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNao huwazuia watu hayo, na wao wenyewe wanajitenga nayo. Nao hawaangamizi isipokuwa nafsi zao tu, wala wao hawatambui.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau ungeona waliposimamishwa kwenye Moto, wakawa wanasema: Laiti tungelirudishwa, wala tusizikadhibishe tena Ishara za Mola wetu Mlezi, na tuwe miongoni mwa Waumini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBali yamewadhihirikia yale waliyokuwa wakiyaficha zamani. Na lau wangelirudishwa, bila ya shaka wangeliyarejea yale yale waliyokatazwa. Na hakika wao ni waongo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau utaona walivyosimamishwa mbele ya Mola wao Mlezi, akasema, "Je, huu si uhakika?" Na wao wakasema, "Ndiyo? Tunaapa kwa Mola wetu Mlezi (ni uhakika)." Yeye akasema: Basi onjeni adhabu kwa sababu ya vile mlivyokuwa mnakufuru.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wamehasirika wale waliokadhibisha kukutana na Mwenyezi Mungu, mpaka ilipowajia Saa kwa ghafla, wakasema: 'Ee majuto yetu kwa yale tuliyoyapuuza!' Nao watabeba mizigo yao juu ya migongo yao. Tazama! Ni maovu mno hayo wanayoyabeba.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa maisha ya dunia si chochote isipokuwa ni mchezo na pumbao tu. Na hakika Nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wale wanaomcha Mwenyezi Mungu. Basi, je, hamtumii akili?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika tunajua ya kwamba yanakuhuzunisha yale wanayoyasema. Basi hakika wao hawakukadhibishi wewe, lakini hao madhalimu wanazikataa Ishara za Mwenyezi Mungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika walikadhibiwa Mitume wa kabla yako. Nao wakavumilia kule kukanushwa, na kuudhiwa, mpaka ilipowafikia nusura yetu. Na hakuna wa kubadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu. Na hakika imekwishakujia katika habari za Mitume hao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ikiwa ni makubwa kwako huku kupeana kwao mgongo, basi kama unaweza kutafuta njia ya chini kwa chini ya ardhi, au ngazi ya kwendea mbinguni ili uwaletee Ishara. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelipenda, angeliwakusanya kwenye uongofu. Basi kamwe usiwe miongoni mwa wajinga.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wanaoitikia ni wale wanaosikia. Na ama wafu, Mwenyezi Mungu atawafufua, kisha kwake Yeye ndiko watakakorejeshwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walisema: Kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuteremsha muujiza. Lakini wengi wao hawajui.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakuna mnyama yeyote katika ardhi, wala ndege anayepaa kwa mbawa zake mbili, isipokuwa ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza kitu chochote katika Kitabu. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliozikadhibisha Ishara zetu ni viziwi na mabubu wamo katika giza mbalimbali. Yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka, anampoteza, na yule ambaye anataka, anamuweka katika Njia iliyonyooka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mwaonaje ikiwajia adhabu ya Mwenyezi Mungu, au ikawajia hiyo Saa, asiyekuwa Mwenyezi Mungu ndiye mtakayemuomba, ikiwa nyinyi ni wakweli?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa yakini tuliwatuma Mitume kwa kaumu zilizokuwa kabla yako, kisha tukawatia katika dhiki na mashaka ili wanyenyekee.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi waliposahau yale waliyokumbushwa, tuliwafungulia milango ya kila kitu. Mpaka walipofurahia yale waliyopewa, tukawashika kwa ghafla, na mara wakawa wenye kukata tamaa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mwaonaje Mwenyezi Mungu akinyakua kusikia kwenu, na kuona kwenu, na akaziziba nyoyo zenu, ni mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayewaletea hayo tena? Angalia vipi tunavyozieleza Ishara, kisha wao wanapuuza.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mwaonaje, ikiwafikia adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa ghafla, au kwa dhahiri, je wataangamizwa isipokuwa kaumu waliodhulumu?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hatuwatumi Mitume isipokuwa huwa ni wabashiri na waonyaji. Basi mwenye kuamini na akatengenea, haitakuwa hofu yoyote juu yao, wala hawatahuzunika.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mimi siwaambii kuwa ninazo hazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyofichikana. Wala siwaambii kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati isipokuwa yanayofunuliwa kwangu. Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi hamfikirii?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waonye kwayo wale wanaohofu kuwa watakusanywa kwa Mola wao Mlezi, hali ya kuwa hawana kando naye mlinzi wala mwombezi, ili wamche Mwenyezi Mungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala usiwafukuze wale wanaomwomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni kwa kutaka radhi yake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata uwafukuze na uwe miongoni mwa wenye kudhulumu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hivi ndivyo tunavyowajaribu wao kwa wao, ili waseme: Ni hao ndio Mwenyezi Mungu amewafadhilisha miongoni mwetu? Kwani Mwenyezi Mungu hawajui vyema wanaoshukuru?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanapokujia wanaoziamini Ishara zetu waambie: Assalamu alaikum! (Amani iwe juu yenu!) Mola wenu Mlezi amejilazimisha rehema, ya kwamba atakayefanya uovu miongoni mwenu kwa ujinga, kisha akatubu baada yake na akatengenea, basi hakika Yeye ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mimi nipo kwenye sheria iliyo wazi itokayo kwa Mola wangu Mlezi, nanyi mnaikanusha. Mimi sina hicho (adhabu) mnachotaka kije haraka. Hakuna hukumu ila ya Mwenyezi Mungu. Yeye anasimulia yaliyo kweli; naye ni Mbora wa kuhukumu kuliko wote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Lau kuwa ninacho hicho mnachotaka kije haraka, ingelikwishakatwa shauri baina yangu na nyinyi. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayewajua zaidi madhalimu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ziko kwake funguo za ghaibu; hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Yeye anajua kilicho katika nchi kavu na baharini. Na halidondoki jani ila analijua. Wala punje katika giza la ardhi, wala kinyevu, wala kikavu ila kimo katika Kitabu kinachobainisha.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye ndiye Mwenye nguvu za kushinda, aliye juu ya waja wake. Na huwapelekea (nyinyi) waangalizi, mpaka mmoja wenu yakimjia mauti wajumbe wetu humfisha, nao hawapuuzi chochote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu, Mola wao wa Haki. Hakika, hukumu ni yake. Naye ni Mwepesi zaidi kuliko wote wanaohisabu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ni nani anayewaokoa kutoka katika giza la nchi kavu na baharini? Mnamwomba kwa unyenyekevu na kwa siri, mkisema: Kama akituokoa na haya, bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanaoshukuru.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mwenyezi Mungu hukuokoeni kutoka katika hayo, na kutoka katika kila mashaka, na kisha nyinyi mnamshirikisha!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Yeye ndiye Muweza wa kuwatumia adhabu kutoka juu yenu au kutoka chini ya miguu yenu, au awavishe fujo la mfarakano, na awaonjeshe baadhi yenu jeuri ya wenzi wenu. Tazama vipi tunavyozieleza Aya ili wafahamu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa unapowaona wanaoziingilia Aya zetu, basi jitenge nao mpaka waingilie mazungumzo mengine. Na kama Shetani atakusahaulisha, basi baada ya kutanabahi usikae pamoja na watu madhalimu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaachilie mbali walioifanya dini yao ni mchezo na pumbao, na uhai wa dunia ukawadanganya. Nawe kumbusha kwayo, isije nafsi ikaangamizwa kwa sababu ya iliyoyachuma, nayo haina mlinzi wala mwombezi ila Mwenyezi Mungu. Na ingetoa kila fidia, haitokubaliwa. Hao ndio walioangamizwa kwa sababu ya yale waliyoyachuma. Wao watapata kinywaji cha maji ya moto kabisa, na adhabu chungu kwa sababu ya walivyokuwa wakikufuru.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Je, tumuombe asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye hatufai wala hatudhuru, na turejee nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuongoa? Tuwe kama ambao mashetani wamempumbaza katika ardhi, amechanganyikiwa? Anao marafiki wanaomwita aende kwenye uwongofu, wakimwambia: 'Njoo kwetu!' Sema: Hakika uongofu wa Mwenyezi Mungu ndio Uongofu. Nasi tumeamrishwa tusilimu kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Siku atakaposema: "Kuwa!" Na yawe. Kauli yake ni Haki. Na ufalme wote ni wake Siku litakapopulizwa barugumu, Mjuzi wa yaliyofichikana na yanayoonekana. Naye ndiye Mwenye hekima, Mwenye habari zote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pale Ibrahim alipomwambia baba yake, Azar: Unayafanya masanamu kuwa ni miungu? Hakika mimi nakuona wewe na watu wako mko katika upotovu ulio wazi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa alipoliona jua linachomoza, akasema: 'Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Huyu ni mkubwa zaidi.' Na lilipotua, akasema: Enyi kaumu yangu! Mimi niko mbali sana na hayo mnayoshirikisha.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika mimi nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi, huku nikiwa mnyoofu, wala mimi si miongoni mwa washirikina.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kaumu yake wakamhoji. Akasema: Je, mnanihoji kuhusiana na Mwenyezi Mungu, na ilhali Yeye hakika amekwishaniongoa? Wala siogopi hao mnaowashirikisha naye, isipokuwa ikiwa Mola wangu Mlezi akipenda kitu. Mola wangu Mlezi amekusanya elimu ya kila kitu. Basi je, hamkumbuki?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa vipi nivihofu hivyo mlivyovishirikisha, ilhali nyinyi hamhofu kuwa nyinyi mmemshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu ambacho hakuwateremshia uthibitisho juu yake. Basi ni kundi gani katika mawili haya lina haki zaidi kupata amani, ikiwa nyinyi mnajua?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale ambao waliamini, na hawakuchanganya imani yao na dhuluma, hao ndio wana amani, na wao ndio walioongoka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hizo ndizo hoja zetu tulizompa Ibrahim dhidi ya kaumu yake. Tunamnyanyua tumtakaye daraja mbalimbali. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hekima, Mwenye kujua yote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukamtunuku (Ibrahim) Is-haq na Yaakub. Kila mmoja wao tulimwongoa. Na Nuhu tulimwongoa kabla. Na katika kizazi chake tulimwongoa Daud na Suleiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tunavyowalipa wafanyao mazuri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuo ni uongofu wa Mwenyezi Mungu, anaongoa kwao amtakaye katika waja wake. Na lau wangelimshirikisha, basi yangeliwaharibikia yale waliyokuwa wakiyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ndio tuliowapa Kitabu, na hukumu, na Unabii. Kwa hivyo, ikiwa hawa (makafiri) watayakufuru, basi hakika tumekwishayawakilisha kwa kaumu wasioyakufuru.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaongoa. Basi fuata uongofu wao. Sema: Mimi siwaombi ujira wowote juu yake. Haya si isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hawakumkadiria Mwenyezi Mungu kwa haki ya kadri yake, waliposema: Mwenyezi Mungu hakumteremshia mwanaadamu chochote. Sema: Nani aliyekiteremsha Kitabu alichokuja nacho Musa, chenye nuru na uwongofu kwa watu, mlichokifanya kurasa kurasa mkizionyesha, na mengi mkiyaficha? Na mkafunzwa mliyokuwa hamyajui nyinyi wala baba zenu? Sema: 'Mwenyezi Mungu.' Kisha waache wacheze katika porojo lao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hiki ni Kitabu tulichokiteremsha, kilichobarikiwa, chenye kusadikisha yale yaliyokitangulia, na ili uuonye Mama wa Miji na wale walio pembezoni mwake. Na wale wanaoiamini Akhera wanakiamini, nao wanazihifadhi Swala zao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu, au anayesema: 'Mimi nimeletewa wahyi'; na ilhali hakuletewa wahyi wowote. Na yule anayesema: Nitateremsha kama alivyoteremsha Mwenyezi Mungu. Na lau ungeliwaona madhalimu wanapokuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ya kudunisha kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyokuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNanyi mlitujia wapweke kama tulivyowaumba mara ya kwanza. Na mkayaacha nyuma yenu yote tuliyowapa, na wala hatuwaoni hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu. Yamekatika mahusiano baina yenu, na yamekupoteeni mliyokuwa mkiyadai.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mwenyezi Mungu ndiye mpasuaji nafaka na mbegu za tende, zikachipua. Humtoa aliye hai kutokana na maiti, na humtoa maiti kutokana na aliye hai. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu. Basi vipi mnadanganywa?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNdiye anayepambaza mwangaza wa asubuhi; na ameufanya usiku kuwa mapumziko, na jua na mwezi kwenda kwa hesabu. Hayo ndiyo makadirio ya Mwenye nguvu kubwa, Mwenye kujua yote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Yeye ndiye aliyewawekea nyota ili mwongoke kwazo katika giza mbalimbali za bara na bahari. Hakika tumezieleza kwa kina Ishara hizi kwa kaumu wanaojua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Yeye ndiye aliyewaanzilisha kutokana na nafsi moja. Pako pahali pa kutulia na pa kupita njia. Hakika tumezichambua Ishara hizi kwa watu wanaofahamu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Yeye ndiye aliyeteremsha maji kutoka mbinguni; na kwayo tukatoa mimea ya kila kitu. Na kutokana na baadhi yake tukatoa mimea ya kijani, tukatoa ndani yake punje zilizopandana; na kutokana na mitende katika makole yake yakatoka mashada yaliyo karibu; na mabustani ya mizabibu na mizaituni, na makomamanga, yanayofanana na yasiyofanana. Angalieni matunda yake yanapozaa na yakaiva. Hakika katika hayo kuna Ishara kwa kaumu wanaoamini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini walimfanyia Mwenyezi Mungu washirika, majini, ilhali Yeye ndiye aliyewaumba. Na wakamzulia kuwa ana wana wa kiume na wa kike, bila ya kuwa na elimu yoyote. Yeye Ametakasika, na ametukuka juu zaidi ya hayo wanayomuelezea kwayo!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye Muumbaji mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Vipi awe na mwana, ilhali hakuwa na mke? Naye ndiye aliyeumba kila kitu. Naye ni Mwenye kujua vyema kila kitu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi, hakuna mungu isipokuwa Yeye, Muumba wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa kila kitu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika zimekwishawajia hoja wazi wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo, mwenye kuona, basi ni kwa faida yake mwenyewe. Na mwenye kupofuka, basi ni hasara yake. Wala mimi si mtunzaji wenu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa namna hivyo tunazileta Aya mbalimbali, na wao wakwambie: 'Umesoma.' Na ili tuyabainishie watu wanaojua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterFuata yale yaliyofunuliwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi. Hakuna mungu isipokuwa Yeye. Na jitenge na washirikina.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau Mwenyezi Mungu angelipenda, wasingelimshirikisha. Na Sisi hatukukufanya wewe uwe mtunzaji wao. Wala wewe si mlinzi juu yao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msiwatukane hao ambao wao wanawaomba badala ya Mwenyezi Mungu, nao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao ni kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia yale waliyokuwa wakiyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waliapa kwa Mwenyezi Mungu viapo vyao vikali zaidi, kuwa ikiwajia Ishara, bila shaka wataiamini. Sema: Hakika Ishara hizo ziko kwa Mwenyezi Mungu. Na ni nini kitawajulisha kuwa zikija, hawataamini?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tutazigeuza nyoyo zao na macho yao kama vile hawakuiamini mara ya kwanza. Kisha tutawaacha katika upotovu wao wakitangatanga kwa upofu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa tungeliwateremshia Malaika, na maiti wakazungumza nao, na tukawakusanyia kila kitu mbele yao, bado hawakuwa ni wa kuamini, isipokuwa Mwenyezi Mungu atake. Lakini wengi wao hawajui.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kadhalika tumemfanyia kila Nabii maadui mashetani wa kiwatu, na kijini, wanafundishana wao kwa wao maneno ya kupambapamba, kwa udanganyifu. Na angelipenda Mola wako Mlezi, wasingelifanya hayo. Basi waache na hayo wanayoyazua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ili ziyaelekee hayo nyoyo za wale wasioiamini Akhera, nao wayaridhie, na wayachume yale wanayoyachuma.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, nimtafute hakimu asiyekuwa Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliyewateremshia Kitabu hiki kilichoelezwa kwa kina? Na wale tuliowapa Kitabu wanajua ya kwamba kimeteremshwa kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa Haki. Basi kamwe usiwe katika wale wanaotia shaka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa ukweli na uadilifu. Hakuna yeyote wa kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ukiwatii wengi wa hawa walio katika dunia, watakupoteza mbali na Njia ya Mwenyezi Mungu. Hawa hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawakuwa isipokuwa ni wenye kusema uongo tu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mna nini msile katika vile vilivyotajiwa jina la Mwenyezi Mungu, naye amekwishawabainishia kwa kina vile alivyowaharamishia, isipokuwa vile mnavyolazimishwa? Na hakika wengi wanapotea kwa matamanio yao bila ya kuwa na elimu. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye kujua vyema wale wanaopindukia mipaka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msile katika vile ambavyo halikutajwa jina la Mwenyezi Mungu juu yake. Kwani huko hakika ni kuvuka mipaka. Na kwa yakini mashetani wanawaletea wahyi marafiki zao ili wabishane nanyi. Na mkiwatii, basi nyinyi kwa hakika mtakuwa washirikina.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, yule aliyekuwa maiti, kisha tukamhuisha, na tukamfanyia nuru akatembea kwayo katika watu, ni kama yule ambaye mfano wake yuko katika giza mbalimbali, sio wa kutoka humo? Kama hivyo ndivyo makafiri walivyopambiwa yale waliyokuwa wakiyafanya.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa namna hivi tumeweka katika kila mji wakubwa wa wahalifu ili wafanye vitimbi ndani yake. Na wala hawafanyii vitimbi isipokuwa nafsi zao ilhali hawatambui.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa inapowajia Ishara, wao husema: 'Hatutaamini mpaka tupewe mfano wa yale waliyopewa Mitume wa Mwenyezi Mungu.' Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi ni wapi anaweka ujumbe wake. Itawafikia wale waliofanya uhalifu udhalili kwa Mwenyezi Mungu, na adhabu kali kwa sababu ya vitimbi walivyokuwa wakivifanya.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi yule ambaye Mwenyezi Mungu anataka kumuongoa, humfungulia kifua chake kwa Uislamu. Na yule anayetaka kumpoteza, hukifanya kifua chake kuwa na dhiki, kimebana, kama kwamba anapanda katika mbingu kwa ugumu mkubwa. Namna hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anaweka uchafu juu ya wale wasioamini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao watapata nyumba ya salama kwa Mola wao Mlezi. Naye ndiye Rafiki Mlinzi wao kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ile Siku atakapowakusanya wote, “Enyi kundi la majini! Hakika nyinyi mmechukua wafuasi wengi katika wanadamu.” Na marafiki zao katika wanadamu watasema: 'Mola wetu Mlezi! Tulinufaishana baadhi yetu kwa wenzi wetu, na tumefikia muda wetu uliotuwekea.' Basi Mwenyezi Mungu atasema: Moto ndiyo makazi yenu, mtadumu humo, isipokuwa apendavyo Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye hekima, Mwenye kujua zaidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa namna hivi ndivyo tunavyowafanya baadhi ya madhalimu wapendane wao kwa wao kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi kundi la majini na watu! Je, hawakuwajia Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakiwabainishia Aya zangu, na wakiwasimulia kukutana na Siku yenu hii? Nao watasema, “Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu.” Na yaliwadanganya maisha ya dunia. Nao watashuhudia dhidi yao wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa sababu ya kuwa Mola wako Mlezi hakuwa ni wa kuiangamiza miji kwa dhuluma, hali ya kuwa wenyewe wameghafilika.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kila mmoja ana daraja mbalimbali kutokana na yale waliyoyatenda. Na Mola wako Mlezi si mwenye kughafilika mbali na yale wanayoyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mola wako Mlezi ndiye asiyemhitaji yeyote, Mwenye rehema. Akitaka, atawaondoa na awaweke nyuma yenu wengine awatakao, kama vile alivyokutoeni kutokana na dhuria ya kaumu wengine.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walimwekea Mwenyezi Mungu fungu katika mimea na wanyama alioumba, wakasema: 'Hii ni sehemu ya Mwenyezi Mungu - kwa madai yao - na hii ni ya washirikishwa wetu.' Basi vile vilivyokuwa vya washirikishwa wao, havimfikii Mwenyezi Mungu, vile vilivyokuwa vya Mwenyezi Mungu, huwafikia washirikishwa wao. Ni uovu mno hayo wanayoyahukumu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kadhalika hao washirika wao wamewapambia wengi katika washirikina kuwaua watoto wao ili kuwaangamiza na kuwachanganyia dini yao. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelipenda, wasingelifanya hayo. Basi waache na hayo wanayozua ya uongo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNao walisema: "Mifugo hawa na mimea ni miiko. Hawavili isipokuwa tumtakaye" - kwa madai yao tu. Na mifugo wengine imeharamishwa migongo. Na mifugo wengine hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu juu yao, kwa kumzulia uongo tu. Atawalipa kwa hayo ya uongo waliyokuwa wakiyazua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walisema: Vile vilivyo katika matumbo ya mifugo hawa ni vya wanaume wetu tu, na vimeharamishwa kwa wake zetu. Lakini wakiwa nyamafu, basi wanashirikiana ndani yake. Atawalipa maelezo yao hayo. Hakika Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye kujua vyema.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika walipata hasara wale waliowaua watoto wao kwa upumbavu bila ya elimu, na wakaharamisha vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu kwa kumzulia Mwenyezi Mungu uongo. Hakika walipotea, wala hawakuwa wenye kuongoka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Yeye ndiye aliyeyaanzisha mabustani yenye kutambaa kwenye fito, na yasiyotambaa kwenye fito, na mitende, na mimea yenye vyakula mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayofanana na isiyofanana. Kuleni katika matunda yake inapozaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa kupitiliza. Hakika Yeye hawapendi watumiao kwa kupitiliza.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika mifugo kuna wale wabebao mizigo na wengine wadogo. Kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu, wala msifuate nyayo za Shetani. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.
Swahili Translation - Rowad Translation Center(Amewaumbia) majozi manane: katika kondoo ni wawili, na katika mbuzi ni wawili. Sema: Je, ameharamisha madume wawili hawa au majike wawili hawa, au wale walio matumboni mwa majike yote mawili haya? Niambieni kwa elimu ikiwa nyinyi ni wakweli.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika ngamia ni wawili, na katika ng'ombe ni wawili. Sema: Je, ameharamisha haya madume yote mawili au majike wawili haya, au walio matumboni mwa majike haya? Au, nyinyi mlishuhudia Mwenyezi Mungu alipowausia haya? Basi ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule aliyemzulia Mwenyezi Mungu uoongo, ili awapoteze watu bila ya elimu? Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Sipati katika yale niliyofunuliwa mimi kitu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa ikiwa ni nyamafu, au damu inayomwagika, au nyama ya nguruwe, kwani huo ni uchafu; au kilichovukiwa mipaka (wakati wa kuchinjwa) kwa kutajiwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini mwenye kushikwa na dharura, bila ya kutamani wala kupita mipaka, basi hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mayahudi tuliwaharamishia kila mwenye kwato au mguu usio na mgawanyiko. Na katika ng'ombe, na kondoo, na mbuzi tuliwaharamishia shahamu yao, isipokuwa ile iliyobeba migongo yao au matumbo yao, au iliyochanganyika na mifupa. Hayo tuliwalipa kwa sababu ya uasi wao. Nasi bila ya shaka ni wakweli.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakikukadhibisha, basi wewe sema: Mola wenu Mlezi ni Mwenye rehema kunjufu. Wala haizuiwi adhabu yake kwa kaumu wahalifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema wale walioshirikisha, "Lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka, tusingelishirikisha, wala baba zetu, wala tusingeliharamisha kitu chochote." Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale waliokuwa kabla yao mpaka walipoionja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo elimu yoyote mtutolee hiyo? Nyinyi hamfuati isipokuwa dhana. Wala hamfanyi isipokuwa kukisia tu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Waleteni mashahidi wenu ambao wanashuhudia kuwa Mwenyezi Mungu amewaharamisha hawa. Kwa hivyo, wakishuhudia, basi wewe usishuhudie pamoja nao. Wala usifuate matamanio ya wale waliozikadhibisha Ishara zetu, na ambao hawaamini katika Akhera, nao wanamlinganisha Mola wao Mlezi na wengine.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Njooni niwasomee yale aliyowaharamishia Mola wenu Mlezi: Kwamba msimshirikishe Yeye na chochote, na wazazi wawili wafanyieni uzuri, wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunawaruzuku nyinyi na wao. Wala msikaribie machafu, yaliyo dhahiri yake, na yaliyofichikana yake. Wala msiiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu aliiharamisha isipokuwa kwa haki. Hayo aliwausia ili myatie akilini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa kile kilicho kizuri kabisa mpaka afike utu uzima wake. Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu. Hatuibebeshi nafsi isipokuwa kwa uwezo wake. Na mnaposema, basi fanyeni uadilifu hata kama ni jamaa. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu, itimizeni. Hayo amewausia ili mkumbuke.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwamba hakika hii ndiyo Njia yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Wala msifuate njia nyinginezo, zikakutengeni mbali na Njia yake. Haya amewausia ili mche (Mwenyezi Mungu).
Swahili Translation - Rowad Translation CenterTena tulimpa Musa Kitabu kwa kumtimizia (neema) yule aliyefanya uzuri, na kuwa ni maelezo ya kina ya kila kitu, na uwongofu na rehema, ili waamini katika kukutana na Mola wao Mlezi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMkaja kusema, “Hakika waliteremshiwa Kitabu makundi mawili tu kabla yetu, na sisi tulikuwa hatuna habari ya waliyokuwa wakiyasoma.”
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu mkasema: "Lau hakika sisi tungeteremshiwa Kitabu hicho, basi tungelikuwa waongofu zaidi kuwaliko wao." Basi hakika imekwishawajia hoja iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uongofu, na rehema. Kwa hivyo, ni nani aliye dhalimu mkubwa zaidi kuliko yule anayekadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo? Tutawalipa wale wanaojitenga na Ishara zetu adhabu mbaya kabisa kwa sababu ya walivyokuwa wakijitenga.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, wanangoja isipokuwa kwamba wajiwe na Malaika, au awajie Mola wako Mlezi, au ziwajie baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapowajia baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini kwa nafsi hapo hakutaifaa kitu, ikiwa haikuwa imeamini kabla yake, au imefanya heri katika Imani yake. Sema, "Ngojeni, nasi hakika pia ni wenye kungoja."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale waliofarakisha Dini yao na wakawa makundi makundi, wewe si miongoni mwao katika chochote. Bila ya shaka jambo lao liko kwa Mwenyezi Mungu; kisha atawajulisha yale waliyokuwa wakiyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenye kuja na jema, basi ana mara kumi mfano wake. Na mwenye kuja na baya, basi hatalipwa isipokuwa mfano wake. Na wao hawatadhulumiwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: "Hakika mimi, Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye njia iliyonyooka, dini iliyo sawa kabisa, mila ya Ibrahim aliyekuwa mnyofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: "Hakika Swala yangu, na kuchinja kwangu , na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Je nimtafute mola mlezi asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ilhali Yeye ndiye Mola Mlezi wa kila kitu? Na wala haichumi kila nafsi isipokuwa ni juu yake. Na wala hatabeba mbeba mzigo, mzigo wa mwingine. Kisha kwa Mola wenu Mlezi ndiyo marejeo yenu, kisha atawajulisha yale mliyokuwa mkihitilafiana ndani yake.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye ndiye aliyewafanya kuwa wafuatizi (makhalifa) katika ardhi, na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja mbalimbali ili akujaribuni katika hayo aliyowapa. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwepesi wa kuadhibu, na hakika Yeye ni Mwenye kufuta dhambi zaidi, Mwenye kurehemu sana.