caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Anfaal الأنفال

Aya 75 · Madina · mpangilio wa kuteremshwa 88

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ يَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلْأَنفَالِ قُلِ ٱلْأَنفَالُ لِلَّهِ وَٱلرَّسُولِ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَصْلِحُوا۟ ذَاتَ بَيْنِكُمْ وَأَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanakuuliza juu ya ngawira. Sema: Ngawira ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na suluhisheni mambo baina yenu, na mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ikiwa nyinyi ni Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّمَا ٱلْمُؤْمِنُونَ ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ ءَايَٰتُهُۥ زَادَتْهُمْ إِيمَٰنًا وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Waumini ni wale ambao anapotajwa Mwenyezi Mungu, nyoyo zao zinaingia hofu. Na wanaposomewa Aya zake, zinawazidishia Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقْنَٰهُمْ يُنفِقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale wanaosimamisha Swala, na wanatoa katika vile tunavyowaruzuku.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُؤْمِنُونَ حَقًّا لَّهُمْ دَرَجَٰتٌ عِندَ رَبِّهِمْ وَمَغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ndio Waumini wa uhakika. Wana vyeo kwa Mola wao Mlezi, na kusitiriwa dhambi, na riziki tukufu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَمَآ أَخْرَجَكَ رَبُّكَ مِنۢ بَيْتِكَ بِٱلْحَقِّ وَإِنَّ فَرِيقًا مِّنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ لَكَٰرِهُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKama alivyokutoa Mola wako Mlezi katika nyumba yako kwa haki, na hakika kundi moja katika Waumini linachukia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يُجَٰدِلُونَكَ فِى ٱلْحَقِّ بَعْدَ مَا تَبَيَّنَ كَأَنَّمَا يُسَاقُونَ إِلَى ٱلْمَوْتِ وَهُمْ يَنظُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanakujadili kuhusu haki baada ya kwisha bainika, kama kwamba wanasukumwa kwenye mauti hali ya kuwa wanatazama.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذْ يَعِدُكُمُ ٱللَّهُ إِحْدَى ٱلطَّآئِفَتَيْنِ أَنَّهَا لَكُمْ وَتَوَدُّونَ أَنَّ غَيْرَ ذَاتِ ٱلشَّوْكَةِ تَكُونُ لَكُمْ وَيُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُحِقَّ ٱلْحَقَّ بِكَلِمَٰتِهِۦ وَيَقْطَعَ دَابِرَ ٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu alipowaahidi moja ya vikundi vile viwili kuwa ni chenu. Nanyi mkapenda kwamba kile kisichokuwa kikali ndicho kiwe chenu. Naye Mwenyezi Mungu anataka ahakikishe haki kwa maneno yake, na aikate mizizi ya makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِيُحِقَّ ٱلْحَقَّ وَيُبْطِلَ ٱلْبَٰطِلَ وَلَوْ كَرِهَ ٱلْمُجْرِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli aihakikishe haki na aibatilishe batili hata kama watachukia wahalifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ تَسْتَغِيثُونَ رَبَّكُمْ فَٱسْتَجَابَ لَكُمْ أَنِّى مُمِدُّكُم بِأَلْفٍ مِّنَ ٱلْمَلَٰٓئِكَةِ مُرْدِفِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMlipokuwa mnamuomba msaada Mola wenu Mlezi, naye akawaitikia kuwa Mimi hakika nitawasaidia kwa elfu moja miongoni mwa Malaika wakifuatana mfululizo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا جَعَلَهُ ٱللَّهُ إِلَّا بُشْرَىٰ وَلِتَطْمَئِنَّ بِهِۦ قُلُوبُكُمْ وَمَا ٱلنَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ ٱللَّهِ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu hakufanya hayo isipokuwa yawe ni bishara na ili nyoyo zenu zitue kwayo. Na nusura haiwi isipokuwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ يُغَشِّيكُمُ ٱلنُّعَاسَ أَمَنَةً مِّنْهُ وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً لِّيُطَهِّرَكُم بِهِۦ وَيُذْهِبَ عَنكُمْ رِجْزَ ٱلشَّيْطَٰنِ وَلِيَرْبِطَ عَلَىٰ قُلُوبِكُمْ وَيُثَبِّتَ بِهِ ٱلْأَقْدَامَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlipowafunika kwa usingizi uwe ni amani kutoka kwake, na akawateremshia maji kutoka mbinguni ili awasafishe kwayo na awaondolee uchafu wa Shetani, na ili azifunge nyoyo zenu, na aimarishe kwayo miguu yenu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ يُوحِى رَبُّكَ إِلَى ٱلْمَلَٰٓئِكَةِ أَنِّى مَعَكُمْ فَثَبِّتُوا۟ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ سَأُلْقِى فِى قُلُوبِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱلرُّعْبَ فَٱضْرِبُوا۟ فَوْقَ ٱلْأَعْنَاقِ وَٱضْرِبُوا۟ مِنْهُمْ كُلَّ بَنَانٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMola wako Mlezi alipowafunulia Malaika: Hakika Mimi niko pamoja nanyi, basi watieni nguvu wale walioamini. Nitatupa woga katika nyoyo za wale waliokufuru. Basi wapigeni juu ya shingo na wapigeni kwenye kila ncha za vidole.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ شَآقُّوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَمَن يُشَاقِقِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَإِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa sababu walimuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكُمْ فَذُوقُوهُ وَأَنَّ لِلْكَٰفِرِينَ عَذَابَ ٱلنَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNdivyo hivyo! Basi ionjeni! Na bila ya shaka makafiri wana adhabu ya Moto.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا لَقِيتُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ زَحْفًا فَلَا تُوَلُّوهُمُ ٱلْأَدْبَارَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi Mlioamini! Mnapokutana na wale waliokufuru vitani, msiwageuzie migongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَن يُوَلِّهِمْ يَوْمَئِذٍ دُبُرَهُۥٓ إِلَّا مُتَحَرِّفًا لِّقِتَالٍ أَوْ مُتَحَيِّزًا إِلَىٰ فِئَةٍ فَقَدْ بَآءَ بِغَضَبٍ مِّنَ ٱللَّهِ وَمَأْوَىٰهُ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo, isipokuwa kwa mbinu za vita au kuungana na kikosi, basi hakika atakuwa amestahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na pahali pake ni Jahannam, na hayo ndiyo marejeo mabaya kabisa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمْ تَقْتُلُوهُمْ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ قَتَلَهُمْ وَمَا رَمَيْتَ إِذْ رَمَيْتَ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ رَمَىٰ وَلِيُبْلِىَ ٱلْمُؤْمِنِينَ مِنْهُ بَلَآءً حَسَنًا إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hivyo, hamkuwaua nyinyi, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaua. Nawe hukutupa ulipotupa, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyetupa, na ili awajaribu Waumini majaribio mazuri kutoka kwake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكُمْ وَأَنَّ ٱللَّهَ مُوهِنُ كَيْدِ ٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo! Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kudhoofisha njama za makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِن تَسْتَفْتِحُوا۟ فَقَدْ جَآءَكُمُ ٱلْفَتْحُ وَإِن تَنتَهُوا۟ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ وَإِن تَعُودُوا۟ نَعُدْ وَلَن تُغْنِىَ عَنكُمْ فِئَتُكُمْ شَيْـًٔا وَلَوْ كَثُرَتْ وَأَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMkiomba msaada wa ushindi, basi msaada wa ushindi ulikwishawajia. Na mkikomeka, basi hilo ndilo heri kwenu. Na mkirejea, Sisi pia tutarejea. Na kundi lenu halitawanufaisha kitu hata kama yatakuwa (makundi) mengi. Kwani hakika Mwenyezi yu pamoja na Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَا تَوَلَّوْا۟ عَنْهُ وَأَنتُمْ تَسْمَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msigeuke mkamuacha hali ya kuwa mnasikia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تَكُونُوا۟ كَٱلَّذِينَ قَالُوا۟ سَمِعْنَا وَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msiwe kama wale wanaosema, "Tumesikia" na hali hawasikii.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ شَرَّ ٱلدَّوَآبِّ عِندَ ٱللَّهِ ٱلصُّمُّ ٱلْبُكْمُ ٱلَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika waovu mno wa wanyama wote mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale viziwi, na mabubu wasiotumia akili zao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْ عَلِمَ ٱللَّهُ فِيهِمْ خَيْرًا لَّأَسْمَعَهُمْ وَلَوْ أَسْمَعَهُمْ لَتَوَلَّوا۟ وَّهُم مُّعْرِضُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu angelijua heri yoyote ndani yao, angewasikilizisha, na lau angewasikilizisha, wangeligeuka hali ya kuwa wamepuuza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱسْتَجِيبُوا۟ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ ٱلْمَرْءِ وَقَلْبِهِۦ وَأَنَّهُۥٓ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapowaitia yale yenye kuwahuisha. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huzuia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye mtakusanywa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱتَّقُوا۟ فِتْنَةً لَّا تُصِيبَنَّ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ مِنكُمْ خَآصَّةً وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa jikingeni kutokana na mtihani ambao hautawasibu wale waliodhulumu pekee miongoni mwenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱذْكُرُوٓا۟ إِذْ أَنتُمْ قَلِيلٌ مُّسْتَضْعَفُونَ فِى ٱلْأَرْضِ تَخَافُونَ أَن يَتَخَطَّفَكُمُ ٱلنَّاسُ فَـَٔاوَىٰكُمْ وَأَيَّدَكُم بِنَصْرِهِۦ وَرَزَقَكُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kumbukeni mlipokuwa wachache, mkidhoofishwa katika ardhi, mkiogopa kwamba watu watawanyakua, naye akawapa pahali pazuri pa kukaa, na akawaunga mkono kwa nusura yake, na akawaruzuku katika vilivyo vizuri ili mshukuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَخُونُوا۟ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ وَتَخُونُوٓا۟ أَمَٰنَٰتِكُمْ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Msimhini Mwenyezi Mungu na Mtume, na mkahini amana zenu, hali ya kuwa mnajua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّمَآ أَمْوَٰلُكُمْ وَأَوْلَٰدُكُمْ فِتْنَةٌ وَأَنَّ ٱللَّهَ عِندَهُۥٓ أَجْرٌ عَظِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa jueni ya kwamba mali zenu na wana wenu ni mtihani, na kwamba Mwenyezi Mungu ana ujira mkubwa kwake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تَتَّقُوا۟ ٱللَّهَ يَجْعَل لَّكُمْ فُرْقَانًا وَيُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّـَٔاتِكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ وَٱللَّهُ ذُو ٱلْفَضْلِ ٱلْعَظِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Mkimcha Mwenyezi Mungu, atawapa kipambanuo, na atawasitiria mabaya yenu, na awafutie dhambi, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذْ يَمْكُرُ بِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِيُثْبِتُوكَ أَوْ يَقْتُلُوكَ أَوْ يُخْرِجُوكَ وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ ٱللَّهُ وَٱللَّهُ خَيْرُ ٱلْمَٰكِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walipokupangia vitimbi wale waliokufuru ili wakufunge, au wakuue, au wakutoe. Na wakapanga vitimbi vyao, naye Mwenyezi Mungu akapanga vitimbi vyake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wapangao vitimbi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ءَايَٰتُنَا قَالُوا۟ قَدْ سَمِعْنَا لَوْ نَشَآءُ لَقُلْنَا مِثْلَ هَٰذَآ إِنْ هَٰذَآ إِلَّآ أَسَٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanaposomewa Aya zetu, wao husema: Hakika tumesikia. Lau tungetaka, tungesema mfano wa haya. Haya si chochote isipokuwa ngano za wa mwanzo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذْ قَالُوا۟ ٱللَّهُمَّ إِن كَانَ هَٰذَا هُوَ ٱلْحَقَّ مِنْ عِندِكَ فَأَمْطِرْ عَلَيْنَا حِجَارَةً مِّنَ ٱلسَّمَآءِ أَوِ ٱئْتِنَا بِعَذَابٍ أَلِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waliposema: Ewe Mwenyezi Mungu! Ikiwa haya ndiyo haki kutoka kwako, basi tunyeshee mawe kutoka mbinguni, au tujie na adhabu yoyote iliyo chungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنتَ فِيهِمْ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaadhibu hali ya kuwa uko miongoni mwao, na Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwaadhibu hali ya kuwa wanaomba msamaha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا لَهُمْ أَلَّا يُعَذِّبَهُمُ ٱللَّهُ وَهُمْ يَصُدُّونَ عَنِ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ وَمَا كَانُوٓا۟ أَوْلِيَآءَهُۥٓ إِنْ أَوْلِيَآؤُهُۥٓ إِلَّا ٱلْمُتَّقُونَ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini wana nini hata Mwenyezi Mungu asiwaadhibu, na hali ya kuwa wanawazuilia watu Msikiti Mtakatifu, wala wao hawakuwa ndio walinzi wake? Bali walinzi wake si isipokuwa wacha Mungu tu, lakini wengi wao hawajui.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا كَانَ صَلَاتُهُمْ عِندَ ٱلْبَيْتِ إِلَّا مُكَآءً وَتَصْدِيَةً فَذُوقُوا۟ ٱلْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakukuwa kuswalia kwao kwenye hiyo Nyumba (Al-Kaaba) isipokuwa ni kupiga miunzi na makofi. Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyokuwa mkikufuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يُنفِقُونَ أَمْوَٰلَهُمْ لِيَصُدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِلَىٰ جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale waliokufuru hutoa mali zao ili waizuilie Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watazitoa, kisha zitakuwa majuto juu yao, kisha watashindwa. Na wale waliokufuru watakusanywa kwenye Jahannam.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِيَمِيزَ ٱللَّهُ ٱلْخَبِيثَ مِنَ ٱلطَّيِّبِ وَيَجْعَلَ ٱلْخَبِيثَ بَعْضَهُۥ عَلَىٰ بَعْضٍ فَيَرْكُمَهُۥ جَمِيعًا فَيَجْعَلَهُۥ فِى جَهَنَّمَ أُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَٰسِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli Mwenyezi Mungu awapambanue waovu kutokana na wazuri, na awaweke waovu juu ya waovu wengine, na awarundike wote pamoja, na awatie katika Jahannam. Hao ndio waliohasirika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِن يَنتَهُوا۟ يُغْفَرْ لَهُم مَّا قَدْ سَلَفَ وَإِن يَعُودُوا۟ فَقَدْ مَضَتْ سُنَّتُ ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaambie wale waliokufuru ikiwa watakoma, watasitiriwa yale yaliyokwisha pita. Na wakiyarudia, basi hakika imekwisha pita mifano ya wa mwanzo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَٰتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ ٱلدِّينُ كُلُّهُۥ لِلَّهِ فَإِنِ ٱنتَهَوْا۟ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِمَا يَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa piganeni nao mpaka kusiwepo majaribio na Dini yote iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Lakini wakiacha, basi hakika Mwenyezi Mungu anayaona vyema wanayayatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن تَوَلَّوْا۟ فَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ مَوْلَىٰكُمْ نِعْمَ ٱلْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ ٱلنَّصِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kama wakigeuka basi jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mola wenu, ni Mola Mwema na Msaidizi Mwema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّمَا غَنِمْتُم مِّن شَىْءٍ فَأَنَّ لِلَّهِ خُمُسَهُۥ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْيَتَٰمَىٰ وَٱلْمَسَٰكِينِ وَٱبْنِ ٱلسَّبِيلِ إِن كُنتُمْ ءَامَنتُم بِٱللَّهِ وَمَآ أَنزَلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا يَوْمَ ٱلْفُرْقَانِ يَوْمَ ٱلْتَقَى ٱلْجَمْعَانِ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa jueni ya kwamba ngawira yoyote mnayoipata, basi humusi yake ni ya Mwenyezi Mungu na ni ya Mtume, na ni ya jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mlimwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoyateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo, siku yalipokutana makundi yale mawili. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ أَنتُم بِٱلْعُدْوَةِ ٱلدُّنْيَا وَهُم بِٱلْعُدْوَةِ ٱلْقُصْوَىٰ وَٱلرَّكْبُ أَسْفَلَ مِنكُمْ وَلَوْ تَوَاعَدتُّمْ لَٱخْتَلَفْتُمْ فِى ٱلْمِيعَٰدِ وَلَٰكِن لِّيَقْضِىَ ٱللَّهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا لِّيَهْلِكَ مَنْ هَلَكَ عَنۢ بَيِّنَةٍ وَيَحْيَىٰ مَنْ حَىَّ عَنۢ بَيِّنَةٍ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَسَمِيعٌ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKumbukeni pale mlipokuwa nyinyi kwenye ng'ambo ya karibu ya bonde, na wao wakawa kwenye ng'ambo ya mbali, na msafara ulipokuwa chini yenu. Na ingelikuwa mliagana, basi mngelihitilafiana katika miadi. Lakini (mkakutana) ili Mwenyezi Mungu atimize jambo liliokuwa lazima litendwe. Ili aangamie wa kuangamia kwa ushahidi ulio wazi, na asalimike wa kusalimika kwa ushahidi ulio wazi. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ يُرِيكَهُمُ ٱللَّهُ فِى مَنَامِكَ قَلِيلًا وَلَوْ أَرَىٰكَهُمْ كَثِيرًا لَّفَشِلْتُمْ وَلَتَنَٰزَعْتُمْ فِى ٱلْأَمْرِ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ سَلَّمَ إِنَّهُۥ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKumbuka Mwenyezi Mungu alipokuonyesha wao katika usingizi wako kwamba wao ni wachache, na lau angelikuonyesha kuwa ni wengi, basi mngeliingiwa na woga, na mngelizozana katika jambo hilo. Lakini Mwenyezi Mungu akawapa salama. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyo vifuani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذْ يُرِيكُمُوهُمْ إِذِ ٱلْتَقَيْتُمْ فِىٓ أَعْيُنِكُمْ قَلِيلًا وَيُقَلِّلُكُمْ فِىٓ أَعْيُنِهِمْ لِيَقْضِىَ ٱللَّهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا وَإِلَى ٱللَّهِ تُرْجَعُ ٱلْأُمُورُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa alipowaonyesha mlipokutana, katika macho yenu kuwa wao ni wachache, na akawafanya nyinyi ni wachache katika macho yao, ili Mwenyezi Mungu atimize jambo lililokuwa lifanywe. Na kwa Mwenyezi Mungu yatarejeshwa mambo yote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا لَقِيتُمْ فِئَةً فَٱثْبُتُوا۟ وَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Mkikutana na kikundi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mfaulu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَطِيعُوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَلَا تَنَٰزَعُوا۟ فَتَفْشَلُوا۟ وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ وَٱصْبِرُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّٰبِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تَكُونُوا۟ كَٱلَّذِينَ خَرَجُوا۟ مِن دِيَٰرِهِم بَطَرًا وَرِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱللَّهُ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msiwe kama wale waliotoka katika majumba yao kwa fahari na kujionyesha kwa watu, na wakiwazuilia watu Njia ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ameyazingira yote wanayoyafanya.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذْ زَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيْطَٰنُ أَعْمَٰلَهُمْ وَقَالَ لَا غَالِبَ لَكُمُ ٱلْيَوْمَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَإِنِّى جَارٌ لَّكُمْ فَلَمَّا تَرَآءَتِ ٱلْفِئَتَانِ نَكَصَ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ وَقَالَ إِنِّى بَرِىٓءٌ مِّنكُمْ إِنِّىٓ أَرَىٰ مَا لَا تَرَوْنَ إِنِّىٓ أَخَافُ ٱللَّهَ وَٱللَّهُ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakati Shetani alipowapambia vitendo vyao, na akasema, "Hakuna yeyote wa kuwashinda leo hii katika watu, nami hakika ni rafiki mlinzi wenu." Basi yalipoonana makundi mawili hayo, akarudi nyuma juu ya visigino vyake, na akasema, "Hakika mimi niko mbali sana nanyi. Hakika mimi naona msiyoyaona. Hakika mimi ninamhofu Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ يَقُولُ ٱلْمُنَٰفِقُونَ وَٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ غَرَّ هَٰٓؤُلَآءِ دِينُهُمْ وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ فَإِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaliposema wanafiki, na wale wenye ugonjwa katika nyoyo zao, "Watu hawa dini yao imewadanganya." Na mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْ تَرَىٰٓ إِذْ يَتَوَفَّى ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ يَضْرِبُونَ وُجُوهَهُمْ وَأَدْبَٰرَهُمْ وَذُوقُوا۟ عَذَابَ ٱلْحَرِيقِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa laiti ungeliona Malaika wanapowafisha wale waliokufuru wakiwapiga nyuso zao na migongo yao, (na kuwaambia), "Ionjeni adhabu iunguzayo!"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيكُمْ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَيْسَ بِظَلَّٰمٍ لِّلْعَبِيدِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa sababu ya yale yaliyotangulizwa na mikono yenu, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَدَأْبِ ءَالِ فِرْعَوْنَ وَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ بِذُنُوبِهِمْ إِنَّ ٱللَّهَ قَوِىٌّ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKama ada ya watu wa Firauni na wale waliokuwa kabla yao, walizikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu. Basi Mwenyezi Mungu akawachukua kwa madhambi yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mkali wa kuadhibu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ لَمْ يَكُ مُغَيِّرًا نِّعْمَةً أَنْعَمَهَا عَلَىٰ قَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا۟ مَا بِأَنفُسِهِمْ وَأَنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHiyo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu hakuwa ni wa kuibadilisha neema aliyowaneemesha kwayo kaumu, mpaka wao wabadilishe yale yaliyo katika nafsi zao, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَدَأْبِ ءَالِ فِرْعَوْنَ وَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمْ فَأَهْلَكْنَٰهُم بِذُنُوبِهِمْ وَأَغْرَقْنَآ ءَالَ فِرْعَوْنَ وَكُلٌّ كَانُوا۟ ظَٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi kama ada ya watu wa Firauni na wale waliokuwa kabla yao, walizikadhibisha Ishara za Mola wao Mlezi, basi tukawaangamiza kwa madhambi yao, na tukawazamisha watu wa Firauni. Na kila mmoja wao walikuwa madhalimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ شَرَّ ٱلدَّوَآبِّ عِندَ ٱللَّهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika waovu zaidi ya wanyama wote mbele ya Mwenyezi Mungu ni wale waliokufuru, basi hao hawaamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ عَٰهَدتَّ مِنْهُمْ ثُمَّ يَنقُضُونَ عَهْدَهُمْ فِى كُلِّ مَرَّةٍ وَهُمْ لَا يَتَّقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale ambao miongoni mwao ulifanya agano nao, kisha wanavunja agano lao katika kila mara, wala wao hawamchi Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِمَّا تَثْقَفَنَّهُمْ فِى ٱلْحَرْبِ فَشَرِّدْ بِهِم مَّنْ خَلْفَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hivyo, ukiwakuta katika vita, basi wakimbize kwa hawa wale walio nyuma yao ili wapate kukumbuka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِمَّا تَخَافَنَّ مِن قَوْمٍ خِيَانَةً فَٱنۢبِذْ إِلَيْهِمْ عَلَىٰ سَوَآءٍ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلْخَآئِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ukichelea hiana kwa kaumu fulani, basi watupilie ahadi yao kwa usawa. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wahaini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا يَحْسَبَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ سَبَقُوٓا۟ إِنَّهُمْ لَا يُعْجِزُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala kamwe wasidhanie wale waliokufuru kwamba wao wametangulia mbele. Hakika, wao hawatashinda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَعِدُّوا۟ لَهُم مَّا ٱسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ ٱلْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِۦ عَدُوَّ ٱللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ وَءَاخَرِينَ مِن دُونِهِمْ لَا تَعْلَمُونَهُمُ ٱللَّهُ يَعْلَمُهُمْ وَمَا تُنفِقُوا۟ مِن شَىْءٍ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waandalieni muwezavyo katika nguvu, na kwa farasi waliofungwa tayari tayari, ili muwatie hofu kwavyo maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo kando na hao ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na chochote mnachotoa kwenda katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mtarudishiwa kikamilifu, nanyi hamtadhulumiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن جَنَحُوا۟ لِلسَّلْمِ فَٱجْنَحْ لَهَا وَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakiielekea amani, basi nawe pia ielekee, na mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن يُرِيدُوٓا۟ أَن يَخْدَعُوكَ فَإِنَّ حَسْبَكَ ٱللَّهُ هُوَ ٱلَّذِىٓ أَيَّدَكَ بِنَصْرِهِۦ وَبِٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakitaka kukufanyia hiana, basi hakika Mwenyezi Mungu atakutosheleza. Yeye ndiye aliyekuunga mkono kwa nusura yake, na kwa Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ لَوْ أَنفَقْتَ مَا فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا مَّآ أَلَّفْتَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ أَلَّفَ بَيْنَهُمْ إِنَّهُۥ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akaziunga pamoja nyoyo zao. Lau wewe ungelitoa vyote vilivyo katika ardhi, usingeliweza kuziunga pamoja nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyewaunganisha. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ حَسْبُكَ ٱللَّهُ وَمَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEwe Nabii! Mwenyezi Mungu anakutosha wewe na mwenye kukufuata miongoni mwa Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ حَرِّضِ ٱلْمُؤْمِنِينَ عَلَى ٱلْقِتَالِ إِن يَكُن مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَٰبِرُونَ يَغْلِبُوا۟ مِا۟ئَتَيْنِ وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّا۟ئَةٌ يَغْلِبُوٓا۟ أَلْفًا مِّنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEwe Nabii! Wahimize Waumini juu ya kupigana vita. Wakiwapo miongoni mwenu ishirini wanaosubiri, watawashinda mia mbili. Na wakiwapo miongoni mwenu mia, watawashinda elfu moja katika wale waliokufuru, kwa sababu wao ni kaumu wasiofahamu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلْـَٰٔنَ خَفَّفَ ٱللَّهُ عَنكُمْ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمْ ضَعْفًا فَإِن يَكُن مِّنكُم مِّا۟ئَةٌ صَابِرَةٌ يَغْلِبُوا۟ مِا۟ئَتَيْنِ وَإِن يَكُن مِّنكُمْ أَلْفٌ يَغْلِبُوٓا۟ أَلْفَيْنِ بِإِذْنِ ٱللَّهِ وَٱللَّهُ مَعَ ٱلصَّٰبِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSasa Mwenyezi Mungu amewapunguzia, na alijua kuwa ndani yenu upo udhaifu. Kwa hivyo, wakiwapo watu mia moja miongoni mwenu wenye kusubiri, watawashinda mia mbili. Na wakiwapo elfu moja, watawashinda elfu mbili, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kusubiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا كَانَ لِنَبِىٍّ أَن يَكُونَ لَهُۥٓ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِى ٱلْأَرْضِ تُرِيدُونَ عَرَضَ ٱلدُّنْيَا وَٱللَّهُ يُرِيدُ ٱلْـَٔاخِرَةَ وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHaikuwa kwa Nabii yeyote kwamba awe na mateka, mpaka awe ameshinda sawasawa katika ardhi. Mnataka vitu vya dunia, na Mwenyezi Mungu anataka Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَّوْلَا كِتَٰبٌ مِّنَ ٱللَّهِ سَبَقَ لَمَسَّكُمْ فِيمَآ أَخَذْتُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLau lisingelikuwa andiko lililokwisha tangulia kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ingewagusa adhabu kubwa kwa vile mlivyochukua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكُلُوا۟ مِمَّا غَنِمْتُمْ حَلَٰلًا طَيِّبًا وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi kuleni katika mlivyoteka, ni halali na vizuri, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri na kusamehe dhambi, Mwenye kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ قُل لِّمَن فِىٓ أَيْدِيكُم مِّنَ ٱلْأَسْرَىٰٓ إِن يَعْلَمِ ٱللَّهُ فِى قُلُوبِكُمْ خَيْرًا يُؤْتِكُمْ خَيْرًا مِّمَّآ أُخِذَ مِنكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEwe Nabii! Waambie wale walio katika mikono yenu miongoni mwa mateka: Kama Mwenyezi Mungu akijua heri yoyote katika nyoyo zenu, atawapa bora kuliko vilivyochukuliwa kutoka kwenu, na atawasitiria dhambi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusitiri na kusamehe dhambi, Mwenye kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن يُرِيدُوا۟ خِيَانَتَكَ فَقَدْ خَانُوا۟ ٱللَّهَ مِن قَبْلُ فَأَمْكَنَ مِنْهُمْ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ikiwa wanataka kukufanyia hiana, basi hakika walikwishamfanyia hiana Mwenyezi Mungu kabla, naye akawawezesha nyinyi kuwashinda. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَهَاجَرُوا۟ وَجَٰهَدُوا۟ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلَّذِينَ ءَاوَوا۟ وَّنَصَرُوٓا۟ أُو۟لَٰٓئِكَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَآءُ بَعْضٍ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَلَمْ يُهَاجِرُوا۟ مَا لَكُم مِّن وَلَٰيَتِهِم مِّن شَىْءٍ حَتَّىٰ يُهَاجِرُوا۟ وَإِنِ ٱسْتَنصَرُوكُمْ فِى ٱلدِّينِ فَعَلَيْكُمُ ٱلنَّصْرُ إِلَّا عَلَىٰ قَوْمٍۭ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُم مِّيثَٰقٌ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale walioamini na wakahama na wakaipigania Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao, na wale waliotoa pahali pa kukaa, na wakanusuru, hao ni marafiki na walinzi wao kwa wao. Na wale walioamini lakini hawakuhama, nyinyi hamna wajibu wa ulinzi kwao hata kidogo mpaka wahame. Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia, isipokuwa juu ya kaumu ambao lipo agano baina yenu na wao. Na Mwenyezi Mungu anayaona vyema yale mnayoyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَآءُ بَعْضٍ إِلَّا تَفْعَلُوهُ تَكُن فِتْنَةٌ فِى ٱلْأَرْضِ وَفَسَادٌ كَبِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliokufuru ni marafiki walinzi wenyewe kwa wenyewe. Msipofanya hivi, itakuwepo fitina katika ardhi na uharibifu mkubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَهَاجَرُوا۟ وَجَٰهَدُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلَّذِينَ ءَاوَوا۟ وَّنَصَرُوٓا۟ أُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُؤْمِنُونَ حَقًّا لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale walioamini, na wakahama, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wale waliotoa pahali pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha (wa Mwenyezi Mungu) na riziki njema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنۢ بَعْدُ وَهَاجَرُوا۟ وَجَٰهَدُوا۟ مَعَكُمْ فَأُو۟لَٰٓئِكَ مِنكُمْ وَأُو۟لُوا۟ ٱلْأَرْحَامِ بَعْضُهُمْ أَوْلَىٰ بِبَعْضٍ فِى كِتَٰبِ ٱللَّهِ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌۢ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale walioamini baadaye, na wakahama, na wakapigana Jihadi pamoja nanyi, basi hao ni miongoni mwenu. Na jamaa wa nasaba wanastahikiana zaidi wenyewe kwa wenyewe katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70