caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-A'raaf, Aya 187

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 39 · 7:187

يَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرْسَىٰهَا قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ رَبِّى لَا يُجَلِّيهَا لِوَقْتِهَآ إِلَّا هُوَ ثَقُلَتْ فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ لَا تَأْتِيكُمْ إِلَّا بَغْتَةً يَسْـَٔلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِىٌّ عَنْهَا قُلْ إِنَّمَا عِلْمُهَا عِندَ ٱللَّهِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanakuuliza kuhusu hiyo Saa (ya Kiyama) kusimama kwake ni lini? Sema: Elimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake isipokuwa Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haitawajia isipokuwa kwa ghafla tu. Wanakuuliza kama kwamba wewe una pupa ya kuijua. Sema: Elimu yake iko tu kwa Mwenyezi Mungu. Lakini wengi wa watu hawajui.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWanakuuliza hiyo Saa (ya mwisho) itakuwa lini? Sema: Kuijua kwake kuko kwa Mola Mlezi wangu. Haidhihirishi hiyo kwa wakati wake ila Yeye. Ni nzito katika mbingu na ardhi. Haikujiini ila kwa ghafla tu. Wanakuuliza kama kwamba wewe una pupa ya kuijua. Sema: Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu. Lakini aghlabu ya watu hawajui.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70