يَٰبَنِىٓ ءَادَمَ لَا يَفْتِنَنَّكُمُ ٱلشَّيْطَٰنُ كَمَآ أَخْرَجَ أَبَوَيْكُم مِّنَ ٱلْجَنَّةِ يَنزِعُ عَنْهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوْءَٰتِهِمَآ إِنَّهُۥ يَرَىٰكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُۥ مِنْ حَيْثُ لَا تَرَوْنَهُمْ إِنَّا جَعَلْنَا ٱلشَّيَٰطِينَ أَوْلِيَآءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi wanadamu! Kamwe Shetani asiwafitini kama alivyowatoa wazazi wenu katika Bustani ile, akawavua vazi lao ili awaonyeshe tupu zao. Hakika yeye anawaona yeye na kabila yake kwa namna ambayo nyinyi hamuwaoni. Hakika Sisi tumewafanya Mashetani kuwa ni marafiki wasaidizi wa wale wasioamini.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniEny wanaadamu! Asije Shet'ani kukufitinini kama alivyo watoa wazazi wenu Peponi, akawavua nguo zao kuwaonyesha tupu zao. Hakika yeye na kabila yake wanakuoneni, na nyinyi hamuwaoni. Hakika Sisi tumewafanya Mashet'ani kuwa ni marafiki wa wasio amini.