قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ ٱللَّهِ ٱلَّتِىٓ أَخْرَجَ لِعِبَادِهِۦ وَٱلطَّيِّبَٰتِ مِنَ ٱلرِّزْقِ قُلْ هِىَ لِلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا خَالِصَةً يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَٰتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ni nani aliyeharamisha pambo la Mwenyezi Mungu alilowatolea waja wake, na vile vilivyo vizuri katika riziki? Sema: Hivyo ni kwa wale walioamini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivyo ndivyo tunavyowaelezea Ishara kaumu wanaojua.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniSema: Ni nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake, na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai wa duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivi tunazieleza Ishara kwa watu wanao jua.