caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-A'raaf, Aya 38

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 39 · 7:38

قَالَ ٱدْخُلُوا۟ فِىٓ أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُم مِّنَ ٱلْجِنِّ وَٱلْإِنسِ فِى ٱلنَّارِ كُلَّمَا دَخَلَتْ أُمَّةٌ لَّعَنَتْ أُخْتَهَا حَتَّىٰٓ إِذَا ٱدَّارَكُوا۟ فِيهَا جَمِيعًا قَالَتْ أُخْرَىٰهُمْ لِأُولَىٰهُمْ رَبَّنَا هَٰٓؤُلَآءِ أَضَلُّونَا فَـَٔاتِهِمْ عَذَابًا ضِعْفًا مِّنَ ٱلنَّارِ قَالَ لِكُلٍّ ضِعْفٌ وَلَٰكِن لَّا تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu atasema: Ingieni (Motoni) pamoja na umma zilizopita kabla yenu miongoni mwa majini na watu. Kila utakapoingia umma, utalaani dada yake. Mpaka watakapokusanyika wote humo, wa mwisho wao atasema juu ya wa mwanzo wao: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio waliotupoteza. Basi wape adhabu ya Motoni maradufu. Atasema: Kila mmoja ana maradufu, lakini nyinyi hamjui tu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu atasema: Ingieni Motoni pamoja na umma zilizo pita kabla yenu za majini na watu. Kila utakapo ingia umma utawalaani wenzake. Mpaka watakapo kusanyika wote humo, wa mwisho wao watawasema wa mwanzo wao: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio walio tupoteza; basi wape adhabu ya Motoni marudufu. Atasema: Itakuwa kwenu nyote marudufu, lakini nyinyi hamjui tu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70