أَوَعَجِبْتُمْ أَن جَآءَكُمْ ذِكْرٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنكُمْ لِيُنذِرَكُمْ وَٱذْكُرُوٓا۟ إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَآءَ مِنۢ بَعْدِ قَوْمِ نُوحٍ وَزَادَكُمْ فِى ٱلْخَلْقِ بَصْۜطَةً فَٱذْكُرُوٓا۟ ءَالَآءَ ٱللَّهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMnaona ajabu kukufikieni mawaidha yanayotoka kwa Mola wenu Mlezi kwa mtu aliye mmoja wenu nyinyi ili awaonye? Na kumbukeni alivyokufanyeni mshike mahali pa kaumu ya Nuhu, na akawazidishia katika umbo. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniMnaona ajabu kukufikieni mawaidha yanayo toka kwa Mola wenu Mlezi kwa mtu aliye mmoja wenu nyinyi ili akuonyeni? Na kumbukeni alivyo kufanyeni mshike pahala pa kaumu ya Nuhu, na akakuzidisheni katika umbo. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa.