caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-A'raaf, Aya 189

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 39 · 7:189

هُوَ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَٰحِدَةٍ وَجَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا لِيَسْكُنَ إِلَيْهَا فَلَمَّا تَغَشَّىٰهَا حَمَلَتْ حَمْلًا خَفِيفًا فَمَرَّتْ بِهِۦ فَلَمَّآ أَثْقَلَت دَّعَوَا ٱللَّهَ رَبَّهُمَا لَئِنْ ءَاتَيْتَنَا صَٰلِحًا لَّنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّٰكِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye aliyewaumba kutoka katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili ajitulize kwake. Na alipomuingilia, akabeba mimba nyepesi, akitembea nao. Anapokuwa mjamzito, wote wawili humwomba Mwenyezi Mungu, Mola wao Mlezi: Kama ukitupa mwana mwema hakika tutakuwa katika wanaoshukuru.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniYeye ndiye aliye kuumbeni katika nafsi moja; na katika hiyo hiyo akamfanya mwenzi wake, ili akae naye kwa utulivu. Na anapo muingilia hubeba mzigo mwepesi, akitembea nao. Anapo kuwa mja mzito, wote wawili humwomba Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wao: Kama ukitupa mwana mwema tutakuwa katika wanao shukuru.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70