قَالُوٓا۟ أُوذِينَا مِن قَبْلِ أَن تَأْتِيَنَا وَمِنۢ بَعْدِ مَا جِئْتَنَا قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَن يُهْلِكَ عَدُوَّكُمْ وَيَسْتَخْلِفَكُمْ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Tumeudhiwa kabla wewe kutujia, na baada ya wewe kutujia! Musa akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamuangamiza adui wenu, na akawafanya nyinyi ndio wa kufuatia kushika ardhi, ili atazame mtakavyokujatenda nyinyi.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWakasema: Tumeudhiwa kabla hujatufikia, na baada ya wewe kutujia! Musa akasema: Huenda Mola wenu Mlezi akamhiliki adui wenu, na akakufanyeni nyinyi ndio wa kufuatia kushika nchi, ili atazame mtavyo kuja tenda nyinyi.