caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Hijr الحجر

Aya 99 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 54

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ الٓر تِلْكَ ءَايَٰتُ ٱلْكِتَٰبِ وَقُرْءَانٍ مُّبِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlif Lam Ra.[1] Hizi ni Aya za Kitabu na Qur-ani inayobainisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

رُّبَمَا يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَوْ كَانُوا۟ مُسْلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuenda ikawa wale waliokufuru wakatamani kwamba wangekuwa Waislamu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَرْهُمْ يَأْكُلُوا۟ وَيَتَمَتَّعُوا۟ وَيُلْهِهِمُ ٱلْأَمَلُ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaache wale, na wastarehe, na yawazuge matumaini. Basi watakujajua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلَّا وَلَهَا كِتَابٌ مَّعْلُومٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hatukuuangamiza mji wowote ule isipokuwa ulikuwa na muda wake maalumu ulioandikiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَّا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَـْٔخِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHawawezi umma wowote kuutangulia muda wao, wala kuchelewa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالُوا۟ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِى نُزِّلَ عَلَيْهِ ٱلذِّكْرُ إِنَّكَ لَمَجْنُونٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walisema, "Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَّوْ مَا تَأْتِينَا بِٱلْمَلَٰٓئِكَةِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wakweli?"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا نُنَزِّلُ ٱلْمَلَٰٓئِكَةَ إِلَّا بِٱلْحَقِّ وَمَا كَانُوٓا۟ إِذًا مُّنظَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSisi hatuwateremshi Malaika isipokuwa kwa sababu ya haki, na hapo hawatapewa muhula.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا ٱلذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَٰفِظُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Sisi ndio tuliouteremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakaoulinda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِى شِيَعِ ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tulikwishatuma Mitume kabla yako kwa mataifa ya mwanzo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakuwajia Mtume yeyote isipokuwa walikuwa wakimfanyia stihizai.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَٰلِكَ نَسْلُكُهُۥ فِى قُلُوبِ ٱلْمُجْرِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kama hivi ndivyo tunavyoyaingiza katika nyoyo za wahalifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا يُؤْمِنُونَ بِهِۦ وَقَدْ خَلَتْ سُنَّةُ ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHawayaamini haya, na ilhali imekwishawapitia desturi ya wa mwanzo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْ فَتَحْنَا عَلَيْهِم بَابًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فَظَلُّوا۟ فِيهِ يَعْرُجُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau tungeliwafungulia mlango huko mbinguni, wakawa wanapanda kupitia humo,

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَقَالُوٓا۟ إِنَّمَا سُكِّرَتْ أَبْصَٰرُنَا بَلْ نَحْنُ قَوْمٌ مَّسْحُورُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wangelisema: Hakika macho yetu yameleweshwa tu. Bali sisi wenyewe ni kaumu tuliofanyiwa uchawi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ جَعَلْنَا فِى ٱلسَّمَآءِ بُرُوجًا وَزَيَّنَّٰهَا لِلنَّٰظِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tumeweka katika mbingu vituo vya sayari, na tumezipamba kwa wenye kuangalia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَحَفِظْنَٰهَا مِن كُلِّ شَيْطَٰنٍ رَّجِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tumezilinda kutokana na kila shetani aliyelaaniwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا مَنِ ٱسْتَرَقَ ٱلسَّمْعَ فَأَتْبَعَهُۥ شِهَابٌ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa mwenye kusikiliza kwa kuibia, naye hufuatwa na kijinga cha moto kilicho dhahiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلْأَرْضَ مَدَدْنَٰهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَٰسِىَ وَأَنۢبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ شَىْءٍ مَّوْزُونٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ardhi tumeitandaza, na humo tumeweka milima madhubuti, na tumeotesha ndani yake katika kila kitu kwa kiasi chake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَٰيِشَ وَمَن لَّسْتُمْ لَهُۥ بِرَٰزِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tumewafanyia humo vitu vya maisha yenu, na ya hao ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن مِّن شَىْءٍ إِلَّا عِندَنَا خَزَآئِنُهُۥ وَمَا نُنَزِّلُهُۥٓ إِلَّا بِقَدَرٍ مَّعْلُومٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakuna chochote ila asili yake inatokana na Sisi; wala hatukiteremshi isipokuwa kwa kipimo maalumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَرْسَلْنَا ٱلرِّيَٰحَ لَوَٰقِحَ فَأَنزَلْنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَأَسْقَيْنَٰكُمُوهُ وَمَآ أَنتُمْ لَهُۥ بِخَٰزِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka mbinguni maji, kisha tukakunywesheni maji hayo. Wala si nyinyi mnayoyaweka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّا لَنَحْنُ نُحْىِۦ وَنُمِيتُ وَنَحْنُ ٱلْوَٰرِثُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Sisi ndio tunaohuisha na tunaofisha. Na Sisi ndio Warithi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ عَلِمْنَا ٱلْمُسْتَقْدِمِينَ مِنكُمْ وَلَقَدْ عَلِمْنَا ٱلْمُسْتَـْٔخِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tunawajua waliotangulia katika nyinyi, na tunawajua waliobaki nyuma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحْشُرُهُمْ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Mola wako Mlezi ndiye atakayewakusanya. Hakika Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye kujua mno.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ خَلَقْنَا ٱلْإِنسَٰنَ مِن صَلْصَٰلٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tulimuumba Mtu kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلْجَآنَّ خَلَقْنَٰهُ مِن قَبْلُ مِن نَّارِ ٱلسَّمُومِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye Jini tulimuumba hapo kabla kutokana na moto wa upepo umoto.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَٰٓئِكَةِ إِنِّى خَٰلِقٌۢ بَشَرًا مِّن صَلْصَٰلٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِذَا سَوَّيْتُهُۥ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِى فَقَعُوا۟ لَهُۥ سَٰجِدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi nitakapomtengeneza sawasawa, na nikampulizia katika roho yangu, basi angukeni kumsujudia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَسَجَدَ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Malaika wote pamoja walimsujudia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّآ إِبْلِيسَ أَبَىٰٓ أَن يَكُونَ مَعَ ٱلسَّٰجِدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na waliosujudu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ يَٰٓإِبْلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ ٱلسَّٰجِدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na waliosujudu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ لَمْ أَكُن لِّأَسْجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقْتَهُۥ مِن صَلْصَٰلٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliyemuumba kutokana na udongo unaotoa sauti, unaotokana na matope yaliyotiwa sura.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ فَٱخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umefukuziliwa mbali!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ عَلَيْكَ ٱللَّعْنَةَ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلدِّينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبِّ فَأَنظِرْنِىٓ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema (Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watakapofufuliwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلْمُنظَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika waliopewa muhula.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْوَقْتِ ٱلْمَعْلُومِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMpaka siku ya wakati maalumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبِّ بِمَآ أَغْوَيْتَنِى لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyokuwa umenipoteza, basi hakika nitawapambia katika dunia na hakika nitawapoteza wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ ٱلْمُخْلَصِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa waja wako walioteuliwa miongoni mwao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ هَٰذَا صِرَٰطٌ عَلَىَّ مُسْتَقِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Hii ni njia ya kujia kwangu iliyonyooka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ عِبَادِى لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَٰنٌ إِلَّا مَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلْغَاوِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipokuwa wale watakaokufuata miongoni mwa wapotovu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوْعِدُهُمْ أَجْمَعِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Jahannamu ndipo mahali pao walipoahidiwa wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَهَا سَبْعَةُ أَبْوَٰبٍ لِّكُلِّ بَابٍ مِّنْهُمْ جُزْءٌ مَّقْسُومٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIna milango saba; kila mlango ulitengewa sehemu miongoni mwao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّٰتٍ وَعُيُونٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wacha Mungu watakuwa katika Mabustani na chemchemi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱدْخُلُوهَا بِسَلَٰمٍ ءَامِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Wataambiwa:) Ingieni humo kwa salama na amani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنَزَعْنَا مَا فِى صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ إِخْوَٰنًا عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَٰبِلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tutaondoa chuki iliyokuwa vifuani mwao, wawe ndugu, juu ya viti vya kifahari huku wameelekeana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا يَمَسُّهُمْ فِيهَا نَصَبٌ وَمَا هُم مِّنْهَا بِمُخْرَجِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHumo hayatawagusa machovu, wala hawatatolewa humo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

نَبِّئْ عِبَادِىٓ أَنِّىٓ أَنَا ٱلْغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWape habari waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe zaidi, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنَّ عَذَابِى هُوَ ٱلْعَذَابُ ٱلْأَلِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwamba adhabu yangu ndiyo adhabu iliyo chungu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنَبِّئْهُمْ عَن ضَيْفِ إِبْرَٰهِيمَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wape habari za wageni wa Ibrahim.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ دَخَلُوا۟ عَلَيْهِ فَقَالُوا۟ سَلَٰمًا قَالَ إِنَّا مِنكُمْ وَجِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalipoingia kwake na wakasema: Salama! Yeye akasema: Hakika sisi tunawaogopa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ لَا تَوْجَلْ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَٰمٍ عَلِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Usiogope. Hakika, Sisi tunakubashiria kijana mwenye elimu mno.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ أَبَشَّرْتُمُونِى عَلَىٰٓ أَن مَّسَّنِىَ ٱلْكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika! Basi ni kwa njia gani mnanibashiria?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ بَشَّرْنَٰكَ بِٱلْحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ ٱلْقَٰنِطِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Tunakubashiria kwa haki, basi usiwe miongoni mwa wanaokata tamaa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِۦٓ إِلَّا ٱلضَّآلُّونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Na ni nani anayekata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi isipokuwa wapotovu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا ٱلْمُرْسَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Hebu mna jambo gani, enyi wajumbe?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوٓا۟ إِنَّآ أُرْسِلْنَآ إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya wahalifu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّآ ءَالَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمْ أَجْمَعِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa watu wa familia ya Lut'. Bila ya shaka sisi tutawaokoa hao wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا ٱمْرَأَتَهُۥ قَدَّرْنَآ إِنَّهَا لَمِنَ ٱلْغَٰبِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa mkewe. Tumekwishapitisha kwamba huyo hakika atakuwa miongoni mwa watakaosalia nyuma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّا جَآءَ ءَالَ لُوطٍ ٱلْمُرْسَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wajumbe hao walipowajia watu wa familia ya Lut'.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Lut') Alisema: Hakika nyinyi ni kaumu msiojulikana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ بَلْ جِئْنَٰكَ بِمَا كَانُوا۟ فِيهِ يَمْتَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Bali sisi tumekuletea yale waliyokuwa wakiyafanyia shaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَتَيْنَٰكَ بِٱلْحَقِّ وَإِنَّا لَصَٰدِقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tumekujia kwa Haki, na hakika sisi ni wakweli.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ ٱلَّيْلِ وَٱتَّبِعْ أَدْبَٰرَهُمْ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ وَٱمْضُوا۟ حَيْثُ تُؤْمَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ondoka na ahali zako usiku ungalipo, nawe ufuate nyuma yao, wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma. Na mwende huko mnakoamrishwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَضَيْنَآ إِلَيْهِ ذَٰلِكَ ٱلْأَمْرَ أَنَّ دَابِرَ هَٰٓؤُلَآءِ مَقْطُوعٌ مُّصْبِحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukamfunulia hukumu hiyo, ya kwamba hata wa mwisho wao hao ikifika asubuhi atakuwa amekwishakatiliwa mbali.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَآءَ أَهْلُ ٱلْمَدِينَةِ يَسْتَبْشِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakaja watu wa mji huo huku wamefurahi mno.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ ضَيْفِى فَلَا تَفْضَحُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Hakika hawa ni wageni wangu. Basi msinifedheheshe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَلَا تُخْزُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوٓا۟ أَوَلَمْ نَنْهَكَ عَنِ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Kwani hatukukukataza (kuwakaribisha) walimwengu hawa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ هَٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِىٓ إِن كُنتُمْ فَٰعِلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema, "Hawa binti zangu (waoeni)[1], ikiwa nyinyi ni watendaji."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِى سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNinaapa kwa uhai wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَخَذَتْهُمُ ٱلصَّيْحَةُ مُشْرِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ukelele ukawatwaa wakipambaukiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَجَعَلْنَا عَٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hivyo, tukaugeuza mji huo juu chini, na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo wa kutoka Motoni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَٰتٍ لِّلْمُتَوَسِّمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika katika hayo zipo ishara kwa wanaotafakari na kuzingatia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلٍ مُّقِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika miji hii ipo kwenye njia wazi inayopitiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika katika hayo ipo ishara kwa Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن كَانَ أَصْحَٰبُ ٱلْأَيْكَةِ لَظَٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika watu wa Kichakani walikuwa madhalimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱنتَقَمْنَا مِنْهُمْ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامٍ مُّبِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hivyo tukawaadhibu. Na hakika miji miwili hii iko kwenye njia iliyo wazi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ كَذَّبَ أَصْحَٰبُ ٱلْحِجْرِ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka wakazi wa Hijr waliwakadhibisha Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَءَاتَيْنَٰهُمْ ءَايَٰتِنَا فَكَانُوا۟ عَنْهَا مُعْرِضِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tuliwaletea ishara zetu, nao wakawa wanazipa migongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكَانُوا۟ يَنْحِتُونَ مِنَ ٱلْجِبَالِ بُيُوتًا ءَامِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNao walikuwa wakichonga majumba katika milima kwa amani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَخَذَتْهُمُ ٱلصَّيْحَةُ مُصْبِحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ukelele ukawatwaa asubuhi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَمَآ أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hayakuwafaa yale waliyokuwa wakiyachuma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا خَلَقْنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَآ إِلَّا بِٱلْحَقِّ وَإِنَّ ٱلسَّاعَةَ لَـَٔاتِيَةٌ فَٱصْفَحِ ٱلصَّفْحَ ٱلْجَمِيلَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo kati yake isipokuwa kwa haki. Na hakika Saa ya Kiyama itafika. Basi samehe msamaha mzuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلْخَلَّٰقُ ٱلْعَلِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji, Mwenye kujua zaidi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ ءَاتَيْنَٰكَ سَبْعًا مِّنَ ٱلْمَثَانِى وَٱلْقُرْءَانَ ٱلْعَظِيمَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tumekupa (aya) saba zinazosomwa mara kwa mara, na Qur-ani Tukufu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِۦٓ أَزْوَٰجًا مِّنْهُمْ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَٱخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKamwe usivinyoshee macho yako vitu tulivyowastarehesha kwavyo makundi fulani kati yao, wala usiwahuzunikie. Na wainamishie bawa lako (la huruma) Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقُلْ إِنِّىٓ أَنَا ٱلنَّذِيرُ ٱلْمُبِينُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa sema: Hakika mimi ndiye mwonyaji mwenye kubainisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَمَآ أَنزَلْنَا عَلَى ٱلْمُقْتَسِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKama hivyo tuliwateremshia waliogawa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ جَعَلُوا۟ ٱلْقُرْءَانَ عِضِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbao waliifanya Qur-ani vipande vipande.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَوَرَبِّكَ لَنَسْـَٔلَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ninaapa kwa Mola wako Mlezi! Lazima tutawauliza wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

عَمَّا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKuhusu yale waliyokuwa wakiyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ ٱلْمُشْرِكِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wewe yadhihirishe yale uliyoamrishwa, na jitenge mbali na washirikina.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا كَفَيْنَٰكَ ٱلْمُسْتَهْزِءِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Sisi tunatosha kukukinga kutokana na wanaofanya stihizai.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ يَجْعَلُونَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbao wanafanya mungu mwingine kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu. Basi watakujajua!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدْرُكَ بِمَا يَقُولُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Sisi tunajua kwa hakika kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo wayasemayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ ٱلسَّٰجِدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumsifu, na uwe miongoni mwa wanaomsujudia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأْتِيَكَ ٱلْيَقِينُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70