caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nahl النحل

Aya 128 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 70

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ أَتَىٰٓ أَمْرُ ٱللَّهِ فَلَا تَسْتَعْجِلُوهُ سُبْحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmri ya Mwenyezi Mungu itafika tu. Basi msiiharakishe. Ametakasika na ametukuka mbali na hayo wanayomshirikisha nayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يُنَزِّلُ ٱلْمَلَٰٓئِكَةَ بِٱلرُّوحِ مِنْ أَمْرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦٓ أَنْ أَنذِرُوٓا۟ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱتَّقُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuwateremsha Malaika na ufunuo kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake kwamba onyeni kuwa hakuna mungu yeyote isipokuwa Mimi, basi nicheni Mimi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ بِٱلْحَقِّ تَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmeziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Ametukuka na hayo wanayomshirikisha nayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

خَلَقَ ٱلْإِنسَٰنَ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmemuumba mtu kwa tone la manii. Na tazama, akawa mshindani aliye dhahiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلْأَنْعَٰمَ خَلَقَهَا لَكُمْ فِيهَا دِفْءٌ وَمَنَٰفِعُ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa aliwaumba wanyama. Katika hao mna vifaa vya kutia joto, na manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَكُمْ فِيهَا جَمَالٌ حِينَ تُرِيحُونَ وَحِينَ تَسْرَحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika hao mnapata furaha pale mnapowarudisha jioni na mnapowapeleka malishoni asubuhi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَحْمِلُ أَثْقَالَكُمْ إِلَىٰ بَلَدٍ لَّمْ تَكُونُوا۟ بَٰلِغِيهِ إِلَّا بِشِقِّ ٱلْأَنفُسِ إِنَّ رَبَّكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNao hubeba mizigo yenu kupeleka kwenye miji msiyoweza kuifikia isipokuwa kwa mashaka ya nafsi. Hakika Mola wenu Mlezi ni Mpole mno, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلْخَيْلَ وَٱلْبِغَالَ وَٱلْحَمِيرَ لِتَرْكَبُوهَا وَزِينَةً وَيَخْلُقُ مَا لَا تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa farasi, nyumbu, na punda ili muwapande, na wawe ni pambo. Na anaumba msivyovijua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَعَلَى ٱللَّهِ قَصْدُ ٱلسَّبِيلِ وَمِنْهَا جَآئِرٌ وَلَوْ شَآءَ لَهَدَىٰكُمْ أَجْمَعِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni juu ya Mwenyezi Mungu kuelekeza Njia. Na zipo njia za upotovu. Na angelipenda, angeliwaongoa nyote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هُوَ ٱلَّذِىٓ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً لَّكُم مِّنْهُ شَرَابٌ وَمِنْهُ شَجَرٌ فِيهِ تُسِيمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye anayewateremshia maji kutoka mbinguni. Katika hayo nyinyi mnapata ya kunywa, na miti ya kulishia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يُنۢبِتُ لَكُم بِهِ ٱلزَّرْعَ وَٱلزَّيْتُونَ وَٱلنَّخِيلَ وَٱلْأَعْنَٰبَ وَمِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hayo Yeye anawaoteshea mimea, na mizaituni, na mitende, na mizabibu, na kila aina ya matunda. Hakika katika hayo ipo ishara kwa kaumu wanaotafakari.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَسَخَّرَ لَكُمُ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ وَٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ وَٱلنُّجُومُ مُسَخَّرَٰتٌۢ بِأَمْرِهِۦٓ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَٰتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa amewatiishia usiku na mchana, na jua na mwezi, na nyota zimetiishwa kwa amri yake. Hakika katika hayo zipo ishara kwa kaumu watumiao akili.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا ذَرَأَ لَكُمْ فِى ٱلْأَرْضِ مُخْتَلِفًا أَلْوَٰنُهُۥٓ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّقَوْمٍ يَذَّكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa vile alivyowaenezea katika ardhi vya rangi mbalimbali. Hakika katika hayo ipo ishara kwa kaumu wanaokumbuka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَهُوَ ٱلَّذِى سَخَّرَ ٱلْبَحْرَ لِتَأْكُلُوا۟ مِنْهُ لَحْمًا طَرِيًّا وَتَسْتَخْرِجُوا۟ مِنْهُ حِلْيَةً تَلْبَسُونَهَا وَتَرَى ٱلْفُلْكَ مَوَاخِرَ فِيهِ وَلِتَبْتَغُوا۟ مِن فَضْلِهِۦ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye aliyeitiisha bahari, ili kutokana na humo mpate kula nyama laini, na mtoe humo mapambo mnayoyavaa. Na utaona merikebu zikikata maji humo, ili mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَلْقَىٰ فِى ٱلْأَرْضِ رَوَٰسِىَ أَن تَمِيدَ بِكُمْ وَأَنْهَٰرًا وَسُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akaweka katika ardhi milima madhubuti ili ardhi isiyumbeyumbe nanyi. Na mito, na njia mbalimbali ili mpate kuongoka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَعَلَٰمَٰتٍ وَبِٱلنَّجْمِ هُمْ يَهْتَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa alama nyinginezo. Na kwa nyota wao wanajiongoza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَمَن يَخْلُقُ كَمَن لَّا يَخْلُقُ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAti yule anayeumba ni kama asiyeumba? Basi hebu hamkumbuki?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن تَعُدُّوا۟ نِعْمَةَ ٱللَّهِ لَا تُحْصُوهَآ إِنَّ ٱللَّهَ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mkizihesabu neema za Mwenyezi Mungu, hamwezi kuzidhibiti. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira mno, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱللَّهُ يَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعْلِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyaficha na mnayoyaweka hadharani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَا يَخْلُقُونَ شَيْـًٔا وَهُمْ يُخْلَقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale wanaowaomba wasiokuwa Mwenyezi Mungu hawaumbi kitu, bali wao wameumbwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْوَٰتٌ غَيْرُ أَحْيَآءٍ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi wafu, si wahai, na wala hawajui watafufuliwa lini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَٰحِدٌ فَٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٌ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMungu wenu ni Mungu Mmoja. Lakini wale wasioiamini Akhera nyoyo zao zinakataa, nao wanatakabari.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا جَرَمَ أَنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلْمُسْتَكْبِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakuna shaka kuwa hakika Mwenyezi Mungu anayajua yale wanayoyaficha na wanayoyaweka hadharani. Hakika, Yeye hawapendi wanaotakabari.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا قِيلَ لَهُم مَّاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمْ قَالُوٓا۟ أَسَٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanapoambiwa, "Ni nini alichoteremsha Mola wenu Mlezi?" Husema: Hadithi za kubuni za wa mwanzo!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِيَحْمِلُوٓا۟ أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ وَمِنْ أَوْزَارِ ٱلَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ أَلَا سَآءَ مَا يَزِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli wabebe mizigo yao kwa ukamilifu Siku ya Kiyama, na sehemu ya mizigo ya wale wanaowapoteza bila ya kujua. Angalia, ni mabaya mno hayo wanayoyabeba!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَدْ مَكَرَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَأَتَى ٱللَّهُ بُنْيَٰنَهُم مِّنَ ٱلْقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيْهِمُ ٱلسَّقْفُ مِن فَوْقِهِمْ وَأَتَىٰهُمُ ٱلْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalipanga njama wale waliokuwa kabla yao, naye Mwenyezi Mungu akayajia majengo yao kutokea kwenye misingi, kwa hivyo dari zake zikaporomoka juu yao, na adhabu ikawajia kutokea wasipohisi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ يُخْزِيهِمْ وَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَآءِىَ ٱلَّذِينَ كُنتُمْ تُشَٰٓقُّونَ فِيهِمْ قَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ إِنَّ ٱلْخِزْىَ ٱلْيَوْمَ وَٱلسُّوٓءَ عَلَى ٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha Siku ya Kiyama atawahizi na atasema: Wako wapi hao washirika wangu ambao kwao mlikuwa mkipinga (Manabii)? Watasema wale waliopewa elimu: Hakika leo ndiyo hizaya na ubaya vitawashukia makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ ظَالِمِىٓ أَنفُسِهِمْ فَأَلْقَوُا۟ ٱلسَّلَمَ مَا كُنَّا نَعْمَلُ مِن سُوٓءٍۭ بَلَىٰٓ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌۢ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale ambao Malaika huwafisha huku wamejidhulumu nafsi zao! Basi wanasalimu amri, waseme: Hatukuwa tukifanya ubaya wowote. (Wataambiwa). Hasha! Hakika Mwenyezi Mungu anajua sana mliyokuwa mkiyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱدْخُلُوٓا۟ أَبْوَٰبَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَا فَلَبِئْسَ مَثْوَى ٱلْمُتَكَبِّرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ingieni milango ya Jahannamu, humo mdumu. Ni mabaya mno makazi ya wafanyao kiburi!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقِيلَ لِلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ مَاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمْ قَالُوا۟ خَيْرًا لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا۟ فِى هَٰذِهِ ٱلدُّنْيَا حَسَنَةٌ وَلَدَارُ ٱلْـَٔاخِرَةِ خَيْرٌ وَلَنِعْمَ دَارُ ٱلْمُتَّقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wataambiwa wale waliomcha Mungu: Mola wenu Mlezi aliteremsha nini? Watasema: "Heri." Kwa wale waliofanya mazuri katika dunia hii watapata mazuri. Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi, na ni njema mno nyumba hiyo ya wacha Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

جَنَّٰتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَٰرُ لَهُمْ فِيهَا مَا يَشَآءُونَ كَذَٰلِكَ يَجْزِى ٱللَّهُ ٱلْمُتَّقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBustani za milele wataziingia; iwe inapita kwa chini yake mito. Humo watapata watakacho. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu awalipavyo wenye kumcha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ تَتَوَفَّىٰهُمُ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ طَيِّبِينَ يَقُولُونَ سَلَٰمٌ عَلَيْكُمُ ٱدْخُلُوا۟ ٱلْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale ambao Malaika huwafisha katika hali nzuri, wanawaambia: Salama iwe juu yenu! Ingieni Bustanini kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأْتِيَهُمُ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ أَوْ يَأْتِىَ أَمْرُ رَبِّكَ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَمَا ظَلَمَهُمُ ٱللَّهُ وَلَٰكِن كَانُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanangojea jingine hawa isipokuwa Malaika wawafikie, au iwafikie amri ya Mola wako Mlezi? Kama hivyo, walitenda wale waliokuwa kabla yao. Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu, lakini walijidhulumu wenyewe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَصَابَهُمْ سَيِّـَٔاتُ مَا عَمِلُوا۟ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi yakawafikia mabaya ya yale waliyoyatenda, na yale waliyokuwa wakiyafanyia stihizai yakawazingira.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ ٱلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ لَوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَا عَبَدْنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَىْءٍ نَّحْنُ وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَىْءٍ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَهَلْ عَلَى ٱلرُّسُلِ إِلَّا ٱلْبَلَٰغُ ٱلْمُبِينُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa washirikina walisema: Mwenyezi Mungu angelitaka, tusingeliabudu chochote badala yake, sisi wala baba zetu, wala tusingeliharamisha chochote bila ya Yeye. Kama hivyo, walifanya wale waliokuwa kabla yao. Basi lipo lolote juu ya Mitume isipokuwa kufikisha tu kwa wazi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِى كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ وَٱجْتَنِبُوا۟ ٱلطَّٰغُوتَ فَمِنْهُم مَّنْ هَدَى ٱللَّهُ وَمِنْهُم مَّنْ حَقَّتْ عَلَيْهِ ٱلضَّلَٰلَةُ فَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَٱنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلْمُكَذِّبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Twaghut. Basi kati yao wapo aliowaongoa Mwenyezi Mungu. Na kati yao wapo ambao uliwathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wale wanaokadhibisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِن تَحْرِصْ عَلَىٰ هُدَىٰهُمْ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى مَن يُضِلُّ وَمَا لَهُم مِّن نَّٰصِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHata ukiwa na pupa juu ya kuongoka kwao, basi hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi yule anayeshikilia kupotea. Wala hawatapata yeyote wa kuwanusuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَقْسَمُوا۟ بِٱللَّهِ جَهْدَ أَيْمَٰنِهِمْ لَا يَبْعَثُ ٱللَّهُ مَن يَمُوتُ بَلَىٰ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waliapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa viapo vyao kwamba Mwenyezi Mungu hatamfufua aliyekufa. Kwani! Ni ahadi iliyo juu yake kikweli; lakini wengi wa watu hawajui.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِيُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِى يَخْتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعْلَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَنَّهُمْ كَانُوا۟ كَٰذِبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli awabainishie yale waliyohitilafiana ndani yake, na ili wajue wale waliokufuru kwamba wao walikuwa waongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّمَا قَوْلُنَا لِشَىْءٍ إِذَآ أَرَدْنَٰهُ أَن نَّقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika, kauli yetu kwa kitu tunapokitaka kiwe, ni kukiambia tu: "Kuwa!" Basi kinakuwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ هَاجَرُوا۟ فِى ٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ مَا ظُلِمُوا۟ لَنُبَوِّئَنَّهُمْ فِى ٱلدُّنْيَا حَسَنَةً وَلَأَجْرُ ٱلْـَٔاخِرَةِ أَكْبَرُ لَوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kudhulumiwa, bila ya shaka tutawaweka katika maskani mazuri katika dunia; na hakika ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi; lau wangekuwa wanajua!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ صَبَرُوا۟ وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale waliosubiri na wakamtegemea Mola wao Mlezi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِىٓ إِلَيْهِمْ فَسْـَٔلُوٓا۟ أَهْلَ ٱلذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNasi hatukuwatuma kabla yako isipokuwa watu wanaume tuliowapa ufunuo (wahyi). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بِٱلْبَيِّنَٰتِ وَٱلزُّبُرِ وَأَنزَلْنَآ إِلَيْكَ ٱلذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa Ishara wazi na Vitabu. Na tumekuteremshia ukumbusho huu ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao, ili wapate kutafakari.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَأَمِنَ ٱلَّذِينَ مَكَرُوا۟ ٱلسَّيِّـَٔاتِ أَن يَخْسِفَ ٱللَّهُ بِهِمُ ٱلْأَرْضَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ ٱلْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe wana amani wale wanaopanga njama mbaya kwamba Mwenyezi Mungu hatawadidimiza katika ardhi, na haitawafikia adhabu kutoka wasipohisi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوْ يَأْخُذَهُمْ فِى تَقَلُّبِهِمْ فَمَا هُم بِمُعْجِزِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu hatawashika katika harakati zao, na wala hawatamshinda?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوْ يَأْخُذَهُمْ عَلَىٰ تَخَوُّفٍ فَإِنَّ رَبَّكُمْ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu hatawashika huku wana hofu? Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye huruma kubwa, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوَلَمْ يَرَوْا۟ إِلَىٰ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ مِن شَىْءٍ يَتَفَيَّؤُا۟ ظِلَٰلُهُۥ عَنِ ٱلْيَمِينِ وَٱلشَّمَآئِلِ سُجَّدًا لِّلَّهِ وَهُمْ دَٰخِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawavioni vitu alivyoviumba Mwenyezi Mungu, vivuli vyao vinaelekea kushotoni na kuliani, vikimsujudia Mwenyezi Mungu na vikinyenyekea?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلِلَّهِ يَسْجُدُ مَا فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ مِن دَآبَّةٍ وَٱلْمَلَٰٓئِكَةُ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa vinamsujudia Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na katika ardhi, miongoni mwa wanyama mpaka Malaika na wala havitakabari.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterVinamhofu Mola wao Mlezi aliye juu yao, na vinafanya vinavyoamrishwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ ٱللَّهُ لَا تَتَّخِذُوٓا۟ إِلَٰهَيْنِ ٱثْنَيْنِ إِنَّمَا هُوَ إِلَٰهٌ وَٰحِدٌ فَإِيَّٰىَ فَٱرْهَبُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu amesema: Msijifanyie miungu wawili! Hakika Yeye ndiye Mungu Mmoja tu. Basi niogopeni sana Mimi tu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَلَهُ ٱلدِّينُ وَاصِبًا أَفَغَيْرَ ٱللَّهِ تَتَّقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni vyake Yeye vilivyo katika mbingu na ardhi. Na Dini ni yake Yeye daima. Je, mnamcha mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا بِكُم مِّن نِّعْمَةٍ فَمِنَ ٱللَّهِ ثُمَّ إِذَا مَسَّكُمُ ٱلضُّرُّ فَإِلَيْهِ تَجْـَٔرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa neema yoyote mliyo nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha yakiwagusa madhara, mnamyayatikia Yeye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ إِذَا كَشَفَ ٱلضُّرَّ عَنكُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِّنكُم بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa anapowaondoshea madhara hayo, mara kundi moja miongoni mwenu linamshirikisha Mola wao Mlezi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِيَكْفُرُوا۟ بِمَآ ءَاتَيْنَٰهُمْ فَتَمَتَّعُوا۟ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakizikataa neema tulizowapa. Basi stareheni. Mtakujajua!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَجْعَلُونَ لِمَا لَا يَعْلَمُونَ نَصِيبًا مِّمَّا رَزَقْنَٰهُمْ تَٱللَّهِ لَتُسْـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَفْتَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hao ambao hata hawawajui wanawawekea sehemu katika vile tunavyowaruzuku. Tallahi! Bila ya shaka mtaulizwa kwa hayo mliyokuwa mnayazua!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَجْعَلُونَ لِلَّهِ ٱلْبَنَٰتِ سُبْحَٰنَهُۥ وَلَهُم مَّا يَشْتَهُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanamfanyia Mwenyezi Mungu mabinti, Subhanahu (ametakasika)! Na wao wenyewe, ati ndiyo wana hayo wanayoyatamani!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِٱلْأُنثَىٰ ظَلَّ وَجْهُهُۥ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mmoja wao akibashiriwa msichana, uso wake unasalia umesawijika na anakuwa na huzuni mno.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَتَوَٰرَىٰ مِنَ ٱلْقَوْمِ مِن سُوٓءِ مَا بُشِّرَ بِهِۦٓ أَيُمْسِكُهُۥ عَلَىٰ هُونٍ أَمْ يَدُسُّهُۥ فِى ٱلتُّرَابِ أَلَا سَآءَ مَا يَحْكُمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnajificha asionekane na watu kwa sababu ya ubaya wa yule aliyebashiriwa! Je, akae naye pamoja na fedheha hiyo au amfukie udongoni? Tazama, ni ubaya mno wanavyohukumu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ مَثَلُ ٱلسَّوْءِ وَلِلَّهِ ٱلْمَثَلُ ٱلْأَعْلَىٰ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale wasioiamini Akhera wana mfano mbaya mno, naye Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye mfano bora zaidi. Naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْ يُؤَاخِذُ ٱللَّهُ ٱلنَّاسَ بِظُلْمِهِم مَّا تَرَكَ عَلَيْهَا مِن دَآبَّةٍ وَلَٰكِن يُؤَخِّرُهُمْ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَـْٔخِرُونَ سَاعَةً وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa Mwenyezi Mungu angeliwaadhibu watu kwa mujibu wa dhuluma zao, basi asingelimwacha juu yake hata mnyama mmoja. Lakini anawaahirisha mpaka muda uliowekwa. Na unapofika muda wao, hawatakawia hata saa moja wala hawatatangulia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَجْعَلُونَ لِلَّهِ مَا يَكْرَهُونَ وَتَصِفُ أَلْسِنَتُهُمُ ٱلْكَذِبَ أَنَّ لَهُمُ ٱلْحُسْنَىٰ لَا جَرَمَ أَنَّ لَهُمُ ٱلنَّارَ وَأَنَّهُم مُّفْرَطُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanampa Mwenyezi Mungu wanavyovichukia wao, na ndimi zao zinasema uongo kwamba wao watapata mazuri zaidi. Hakuna shaka kwamba hakika wana Moto, na kwamba kwa yakini wataachwa humo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تَٱللَّهِ لَقَدْ أَرْسَلْنَآ إِلَىٰٓ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيْطَٰنُ أَعْمَٰلَهُمْ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ ٱلْيَوْمَ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTallahi! Hakika tuliwatuma Mitume kwa umma zilizokuwa kabla yako, lakini Shetani akawapambia matendo yao. Kwa hivyo leo, yeye ndiye kipenzi chao msaidizi, nao wana adhabu chungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَنزَلْنَا عَلَيْكَ ٱلْكِتَٰبَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِى ٱخْتَلَفُوا۟ فِيهِ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hatukukuteremshia Kitabu hiki isipokuwa ili uwabainishie yale ambayo wanahitilafiana ndani yake, na kiwe uwongofu na rehema kwa kaumu wanaoamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱللَّهُ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَأَحْيَا بِهِ ٱلْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَآ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu ameteremsha maji kutoka mbinguni na kwa hayo akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Kwa hakika, katika hayo imo Ishara kwa kaumu wanaosikia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ لَكُمْ فِى ٱلْأَنْعَٰمِ لَعِبْرَةً نُّسْقِيكُم مِّمَّا فِى بُطُونِهِۦ مِنۢ بَيْنِ فَرْثٍ وَدَمٍ لَّبَنًا خَالِصًا سَآئِغًا لِّلشَّٰرِبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika katika wanyama wa kufugwa[1], mna mazingatio. Tunawanywesha katika vile vilivyomo matumboni mwao - baina ya mavi na damu - maziwa safi, mazuri kwa wanywao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِن ثَمَرَٰتِ ٱلنَّخِيلِ وَٱلْأَعْنَٰبِ تَتَّخِذُونَ مِنْهُ سَكَرًا وَرِزْقًا حَسَنًا إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kutokana na matunda ya mitende na mizabibu mnatengeneza vileo na riziki nzuri. Hakika katika hayo ipo Ishara kwa kaumu watumiao akili.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَوْحَىٰ رَبُّكَ إِلَى ٱلنَّحْلِ أَنِ ٱتَّخِذِى مِنَ ٱلْجِبَالِ بُيُوتًا وَمِنَ ٱلشَّجَرِ وَمِمَّا يَعْرِشُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mola wako Mlezi alimfunulia nyuki kwamba: Jitengenezee majumba yako katika milima, na katika miti, na katika vile wanavyojenga watu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ كُلِى مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ فَٱسْلُكِى سُبُلَ رَبِّكِ ذُلُلًا يَخْرُجُ مِنۢ بُطُونِهَا شَرَابٌ مُّخْتَلِفٌ أَلْوَٰنُهُۥ فِيهِ شِفَآءٌ لِّلنَّاسِ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha kula katika kila matunda, na upite katika njia za Mola wako Mlezi zilizofanywa nyepesi kuzipita. Na kwenye matumbo yao kinatoka kinywaji chenye rangi mbalimbali; ndani yake kuna ponya kwa watu. Hakika katika haya ipo Ishara kwa kaumu wanaotafakari.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱللَّهُ خَلَقَكُمْ ثُمَّ يَتَوَفَّىٰكُمْ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰٓ أَرْذَلِ ٱلْعُمُرِ لِكَىْ لَا يَعْلَمَ بَعْدَ عِلْمٍ شَيْـًٔا إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ قَدِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu aliwaumba; kisha atawafisha. Na miongoni mwenu wapo wanaorudishwa kwenye umri mbaya kabisa, hata akawa hajui kitu baada ya kuwa alikuwa anajua. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi, Muweza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱللَّهُ فَضَّلَ بَعْضَكُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ فِى ٱلرِّزْقِ فَمَا ٱلَّذِينَ فُضِّلُوا۟ بِرَآدِّى رِزْقِهِمْ عَلَىٰ مَا مَلَكَتْ أَيْمَٰنُهُمْ فَهُمْ فِيهِ سَوَآءٌ أَفَبِنِعْمَةِ ٱللَّهِ يَجْحَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu amewaboresha baadhi yenu kuliko wengine katika riziki. Na wale walioboreshwa hawarudishi riziki zao kwa wale iliowamiliki mikono yao ya kulia ili wawe sawa katika riziki hiyo. Basi je, wanazikataa neema za Mwenyezi Mungu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَٰجًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنْ أَزْوَٰجِكُم بَنِينَ وَحَفَدَةً وَرَزَقَكُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ أَفَبِٱلْبَٰطِلِ يُؤْمِنُونَ وَبِنِعْمَتِ ٱللَّهِ هُمْ يَكْفُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu amewaumbia wake kutokana na nyinyi wenyewe, na akawafanyia kutoka kwa wake zenu wana na wajukuu, na akawaruzuku vitu vizuri. Basi je, wanaamini upotovu na wanazikufuru neema za Mwenyezi Mungu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَهُمْ رِزْقًا مِّنَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ شَيْـًٔا وَلَا يَسْتَطِيعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa badala ya Mwenyezi Mungu wanawaabudu wasiowamilikia riziki kutoka mbinguni wala kwenye ardhi, wala hawawezi kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَا تَضْرِبُوا۟ لِلَّهِ ٱلْأَمْثَالَ إِنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi msimpigie Mwenyezi Mungu mifano. Hakika Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا لَّا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَىْءٍ وَمَن رَّزَقْنَٰهُ مِنَّا رِزْقًا حَسَنًا فَهُوَ يُنفِقُ مِنْهُ سِرًّا وَجَهْرًا هَلْ يَسْتَوُۥنَ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu amepiga mfano wa mtumwa aliyemilikiwa, asiyeweza kitu, na mwingine tuliyemruzuku riziki njema inayotoka kwetu, naye akawa anatoa katika riziki hiyo kwa siri na dhahiri. Je, hao watakuwa sawa? Alhamdu Lillahi (sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu)! Lakini wengi wao hawajui.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَآ أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَىْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوْلَىٰهُ أَيْنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ هَلْ يَسْتَوِى هُوَ وَمَن يَأْمُرُ بِٱلْعَدْلِ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa wanaume wawili. Mmoja wao ni bubu, hawezi chochote, naye ni mzigo kwa mlezi wake. Popote anapomuelekeza, haleti heri yoyote. Je, huyo anaweza kuwa sawa na yule anayeamrisha uadilifu, naye yuko kwenye njia iliyonyooka?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلِلَّهِ غَيْبُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَآ أَمْرُ ٱلسَّاعَةِ إِلَّا كَلَمْحِ ٱلْبَصَرِ أَوْ هُوَ أَقْرَبُ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siri zote za mbinguni na ardhini ni za Mwenyezi Mungu. Wala halikuwa jambo la Saa (ya Kiyama) isipokuwa kama kupepesa kwa jicho, au chini zaidi ya hivyo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱللَّهُ أَخْرَجَكُم مِّنۢ بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمْ لَا تَعْلَمُونَ شَيْـًٔا وَجَعَلَ لَكُمُ ٱلسَّمْعَ وَٱلْأَبْصَٰرَ وَٱلْأَفْـِٔدَةَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu aliwatoa matumboni mwa mama zenu hali ya kuwa hamjui kitu, na akawajaalia kusikia na kuona na ufahamu wa nyoyo ili mpate kushukuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ يَرَوْا۟ إِلَى ٱلطَّيْرِ مُسَخَّرَٰتٍ فِى جَوِّ ٱلسَّمَآءِ مَا يُمْسِكُهُنَّ إِلَّا ٱللَّهُ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَٰتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawawaoni ndege walivyotiishwa katika anga la mbingu? Hakuna mwenye kuwashikilia isipokuwa Mwenyezi Mungu. Hakika katika haya zipo ishara kwa kaumu wanaoamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّنۢ بُيُوتِكُمْ سَكَنًا وَجَعَلَ لَكُم مِّن جُلُودِ ٱلْأَنْعَٰمِ بُيُوتًا تَسْتَخِفُّونَهَا يَوْمَ ظَعْنِكُمْ وَيَوْمَ إِقَامَتِكُمْ وَمِنْ أَصْوَافِهَا وَأَوْبَارِهَا وَأَشْعَارِهَآ أَثَٰثًا وَمَتَٰعًا إِلَىٰ حِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu amewajaalia majumba yenu yawe ni maskani yenu, na amewajaalia kutokana na ngozi za wanyama, nyumba mnazoziona nyepesi wakati wa safari zenu na wakati wa kutua kwenu. Na kutokana na sufu zao, na manyoya yao, na nywele zao, mnafanya vyombo na mapambo ya kutumia kwa muda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُم مِّمَّا خَلَقَ ظِلَٰلًا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلْجِبَالِ أَكْنَٰنًا وَجَعَلَ لَكُمْ سَرَٰبِيلَ تَقِيكُمُ ٱلْحَرَّ وَسَرَٰبِيلَ تَقِيكُم بَأْسَكُمْ كَذَٰلِكَ يُتِمُّ نِعْمَتَهُۥ عَلَيْكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْلِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu amewafanyia vivuli katika vitu alivyoviumba, na amewafanyia maskani milimani, na amewafanyia nguo za kuwakinga kutokana na joto, na nguo za kuwakinga katika vita vyenu. Ndivyo hivyo anavyowatimizia neema zake ili mpate kujisalimisha kwake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَإِنَّمَا عَلَيْكَ ٱلْبَلَٰغُ ٱلْمُبِينُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hivyo, wakikengeuka, basi lililo juu yako wewe ni kufikisha ujumbe wazi wazi tu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَعْرِفُونَ نِعْمَتَ ٱللَّهِ ثُمَّ يُنكِرُونَهَا وَأَكْثَرُهُمُ ٱلْكَٰفِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanazijua neema za Mwenyezi Mungu, kisha wanazikanusha, na wengi wao ni makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَوْمَ نَبْعَثُ مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا ثُمَّ لَا يُؤْذَنُ لِلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku tutakapomtoa shahidi kutoka katika kila umma, kisha hawataruhusiwa wale waliokufuru wala hawataachiliwa kutaka radhi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا رَءَا ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ ٱلْعَذَابَ فَلَا يُخَفَّفُ عَنْهُمْ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliodhulumu watakapoiona adhabu, hawatapunguziwa adhabu hiyo, wala hawatapewa muhula.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا رَءَا ٱلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ شُرَكَآءَهُمْ قَالُوا۟ رَبَّنَا هَٰٓؤُلَآءِ شُرَكَآؤُنَا ٱلَّذِينَ كُنَّا نَدْعُوا۟ مِن دُونِكَ فَأَلْقَوْا۟ إِلَيْهِمُ ٱلْقَوْلَ إِنَّكُمْ لَكَٰذِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale walioshirikisha watakapowaona hao waliowashirikisha na Mwenyezi Mungu, watasema: "Mola wetu Mlezi! Hawa ndio washirikishwa wetu ambao tulikuwa tukiwaomba badala yako." Lakini hao watawatupia kauli: Hakika nyinyi ni waongo!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَلْقَوْا۟ إِلَى ٱللَّهِ يَوْمَئِذٍ ٱلسَّلَمَ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَفْتَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku hiyo watasalimu amri mbele ya Mwenyezi Mungu, na yatapotea yale waliyokuwa wakiyazua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَصَدُّوا۟ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ زِدْنَٰهُمْ عَذَابًا فَوْقَ ٱلْعَذَابِ بِمَا كَانُوا۟ يُفْسِدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale waliokufuru na kuzuilia njia ya Mwenyezi Mungu, tutawazidishia adhabu juu ya adhabu, kwa walivyokuwa wakifanya uharibifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَوْمَ نَبْعَثُ فِى كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا عَلَيْهِم مِّنْ أَنفُسِهِمْ وَجِئْنَا بِكَ شَهِيدًا عَلَىٰ هَٰٓؤُلَآءِ وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ ٱلْكِتَٰبَ تِبْيَٰنًا لِّكُلِّ شَىْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa (waonye) siku tutakapomtoa shahidi katika kila umma kutokana na wao wenyewe, na tutakuleta wewe uwe shahidi juu ya hawa. Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinachobainisha kila kitu, na ni uongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱللَّهَ يَأْمُرُ بِٱلْعَدْلِ وَٱلْإِحْسَٰنِ وَإِيتَآئِ ذِى ٱلْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ ٱلْفَحْشَآءِ وَٱلْمُنكَرِ وَٱلْبَغْىِ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani, na kuwapa jamaa, na anakataza uchafu, na uovu, na dhuluma. Anawaaidhi ili mpate kukumbuka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَوْفُوا۟ بِعَهْدِ ٱللَّهِ إِذَا عَٰهَدتُّمْ وَلَا تَنقُضُوا۟ ٱلْأَيْمَٰنَ بَعْدَ تَوْكِيدِهَا وَقَدْ جَعَلْتُمُ ٱللَّهَ عَلَيْكُمْ كَفِيلًا إِنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa timizeni agano la Mwenyezi Mungu mnapoagana, wala msivunje viapo baada ya kuvifunga imara, ilhali mmekwishamfanya Mwenyezi Mungu ndiye mdhamini wenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayajua myafanyayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تَكُونُوا۟ كَٱلَّتِى نَقَضَتْ غَزْلَهَا مِنۢ بَعْدِ قُوَّةٍ أَنكَٰثًا تَتَّخِذُونَ أَيْمَٰنَكُمْ دَخَلًۢا بَيْنَكُمْ أَن تَكُونَ أُمَّةٌ هِىَ أَرْبَىٰ مِنْ أُمَّةٍ إِنَّمَا يَبْلُوكُمُ ٱللَّهُ بِهِۦ وَلَيُبَيِّنَنَّ لَكُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ مَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msiwe kama mwanamke yule aliyeufumua uzi wake baada ya kwishausokota ukawa mgumu. Mnavifanya viapo vyenu kuwa ni njia ya kudanganyana baina yenu kwa kuwa ati umma mmoja una nguvu zaidi kuliko mwingine? Hakika Mwenyezi Mungu anawajaribu kwa njia hiyo. Na bila ya shaka atawabainishia Siku ya Kiyama yale mliyokuwa mkihitilafiana ndani yake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَٰحِدَةً وَلَٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهْدِى مَن يَشَآءُ وَلَتُسْـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu angelitaka, kwa yakini angeliwafanya kuwa umma mmoja. Lakini anampoteza amtakaye, na anamwongoa amtakaye. Na hakika mtaulizwa juu ya yale mliyokuwa mkiyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تَتَّخِذُوٓا۟ أَيْمَٰنَكُمْ دَخَلًۢا بَيْنَكُمْ فَتَزِلَّ قَدَمٌۢ بَعْدَ ثُبُوتِهَا وَتَذُوقُوا۟ ٱلسُّوٓءَ بِمَا صَدَدتُّمْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَكُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msifanye viapo vyenu kuwa njia ya kudanganyana baina yenu, mguu ukajateleza baada ya kuwa thabiti, na mkaonja mabaya kwa sababu ya kule kuzuilia kwenu njia ya Mwenyezi Mungu, na mkapata adhabu kubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تَشْتَرُوا۟ بِعَهْدِ ٱللَّهِ ثَمَنًا قَلِيلًا إِنَّمَا عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msinunue kwa agano la Mwenyezi Mungu thamani ndogo. Hakika kilicho kwa Mwenyezi Mungu ndicho bora kwenu, ikiwa mnajua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا عِندَكُمْ يَنفَدُ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ بَاقٍ وَلَنَجْزِيَنَّ ٱلَّذِينَ صَبَرُوٓا۟ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMlivyo navyo vitakwisha, na vilivyo kwa Mwenyezi Mungu ndivyo vitakavyobakia. Na kwa yakini Sisi tutawapa wale waliosubiri ujira wao kwa bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَنْ عَمِلَ صَٰلِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُۥ حَيَوٰةً طَيِّبَةً وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, hakika tutamhuisha uhai mwema, na hakika tutawapa ujira wao kwa bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِذَا قَرَأْتَ ٱلْقُرْءَانَ فَٱسْتَعِذْ بِٱللَّهِ مِنَ ٱلشَّيْطَٰنِ ٱلرَّجِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa unaposoma Qur-ani, mwombe Mwenyezi Mungu akulinde kutokana na Shetani aliyelaaniwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّهُۥ لَيْسَ لَهُۥ سُلْطَٰنٌ عَلَى ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَلَىٰ رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika yeye hana mamlaka juu ya wale walioamini na wakamtegemea Mola wao Mlezi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّمَا سُلْطَٰنُهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ يَتَوَلَّوْنَهُۥ وَٱلَّذِينَ هُم بِهِۦ مُشْرِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika mamlaka yake yako juu ya wale wanaomfanya kuwa rafiki yao msaidizi, na wale wanaofanya ushirika naye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا بَدَّلْنَآ ءَايَةً مَّكَانَ ءَايَةٍ وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُنَزِّلُ قَالُوٓا۟ إِنَّمَآ أَنتَ مُفْتَرٍۭ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tunapobadilisha Ishara pahala pa Ishara, na Mwenyezi Mungu anayajua anayoyateremsha, wanasema: "Wewe si chochote ila ni mzushi tu", lakini wengi wao hawajui tu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ نَزَّلَهُۥ رُوحُ ٱلْقُدُسِ مِن رَّبِّكَ بِٱلْحَقِّ لِيُثَبِّتَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَهُدًى وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ameiteremsha Roho Mtakatifu kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa haki, ili iwaimarishe wale walioamini, na kuwa ni uongofu, na bishara kwa Waislamu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُۥ بَشَرٌ لِّسَانُ ٱلَّذِى يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِىٌّ وَهَٰذَا لِسَانٌ عَرَبِىٌّ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Sisi hakika tunajua kwamba wanasema: "Hakika yuko mtu anayemfundisha." Lugha ya huyo wanayemuelekezea ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu iliyo bainifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ لَا يَهْدِيهِمُ ٱللَّهُ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale wasioziamini Ishara za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu hawaongoi, nao wana adhabu chungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّمَا يَفْتَرِى ٱلْكَذِبَ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَأُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْكَٰذِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wanazua uongo tu wale wasioziamini Ishara za Mwenyezi Mungu. Na hao ndio waongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَن كَفَرَ بِٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ إِيمَٰنِهِۦٓ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُۥ مُطْمَئِنٌّۢ بِٱلْإِيمَٰنِ وَلَٰكِن مَّن شَرَحَ بِٱلْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnayemkufuru Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipokuwa yule aliyelazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani, lakini yule aliyekifungulia kifua chake ukafiri - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao wana adhabu kubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ ٱسْتَحَبُّوا۟ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا عَلَى ٱلْـَٔاخِرَةِ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa sababu wameupendelea uhai wa dunia hii kuliko Akhera, na kwa sababu Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أُو۟لَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَسَمْعِهِمْ وَأَبْصَٰرِهِمْ وَأُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْغَٰفِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ndio ambao Mwenyezi Mungu ameziziba nyoyo zao na kusikia kwao na kuona kwao. Na hao ndio walioghafilika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا جَرَمَ أَنَّهُمْ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ هُمُ ٱلْخَٰسِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakuna shaka ya kwamba hao ndio waliohasirika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُوا۟ مِنۢ بَعْدِ مَا فُتِنُوا۟ ثُمَّ جَٰهَدُوا۟ وَصَبَرُوٓا۟ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha hakika Mola wako Mlezi, kwa wale waliohama makwao baada ya kuteswa, kisha wakapigania Dini na wakasubiri, bila ya shaka Mola wako Mlezi baada ya hayo ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَوْمَ تَأْتِى كُلُّ نَفْسٍ تُجَٰدِلُ عَن نَّفْسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku ambayo kila nafsi itakuja ikijitetea, na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyotenda, nao hawatadhulumiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا قَرْيَةً كَانَتْ ءَامِنَةً مُّطْمَئِنَّةً يَأْتِيهَا رِزْقُهَا رَغَدًا مِّن كُلِّ مَكَانٍ فَكَفَرَتْ بِأَنْعُمِ ٱللَّهِ فَأَذَٰقَهَا ٱللَّهُ لِبَاسَ ٱلْجُوعِ وَٱلْخَوْفِ بِمَا كَانُوا۟ يَصْنَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mji uliokuwa na amani na utulivu, riziki yake ikiufikia kwa wingi kutokea kila mahali. Lakini ukazikufuru neema za Mwenyezi Mungu; kwa hivyo Mwenyezi Mungu akauvisha vazi la njaa na hofu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyafanya.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ جَآءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْهُمْ فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمُ ٱلْعَذَابُ وَهُمْ ظَٰلِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa alikwishawajia Mjumbe kutoka miongoni mwao. Lakini wakamkadhibisha; basi ikawachukua adhabu hali ya kuwa ni madhalimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكُلُوا۟ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ حَلَٰلًا طَيِّبًا وَٱشْكُرُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu, vilivyo halali na vizuri. Na shukuruni neema za Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ ٱلْمَيْتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحْمَ ٱلْخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيْرِ ٱللَّهِ بِهِۦ فَمَنِ ٱضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika amewaharimishia tu nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliyechinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini anayelazimishwa bila ya kuasi, wala kuvuka mipaka, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تَقُولُوا۟ لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ ٱلْكَذِبَ هَٰذَا حَلَٰلٌ وَهَٰذَا حَرَامٌ لِّتَفْتَرُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msiseme uongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hiki ni halali, na hiki ni haramu - mkimzulia uongo Mwenyezi Mungu. Hakika wale wanaomzulia uongo Mwenyezi Mungu hawatafaulu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَتَٰعٌ قَلِيلٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi starehe ndogo tu, nao wana adhabu chungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُوا۟ حَرَّمْنَا مَا قَصَصْنَا عَلَيْكَ مِن قَبْلُ وَمَا ظَلَمْنَٰهُمْ وَلَٰكِن كَانُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mayahudi tuliwaharimishia yale tuliyokuhadithia zamani. Na Sisi hatukuwadhulumu, bali walikuwa wakijudhulumu wenyewe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُوا۟ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَٰلَةٍ ثُمَّ تَابُوا۟ مِنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوٓا۟ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha hakika Mola wako Mlezi kwa wale waliotenda mabaya kwa ujinga, kisha wakatubia baada ya hayo na wakatenda mazuri; bila ya shaka Mola wako Mlezi baada ya hayo ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ إِبْرَٰهِيمَ كَانَ أُمَّةً قَانِتًا لِّلَّهِ حَنِيفًا وَلَمْ يَكُ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Ibrahim alikuwa mfano mwema, mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, mnyoofu kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

شَاكِرًا لِّأَنْعُمِهِ ٱجْتَبَىٰهُ وَهَدَىٰهُ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenye kuzishukuru neema zake. Yeye alimteua, na akamwongoa kwenye njia iliyonyooka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَءَاتَيْنَٰهُ فِى ٱلدُّنْيَا حَسَنَةً وَإِنَّهُۥ فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ لَمِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukampa mazuri katika dunia, naye hakika Akhera atakuwa miongoni mwa walio wema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ أَنِ ٱتَّبِعْ مِلَّةَ إِبْرَٰهِيمَ حَنِيفًا وَمَا كَانَ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukakufunulia ya kwamba ufuate mila ya Ibrahim, mnyoofu kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّمَا جُعِلَ ٱلسَّبْتُ عَلَى ٱلَّذِينَ ٱخْتَلَفُوا۟ فِيهِ وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ فِيمَا كَانُوا۟ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika siku ya Sabato (Jumamosi) waliwekewa wale waliohitilafiana kuhusiana nayo. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitilafiana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱدْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِٱلْحِكْمَةِ وَٱلْمَوْعِظَةِ ٱلْحَسَنَةِ وَجَٰدِلْهُم بِٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعْلَمُ بِٱلْمُهْتَدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLingania kwenye njia ya Mola wako Mlezi kwa hekima na mawaidha mazuri, na ujadiliane nao kwa namna iliyo nzuri zaidi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anayemjua zaidi yule aliyeipotea njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi wale walioongoka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا۟ بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُم بِهِۦ وَلَئِن صَبَرْتُمْ لَهُوَ خَيْرٌ لِّلصَّٰبِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mkilipiza, basi lipizeni sawa na vile mlivyoadhibiwa. Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanaosubiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱصْبِرْ وَمَا صَبْرُكَ إِلَّا بِٱللَّهِ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَلَا تَكُ فِى ضَيْقٍ مِّمَّا يَمْكُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa subiri. Na kusubiri kwako kusiwe isipokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu. Wala usiwahuzunikie, wala usiwe katika dhiki kwa sababu ya njama wanazozifanya.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوا۟ وَّٱلَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wenye kumcha, na wale watendao mazuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70