caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Muminoon المؤمنون

Aya 118 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 74

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ قَدْ أَفْلَحَ ٱلْمُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wamefaulu Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ هُمْ فِى صَلَاتِهِمْ خَٰشِعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbao ni wanyenyekevu katika Swala zao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ هُمْ عَنِ ٱللَّغْوِ مُعْرِضُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ هُمْ لِلزَّكَوٰةِ فَٰعِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ambao wanatoa Zaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَٰفِظُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ambao wanazilinda tupu zao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا عَلَىٰٓ أَزْوَٰجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَٰنُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa kwa wake zao au kwa wale iliyowamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si wenye kulaumiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَمَنِ ٱبْتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْعَادُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio wavukao mipaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ هُمْ لِأَمَٰنَٰتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَٰعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ambao wanazitunza amana zao na maagano yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَوَٰتِهِمْ يُحَافِظُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ambao Swala zao wanazihifadhi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْوَٰرِثُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ndio warithi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ يَرِثُونَ ٱلْفِرْدَوْسَ هُمْ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbao watairithi Bustani ya Firdausi, nao watadumu humo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ خَلَقْنَا ٱلْإِنسَٰنَ مِن سُلَٰلَةٍ مِّن طِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asili ya udongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ جَعَلْنَٰهُ نُطْفَةً فِى قَرَارٍ مَّكِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukamfanya kuwa tone la mbegu ya uzazi katika mahali patulivu palipo madhubuti.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ خَلَقْنَا ٱلنُّطْفَةَ عَلَقَةً فَخَلَقْنَا ٱلْعَلَقَةَ مُضْغَةً فَخَلَقْنَا ٱلْمُضْغَةَ عِظَٰمًا فَكَسَوْنَا ٱلْعِظَٰمَ لَحْمًا ثُمَّ أَنشَأْنَٰهُ خَلْقًا ءَاخَرَ فَتَبَارَكَ ٱللَّهُ أَحْسَنُ ٱلْخَٰلِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukaliumba tone hilo kuwa damu iliyoganda, na tukaiumba damu hiyo kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande hilo la nyama kuwa mifupa, na mifupa hiyo tukaivisha nyama. Kisha tukamfanya kuwa kiumbe mwingine. Basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa baraka, Mbora zaidi wa waumbaji.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ إِنَّكُم بَعْدَ ذَٰلِكَ لَمَيِّتُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha hakika nyinyi baada ya hayo mtakufa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ تُبْعَثُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha hakika nyinyi Siku ya Kiyama mtafufuliwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ خَلَقْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعَ طَرَآئِقَ وَمَا كُنَّا عَنِ ٱلْخَلْقِ غَٰفِلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa yakini tumeziumba juu yenu njia saba. Nasi hatukuwa wenye kughafilika na viumbe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنزَلْنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءًۢ بِقَدَرٍ فَأَسْكَنَّٰهُ فِى ٱلْأَرْضِ وَإِنَّا عَلَىٰ ذَهَابٍۭ بِهِۦ لَقَٰدِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi na tukayatuliza katika ardhi. Na hakika Sisi tunaweza kuyaondoa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَنشَأْنَا لَكُم بِهِۦ جَنَّٰتٍ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَٰبٍ لَّكُمْ فِيهَا فَوَٰكِهُ كَثِيرَةٌ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa maji hayo tukawafanyia bustani za mitende na mizabibu, mnapata humo matunda mengi, na katika hayo mnakula.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَشَجَرَةً تَخْرُجُ مِن طُورِ سَيْنَآءَ تَنۢبُتُ بِٱلدُّهْنِ وَصِبْغٍ لِّلْـَٔاكِلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mti utokao katika mlima wa Sinai, unaotoa mafuta na kuwa kitoweo kwa walao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ لَكُمْ فِى ٱلْأَنْعَٰمِ لَعِبْرَةً نُّسْقِيكُم مِّمَّا فِى بُطُونِهَا وَلَكُمْ فِيهَا مَنَٰفِعُ كَثِيرَةٌ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika mnayo mazingatio makubwa katika wanyama wa kufugwa waliwao. Tunawanywesha nyinyi katika vile vilivyo matumboni mwao, na nyinyi mnapata katika hao manufaa mengi, na pia mnawala.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَعَلَيْهَا وَعَلَى ٱلْفُلْكِ تُحْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa juu yao na juu ya marikebu mnabebwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِۦ فَقَالَ يَٰقَوْمِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُۥٓ أَفَلَا تَتَّقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tulimtuma Nuhu kwa kaumu yake, akasema, "Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu yeyote asiyekuwa Yeye. Basi je, hamwogopi?"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَقَالَ ٱلْمَلَؤُا۟ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن قَوْمِهِۦ مَا هَٰذَآ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُرِيدُ أَن يَتَفَضَّلَ عَلَيْكُمْ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَأَنزَلَ مَلَٰٓئِكَةً مَّا سَمِعْنَا بِهَٰذَا فِىٓ ءَابَآئِنَا ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema wale wakuu waliokufuru katika kaumu yake, "Huyu si chochote isipokuwa ni mtu tu kama nyinyi. Anataka kujipa ubora juu yenu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka, basi kwa yakini angeliteremsha Malaika. Hatukusikia haya kwa baba zetu wa mwanzoni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنْ هُوَ إِلَّا رَجُلٌۢ بِهِۦ جِنَّةٌ فَتَرَبَّصُوا۟ بِهِۦ حَتَّىٰ حِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuyu si lolote isipokuwa ni mwanamume mwenye wazimu. Basi mngojeeni tu kwa muda."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبِّ ٱنصُرْنِى بِمَا كَذَّبُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema (Nuhu), "Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa kuwa wamenikanusha."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَوْحَيْنَآ إِلَيْهِ أَنِ ٱصْنَعِ ٱلْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا فَإِذَا جَآءَ أَمْرُنَا وَفَارَ ٱلتَّنُّورُ فَٱسْلُكْ فِيهَا مِن كُلٍّ زَوْجَيْنِ ٱثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيْهِ ٱلْقَوْلُ مِنْهُمْ وَلَا تُخَٰطِبْنِى فِى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓا۟ إِنَّهُم مُّغْرَقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTukamfunulia wahyi kwamba, "Unda jahazi mbele ya macho yetu na ufunuo wetu! Na itakapofika amri yetu na ikafurika tanuri, hapo waingize ndani yake kutoka kwa kila jozi, dume na jike, na ahali zako, isipokuwa yule ambaye katika wao juu yake imekwisha tangulia kauli. Wala usiniongeleshe kuhusu hao waliodhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِذَا ٱسْتَوَيْتَ أَنتَ وَمَن مَّعَكَ عَلَى ٱلْفُلْكِ فَقُلِ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِى نَجَّىٰنَا مِنَ ٱلْقَوْمِ ٱلظَّٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi utakapotulia sawasawa wewe na wale walio pamoja nawe humo merikebuni, sema: Alhamdulillahi (Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu), aliyetuokoa kutoka kwa kaumu madhalimu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقُل رَّبِّ أَنزِلْنِى مُنزَلًا مُّبَارَكًا وَأَنتَ خَيْرُ ٱلْمُنزِلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa sema: Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ndiye Mbora wa wateremshaji."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَٰتٍ وَإِن كُنَّا لَمُبْتَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika katika hayo zipo ishara. Na kwa yakini Sisi ni wenye kuwajaribu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ أَنشَأْنَا مِنۢ بَعْدِهِمْ قَرْنًا ءَاخَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha baada yao tukaanzisha kizazi kingine.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَرْسَلْنَا فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ أَنِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُۥٓ أَفَلَا تَتَّقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukawatumia Mtume miongoni mwao, kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna mungu yeyote asiyekuwa Yeye. Je, hamumchi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ ٱلْمَلَأُ مِن قَوْمِهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَكَذَّبُوا۟ بِلِقَآءِ ٱلْـَٔاخِرَةِ وَأَتْرَفْنَٰهُمْ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا مَا هَٰذَآ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يَأْكُلُ مِمَّا تَأْكُلُونَ مِنْهُ وَيَشْرَبُ مِمَّا تَشْرَبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakubwa katika kaumu yake, wale waliokufuru na wakakadhibisha mkutano wa Akhera, na tukawastarehesha katika uhai wa dunia hii, walisema: Huyu si chochote isipokuwa ni mtu kama nyinyi. Anakula katika mnavyokula, na anakunywa katika mnavyokunywa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَئِنْ أَطَعْتُم بَشَرًا مِّثْلَكُمْ إِنَّكُمْ إِذًا لَّخَٰسِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hivyo, nyinyi mkimtii mtu kama nyinyi, basi hakika mtakuwa hasarani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَيَعِدُكُمْ أَنَّكُمْ إِذَا مِتُّمْ وَكُنتُمْ تُرَابًا وَعِظَٰمًا أَنَّكُم مُّخْرَجُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHivi anawaahidi ati mtakapokufa na mkawa udongo na mifupa, kuwa hakika mtatolewa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَيْهَاتَ هَيْهَاتَ لِمَا تُوعَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayawi! Hayawi hayo mnayoahidiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنْ هِىَ إِلَّا حَيَاتُنَا ٱلدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHapana isipokuwa uhai wetu wa duniani tu, tunakufa na kuishi tu. Wala sisi hatutafufuliwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنْ هُوَ إِلَّا رَجُلٌ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا وَمَا نَحْنُ لَهُۥ بِمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuyu si lolote isipokuwa ni mwanamume anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo, wala sisi sio wa kumuamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبِّ ٱنصُرْنِى بِمَا كَذَّبُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa sababu wananikanusha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ عَمَّا قَلِيلٍ لَّيُصْبِحُنَّ نَٰدِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Mwenyezi Mungu) akasema: Baada ya muda mchache watakuwa wenye kujuta.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَخَذَتْهُمُ ٱلصَّيْحَةُ بِٱلْحَقِّ فَجَعَلْنَٰهُمْ غُثَآءً فَبُعْدًا لِّلْقَوْمِ ٱلظَّٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ukawanyakua ukelele kwa haki, na tukawafanya kama takataka zinazoelea juu ya maji. Ikapotelea mbali kaumu ya madhalimu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ أَنشَأْنَا مِنۢ بَعْدِهِمْ قُرُونًا ءَاخَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukaleta baada yao vizazi vingine.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَـْٔخِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHapana umma uwezao kutanguliza muda wake wala kuuchelewesha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا تَتْرَا كُلَّ مَا جَآءَ أُمَّةً رَّسُولُهَا كَذَّبُوهُ فَأَتْبَعْنَا بَعْضَهُم بَعْضًا وَجَعَلْنَٰهُمْ أَحَادِيثَ فَبُعْدًا لِّقَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukawatuma Mitume wetu, mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipowafikia Mtume wao, walimkadhibisha. Tukawafuatanisha hawa baada ya hawa, na tukawafanya kuwa hadithi za kusimuliwa. Basi wakapotelea mbali kaumu wasioamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ وَأَخَاهُ هَٰرُونَ بِـَٔايَٰتِنَا وَسُلْطَٰنٍ مُّبِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukamtuma Musa na kakaye, Harun, pamoja na ishara zetu na hoja zilizo wazi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَإِي۟هِۦ فَٱسْتَكْبَرُوا۟ وَكَانُوا۟ قَوْمًا عَالِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKumwendea Firauni na wakuu wake. Lakini wakatakabari, nao walikuwa kaumu majeuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَقَالُوٓا۟ أَنُؤْمِنُ لِبَشَرَيْنِ مِثْلِنَا وَقَوْمُهُمَا لَنَا عَٰبِدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema, "Je, tuwaamini watu wawili hawa kama sisi, na ambao kaumu yao ni watumwa wetu?"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكَذَّبُوهُمَا فَكَانُوا۟ مِنَ ٱلْمُهْلَكِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakawakadhibisha, na wakawa miongoni mwa walioangamizwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَٰبَ لَعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tulimpa Musa Kitabu ili wapate kuongoka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَعَلْنَا ٱبْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُۥٓ ءَايَةً وَءَاوَيْنَٰهُمَآ إِلَىٰ رَبْوَةٍ ذَاتِ قَرَارٍ وَمَعِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukamfanya mwana wa Mariamu na mama yake kuwa ni Ishara, na tukawapa makimbilio kwenda mahali palipoinuka penye utulivu na chemchemi za maji.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلرُّسُلُ كُلُوا۟ مِنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ وَٱعْمَلُوا۟ صَٰلِحًا إِنِّى بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ninajua vyema mnayoyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ هَٰذِهِۦٓ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَٰحِدَةً وَأَنَا۠ رَبُّكُمْ فَٱتَّقُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi nicheni Mimi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَتَقَطَّعُوٓا۟ أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ زُبُرًا كُلُّ حِزْبٍۭ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini walikatiana jambo lao mapande mbalimbali. Kila kundi likifurahia kwa waliyo nayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَذَرْهُمْ فِى غَمْرَتِهِمْ حَتَّىٰ حِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi waache katika ghafla yao kwa muda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَيَحْسَبُونَ أَنَّمَا نُمِدُّهُم بِهِۦ مِن مَّالٍ وَبَنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, wanadhani ya kuwa kwa vile tunavyowapa mali na watoto.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

نُسَارِعُ لَهُمْ فِى ٱلْخَيْرَٰتِ بَل لَّا يَشْعُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNdiyo tunawaharakishia heri? Lakini wenyewe hawatambui.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ هُم مِّنْ خَشْيَةِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika hao ambao kwa kumwogopa Mola wao Mlezi wananyenyekea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ هُم بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale ambao Ishara za Mola wao Mlezi wanaziamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ هُم بِرَبِّهِمْ لَا يُشْرِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale ambao Mola wao Mlezi hawamshirikishi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ يُؤْتُونَ مَآ ءَاتَوا۟ وَّقُلُوبُهُمْ وَجِلَةٌ أَنَّهُمْ إِلَىٰ رَبِّهِمْ رَٰجِعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale ambao wanatoa kile walichopewa, na hali nyoyo zao zinaogopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أُو۟لَٰٓئِكَ يُسَٰرِعُونَ فِى ٱلْخَيْرَٰتِ وَهُمْ لَهَا سَٰبِقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wote hao ndio wanaokimbilia mambo ya heri, na ndio watakaotangulia kuyafikia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا وَلَدَيْنَا كِتَٰبٌ يَنطِقُ بِٱلْحَقِّ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hatuitwiki nafsi isipokuwa kwa kiasi cha uwezo wake. Na tunacho kitabu kisemacho kweli. Nao hawatadhulumiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بَلْ قُلُوبُهُمْ فِى غَمْرَةٍ مِّنْ هَٰذَا وَلَهُمْ أَعْمَٰلٌ مِّن دُونِ ذَٰلِكَ هُمْ لَهَا عَٰمِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini nyoyo zao zimefunikwa hazitambui hayo, na wanavyo vitendo vinginevyo wanavyovifanya.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

حَتَّىٰٓ إِذَآ أَخَذْنَا مُتْرَفِيهِم بِٱلْعَذَابِ إِذَا هُمْ يَجْـَٔرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHata tutakapowatia katika adhabu wale waliodekezwa kwa starehe kati yao, hapo ndipo watakapoyayatika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا تَجْـَٔرُوا۟ ٱلْيَوْمَ إِنَّكُم مِّنَّا لَا تُنصَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMsiyayatike leo! Hakika nyinyi hamtanusurika kutokana nasi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَدْ كَانَتْ ءَايَٰتِى تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَكُنتُمْ عَلَىٰٓ أَعْقَٰبِكُمْ تَنكِصُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika zilikuwa Aya zangu mkisomewa, nanyi mkirudi nyuma juu ya visigino vyenu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مُسْتَكْبِرِينَ بِهِۦ سَٰمِرًا تَهْجُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa huku mkiitakabari na usiku mkiizungumzia (Qur-ani) kwa dharau.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَلَمْ يَدَّبَّرُوا۟ ٱلْقَوْلَ أَمْ جَآءَهُم مَّا لَمْ يَأْتِ ءَابَآءَهُمُ ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawakuifikiri kauli, au yamewajia ambayo hayakuwafikia baba zao wa zamani?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ لَمْ يَعْرِفُوا۟ رَسُولَهُمْ فَهُمْ لَهُۥ مُنكِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu hawakumjua Mtume wao, ndiyo maana wanamkataa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ يَقُولُونَ بِهِۦ جِنَّةٌۢ بَلْ جَآءَهُم بِٱلْحَقِّ وَأَكْثَرُهُمْ لِلْحَقِّ كَٰرِهُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu wanasema: Ana wazimu? Bali amewajia kwa Haki, na wengi wao wanaichukia Haki.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوِ ٱتَّبَعَ ٱلْحَقُّ أَهْوَآءَهُمْ لَفَسَدَتِ ٱلسَّمَٰوَٰتُ وَٱلْأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ بَلْ أَتَيْنَٰهُم بِذِكْرِهِمْ فَهُمْ عَن ذِكْرِهِم مُّعْرِضُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa Haki ingelifuata matamanio yao, basi zingeliharibika mbingu na ardhi na waliomo ndani yake. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga mbali na ukumbusho wao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ تَسْـَٔلُهُمْ خَرْجًا فَخَرَاجُ رَبِّكَ خَيْرٌ وَهُوَ خَيْرُ ٱلرَّٰزِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu unawaomba ujira? Lakini ujira wa Mola wako Mlezi ni bora, na Yeye ndiye Mbora wa wanaoruzuku.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّكَ لَتَدْعُوهُمْ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa yakini, wewe unawaita kwenye njia iliyonyooka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ عَنِ ٱلصِّرَٰطِ لَنَٰكِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika wale wasioiamini Akhera wanajitenga mbali na njia hiyo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْ رَحِمْنَٰهُمْ وَكَشَفْنَا مَا بِهِم مِّن ضُرٍّ لَّلَجُّوا۟ فِى طُغْيَٰنِهِمْ يَعْمَهُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau tungeliwarehemu na tukawaondolea shida waliyo nayo, bila ya shaka wangeliendelea katika upotovu wao, vile vile wakitangatanga.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ أَخَذْنَٰهُم بِٱلْعَذَابِ فَمَا ٱسْتَكَانُوا۟ لِرَبِّهِمْ وَمَا يَتَضَرَّعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tuliwatia adhabu kali; lakini hawakuelekea kwa Mola wao Mlezi wala hawakunyenyekea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

حَتَّىٰٓ إِذَا فَتَحْنَا عَلَيْهِم بَابًا ذَا عَذَابٍ شَدِيدٍ إِذَا هُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMpaka tulipowafungulia mlango wa adhabu, hapo ndipo wakawa wenye kukata tamaa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَهُوَ ٱلَّذِىٓ أَنشَأَ لَكُمُ ٱلسَّمْعَ وَٱلْأَبْصَٰرَ وَٱلْأَفْـِٔدَةَ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Yeye ndiye aliyewaumbia kusikia na kuona na nyoyo za kufahamu. Ni kuchache mno kushukuru kwenu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَهُوَ ٱلَّذِى ذَرَأَكُمْ فِى ٱلْأَرْضِ وَإِلَيْهِ تُحْشَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Yeye ndiye aliyewaeneza katika ardhi, na kwake Yeye mtakusanywa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَهُوَ ٱلَّذِى يُحْىِۦ وَيُمِيتُ وَلَهُ ٱخْتِلَٰفُ ٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ أَفَلَا تَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Yeye ndiye anayehuisha na kufisha, na ni yake Yeye mabadiliko ya usiku na mchana. Basi je, hamfahamu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بَلْ قَالُوا۟ مِثْلَ مَا قَالَ ٱلْأَوَّلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBali wanasema kama walivyosema watu wa kwanza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوٓا۟ أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalisema: Je, tukishakufa tukawa udongo na mifupa, ndio tutafufuliwa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَقَدْ وُعِدْنَا نَحْنُ وَءَابَآؤُنَا هَٰذَا مِن قَبْلُ إِنْ هَٰذَآ إِلَّآ أَسَٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTuliahidiwa haya sisi na baba zetu wa zamani. Hayakuwa haya ila ni visa vya uongo vya watu wa zamani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُل لِّمَنِ ٱلْأَرْضُ وَمَن فِيهَآ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ni ya nani ardhi na vilivyo ndani yake, kama nyinyi mnajua?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَيَقُولُونَ لِلَّهِ قُلْ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema: Ni vya Mwenyezi Mungu! Sema: Basi, je, hamkumbuki?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ مَن رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ ٱلسَّبْعِ وَرَبُّ ٱلْعَرْشِ ٱلْعَظِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu saba na Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَيَقُولُونَ لِلَّهِ قُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Sema, Basi, je, hamwogopi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ مَنۢ بِيَدِهِۦ مَلَكُوتُ كُلِّ شَىْءٍ وَهُوَ يُجِيرُ وَلَا يُجَارُ عَلَيْهِ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu, naye ndiye anayelinda, wala hakilindwi asichotaka, kama mnajua?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَيَقُولُونَ لِلَّهِ قُلْ فَأَنَّىٰ تُسْحَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema, "Ufalme huo ni wa Mwenyezi Mungu." Sema: Basi vipi mnadanganyika?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بَلْ أَتَيْنَٰهُم بِٱلْحَقِّ وَإِنَّهُمْ لَكَٰذِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBali tumewaletea Haki, na kwa yakini hao ni waongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ مِن وَلَدٍ وَمَا كَانَ مَعَهُۥ مِنْ إِلَٰهٍ إِذًا لَّذَهَبَ كُلُّ إِلَٰهٍۭ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلَا بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ سُبْحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwingine. Ingekuwa hivyo basi kila mungu angelichukua alivyoumba, na baadhi yao wangeliwashinda wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazomsifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

عَٰلِمِ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye ajuaye siri na dhahiri, na ametukuka juu ya hayo wanayomshirikisha nayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُل رَّبِّ إِمَّا تُرِيَنِّى مَا يُوعَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mola wangu Mlezi! Ukinionyesha adhabu waliyoahidiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

رَبِّ فَلَا تَجْعَلْنِى فِى ٱلْقَوْمِ ٱلظَّٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMola wangu Mlezi! Usinifanye katika hao watu madhalimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّا عَلَىٰٓ أَن نُّرِيَكَ مَا نَعِدُهُمْ لَقَٰدِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Sisi ni waweza wa kukuonyesha tuliyowaahidi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱدْفَعْ بِٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ ٱلسَّيِّئَةَ نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَصِفُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi. Sisi tunayajua vyema wayasemayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقُل رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَٰتِ ٱلشَّيَٰطِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa sema: Mola wangu Mlezi! Ninajikinga kwako kutokana na wasiwasi wa mashetani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ninajikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَحَدَهُمُ ٱلْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ٱرْجِعُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMpaka yanapomfikia mmoja wao mauti, husema: "Mola wangu Mlezi! Nirudishe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَعَلِّىٓ أَعْمَلُ صَٰلِحًا فِيمَا تَرَكْتُ كَلَّآ إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ قَآئِلُهَا وَمِن وَرَآئِهِم بَرْزَخٌ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli nitende mema sasa badala ya yale niliyoyaacha." Wapi! Hii ni kauli aisemayo yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi mpaka siku watakapofufuliwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِذَا نُفِخَ فِى ٱلصُّورِ فَلَآ أَنسَابَ بَيْنَهُمْ يَوْمَئِذٍ وَلَا يَتَسَآءَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi litakapopulizwa baragumu, hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala hawataulizana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَمَن ثَقُلَتْ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAma wale ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio wenye kufanikiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَنْ خَفَّتْ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُو۟لَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ فِى جَهَنَّمَ خَٰلِدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale ambao mizani zao zitakuwa nyepesi, hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao, na katika Jahannamu watadumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تَلْفَحُ وُجُوهَهُمُ ٱلنَّارُ وَهُمْ فِيهَا كَٰلِحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMoto utababua nyuso zao, nao watakuwa na nyuso zilizo kunjana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ تَكُنْ ءَايَٰتِى تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَكُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hazikuwa Aya zangu mkisomewa, na nyinyi mkizikanusha?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ رَبَّنَا غَلَبَتْ عَلَيْنَا شِقْوَتُنَا وَكُنَّا قَوْمًا ضَآلِّينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema: Mola wetu Mlezi! Tulizidiwa na uovu wetu na tukawa watu tuliopotea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

رَبَّنَآ أَخْرِجْنَا مِنْهَا فَإِنْ عُدْنَا فَإِنَّا ظَٰلِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tukirudia tena (ya zamani), basi kweli sisi ni wenye kudhulumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ ٱخْسَـُٔوا۟ فِيهَا وَلَا تُكَلِّمُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAtasema Mwenyezi Mungu: Tokomeeni humo, wala msinisemeshe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّهُۥ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْ عِبَادِى يَقُولُونَ رَبَّنَآ ءَامَنَّا فَٱغْفِرْ لَنَا وَٱرْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ ٱلرَّٰحِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBila ya shaka lilikuwapo kundi katika waja wangu likisema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini; basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanaorehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱتَّخَذْتُمُوهُمْ سِخْرِيًّا حَتَّىٰٓ أَنسَوْكُمْ ذِكْرِى وَكُنتُم مِّنْهُمْ تَضْحَكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini nyinyi mliwakejeli hata wakakusahaulisheni kunikumbuka, na mlikuwa mkiwacheka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنِّى جَزَيْتُهُمُ ٱلْيَوْمَ بِمَا صَبَرُوٓا۟ أَنَّهُمْ هُمُ ٱلْفَآئِزُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mimi leo nimewalipa kwa vile walivyosubiri. Bila ya shaka hao ndio wenye kufuzu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَٰلَ كَمْ لَبِثْتُمْ فِى ٱلْأَرْضِ عَدَدَ سِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAtasema: Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hisabu ya miaka?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ فَسْـَٔلِ ٱلْعَآدِّينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema: Tulikaa siku moja au sehemu ya siku. Basi waulize wanaoweka hisabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَٰلَ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا لَّوْ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAtasema: Nyinyi hamkukaa huko duniani ila kidogo, laiti ingelikuwa mnajua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَٰكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا تُرْجَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, mlidhani ya kwamba tuliwaumba bure, na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَتَعَٰلَى ٱللَّهُ ٱلْمَلِكُ ٱلْحَقُّ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ ٱلْعَرْشِ ٱلْكَرِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmetukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki. Hakuna mungu yeyote isipokuwa Yeye, Mola Mlezi wa Kiti cha Enzi Kitukufu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَن يَدْعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَٰهًا ءَاخَرَ لَا بُرْهَٰنَ لَهُۥ بِهِۦ فَإِنَّمَا حِسَابُهُۥ عِندَ رَبِّهِۦٓ إِنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلْكَٰفِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa anayemuomba - pamoja na Mwenyezi Mungu - mungu mwenginewe, hana ushahidi wa hili; basi bila ya shaka hisabu yake iko kwa Mola wake Mlezi. Kwa hakika makafiri hawafanikiwi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقُل رَّبِّ ٱغْفِرْ وَٱرْحَمْ وَأَنتَ خَيْرُ ٱلرَّٰحِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNawe sema, "Mola wangu Mlezi, samehe na urehemu nawe ni Mbora wa wanaorehemu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70