caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Hajj الحج

Aya 78 · Madina · mpangilio wa kuteremshwa 103

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُوا۟ رَبَّكُمْ إِنَّ زَلْزَلَةَ ٱلسَّاعَةِ شَىْءٌ عَظِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi. Hakika mtetemeko wa Saa (ya Kiyama) ni jambo kuu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّآ أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى ٱلنَّاسَ سُكَٰرَىٰ وَمَا هُم بِسُكَٰرَىٰ وَلَٰكِنَّ عَذَابَ ٱللَّهِ شَدِيدٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku mtakapoiona, kila mwenye kunyonyesha atamsahau amnyonyeshaye, na kila mwenye mimba, ataharibu mimba yake. Na utaona watu wamelewa, na kumbe hawakulewa. Lakini adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُجَٰدِلُ فِى ٱللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّبِعُ كُلَّ شَيْطَٰنٍ مَّرِيدٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa miongoni mwa watu wapo wanaobishana juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu, na wanamfuata kila shetani aliyeasi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كُتِبَ عَلَيْهِ أَنَّهُۥ مَن تَوَلَّاهُ فَأَنَّهُۥ يُضِلُّهُۥ وَيَهْدِيهِ إِلَىٰ عَذَابِ ٱلسَّعِيرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmeandikiwa kwamba anayemfanya kuwa rafiki, basi huyo hakika atampoteza na atamwongoza kwenye adhabu ya Moto mkali.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِن كُنتُمْ فِى رَيْبٍ مِّنَ ٱلْبَعْثِ فَإِنَّا خَلَقْنَٰكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ مِن مُّضْغَةٍ مُّخَلَّقَةٍ وَغَيْرِ مُخَلَّقَةٍ لِّنُبَيِّنَ لَكُمْ وَنُقِرُّ فِى ٱلْأَرْحَامِ مَا نَشَآءُ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى ثُمَّ نُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوٓا۟ أَشُدَّكُمْ وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ وَمِنكُم مَّن يُرَدُّ إِلَىٰٓ أَرْذَلِ ٱلْعُمُرِ لِكَيْلَا يَعْلَمَ مِنۢ بَعْدِ عِلْمٍ شَيْـًٔا وَتَرَى ٱلْأَرْضَ هَامِدَةً فَإِذَآ أَنزَلْنَا عَلَيْهَا ٱلْمَآءَ ٱهْتَزَّتْ وَرَبَتْ وَأَنۢبَتَتْ مِن كُلِّ زَوْجٍۭ بَهِيجٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi watu! Ikiwa nyinyi mna shaka juu ya kufufuliwa, basi kwa hakika Sisi tulikuumbeni kutokana na udongo, kisha kutokana na manii, kisha kutokana na kipande cha damu iliyogandana, kisha kutokana na kipande cha nyama chenye umbo na kisichokuwa na umbo, ili tuwabainishie. Nasi tunakiweka katika matumbo ya uzazi tunachokitaka mpaka muda uliowekwa. Kisha tunawatoa kwa hali ya mtoto mchanga, kisha mfikie kutimia akili. Na wapo katika nyinyi wanaokufa, na wapo katika nyinyi wanaorudishwa kwenye umri wa unyonge kabisa, hata mtu awe hajui kitu baada ya kuwa anakijua. Na unaiona ardhi imetulia kimya, lakini tunapoyateremsha maji juu yake, husisimka na kututumka, na kumea kila namna ya mimea mizuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْحَقُّ وَأَنَّهُۥ يُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰ وَأَنَّهُۥ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ndiye Haki, na kwamba hakika Yeye ndiye mwenye kuhuisha wafu, na kwamba hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنَّ ٱلسَّاعَةَ ءَاتِيَةٌ لَّا رَيْبَ فِيهَا وَأَنَّ ٱللَّهَ يَبْعَثُ مَن فِى ٱلْقُبُورِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwamba hakika Saa (ya Kiyama) itakuja hakuna shaka kwa hilo, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu atawafufua walio makaburini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يُجَٰدِلُ فِى ٱللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَلَا هُدًى وَلَا كِتَٰبٍ مُّنِيرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika watu wapo wanaobishana juu ya Mwenyezi Mungu bila ya elimu, wala uongofu, wala Kitabu chenye nuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثَانِىَ عِطْفِهِۦ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ لَهُۥ فِى ٱلدُّنْيَا خِزْىٌ وَنُذِيقُهُۥ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ عَذَابَ ٱلْحَرِيقِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnayegeuza shingo yake ili kupoteza watu waiache njia ya Mwenyezi Mungu. Duniani atapata hizaya, na Siku ya Kiyama tutamwonjesha adhabu ya kuunguza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ يَدَاكَ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَيْسَ بِظَلَّٰمٍ لِّلْعَبِيدِ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Ataambiwa): Hayo ni kwa sababu ya yale iliyoyatanguliza mikono yako. Na hakika Mwenyezi Mungu si dhalimu kwa waja.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَعْبُدُ ٱللَّهَ عَلَىٰ حَرْفٍ فَإِنْ أَصَابَهُۥ خَيْرٌ ٱطْمَأَنَّ بِهِۦ وَإِنْ أَصَابَتْهُ فِتْنَةٌ ٱنقَلَبَ عَلَىٰ وَجْهِهِۦ خَسِرَ ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةَ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْخُسْرَانُ ٱلْمُبِينُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika watu wapo wanaomuabudu Mwenyezi Mungu kwa ukingoni. Ikimfikia heri, hutulia kwayo. Na ukimfikia msukosuko, hugeuza uso wake. Amehasiri dunia na Akhera. Hiyo ndiyo hasara iliyo wazi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَدْعُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُۥ وَمَا لَا يَنفَعُهُۥ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلضَّلَٰلُ ٱلْبَعِيدُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBadala ya Mwenyezi Mungu, yeye huomba kisichomdhuru wala kumnufaisha. Huko ndiko kupotea kwa mbali!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَدْعُوا۟ لَمَن ضَرُّهُۥٓ أَقْرَبُ مِن نَّفْعِهِۦ لَبِئْسَ ٱلْمَوْلَىٰ وَلَبِئْسَ ٱلْعَشِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHumuomba yule ambaye bila ya shaka madhara yake yapo karibu zaidi kuliko manufaa yake. Kwa hakika huyo ni mlinzi muovu, na rafiki muovu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱللَّهَ يُدْخِلُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ جَنَّٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَٰرُ إِنَّ ٱللَّهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mwenyezi Mungu atawaingiza wale walioamini na wakatenda mema katika Bustani zipitazo mito kwa chini yake. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda atakayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَن كَانَ يَظُنُّ أَن لَّن يَنصُرَهُ ٱللَّهُ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ فَلْيَمْدُدْ بِسَبَبٍ إِلَى ٱلسَّمَآءِ ثُمَّ لْيَقْطَعْ فَلْيَنظُرْ هَلْ يُذْهِبَنَّ كَيْدُهُۥ مَا يَغِيظُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnayedhani kwamba Mwenyezi Mungu hatamnusuru (Mtume) katika dunia na Akhera, basi na afunge kamba kwenye dari kisha na aikate, na atazame je hila yake itayaondoa hayo yaliyomkasirisha?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَٰهُ ءَايَٰتٍۭ بَيِّنَٰتٍ وَأَنَّ ٱللَّهَ يَهْدِى مَن يُرِيدُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa namna hivyo tumeiteremsha (Qur-ani) kuwa ni Aya zilizo wazi, na hakika Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱلَّذِينَ هَادُوا۟ وَٱلصَّٰبِـِٔينَ وَٱلنَّصَٰرَىٰ وَٱلْمَجُوسَ وَٱلَّذِينَ أَشْرَكُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ يَفْصِلُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika walioamini, na Mayahudi na Wasabai na Wakristo na Majusi na wale walioshirikisha, hakika Mwenyezi Mungu atawapambanua baina yao Siku ya Kiyama. Hakika Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa kila kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يَسْجُدُ لَهُۥ مَن فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَن فِى ٱلْأَرْضِ وَٱلشَّمْسُ وَٱلْقَمَرُ وَٱلنُّجُومُ وَٱلْجِبَالُ وَٱلشَّجَرُ وَٱلدَّوَآبُّ وَكَثِيرٌ مِّنَ ٱلنَّاسِ وَكَثِيرٌ حَقَّ عَلَيْهِ ٱلْعَذَابُ وَمَن يُهِنِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِن مُّكْرِمٍ إِنَّ ٱللَّهَ يَفْعَلُ مَا يَشَآءُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe! Huoni kwamba vinamsujudia Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini, na jua, na mwezi, na nyota, na milima, na miti, na wanyama, na wengi miongoni mwa watu. Na wengi imewastahiki adhabu. Na anayefedheheshwa na Mwenyezi Mungu, huyo hana wa kumheshimu. Hakika Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَٰذَانِ خَصْمَانِ ٱخْتَصَمُوا۟ فِى رَبِّهِمْ فَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ قُطِّعَتْ لَهُمْ ثِيَابٌ مِّن نَّارٍ يُصَبُّ مِن فَوْقِ رُءُوسِهِمُ ٱلْحَمِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHawa ni wagomvi wawili waliogombana kwa ajili ya Mola wao Mlezi. Basi waliokufuru watakatiwa nguo za moto, na yatamiminwa juu ya vichwa vyao maji yanayochemka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يُصْهَرُ بِهِۦ مَا فِى بُطُونِهِمْ وَٱلْجُلُودُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa maji hayo, vitayeyushwa vilivyomo matumboni mwao, na ngozi zao pia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَهُم مَّقَٰمِعُ مِنْ حَدِيدٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa ajili yao yatakuwapo marungu ya chuma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كُلَّمَآ أَرَادُوٓا۟ أَن يَخْرُجُوا۟ مِنْهَا مِنْ غَمٍّ أُعِيدُوا۟ فِيهَا وَذُوقُوا۟ عَذَابَ ٱلْحَرِيقِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKila wakitaka kutoka humo kwa sababu ya uchungu, watarudishwa humo humo, na wataambiwa: Onjeni adhabu ya kuunguza!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱللَّهَ يُدْخِلُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ جَنَّٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَٰرُ يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَلُؤْلُؤًا وَلِبَاسُهُمْ فِيهَا حَرِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walioamini na wakatenda mema katika Bustani ambazo mito inapita kati yake. Watapambwa humo kwa mapambo ya mikononi ya dhahabu na lulu. Na mavazi yao humo ni hariri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَهُدُوٓا۟ إِلَى ٱلطَّيِّبِ مِنَ ٱلْقَوْلِ وَهُدُوٓا۟ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلْحَمِيدِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wataongozwa kwenye maneno mazuri, na wataongozwa kwenye njia ya Msifiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ ٱلَّذِى جَعَلْنَٰهُ لِلنَّاسِ سَوَآءً ٱلْعَٰكِفُ فِيهِ وَٱلْبَادِ وَمَن يُرِدْ فِيهِ بِإِلْحَادٍۭ بِظُلْمٍ نُّذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu na Msikiti Mtakatifu, ambao tumeufanya kwa ajili ya watu wote sawasawa, kwa wakaao humo na wageni. Na kila atakayetaka kufanya upotovu humo kwa dhuluma, basi tutamwonjesha adhabu chungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذْ بَوَّأْنَا لِإِبْرَٰهِيمَ مَكَانَ ٱلْبَيْتِ أَن لَّا تُشْرِكْ بِى شَيْـًٔا وَطَهِّرْ بَيْتِىَ لِلطَّآئِفِينَ وَٱلْقَآئِمِينَ وَٱلرُّكَّعِ ٱلسُّجُودِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pale tulipomweka Ibrahim pahala penye ile Nyumba tukamwambia: Usinishirikishe na chochote; na isafishe Nyumba yangu kwa ajili ya wanaoizunguka kwa kutufu, na wanaokaa hapo kwa ibada, na wanaorukuu, na wanaosujudu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَذِّن فِى ٱلنَّاسِ بِٱلْحَجِّ يَأْتُوكَ رِجَالًا وَعَلَىٰ كُلِّ ضَامِرٍ يَأْتِينَ مِن كُلِّ فَجٍّ عَمِيقٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِّيَشْهَدُوا۟ مَنَٰفِعَ لَهُمْ وَيَذْكُرُوا۟ ٱسْمَ ٱللَّهِ فِىٓ أَيَّامٍ مَّعْلُومَٰتٍ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّنۢ بَهِيمَةِ ٱلْأَنْعَٰمِ فَكُلُوا۟ مِنْهَا وَأَطْعِمُوا۟ ٱلْبَآئِسَ ٱلْفَقِيرَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu juu ya wanyama wa mifugo aliowaruzuku. Basi kuleni katika hao na mlisheni mwenye shida aliye fakiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ لْيَقْضُوا۟ تَفَثَهُمْ وَلْيُوفُوا۟ نُذُورَهُمْ وَلْيَطَّوَّفُوا۟ بِٱلْبَيْتِ ٱلْعَتِيقِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha wajisafishe taka zao, na watimize nadhiri zao, na waizunguke Nyumba ya Kale.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَٰتِ ٱللَّهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُۥ عِندَ رَبِّهِۦ وَأُحِلَّتْ لَكُمُ ٱلْأَنْعَٰمُ إِلَّا مَا يُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَٱجْتَنِبُوا۟ ٱلرِّجْسَ مِنَ ٱلْأَوْثَٰنِ وَٱجْتَنِبُوا۟ قَوْلَ ٱلزُّورِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi hivyo! Na anayevitukuza vitakatifu vya Mwenyezi Mungu, basi hayo ndiyo heri yake mbele ya Mola wake Mlezi. Na mmehalalishiwa wanyama wa mifugo ila wale mliosomewa. Basi jiepusheni na uchafu wa masanamu, na jiepusheni na usemi wa uongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

حُنَفَآءَ لِلَّهِ غَيْرَ مُشْرِكِينَ بِهِۦ وَمَن يُشْرِكْ بِٱللَّهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ ٱلسَّمَآءِ فَتَخْطَفُهُ ٱلطَّيْرُ أَوْ تَهْوِى بِهِ ٱلرِّيحُ فِى مَكَانٍ سَحِيقٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa kumtakasikia Imani Mwenyezi Mungu, bila ya kumshirikisha. Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, basi ni kama kwamba ameporomoka kutoka mbinguni, kisha ndege wakamnyakua au upepo ukamtupa mahali mbali mno.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَٰٓئِرَ ٱللَّهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى ٱلْقُلُوبِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNdiyo hivyo! Na anayetukuza alama za dini za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَكُمْ فِيهَا مَنَٰفِعُ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى ثُمَّ مَحِلُّهَآ إِلَى ٱلْبَيْتِ ٱلْعَتِيقِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKatika hao nyinyi mna manufaa mpaka muda maalumu. Kisha mahali pa kuchinjiwa kwake ni kwenye Nyumba ya Kale.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلِكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنسَكًا لِّيَذْكُرُوا۟ ٱسْمَ ٱللَّهِ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّنۢ بَهِيمَةِ ٱلْأَنْعَٰمِ فَإِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَٰحِدٌ فَلَهُۥٓ أَسْلِمُوا۟ وَبَشِّرِ ٱلْمُخْبِتِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kila umma tumewafanyia mahali pa kuchinjia mihanga ya ibada ili walitaje jina la Mwenyezi Mungu juu ya vile walivyoruzukiwa katika wanyama wa mifugo. Basi Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Kwa hivyo, jisalimisheni kwake tu, na wabashirie wanyenyekevu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَٱلصَّٰبِرِينَ عَلَىٰ مَآ أَصَابَهُمْ وَٱلْمُقِيمِى ٱلصَّلَوٰةِ وَمِمَّا رَزَقْنَٰهُمْ يُنفِقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale ambao, anapotajwa Mwenyezi Mungu, nyoyo zao hutetemeka, na wanavumilia kwa yanayowasibu, na wanashika Sala, na wanatoa katika tulivyowaruzuku.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلْبُدْنَ جَعَلْنَٰهَا لَكُم مِّن شَعَٰٓئِرِ ٱللَّهِ لَكُمْ فِيهَا خَيْرٌ فَٱذْكُرُوا۟ ٱسْمَ ٱللَّهِ عَلَيْهَا صَوَآفَّ فَإِذَا وَجَبَتْ جُنُوبُهَا فَكُلُوا۟ مِنْهَا وَأَطْعِمُوا۟ ٱلْقَانِعَ وَٱلْمُعْتَرَّ كَذَٰلِكَ سَخَّرْنَٰهَا لَكُمْ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ngamia (na ng'ombe) wa zawadi ya Nyumba Tukufu, tumewafanyia kuwa ni kudhihirisha alama za dini ya Mwenyezi Mungu. Kwa hao mna heri nyingi. Basi litajeni jina la Mwenyezi Mungu juu yao wanaposimama kwa safu. Na waangukapo kwenye ubavu, kuleni katika hao na walisheni waliokinai na wanaolazimika kuomba. Ndiyo kama hivi tumewafanya hawa wanyama dhalili kwenu ili mpate kushukuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَن يَنَالَ ٱللَّهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَآؤُهَا وَلَٰكِن يَنَالُهُ ٱلتَّقْوَىٰ مِنكُمْ كَذَٰلِكَ سَخَّرَهَا لَكُمْ لِتُكَبِّرُوا۟ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَىٰكُمْ وَبَشِّرِ ٱلْمُحْسِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNyama zao hazimfikii Mwenyezi Mungu wala damu zao, lakini unamfikia ucha Mungu wenu. Namna hivi tumewadhalilisha kwenu ili mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa alivyowaongoa. Na wabashirie wafanyao mema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱللَّهَ يُدَٰفِعُ عَنِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mwenyezi Mungu huwakinga walioamini. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila haini, mwingi wa kukufuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَٰتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا۟ وَإِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ أُخْرِجُوا۟ مِن دِيَٰرِهِم بِغَيْرِ حَقٍّ إِلَّآ أَن يَقُولُوا۟ رَبُّنَا ٱللَّهُ وَلَوْلَا دَفْعُ ٱللَّهِ ٱلنَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّهُدِّمَتْ صَوَٰمِعُ وَبِيَعٌ وَصَلَوَٰتٌ وَمَسَٰجِدُ يُذْكَرُ فِيهَا ٱسْمُ ٱللَّهِ كَثِيرًا وَلَيَنصُرَنَّ ٱللَّهُ مَن يَنصُرُهُۥٓ إِنَّ ٱللَّهَ لَقَوِىٌّ عَزِيزٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale ambao walitolewa majumbani mwao pasina haki, ila kwa kuwa wanasema: "Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu!" Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingelivunjwa nyumba za watawa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anayemsaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mtukufu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ إِن مَّكَّنَّٰهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ أَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُا۟ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَمَرُوا۟ بِٱلْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا۟ عَنِ ٱلْمُنكَرِ وَلِلَّهِ عَٰقِبَةُ ٱلْأُمُورِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale ambao tukiwapa madaraka katika nchi, hudumisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndiko marejeo ya mambo yote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن يُكَذِّبُوكَ فَقَدْ كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَعَادٌ وَثَمُودُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakikukanusha, basi walikwishakanusha kabla yao watu wa Nuhu, na kina 'Aad na kina Thamud.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَوْمُ إِبْرَٰهِيمَ وَقَوْمُ لُوطٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watu wa Ibrahim na watu wa Luti.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَصْحَٰبُ مَدْيَنَ وَكُذِّبَ مُوسَىٰ فَأَمْلَيْتُ لِلْكَٰفِرِينَ ثُمَّ أَخَذْتُهُمْ فَكَيْفَ كَانَ نَكِيرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watu wa Madiana. Na Musa pia alikanushwa. Nikawapa muda makafiri, kisha nikawatia mkononi. Basi ilikuwaje adhabu yangu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَٰهَا وَهِىَ ظَالِمَةٌ فَهِىَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا وَبِئْرٍ مُّعَطَّلَةٍ وَقَصْرٍ مَّشِيدٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ni miji mingapi iliyokuwa ikidhulumu tuliiangamiza, ikawa imebaki magofu, na visima vilivyoachwa, na majumba yaliyokuwa madhubuti?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَلَمْ يَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَتَكُونَ لَهُمْ قُلُوبٌ يَعْقِلُونَ بِهَآ أَوْ ءَاذَانٌ يَسْمَعُونَ بِهَا فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى ٱلْأَبْصَٰرُ وَلَٰكِن تَعْمَى ٱلْقُلُوبُ ٱلَّتِى فِى ٱلصُّدُورِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawatembei katika ardhi ili wapate kuwa na nyoyo za kuzingatia, au masikio ya kusikilia? Kwani hakika si macho yanayopofuka. Lakini zinazopofuka ni nyoyo zilizomo vifuani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِٱلْعَذَابِ وَلَن يُخْلِفَ ٱللَّهُ وَعْدَهُۥ وَإِنَّ يَوْمًا عِندَ رَبِّكَ كَأَلْفِ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanakuharakisha ulete adhabu, lakini kamwe Mwenyezi Mungu hatakwenda kinyume na ahadi yake. Na hakika siku moja kwa Mola wako Mlezi ni kama miaka elfu mnavyohesabu nyinyi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ أَمْلَيْتُ لَهَا وَهِىَ ظَالِمَةٌ ثُمَّ أَخَذْتُهَا وَإِلَىَّ ٱلْمَصِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni miji mingapi niliipa muda na hali ilikuwa imedhulumu, na kisha nikaitia mkononi? Na kwangu Mimi ndiko marejeo yote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّمَآ أَنَا۠ لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Enyi watu! Hakika mimi ni mwonyaji kwenu niliye dhahiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi walioamini na wakatenda mema watapata kufutiwa dhambi na riziki za ukarimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ سَعَوْا۟ فِىٓ ءَايَٰتِنَا مُعَٰجِزِينَ أُو۟لَٰٓئِكَ أَصْحَٰبُ ٱلْجَحِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanaojitahidi kuzipinga Aya zetu, hao ndio watu wa Motoni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ وَلَا نَبِىٍّ إِلَّآ إِذَا تَمَنَّىٰٓ أَلْقَى ٱلشَّيْطَٰنُ فِىٓ أُمْنِيَّتِهِۦ فَيَنسَخُ ٱللَّهُ مَا يُلْقِى ٱلشَّيْطَٰنُ ثُمَّ يُحْكِمُ ٱللَّهُ ءَايَٰتِهِۦ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hatukumtuma kabla yako Mtume wala Nabii ila anaposoma, Shetani hutumbukiza katika usomi wake. Lakini Mwenyezi Mungu huyaondoa anayoyatia Shetani; kisha Mwenyezi Mungu huzithibitisha Aya zake. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِّيَجْعَلَ مَا يُلْقِى ٱلشَّيْطَٰنُ فِتْنَةً لِّلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَٱلْقَاسِيَةِ قُلُوبُهُمْ وَإِنَّ ٱلظَّٰلِمِينَ لَفِى شِقَاقٍۭ بَعِيدٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni ili alifanye lile analolitia Shetani liwe ni majaribu kwa wale wenye maradhi ndani ya nyoyo zao, na wale ambao nyoyo zao ni ngumu. Na hakika madhalimu wako katika upinzani wa mbali.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلِيَعْلَمَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ أَنَّهُ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَيُؤْمِنُوا۟ بِهِۦ فَتُخْبِتَ لَهُۥ قُلُوبُهُمْ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَهَادِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ili waliopewa elimu wajue kuwa hayo ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi na waamini, na zipate kutua nyoyo zao. Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye anayewaongoa wenye kuamini kwenye njia iliyonyooka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا يَزَالُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فِى مِرْيَةٍ مِّنْهُ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ ٱلسَّاعَةُ بَغْتَةً أَوْ يَأْتِيَهُمْ عَذَابُ يَوْمٍ عَقِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waliokufuru hawataacha kuwa katika wasiwasi kwa hilo mpaka Saa ya Kiyama iwafikie ghafla, au iwafikie adhabu ya Siku Tasa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلْمُلْكُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّهِ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ فَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ فِى جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterUfalme wote siku hiyo utakuwa wa Mwenyezi Mungu. Atahukumu baina yao. Basi walioamini na wakatenda mema, watakuwa katika Bustani zenye neema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَكَذَّبُوا۟ بِـَٔايَٰتِنَا فَأُو۟لَٰٓئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waliokufuru na kuzikanusha Ishara zetu, basi hao watapata adhabu ya kufedhehesha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ هَاجَرُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ثُمَّ قُتِلُوٓا۟ أَوْ مَاتُوا۟ لَيَرْزُقَنَّهُمُ ٱللَّهُ رِزْقًا حَسَنًا وَإِنَّ ٱللَّهَ لَهُوَ خَيْرُ ٱلرَّٰزِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waliohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha wakauawa au wakafa, bila ya shaka Mwenyezi Mungu atawaruzuku riziki njema. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mbora wa wanaoruzuku.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَيُدْخِلَنَّهُم مُّدْخَلًا يَرْضَوْنَهُۥ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَعَلِيمٌ حَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBila ya shaka atawaingiza mahali watakapoparidhia. Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi, Mstahamilivu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ وَمَنْ عَاقَبَ بِمِثْلِ مَا عُوقِبَ بِهِۦ ثُمَّ بُغِىَ عَلَيْهِ لَيَنصُرَنَّهُ ٱللَّهُ إِنَّ ٱللَّهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNdiyo namna hivi. Na anayelipiza mfano wa alivyoadhibiwa, kisha akadhulumiwa, basi hakuna shaka Mwenyezi Mungu atamsaidia. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye maghfira.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ يُولِجُ ٱلَّيْلَ فِى ٱلنَّهَارِ وَيُولِجُ ٱلنَّهَارَ فِى ٱلَّيْلِ وَأَنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌۢ بَصِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu huingiza usiku katika mchana, na huuingiza mchana katika usiku, na ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِۦ هُوَ ٱلْبَٰطِلُ وَأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْعَلِىُّ ٱلْكَبِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye wa kweli, na kwamba wale wanaowaomba badala yake, ni batili, na hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu, Mkubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَتُصْبِحُ ٱلْأَرْضُ مُخْضَرَّةً إِنَّ ٱللَّهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, huoni kwamba Mwenyezi Mungu huteremsha maji kutoka mbinguni, na mara ardhi inakuwa kijani kibichi? Hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole, Mwenye habari zote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَّهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَهُوَ ٱلْغَنِىُّ ٱلْحَمِيدُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi vyake vilivyomo mbinguni na vilivyo katika ardhi. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha, Mwenye kusifiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ سَخَّرَ لَكُم مَّا فِى ٱلْأَرْضِ وَٱلْفُلْكَ تَجْرِى فِى ٱلْبَحْرِ بِأَمْرِهِۦ وَيُمْسِكُ ٱلسَّمَآءَ أَن تَقَعَ عَلَى ٱلْأَرْضِ إِلَّا بِإِذْنِهِۦٓ إِنَّ ٱللَّهَ بِٱلنَّاسِ لَرَءُوفٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, huoni kwamba Mwenyezi Mungu amevidhalilisha kwenu vilivyo katika ardhi, na merikebu zipitazo baharini kwa amri yake, na amezishika mbingu zisianguke juu ya ardhi, ila kwa idhini yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa watu, Mwenye kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَهُوَ ٱلَّذِىٓ أَحْيَاكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ إِنَّ ٱلْإِنسَٰنَ لَكَفُورٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Yeye ndiye aliyewahuisha kisha atawafisha, na kisha atawafufua. Hakika mwanadamu ni mwingi wa kukufuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِّكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنسَكًا هُمْ نَاسِكُوهُ فَلَا يُنَٰزِعُنَّكَ فِى ٱلْأَمْرِ وَٱدْعُ إِلَىٰ رَبِّكَ إِنَّكَ لَعَلَىٰ هُدًى مُّسْتَقِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKila umma tumewawekea ibada zao wanazozishika. Basi wasizozane nawe katika jambo hili. Na waite watu kwenda kwa Mola wako Mlezi. Hakika wewe uko kwenye uongofu ulionyooka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن جَٰدَلُوكَ فَقُلِ ٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا تَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakikujadili, basi sema: Mwenyezi Mungu anajua zaidi mnayoyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱللَّهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ فِيمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama katika hayo mnayohitilafiana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ مَا فِى ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ إِنَّ ذَٰلِكَ فِى كِتَٰبٍ إِنَّ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo mbinguni na katika ardhi? Hakika hayo yamo Kitabuni. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِۦ سُلْطَٰنًا وَمَا لَيْسَ لَهُم بِهِۦ عِلْمٌ وَمَا لِلظَّٰلِمِينَ مِن نَّصِيرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ambavyo hakuviteremshia ushahidi, na ambavyo hawana elimu navyo. Na madhalimu hawatakuwa na wa kuwasaidia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ءَايَٰتُنَا بَيِّنَٰتٍ تَعْرِفُ فِى وُجُوهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱلْمُنكَرَ يَكَادُونَ يَسْطُونَ بِٱلَّذِينَ يَتْلُونَ عَلَيْهِمْ ءَايَٰتِنَا قُلْ أَفَأُنَبِّئُكُم بِشَرٍّ مِّن ذَٰلِكُمُ ٱلنَّارُ وَعَدَهَا ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, utaona chuki katika nyuso za waliokufuru. Hukaribia kuwavamia wale wanaowasomea hizo Aya zetu. Sema: Je, nikuambieni yaliyo mabaya zaidi kuliko haya? Ni Moto. Mwenyezi Mungu amewaahidi waliokufuru, na ni marudio mabaya hayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ضُرِبَ مَثَلٌ فَٱسْتَمِعُوا۟ لَهُۥٓ إِنَّ ٱلَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَن يَخْلُقُوا۟ ذُبَابًا وَلَوِ ٱجْتَمَعُوا۟ لَهُۥ وَإِن يَسْلُبْهُمُ ٱلذُّبَابُ شَيْـًٔا لَّا يَسْتَنقِذُوهُ مِنْهُ ضَعُفَ ٱلطَّالِبُ وَٱلْمَطْلُوبُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi watu! Unapigwa mfano, basi usikilizeni. Hakika wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, hawawezi kuumba hata nzi ijapokuwa watajumuika kwa hilo. Na nzi akiwapokonya kitu, hawawezi kukiokoa kutoka kwake. Amedhoofika kweli huyo mwenye kutaka na mwenye kutakiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا قَدَرُوا۟ ٱللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِۦٓ إِنَّ ٱللَّهَ لَقَوِىٌّ عَزِيزٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHawakumpa taadhima Mwenyezi Mungu anavyostahiki kupewa taadhima. Hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mwenye nguvu, Mtukufu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱللَّهُ يَصْطَفِى مِنَ ٱلْمَلَٰٓئِكَةِ رُسُلًا وَمِنَ ٱلنَّاسِ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌۢ بَصِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu huteua Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرْجَعُ ٱلْأُمُورُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Na kwa Mwenyezi Mungu yatarejeshwa mambo yote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱرْكَعُوا۟ وَٱسْجُدُوا۟ وَٱعْبُدُوا۟ رَبَّكُمْ وَٱفْعَلُوا۟ ٱلْخَيْرَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Rukuuni na sujuduni, na muabuduni Mola wenu Mlezi, na tendeni mema, ili mfanikiwe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَٰهِدُوا۟ فِى ٱللَّهِ حَقَّ جِهَادِهِۦ هُوَ ٱجْتَبَىٰكُمْ وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِى ٱلدِّينِ مِنْ حَرَجٍ مِّلَّةَ أَبِيكُمْ إِبْرَٰهِيمَ هُوَ سَمَّىٰكُمُ ٱلْمُسْلِمِينَ مِن قَبْلُ وَفِى هَٰذَا لِيَكُونَ ٱلرَّسُولُ شَهِيدًا عَلَيْكُمْ وَتَكُونُوا۟ شُهَدَآءَ عَلَى ٱلنَّاسِ فَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱعْتَصِمُوا۟ بِٱللَّهِ هُوَ مَوْلَىٰكُمْ فَنِعْمَ ٱلْمَوْلَىٰ وَنِعْمَ ٱلنَّصِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama inavyostahiki kumfanyia juhudi. Yeye amewateua. Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi Mungu) aliwaita Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur'ani) pia, ili awe Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Swala na toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye mlinzi wenu. Ni mlinzi mzuri kabisa, na msaidizi bora kabisa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70