caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Muminoon, Aya 27

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 74 · 23:27

فَأَوْحَيْنَآ إِلَيْهِ أَنِ ٱصْنَعِ ٱلْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا فَإِذَا جَآءَ أَمْرُنَا وَفَارَ ٱلتَّنُّورُ فَٱسْلُكْ فِيهَا مِن كُلٍّ زَوْجَيْنِ ٱثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيْهِ ٱلْقَوْلُ مِنْهُمْ وَلَا تُخَٰطِبْنِى فِى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓا۟ إِنَّهُم مُّغْرَقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTukamfunulia wahyi kwamba, "Unda jahazi mbele ya macho yetu na ufunuo wetu! Na itakapofika amri yetu na ikafurika tanuri, hapo waingize ndani yake kutoka kwa kila jozi, dume na jike, na ahali zako, isipokuwa yule ambaye katika wao juu yake imekwisha tangulia kauli. Wala usiniongeleshe kuhusu hao waliodhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniTukampa wahyi: Unda jahazi mbele ya macho yetu na uwongozi wetu! Basi itapo fika amri yetu na ikafurika tanuri, hapo waingize ndani yake wa kila namna dume na jike, na ahali zako, isipo kuwa yule ambaye katika wao juu yake imekwisha tangulia kauli. Wala usinitajie hao walio dhulumu. Kwani hao bila ya shaka watazamishwa.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70