Mwanzo › Sura › Sura Al-Anbiyaa
Sura Al-Anbiyaa الأنبياء
Aya 112 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 73
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ ٱقْتَرَبَ لِلنَّاسِ حِسَابُهُمْ وَهُمْ فِى غَفْلَةٍ مُّعْرِضُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Imewakaribia watu hesabu yao, nao wako katika kughafilika wanapuuza.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّن رَّبِّهِم مُّحْدَثٍ إِلَّا ٱسْتَمَعُوهُ وَهُمْ يَلْعَبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hauwajii ukumbusho mpya kutoka kwa Mola wao Mlezi isipokuwa huusikiliza na huku wanafanya mchezo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَاهِيَةً قُلُوبُهُمْ وَأَسَرُّوا۟ ٱلنَّجْوَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ هَلْ هَٰذَآ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ أَفَتَأْتُونَ ٱلسِّحْرَ وَأَنتُمْ تُبْصِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Zimeghafilika nyoyo zao. Na wale waliodhulumu hunong'onezana kwa siri: Ni nani huyu isipokuwa ni mtu tu kama nyinyi! Je, mnauendea uchawi ilhali nyinyi mnaona?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ رَبِّى يَعْلَمُ ٱلْقَوْلَ فِى ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Alisema: Mola wangu Mlezi anayajua yasemwayo mbinguni na katika ardhi. Na Yeye ni Mwenye kusikia yote, Mwenye kujua vyema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
بَلْ قَالُوٓا۟ أَضْغَٰثُ أَحْلَٰمٍۭ بَلِ ٱفْتَرَىٰهُ بَلْ هُوَ شَاعِرٌ فَلْيَأْتِنَا بِـَٔايَةٍ كَمَآ أُرْسِلَ ٱلْأَوَّلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lakini wao walisema: "Hizo ni ndoto za ovyo ovyo, bali amezizua tu, bali huyo ni mtunga mashairi. Basi atuletee miujiza kama walivyotumwa wale wa mwanzo."
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَآ ءَامَنَتْ قَبْلَهُم مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَٰهَآ أَفَهُمْ يُؤْمِنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hawakuamini kabla yao watu wa mji wowote tuliouangamiza. Basi, je, hawa ndio wataamini?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَآ أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِىٓ إِلَيْهِمْ فَسْـَٔلُوٓا۟ أَهْلَ ٱلذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hatukuwatuma kabla yako isipokuwa wanaume tuliowafunulia ufunuo (wahyi). Basi waulizeni wenye elimu ikiwa nyinyi hamjui.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا جَعَلْنَٰهُمْ جَسَدًا لَّا يَأْكُلُونَ ٱلطَّعَامَ وَمَا كَانُوا۟ خَٰلِدِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala hatukuwafanya miili isiyokula chakula, wala hawakuwa wenye kuishi milele.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ثُمَّ صَدَقْنَٰهُمُ ٱلْوَعْدَ فَأَنجَيْنَٰهُمْ وَمَن نَّشَآءُ وَأَهْلَكْنَا ٱلْمُسْرِفِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kisha tukawatimizia miadi, na tukawaokoa wao na wale tuliowataka, na tukawaangamiza wale waliopitiliza mipaka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَقَدْ أَنزَلْنَآ إِلَيْكُمْ كِتَٰبًا فِيهِ ذِكْرُكُمْ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika tumewateremshia Kitabu ambacho ndani yake kuna ukumbusho wenu. Je, hamtumii akili?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَكَمْ قَصَمْنَا مِن قَرْيَةٍ كَانَتْ ظَالِمَةً وَأَنشَأْنَا بَعْدَهَا قَوْمًا ءَاخَرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ni mingapi katika miji iliyokuwa ikidhulumu tumeiteketeza, na tukawaanzisha baada yao kaumu wengine.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَلَمَّآ أَحَسُّوا۟ بَأْسَنَآ إِذَا هُم مِّنْهَا يَرْكُضُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi walipoihisi adhabu yetu, tazama, wakaanza kuikimbia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَا تَرْكُضُوا۟ وَٱرْجِعُوٓا۟ إِلَىٰ مَآ أُتْرِفْتُمْ فِيهِ وَمَسَٰكِنِكُمْ لَعَلَّكُمْ تُسْـَٔلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Msikimbie! Na rejeeni kwenye yale yale mliyostareheshwa kwayo, na maskani zenu, ili mpate kuulizwa!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالُوا۟ يَٰوَيْلَنَآ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakasema: "Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa madhalimu."
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَمَا زَالَت تِّلْكَ دَعْوَىٰهُمْ حَتَّىٰ جَعَلْنَٰهُمْ حَصِيدًا خَٰمِدِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi hakikuacha hicho kuwa ndicho kilio chao mpaka tukawafanya kama waliofyekwa, wamezimika.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا خَلَقْنَا ٱلسَّمَآءَ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَٰعِبِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo baina ya hivyo kwa mchezo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَوْ أَرَدْنَآ أَن نَّتَّخِذَ لَهْوًا لَّٱتَّخَذْنَٰهُ مِن لَّدُنَّآ إِن كُنَّا فَٰعِلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kama tungelitaka kufanya pumbao, tungejifanyia Sisi wenyewe, lau kwamba tungelikuwa ni wafanyao hivyo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
بَلْ نَقْذِفُ بِٱلْحَقِّ عَلَى ٱلْبَٰطِلِ فَيَدْمَغُهُۥ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ وَلَكُمُ ٱلْوَيْلُ مِمَّا تَصِفُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Bali tunaitupa haki juu ya batili, ikaivunja na mara ikatoweka. Na ole wenu kwa mnayoyazua.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَهُۥ مَن فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَنْ عِندَهُۥ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِۦ وَلَا يَسْتَحْسِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ni vyake Yeye tu vilivyomo mbinguni na katika ardhi. Na wale walioko kwake hawafanyi kiburi wakaacha kumuabudu, wala hawachoki.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يُسَبِّحُونَ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ لَا يَفْتُرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wanamtakasa usiku na mchana, wala hawanyong'onyei.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمِ ٱتَّخَذُوٓا۟ ءَالِهَةً مِّنَ ٱلْأَرْضِ هُمْ يُنشِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au wamejifanyia miungu katika ardhi inayofufua?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَوْ كَانَ فِيهِمَآ ءَالِهَةٌ إِلَّا ٱللَّهُ لَفَسَدَتَا فَسُبْحَٰنَ ٱللَّهِ رَبِّ ٱلْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lau wangelikuwamo humo miungu wengine isipokuwa Mwenyezi Mungu, basi bila ya shaka hizo mbingu na ardhi zingeliharibika. Subhanallah (Ametakasika Mwenyezi Mungu), Bwana wa Kiti cha Enzi mbali na hayo wanayoyazua.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَا يُسْـَٔلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْـَٔلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Yeye haulizwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanaoulizwa kwa wayatendayo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمِ ٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةً قُلْ هَاتُوا۟ بُرْهَٰنَكُمْ هَٰذَا ذِكْرُ مَن مَّعِىَ وَذِكْرُ مَن قَبْلِى بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ٱلْحَقَّ فَهُم مُّعْرِضُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au wamejifanyia miungu mingine badala yake? Sema: Leteni ushahidi wenu! Haya ni ukumbusho wa hawa walio pamoja nami, na ukumbusho wa walio kabla yangu. Lakini wengi wao hawaijui haki, na kwa hivyo wanapeana mgongo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِىٓ إِلَيْهِ أَنَّهُۥ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱعْبُدُونِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa tulimfunulia ya kwamba hakuna mungu isipokuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَقَالُوا۟ ٱتَّخَذَ ٱلرَّحْمَٰنُ وَلَدًا سُبْحَٰنَهُۥ بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na walisema: Arrahman (Mwingi wa rehema) alijifanyia mwana! Subhanahu (Ametakasika mbali na hayo!) Bali hao (wanaowaita wana) ni waja waliotukuzwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَا يَسْبِقُونَهُۥ بِٱلْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِۦ يَعْمَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hawamtangulii kwa neno, nao wanafanya amri zake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ ٱرْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِۦ مُشْفِقُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawamfanyii yeyote uombezi isipokuwa yule anayemridhia Yeye, nao kwa sababu ya kumhofu wanaogopa mno.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّىٓ إِلَٰهٌ مِّن دُونِهِۦ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلظَّٰلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na yeyote kati yao atakayesema: "Hakika mimi ni mungu, badala yake", basi huyo tutamlipa Jahannamu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo madhalimu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَوَلَمْ يَرَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَنَّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ كَانَتَا رَتْقًا فَفَتَقْنَٰهُمَا وَجَعَلْنَا مِنَ ٱلْمَآءِ كُلَّ شَىْءٍ حَىٍّ أَفَلَا يُؤْمِنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Je, hao waliokufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibandua? Na tukafanya kwa maji kila kilicho hai? Basi je, hawaamini?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَجَعَلْنَا فِى ٱلْأَرْضِ رَوَٰسِىَ أَن تَمِيدَ بِهِمْ وَجَعَلْنَا فِيهَا فِجَاجًا سُبُلًا لَّعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thabiti ili isiwayumbishe, na tukaweka humo njia pana ili wapate kuongoka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَجَعَلْنَا ٱلسَّمَآءَ سَقْفًا مَّحْفُوظًا وَهُمْ عَنْ ءَايَٰتِهَا مُعْرِضُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyohifadhiwa, lakini wanazipuuza Ishara zake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَهُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ وَٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ كُلٌّ فِى فَلَكٍ يَسْبَحُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Yeye ndiye aliyeumba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا جَعَلْنَا لِبَشَرٍ مِّن قَبْلِكَ ٱلْخُلْدَ أَفَإِي۟ن مِّتَّ فَهُمُ ٱلْخَٰلِدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nasi hatukumfanya mwanadamu yeyote kabla yako kuwa na uhai wa milele. Basi je, ukifa wewe, wao wataishi milele?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كُلُّ نَفْسٍ ذَآئِقَةُ ٱلْمَوْتِ وَنَبْلُوكُم بِٱلشَّرِّ وَٱلْخَيْرِ فِتْنَةً وَإِلَيْنَا تُرْجَعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kila nafsi itaonja mauti; na tunawajaribu kwa mtihani wa maovu na heri. Na kwetu Sisi mtarejeshwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِذَا رَءَاكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَٰذَا ٱلَّذِى يَذْكُرُ ءَالِهَتَكُمْ وَهُم بِذِكْرِ ٱلرَّحْمَٰنِ هُمْ كَٰفِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na wanapokuona wale waliokufuru, hawakufanyi wewe isipokuwa ni kitu cha masihara tu, (wakisema): Je, huyu ndiye anayeitaja miungu yenu? Na hali wao wanakufuru kumkumbuka Arrahman (Mwingi wa rehema)!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
خُلِقَ ٱلْإِنسَٰنُ مِنْ عَجَلٍ سَأُو۟رِيكُمْ ءَايَٰتِى فَلَا تَسْتَعْجِلُونِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mwanadamu ameumbwa na haraka. Nitawaonyesha Ishara zangu. Basi msiniharakishe.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَٰدِقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَوْ يَعْلَمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ حِينَ لَا يَكُفُّونَ عَن وُجُوهِهِمُ ٱلنَّارَ وَلَا عَن ظُهُورِهِمْ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lau wangelijua wale waliokufuru wakati ambao hawatauzuia Moto kwenye nyuso zao wala migongo yao, na wala hawatanusuriwa!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
بَلْ تَأْتِيهِم بَغْتَةً فَتَبْهَتُهُمْ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ رَدَّهَا وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Bali itawafikia kwa ghafla, na itawashitua na wala hawataweza kuirudisha, wala hawatapewa muhula!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَقَدِ ٱسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِٱلَّذِينَ سَخِرُوا۟ مِنْهُم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Mitume walio kabla yako walikwishadhihakiwa. Kwa hivyo wale waliowafanyia masihara yaliwafika yale waliyokuwa wakiyafanyia dhihaka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قُلْ مَن يَكْلَؤُكُم بِٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ مِنَ ٱلرَّحْمَٰنِ بَلْ هُمْ عَن ذِكْرِ رَبِّهِم مُّعْرِضُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sema: Ni nani anayewalinda usiku na mchana mbali na Arrahmani (Mwingi wa rehema)? Bali wao wanapuuza kumkumbuka Mola wao Mlezi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ لَهُمْ ءَالِهَةٌ تَمْنَعُهُم مِّن دُونِنَا لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَ أَنفُسِهِمْ وَلَا هُم مِّنَّا يُصْحَبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au wao wanao miungu watakaoweza kuwakinga kutokana nasi? Hao hawawezi kujinusuru wao wenyewe, wala hawatalindwa kutokana nasi!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
بَلْ مَتَّعْنَا هَٰٓؤُلَآءِ وَءَابَآءَهُمْ حَتَّىٰ طَالَ عَلَيْهِمُ ٱلْعُمُرُ أَفَلَا يَرَوْنَ أَنَّا نَأْتِى ٱلْأَرْضَ نَنقُصُهَا مِنْ أَطْرَافِهَآ أَفَهُمُ ٱلْغَٰلِبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je, hawaoni ya kwamba Sisi tunaijia ardhi tukiipunguza kutokea kwenye ncha zake? Basi je, hao ndio watashinda?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قُلْ إِنَّمَآ أُنذِرُكُم بِٱلْوَحْىِ وَلَا يَسْمَعُ ٱلصُّمُّ ٱلدُّعَآءَ إِذَا مَا يُنذَرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sema: Mimi ninawaonya kwa ufunuo (wahyi). Na viziwi hawasikii wito wanapoonywa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَئِن مَّسَّتْهُمْ نَفْحَةٌ مِّنْ عَذَابِ رَبِّكَ لَيَقُولُنَّ يَٰوَيْلَنَآ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na wanapoguswa na mpulizo mmoja tu wa adhabu itokayo kwa Mola wako Mlezi, bila ya shaka wao husema: Ole wetu! Hakika tulikuwa wenye kudhulumu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَنَضَعُ ٱلْمَوَٰزِينَ ٱلْقِسْطَ لِيَوْمِ ٱلْقِيَٰمَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْـًٔا وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا وَكَفَىٰ بِنَا حَٰسِبِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nasi tutaweka mizani za uadilifu kwa Siku ya Kiyama. Basi nafsi haitadhulumiwa kitu chochote. Hata ikiwa ni uzito wa chembe ya khardali, tutaileta. Nasi tunatosha kuwa wenye kufanya hisabu sawasawa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ ٱلْفُرْقَانَ وَضِيَآءً وَذِكْرًا لِّلْمُتَّقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa yakini tuliwapa Musa na Harun kipambanuzi, na mwangaza, na makumbusho kwa wacha Mungu,
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱلَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِٱلْغَيْبِ وَهُم مِّنَ ٱلسَّاعَةِ مُشْفِقُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ambao wanamhofu Mola wao Mlezi faraghani, na wanaiogopa Saa ya Kiyama.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَهَٰذَا ذِكْرٌ مُّبَارَكٌ أَنزَلْنَٰهُ أَفَأَنتُمْ لَهُۥ مُنكِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na haya ni makumbusho yaliyobarikiwa, tuliyoyateremsha. Basi je! Mnayakataa?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَقَدْ ءَاتَيْنَآ إِبْرَٰهِيمَ رُشْدَهُۥ مِن قَبْلُ وَكُنَّا بِهِۦ عَٰلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika tulikwishampa Ibrahim uongofu wake zamani, na tulikuwa tunamjua.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِۦ مَا هَٰذِهِ ٱلتَّمَاثِيلُ ٱلَّتِىٓ أَنتُمْ لَهَا عَٰكِفُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Alipomwambia baba yake na watu wake: Ni nini haya masanamu mnayoshughulika kuyaabudu?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالُوا۟ وَجَدْنَآ ءَابَآءَنَا لَهَا عَٰبِدِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakasema: Tuliwakuta baba zetu wakiyaabudu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ لَقَدْ كُنتُمْ أَنتُمْ وَءَابَآؤُكُمْ فِى ضَلَٰلٍ مُّبِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Akasema: Bila ya shaka nyinyi na baba zenu mmekuwa katika upotovu ulio dhahiri.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالُوٓا۟ أَجِئْتَنَا بِٱلْحَقِّ أَمْ أَنتَ مِنَ ٱللَّٰعِبِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakasema: Je, umetujia kwa maneno ya kweli au wewe ni katika wachezao tu?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ بَل رَّبُّكُمْ رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ٱلَّذِى فَطَرَهُنَّ وَأَنَا۠ عَلَىٰ ذَٰلِكُم مِّنَ ٱلشَّٰهِدِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Akasema: Bali Mola wenu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ambaye ndiye aliyeziumba. Na mimi ni katika wenye kuyashuhudia hayo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَتَٱللَّهِ لَأَكِيدَنَّ أَصْنَٰمَكُم بَعْدَ أَن تُوَلُّوا۟ مُدْبِرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ninaapa kwa Mwenyezi Mungu! Nitayafanyia vitimbi masanamu yenu haya baada ya mkishageuka kwenda zenu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَجَعَلَهُمْ جُذَٰذًا إِلَّا كَبِيرًا لَّهُمْ لَعَلَّهُمْ إِلَيْهِ يَرْجِعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi akayavunja vipande vipande, ila kubwa lao, ili wao walirudie.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالُوا۟ مَن فَعَلَ هَٰذَا بِـَٔالِهَتِنَآ إِنَّهُۥ لَمِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakasema: Ni nani aliyeifanyia haya miungu yetu? Hakika yeye ni katika waliodhulumu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالُوا۟ سَمِعْنَا فَتًى يَذْكُرُهُمْ يُقَالُ لَهُۥٓ إِبْرَٰهِيمُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakasema: Tumemsikia kijana mmoja akiwataja. Anaitwa Ibrahim.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالُوا۟ فَأْتُوا۟ بِهِۦ عَلَىٰٓ أَعْيُنِ ٱلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَشْهَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakasema: Mleteni mbele ya macho ya watu, ili wapate kumshuhudia!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالُوٓا۟ ءَأَنتَ فَعَلْتَ هَٰذَا بِـَٔالِهَتِنَا يَٰٓإِبْرَٰهِيمُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakasema: Je! Wewe umeifanyia haya miungu yetu, ewe Ibrahim?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ بَلْ فَعَلَهُۥ كَبِيرُهُمْ هَٰذَا فَسْـَٔلُوهُمْ إِن كَانُوا۟ يَنطِقُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Akasema: Bali amefanya hayo huyu mkubwa wao. Basi waulizeni ikiwa wanaweza kutamka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَرَجَعُوٓا۟ إِلَىٰٓ أَنفُسِهِمْ فَقَالُوٓا۟ إِنَّكُمْ أَنتُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi wakajirudia, wakasema: Hakika nyinyi mlikuwa madhalimu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ثُمَّ نُكِسُوا۟ عَلَىٰ رُءُوسِهِمْ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا هَٰٓؤُلَآءِ يَنطِقُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kisha wakarejea kwenye ule ule upotovu wao wakasema: Hakika wewe unajua kwamba hawa hawasemi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ أَفَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُكُمْ شَيْـًٔا وَلَا يَضُرُّكُمْ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Akasema: Basi nyinyi mnawaabudu wasiokuwa Mwenyezi Mungu wasiowafaa kitu wala kuwadhuru?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أُفٍّ لَّكُمْ وَلِمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Aibu yenu nyinyi na hivyo mnavyoviabudu badala ya Mwenyezi Mungu! Basi nyinyi hamtii akilini?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالُوا۟ حَرِّقُوهُ وَٱنصُرُوٓا۟ ءَالِهَتَكُمْ إِن كُنتُمْ فَٰعِلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakasema: Mchomeni moto, na muinusuru miungu yenu, ikiwa nyinyi ni watendao jambo!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قُلْنَا يَٰنَارُ كُونِى بَرْدًا وَسَلَٰمًا عَلَىٰٓ إِبْرَٰهِيمَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sisi tukasema: Ewe moto! Kuwa baridi na salama kwa Ibrahim!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَرَادُوا۟ بِهِۦ كَيْدًا فَجَعَلْنَٰهُمُ ٱلْأَخْسَرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wao walimkusudia maovu, lakini Sisi tukawafanya wao ndio waliohasiri zaidi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَنَجَّيْنَٰهُ وَلُوطًا إِلَى ٱلْأَرْضِ ٱلَّتِى بَٰرَكْنَا فِيهَا لِلْعَٰلَمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tukamwokoa yeye na Luuti, tukawapeleka kwenye nchi tuliyoibariki kwa ajili ya walimwengu wote.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَوَهَبْنَا لَهُۥٓ إِسْحَٰقَ وَيَعْقُوبَ نَافِلَةً وَكُلًّا جَعَلْنَا صَٰلِحِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Naye tukampa Is-haq, na Yaaqub kuwa ni ziada. Na wote tukawafanya kuwa watu wema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَجَعَلْنَٰهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا وَأَوْحَيْنَآ إِلَيْهِمْ فِعْلَ ٱلْخَيْرَٰتِ وَإِقَامَ ٱلصَّلَوٰةِ وَإِيتَآءَ ٱلزَّكَوٰةِ وَكَانُوا۟ لَنَا عَٰبِدِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tukawafanya maimamu wakiongoa watu kwa amri yetu. Na tukawafunulia watende heri, na washike Sala, na watoe Zaka; na walikuwa wanatuabudu Sisi tu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلُوطًا ءَاتَيْنَٰهُ حُكْمًا وَعِلْمًا وَنَجَّيْنَٰهُ مِنَ ٱلْقَرْيَةِ ٱلَّتِى كَانَت تَّعْمَلُ ٱلْخَبَٰٓئِثَ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمَ سَوْءٍ فَٰسِقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Lut tukampa hukumu na elimu na tukamwokoa kutokana na ule mji uliokuwa ukifanya machafu. Hakika hao walikuwa watu wabaya, wavukao mipaka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَدْخَلْنَٰهُ فِى رَحْمَتِنَآ إِنَّهُۥ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tukamuingiza katika rehema yetu. Hakika yeye ni miongoni mwa walio wema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَنُوحًا إِذْ نَادَىٰ مِن قَبْلُ فَٱسْتَجَبْنَا لَهُۥ فَنَجَّيْنَٰهُ وَأَهْلَهُۥ مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Nuhu alipoita zamani, nasi tukamuitikia, na tukamwokoa yeye na watu wake kutokana na shida kubwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَنَصَرْنَٰهُ مِنَ ٱلْقَوْمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَٰتِنَآ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمَ سَوْءٍ فَأَغْرَقْنَٰهُمْ أَجْمَعِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tukamnusuru kutokana na watu waliozikanusha Ishara zetu. Hakika hao walikuwa watu wabaya. Basi tukawazamisha wote.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَدَاوُۥدَ وَسُلَيْمَٰنَ إِذْ يَحْكُمَانِ فِى ٱلْحَرْثِ إِذْ نَفَشَتْ فِيهِ غَنَمُ ٱلْقَوْمِ وَكُنَّا لِحُكْمِهِمْ شَٰهِدِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Daud na Suleiman walipokata hukumu katika suala la konde walipolisha humo mbuzi wa watu usiku. Na Sisi tulikuwa wenye kushuhudia hukumu yao hiyo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَفَهَّمْنَٰهَا سُلَيْمَٰنَ وَكُلًّا ءَاتَيْنَا حُكْمًا وَعِلْمًا وَسَخَّرْنَا مَعَ دَاوُۥدَ ٱلْجِبَالَ يُسَبِّحْنَ وَٱلطَّيْرَ وَكُنَّا فَٰعِلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na elimu. Na tuliifanya milima na ndege kuwa pamoja na Daud imnyenyekee na imtakase Mwenyezi Mungu. Na Sisi ndio tulioyafanya hayo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَعَلَّمْنَٰهُ صَنْعَةَ لَبُوسٍ لَّكُمْ لِتُحْصِنَكُم مِّنۢ بَأْسِكُمْ فَهَلْ أَنتُمْ شَٰكِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tukamfundisha kuunda mavazi ya vita kwa ajili yenu ili yawahifadhi katika kupigana kwenu. Je, mtakuwa wenye kushukuru?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلِسُلَيْمَٰنَ ٱلرِّيحَ عَاصِفَةً تَجْرِى بِأَمْرِهِۦٓ إِلَى ٱلْأَرْضِ ٱلَّتِى بَٰرَكْنَا فِيهَا وَكُنَّا بِكُلِّ شَىْءٍ عَٰلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tukamsahilishia Suleiman upepo wa kimbunga uendao kwa amri yake kwenye ardhi tuliyoibariki. Na Sisi ndio tunaojua kila kitu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمِنَ ٱلشَّيَٰطِينِ مَن يَغُوصُونَ لَهُۥ وَيَعْمَلُونَ عَمَلًا دُونَ ذَٰلِكَ وَكُنَّا لَهُمْ حَٰفِظِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na pia mashetani wanaompigia mbizi na kufanya kazi nyenginezo. Na Sisi tulikuwa walinzi wao.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُۥٓ أَنِّى مَسَّنِىَ ٱلضُّرُّ وَأَنتَ أَرْحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Ayyubu, alipomwita Mola wake Mlezi, akasema: Mimi yamenipata madhara. Na Wewe ndiye unayerehemu kuliko wote wanaorehemu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱسْتَجَبْنَا لَهُۥ فَكَشَفْنَا مَا بِهِۦ مِن ضُرٍّ وَءَاتَيْنَٰهُ أَهْلَهُۥ وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَذِكْرَىٰ لِلْعَٰبِدِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi tukamwitikia, na tukamwondolea madhara aliyokuwa nayo, na tukampa watu wake na mfano wao pamoja nao kuwa ni rehema inayotoka kwetu, na ukumbusho kwa wafanyao ibada.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِسْمَٰعِيلَ وَإِدْرِيسَ وَذَا ٱلْكِفْلِ كُلٌّ مِّنَ ٱلصَّٰبِرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Ismail, na Idris, na Dhulkifli, wote walikuwa miongoni mwa wanaosubiri.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَدْخَلْنَٰهُمْ فِى رَحْمَتِنَآ إِنَّهُم مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tukawaingiza katika rehema yetu. Hakika wao walikuwa katika watu wema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَذَا ٱلنُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَٰضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ فَنَادَىٰ فِى ٱلظُّلُمَٰتِ أَن لَّآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنتَ سُبْحَٰنَكَ إِنِّى كُنتُ مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhabika, na akadhani ya kwamba hatutamtia dhikini. Basi aliita katika giza: Hakuna mungu isipokuwa Wewe Subhanaka (Uliyetakasika). Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱسْتَجَبْنَا لَهُۥ وَنَجَّيْنَٰهُ مِنَ ٱلْغَمِّ وَكَذَٰلِكَ نُـۨجِى ٱلْمُؤْمِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi tukamwitikia na tukamwokoa kutokana na dhiki. Na hivyo ndivyo tunavyowaokoa Waumini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَزَكَرِيَّآ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُۥ رَبِّ لَا تَذَرْنِى فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ ٱلْوَٰرِثِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Zakariya alipomwita Mola wake Mlezi: Mola wangu Mlezi! Usiniache peke yangu, na Wewe ndiye Mbora wa wanaorithi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱسْتَجَبْنَا لَهُۥ وَوَهَبْنَا لَهُۥ يَحْيَىٰ وَأَصْلَحْنَا لَهُۥ زَوْجَهُۥٓ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ يُسَٰرِعُونَ فِى ٱلْخَيْرَٰتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا وَكَانُوا۟ لَنَا خَٰشِعِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi tukamwitikia, na tukampa Yahya na tukamponyeshea mkewe. Hakika wao walikuwa wepesi wa kutenda mema, na wakituomba kwa shauku na hofu. Nao walikuwa wakitunyenyekea.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلَّتِىٓ أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهَا مِن رُّوحِنَا وَجَعَلْنَٰهَا وَٱبْنَهَآ ءَايَةً لِّلْعَٰلَمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na yule mwanamke aliyeulinda uke wake, na tukampulizia katika roho yetu, na tukamfanya yeye na mwanawe kuwa ni Ishara kwa walimwengu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ هَٰذِهِۦٓ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَٰحِدَةً وَأَنَا۠ رَبُّكُمْ فَٱعْبُدُونِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَتَقَطَّعُوٓا۟ أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ كُلٌّ إِلَيْنَا رَٰجِعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nao wakalikata jambo lao hili mapande mapande baina yao. Wote watarudi kwetu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَمَن يَعْمَلْ مِنَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَا كُفْرَانَ لِسَعْيِهِۦ وَإِنَّا لَهُۥ كَٰتِبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na atendaye mema naye ni Muumini, basi haitakataliwa juhudi yake. Na hakika Sisi tunamwandikia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَحَرَٰمٌ عَلَىٰ قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَٰهَآ أَنَّهُمْ لَا يَرْجِعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na haiwi kwa wana mji tuliouangamiza, ya kwamba hawatarejea.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
حَتَّىٰٓ إِذَا فُتِحَتْ يَأْجُوجُ وَمَأْجُوجُ وَهُم مِّن كُلِّ حَدَبٍ يَنسِلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mpaka watakapofunguliwa Yaajuju na Maajuju wakawa wanateremka haraka kutoka kwenye kila kilima.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱقْتَرَبَ ٱلْوَعْدُ ٱلْحَقُّ فَإِذَا هِىَ شَٰخِصَةٌ أَبْصَٰرُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يَٰوَيْلَنَا قَدْ كُنَّا فِى غَفْلَةٍ مِّنْ هَٰذَا بَلْ كُنَّا ظَٰلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Miadi ya haki ikakaribia. Hapo ndipo yatakapokodoka macho ya waliokufuru (na watasema): Ole wetu! Bila ya shaka tulikuwa tumeghafilika mbali na haya, bali tulikuwa wenye kudhulumu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمْ لَهَا وَٰرِدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika nyinyi na hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَوْ كَانَ هَٰٓؤُلَآءِ ءَالِهَةً مَّا وَرَدُوهَا وَكُلٌّ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lau kuwa hawa ni miungu, wasingelingia humo. Na wote watadumu humo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَهُمْ فِيهَا لَا يَسْمَعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lao wao humo ni kupiga mayowe, na wala hawatasikia (jinginelo).
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ ٱلَّذِينَ سَبَقَتْ لَهُم مِّنَّا ٱلْحُسْنَىٰٓ أُو۟لَٰٓئِكَ عَنْهَا مُبْعَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ama wale ambao wema wetu umewatangulia, hao watatenganishwa na hayo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَا يَسْمَعُونَ حَسِيسَهَا وَهُمْ فِى مَا ٱشْتَهَتْ أَنفُسُهُمْ خَٰلِدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hawatausikia mvumo wake, na wao watadumu katika yale ambayo nafsi zao zinayatamani.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَا يَحْزُنُهُمُ ٱلْفَزَعُ ٱلْأَكْبَرُ وَتَتَلَقَّىٰهُمُ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ هَٰذَا يَوْمُكُمُ ٱلَّذِى كُنتُمْ تُوعَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hicho Kitisho Kikubwa hakitawahuzunisha. Na Malaika watawapokea (kwa kuwaambia): Hii ndiyo Siku yenu mliyokuwa mkiahidiwa!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ نَطْوِى ٱلسَّمَآءَ كَطَىِّ ٱلسِّجِلِّ لِلْكُتُبِ كَمَا بَدَأْنَآ أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُۥ وَعْدًا عَلَيْنَآ إِنَّا كُنَّا فَٰعِلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku tutakapozikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi za vitabu. Kama tulivyoanza uumbaji wa mwanzo, tutaurudisha tena. Ni ahadi iliyo juu yetu. Hakika Sisi ni watendao.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَقَدْ كَتَبْنَا فِى ٱلزَّبُورِ مِنۢ بَعْدِ ٱلذِّكْرِ أَنَّ ٱلْأَرْضَ يَرِثُهَا عِبَادِىَ ٱلصَّٰلِحُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika tulikwishaandika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba ardhi watairithi waja wangu walio wema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ فِى هَٰذَا لَبَلَٰغًا لِّقَوْمٍ عَٰبِدِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَآ أَرْسَلْنَٰكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَٰلَمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nasi hatukukutuma ila uwe ni rehema kwa walimwengu wote.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قُلْ إِنَّمَا يُوحَىٰٓ إِلَىَّ أَنَّمَآ إِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَٰحِدٌ فَهَلْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sema: Hakika imefunuliwa kwangu ya kwamba hakika Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Je, Mmesilimu?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَقُلْ ءَاذَنتُكُمْ عَلَىٰ سَوَآءٍ وَإِنْ أَدْرِىٓ أَقَرِيبٌ أَم بَعِيدٌ مَّا تُوعَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kama wakigeuka, basi sema: Nimewatangazieni sawa sawa, wala sijui yako karibu au mbali hayo mliyoahidiwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّهُۥ يَعْلَمُ ٱلْجَهْرَ مِنَ ٱلْقَوْلِ وَيَعْلَمُ مَا تَكْتُمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Yeye anajua kauli ya dhahiri na anajua myafichayo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِنْ أَدْرِى لَعَلَّهُۥ فِتْنَةٌ لَّكُمْ وَمَتَٰعٌ إِلَىٰ حِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala sijui pengine huu ni mtihani tu kwenu na starehe mpaka muda kidogo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَٰلَ رَبِّ ٱحْكُم بِٱلْحَقِّ وَرَبُّنَا ٱلرَّحْمَٰنُ ٱلْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sema: Mola wangu Mlezi! Hukumu kwa haki. Na Mola wetu Mlezi ndiye Mwingi wa rehema, aombwaye msaada juu ya mnayoyazua.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Taa-Haa
Sura Al-Hajj →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.