Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi vyake vyote vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi, na vilivyo baina yake, na vilivyo chini ya ardhi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hakuna mungu isipokuwa Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na udumishe Swala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Hii ni fimbo yangu; ninaiegemea na ninawaangushia majani kwayo kondoo na mbuzi wangu. Tena inanifaa kwa matumizi mengine.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterYa kuwa mtie katika kisanduku, na kisha kitie mtoni, na mto utamfikisha ufukweni. Atamchukua adui yangu naye ni adui yake. Na nimekutilia mapenzi yanayotoka kwangu, na ili ulelewe machoni mwangu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterDada yako alipokwenda na akasema: Je! Niwajulishe mtu wa kuweza kumlea? Basi tukakurejesha kwa mama yako ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na ulimuua mtu, nasi tukakuokoa katika dhiki, na tukakujaribu kwa majaribio mengi. Ukakaa miaka kwa watu wa Madyana. Kisha ukaja kama ilivyokadiriwa, ewe Musa!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mwendeeni, na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi! Basi waache Wana wa Israili watoke nasi, wala usiwaadhibu. Sisi tumekuletea ishara itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na amani iwe juu ya atakayefuata uongofu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbaye amewafanyia ardhi kuwa tandiko, na akawapitishia humo njia, na akawateremshia kutoka mbinguni maji. Na kwa hayo tukatoa namna mbalimbali za mimea.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi sisi hakika tutakuletea uchawi kama huo. Basi weka miadi baina yetu na wewe, ambayo tusiivunje sisi wala wewe, mahali patakapokuwa sawa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMusa akawaambia: Ole wenu! Msimzulie Mwenyezi Mungu uongo, akaja kuwafutilia mbali kwa adhabu. Na hakika mwenye kuzua lazima ashindwe!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Hakika hawa wawili ni wachawi, wanataka kuwatoa katika nchi yenu kwa uchawi wao, na waondoe mila zenu zilizo bora kabisa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hivyo kusanyeni hila zenu zote, kisha mfike kwa kujipanga safu, na kwa yakini atafuzu kweli kweli leo atakayeshinda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Bali tupeni nyinyi! Tahamaki! Kamba zao na fimbo zao zikaonekana mbele yake, kwa uchawi wao, kuwa zinakwenda mbio.
Swahili Translation - Rowad Translation Center(Firauni) akasema: Oh! Mmemuamini kabla ya mimi kuwapa ruhusa? Hakika yeye ndiye mkubwa wenu aliyewafundisha uchawi huu. Basi kwa yakini nitawakatakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha. Na lazima nitawatundika misalabani katika vigogo vya mitende, na hapo kwa yakini mtajua ni nani katika sisi ndiye mkali zaidi wa kuadhibu na kuiendeleza zaidi adhabu yake.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Hatutakupendelea wewe kuliko ishara waziwazi zilizotujia, na kuliko yule aliyetuumba. Basi hukumu utavyohukumu; kwani wewe hakika unahukumu tu haya ya maisha ya duniani.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika sisi tumemuamini Mola wetu Mlezi ili atusamehe makosa yetu na uchawi uliotulazimisha kuufanya. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mbora na Mwenye kudumu zaidi (katika kuadhibu).
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika atakayemjia Mola wake Mlezi naye ni mhalifu, basi kwa yakini, yake huyo ni Jahannamu. Hafi humo wala haishi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi Wana wa Israili! Hakika tuliwaokoa kutokana na adui yenu, na tukawaahidi upande wa kulia wa mlima na tukawateremshia Manna na Salwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na kusikitika. Akasema: Enyi watu wangu! Kwani Mola wenu Mlezi hakuwaahidi ahadi nzuri? Je, umekuwa muda mrefu kwenu au mmetaka ghadhabu ya Mola wenu Mlezi iwashukie, ndiyo maana mkavunja miadi yangu?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Sisi hatukuvunja miadi yako kwa hiari yetu, lakini tulibebeshwa mizigo ya mapambo ya watu, basi tukaitupa. Na hivyo ndivyo alivyotupa yule Msamaria.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akawaundia ndama, kiwiliwili chenye sauti. Na wakasema: Huyu ndiye mungu wenu, na mungu wa Musa, lakini alisahau.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Harun alikwishawaambia kabla yake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmetiwa mtihanini tu kwa kitu hiki. Na kwa yakini Mola wenu Mlezi ni Arrahmani (Mwingi wa rehema). Basi nifuateni mimi, na tiini amri yangu!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu. Kwa hakika naliogopa usijesema: Umewatenganisha Wana wa Israili, na hukungojea kauli yangu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Niliona wasiyoyaona wao, nikachukua mkamato wa mkono katika athari za unyayo wa Mtume. Kisha nikaitupa. Na hivi ndivyo ilivyonielekeza nafsi yangu.
Swahili Translation - Rowad Translation Center(Musa) akasema: Basi ondoka! Na kwa yakini utakuwa katika maisha ukisema: Usiniguse. Na hakika una ahadi kwako isiyovunjwa. Na mtazame huyo mungu wako uliyeendelea kumuabudu. Sisi kwa hakika tutamchoma moto, kisha tutamtawanya sawasawa baharini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika mungu wenu ni Allah (Mwenyezi Mungu) tu. Hakuna mungu isipokuwa Yeye. Amekienea kila kitu kwa elimu yake.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNamna hivi tunakuhadithia katika khabari za yaliyotangulia. Na hakika tumekuletea kutoka kwetu mawaidha ya kukumbukwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSisi tunajua zaidi watakayoyasema, atakaposema mbora wao katika mwendo: Nyinyi hamkukaa ila siku moja tu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku hiyo watamfuata muitaji huyo bila ya yeyote kumkengeuka. Na sauti zote zitamnyenyekea Arrahmani (Mwingi wa rehema). Basi hutasikia ila mnong'ono tu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku hiyo uombezi hautafaa kitu, ila kwa atakayeruhusiwa na Arrahmani (Mwingi wa rehema) na akaridhia na maneno yake.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa zitadhalilika nyuso mbele ya Aliye Hai milele, Msimamia yote milele. Na atakuwa ameharibikiwa mwenye kubeba dhuluma.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa namna hivi tumeiteremsha Qur-ani kwa Kiarabu, na tumekariri humo vitisho ili wapate kuogopa na kujilinda na iwaletee makumbusho.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki. Wala usiifanyie haraka hii Qur-ani, kabla haujamalizika ufunuo wake. Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie elimu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterTukasema: Ewe Adam! Hakika huyu ni adui yako na wa mkeo. Basi asiwatoe katika Bustani hii, mkaingia mashakani.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakaula wote wawili, na uchi wao ukawadhihirikia na wakaanza kujibandika majani ya Bustanini. Na Adam akamuasi Mola wake Mlezi, na akapotea njia.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Ondokeni humo nyote, hali ya kuwa ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Na ukiwafikia uongofu kutoka kwangu basi atakayeufuata uongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa atakayeupa ukumbusho wangu mgongo, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa ni kipofu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hivyo ndivyo tutakavyomlipa kila apitaye kiasi, na asiziamini ishara za Mola wake Mlezi. Na hakika adhabu ya Akhera ni kali zaidi, na inadumu zaidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, haikuwabainikia ni ngapi katika vizazi tuliviangamiza kabla yao, nao wanatembea katika maskani zao? Hakika katika hayo zimo ishara kwa wenye akili.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa si neno lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi na muda uliowekwa, bila ya shaka ingefika adhabu (duniani).
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi yavumilie haya wayasemayo. Na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumsifu kabla ya kuchomoza jua, na kabla ya kuzama kwake, na nyakati za usiku pia umtakase, na nyakati za mwisho za mchana ili upate ya kukuridhisha.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala kamwe usivikodolee macho tulivyowastarehesha kwavyo baadhi ya watu miongoni mwao, kwa ajili ya mapambo ya duniani, ili tuwajaribu katika hivyo. Na riziki ya Mola wako Mlezi ni bora na yenye kudumu zaidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waamrishe ahali zako kuswali, na usubiri juu yake. Sisi hatukuombi wewe riziki, bali Sisi ndio tunakuruzuku. Na mwisho mwema ni kwa ucha Mungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walisema: "Kwa nini hakutuletea muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi?" Je, haukuwajia ushahidi wazi wa yaliyo katika Vitabu vya mwanzo?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa tuliwaangamiza kwa adhabu kabla yake, wangelisema: Ewe Mola wetu Mlezi! Kama ungetuletea Mtume (ingekuwa bora), tukazifuata ishara zako kabla ya kudhalilika na kuhizika.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Kila mmoja anangoja. Basi ngojeni! Hivi karibuni mtajua ni akina nani ndio wenye njia sawa na ni nani aliyeongoka.