Mwanzo › Sura › Sura Maryam
Sura Maryam مريم
Aya 98 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 44
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ كٓهيعٓصٓ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kaf Ha Ya 'Ayn Swad.[1]
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ذِكْرُ رَحْمَتِ رَبِّكَ عَبْدَهُۥ زَكَرِيَّآ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Huu ni ukumbusho wa rehema ya Mola wako Mlezi kwa mja wake, Zakariya.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُۥ نِدَآءً خَفِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Alipomwita Mola wake Mlezi kwa siri.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ رَبِّ إِنِّى وَهَنَ ٱلْعَظْمُ مِنِّى وَٱشْتَعَلَ ٱلرَّأْسُ شَيْبًا وَلَمْ أَكُنۢ بِدُعَآئِكَ رَبِّ شَقِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi, mifupa yangu imedhoofika, na kichwa kinametameta kwa mvi; wala, Mola wangu Mlezi, sikuwa mwenye bahati mbaya kwa kukuomba Wewe.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِنِّى خِفْتُ ٱلْمَوَٰلِىَ مِن وَرَآءِى وَكَانَتِ ٱمْرَأَتِى عَاقِرًا فَهَبْ لِى مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika mimi ninawahofia wasimamizi wa baada yangu. Na mke wangu ni tasa. Basi nitunuku mrithi kutoka kwako.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَرِثُنِى وَيَرِثُ مِنْ ءَالِ يَعْقُوبَ وَٱجْعَلْهُ رَبِّ رَضِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Anirithi na awarithi ukoo wa Yaaqub. Na umjaalie ewe Mola wangu Mlezi awe mwenye kuridhisha.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَٰزَكَرِيَّآ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَٰمٍ ٱسْمُهُۥ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَل لَّهُۥ مِن قَبْلُ سَمِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center (Akaambiwa): Ewe Zakariya! Hakika Sisi tunakubashiria mwana; jina lake ni Yahya. Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِى غُلَٰمٌ وَكَانَتِ ٱمْرَأَتِى عَاقِرًا وَقَدْ بَلَغْتُ مِنَ ٱلْكِبَرِ عِتِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Vipi nitakuwa na mwana na ilhali mke wangu ni tasa, na mimi nimeshafikia ukongwe katika uzee?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ كَذَٰلِكَ قَالَ رَبُّكَ هُوَ عَلَىَّ هَيِّنٌ وَقَدْ خَلَقْتُكَ مِن قَبْلُ وَلَمْ تَكُ شَيْـًٔا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Akasema: Hivyo ndivyo alivyosema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu. Na hakika Mimi nilikwishakuumba wewe zamani na wala hukuwa kitu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ رَبِّ ٱجْعَل لِّىٓ ءَايَةً قَالَ ءَايَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ ٱلنَّاسَ ثَلَٰثَ لَيَالٍ سَوِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Akasema: Mola wangu Mlezi nijaalie Ishara. Akasema: Ishara yako ni kuwa hutasema na watu kwa usiku tatu, na ilhali u mzima sawasawa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِۦ مِنَ ٱلْمِحْرَابِ فَأَوْحَىٰٓ إِلَيْهِمْ أَن سَبِّحُوا۟ بُكْرَةً وَعَشِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi akawatokea kaumu yake kutoka mihirabuni. Akawaashiria kwamba: Msabihini Mwenyezi Mungu asubuhi na jioni.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَٰيَحْيَىٰ خُذِ ٱلْكِتَٰبَ بِقُوَّةٍ وَءَاتَيْنَٰهُ ٱلْحُكْمَ صَبِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ewe Yahya! Kishike Kitabu kwa nguvu! Nasi tulimpa hekima angali mtoto.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَحَنَانًا مِّن لَّدُنَّا وَزَكَوٰةً وَكَانَ تَقِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tukampa huruma itokayo kwetu, na utakaso, na akawa mcha Mungu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَبَرًّۢا بِوَٰلِدَيْهِ وَلَمْ يَكُن جَبَّارًا عَصِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na akawa mwema kwa wazazi wake, wala hakuwa jabari muasi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَسَلَٰمٌ عَلَيْهِ يَوْمَ وُلِدَ وَيَوْمَ يَمُوتُ وَيَوْمَ يُبْعَثُ حَيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na salama iwe juu yake siku ya kuzaliwa, na siku ya kufa, na siku ya kufufuliwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱذْكُرْ فِى ٱلْكِتَٰبِ مَرْيَمَ إِذِ ٱنتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipojitenga mbali na jamaa zake mahali upande wa mashariki.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱتَّخَذَتْ مِن دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَآ إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na akaweka pazia kujikinga nao. Basi tukamtumia Roho wetu, naye akajifananisha kwake sawa sawa na mtu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَتْ إِنِّىٓ أَعُوذُ بِٱلرَّحْمَٰنِ مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center (Maryamu) akasema: Hakika mimi ninajikinga kwa Mwingi wa rehema aniepushe nawe, ikiwa wewe ni mcha Mungu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ إِنَّمَآ أَنَا۠ رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَٰمًا زَكِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center (Malaika huyo) akasema: Hakika mimi ni mtume tu kutoka kwa Mola wako Mlezi ili nikutunuku mwana aliyetakasika.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَتْ أَنَّىٰ يَكُونُ لِى غُلَٰمٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِى بَشَرٌ وَلَمْ أَكُ بَغِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Akasema: Nitampataje mwana ilhali mtu yeyote hajawahi kunigusa, wala sikuwahi kuwa kahaba?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَىَّ هَيِّنٌ وَلِنَجْعَلَهُۥٓ ءَايَةً لِّلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِّنَّا وَكَانَ أَمْرًا مَّقْضِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center (Malaika) akasema: Hivyo ndiyo alivyosema Mola wako Mlezi: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na rehema kutoka kwetu, na hilo ni jambo lililokwishahukumiwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَحَمَلَتْهُ فَٱنتَبَذَتْ بِهِۦ مَكَانًا قَصِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَأَجَآءَهَا ٱلْمَخَاضُ إِلَىٰ جِذْعِ ٱلنَّخْلَةِ قَالَتْ يَٰلَيْتَنِى مِتُّ قَبْلَ هَٰذَا وَكُنتُ نَسْيًا مَّنسِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kisha uchungu wa kuzaa ukamlazimu kwenda kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya, na nikawa niliyesahaulika kabisa!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَنَادَىٰهَا مِن تَحْتِهَآ أَلَّا تَحْزَنِى قَدْ جَعَلَ رَبُّكِ تَحْتَكِ سَرِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa hivyo, akamnadi kutokea chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi ameshafanya chini yako kijito kidogo cha maji!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَهُزِّىٓ إِلَيْكِ بِجِذْعِ ٱلنَّخْلَةِ تُسَٰقِطْ عَلَيْكِ رُطَبًا جَنِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَكُلِى وَٱشْرَبِى وَقَرِّى عَيْنًا فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ ٱلْبَشَرِ أَحَدًا فَقُولِىٓ إِنِّى نَذَرْتُ لِلرَّحْمَٰنِ صَوْمًا فَلَنْ أُكَلِّمَ ٱلْيَوْمَ إِنسِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi kula, na kunywa, na litulize jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote, basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwingi wa rehema, ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu yeyote.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَأَتَتْ بِهِۦ قَوْمَهَا تَحْمِلُهُۥ قَالُوا۟ يَٰمَرْيَمُ لَقَدْ جِئْتِ شَيْـًٔا فَرِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi akaenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu sana!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَٰٓأُخْتَ هَٰرُونَ مَا كَانَ أَبُوكِ ٱمْرَأَ سَوْءٍ وَمَا كَانَتْ أُمُّكِ بَغِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu mbaya, wala mama yako hakuwa kahaba.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَأَشَارَتْ إِلَيْهِ قَالُوا۟ كَيْفَ نُكَلِّمُ مَن كَانَ فِى ٱلْمَهْدِ صَبِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa hivyo, akamuashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeshe aliye bado mtoto mdogo yumo katika mlezi?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ إِنِّى عَبْدُ ٱللَّهِ ءَاتَىٰنِىَ ٱلْكِتَٰبَ وَجَعَلَنِى نَبِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center (Mtoto huyo) akasema: Hakika mimi ni mja wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَجَعَلَنِى مُبَارَكًا أَيْنَ مَا كُنتُ وَأَوْصَٰنِى بِٱلصَّلَوٰةِ وَٱلزَّكَوٰةِ مَا دُمْتُ حَيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na amenifanya ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Swala na Zaka maadamu ni hai.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَبَرًّۢا بِوَٰلِدَتِى وَلَمْ يَجْعَلْنِى جَبَّارًا شَقِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلسَّلَٰمُ عَلَىَّ يَوْمَ وُلِدتُّ وَيَوْمَ أَمُوتُ وَيَوْمَ أُبْعَثُ حَيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na amani iko juu yangu siku niliyozaliwa, na siku nitakayokufa, na siku nitakayofufuliwa kuwa hai.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ذَٰلِكَ عِيسَى ٱبْنُ مَرْيَمَ قَوْلَ ٱلْحَقِّ ٱلَّذِى فِيهِ يَمْتَرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَا كَانَ لِلَّهِ أَن يَتَّخِذَ مِن وَلَدٍ سُبْحَٰنَهُۥٓ إِذَا قَضَىٰٓ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kujifanyia mwana, Subhanahu (Yeye ametakasika)! Anapolihukumia jambo, basi hakika huliambia tu: "Kuwa!" Na linakuwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِنَّ ٱللَّهَ رَبِّى وَرَبُّكُمْ فَٱعْبُدُوهُ هَٰذَا صِرَٰطٌ مُّسْتَقِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Hii ndiyo njia iliyonyooka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱخْتَلَفَ ٱلْأَحْزَابُ مِنۢ بَيْنِهِمْ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن مَّشْهَدِ يَوْمٍ عَظِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lakini makundi yakahitilafiana wao kwa wao. Basi ole wao hao waliokufuru kwa kuhudhuria Siku iliyo kuu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَسْمِعْ بِهِمْ وَأَبْصِرْ يَوْمَ يَأْتُونَنَا لَٰكِنِ ٱلظَّٰلِمُونَ ٱلْيَوْمَ فِى ضَلَٰلٍ مُّبِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Watasikia na wataona vizuri vilivyoje Siku watakayotujia! Lakini madhalimu sasa wamo katika upotovu ulio dhahiri.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ ٱلْحَسْرَةِ إِذْ قُضِىَ ٱلْأَمْرُ وَهُمْ فِى غَفْلَةٍ وَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na waonye siku ya majuto makubwa itapokatwa amri. Nao wako katika ghafla, wala hawaamini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّا نَحْنُ نَرِثُ ٱلْأَرْضَ وَمَنْ عَلَيْهَا وَإِلَيْنَا يُرْجَعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Sisi ndio tutairithi ardhi na wale walio juu yake. Na kwetu watarejeshwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱذْكُرْ فِى ٱلْكِتَٰبِ إِبْرَٰهِيمَ إِنَّهُۥ كَانَ صِدِّيقًا نَّبِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na mtaje katika Kitabu hiki Ibrahim. Hakika yeye alikuwa mkweli mno, na Nabii.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ يَٰٓأَبَتِ لِمَ تَعْبُدُ مَا لَا يَسْمَعُ وَلَا يُبْصِرُ وَلَا يُغْنِى عَنكَ شَيْـًٔا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Alipomwambia baba yake: Ewe baba yangu! Kwa nini unaabudu visivyosikia, na visivyoona, na visivyokufaa chochote?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَٰٓأَبَتِ إِنِّى قَدْ جَآءَنِى مِنَ ٱلْعِلْمِ مَا لَمْ يَأْتِكَ فَٱتَّبِعْنِىٓ أَهْدِكَ صِرَٰطًا سَوِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ewe baba yangu! Kwa yakini imenifikia elimu ambayo haikukujia wewe. Basi nifuate mimi, nami nitakuongoza njia iliyo sawa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَٰٓأَبَتِ لَا تَعْبُدِ ٱلشَّيْطَٰنَ إِنَّ ٱلشَّيْطَٰنَ كَانَ لِلرَّحْمَٰنِ عَصِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ewe baba yangu! Usimuabudu Shetani. Hakika Shetani ni mwenye kumuasi sana Mwingi wa rehema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَٰٓأَبَتِ إِنِّىٓ أَخَافُ أَن يَمَسَّكَ عَذَابٌ مِّنَ ٱلرَّحْمَٰنِ فَتَكُونَ لِلشَّيْطَٰنِ وَلِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ewe baba yangu! Hakika mimi ninahofu ije kukupata adhabu inayotoka kwa Mwingi wa rehema, ukaja kuwa mwenziwe Shetani.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ أَرَاغِبٌ أَنتَ عَنْ ءَالِهَتِى يَٰٓإِبْرَٰهِيمُ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ لَأَرْجُمَنَّكَ وَٱهْجُرْنِى مَلِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center (Baba) akasema: Je huitaki miungu yangu, ewe Ibrahim? Kama huachi, basi lazima nitakupiga mawe. Na niondokee mbali kwa muda mrefu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالَ سَلَٰمٌ عَلَيْكَ سَأَسْتَغْفِرُ لَكَ رَبِّىٓ إِنَّهُۥ كَانَ بِى حَفِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center (Ibrahim) akasema: Salamun 'alaika (Amani iwe juu yako)! Mimi nitakuombea msamaha kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ananihurumia sana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَعْتَزِلُكُمْ وَمَا تَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَأَدْعُوا۟ رَبِّى عَسَىٰٓ أَلَّآ أَكُونَ بِدُعَآءِ رَبِّى شَقِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nami ninajitenga mbali nanyi na hayo mnayoyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Na ninamwomba Mola wangu Mlezi; asaa nisiwe mwenye kukosa bahati kwa kumwomba Mola wangu Mlezi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَلَمَّا ٱعْتَزَلَهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَهَبْنَا لَهُۥٓ إِسْحَٰقَ وَيَعْقُوبَ وَكُلًّا جَعَلْنَا نَبِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi alipojitenga mbali nao na yale waliyokuwa wakiyaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, tukamtunuku Is-haq na Yaaqub, na kila mmoja wao tukamfanya Nabii.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَوَهَبْنَا لَهُم مِّن رَّحْمَتِنَا وَجَعَلْنَا لَهُمْ لِسَانَ صِدْقٍ عَلِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tukawatunuku katika rehema zetu na tukawafanya kupewa sifa za kweli tukufu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱذْكُرْ فِى ٱلْكِتَٰبِ مُوسَىٰٓ إِنَّهُۥ كَانَ مُخْلَصًا وَكَانَ رَسُولًا نَّبِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na mtaje Musa katika Kitabu. Hakika yeye alikuwa ni mwenye kuchaguliwa, na alikuwa Mtume, Nabii.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَنَٰدَيْنَٰهُ مِن جَانِبِ ٱلطُّورِ ٱلْأَيْمَنِ وَقَرَّبْنَٰهُ نَجِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tulimwitia upande wa kulia wa mlima na tukamsogeza kunong'ona naye.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَوَهَبْنَا لَهُۥ مِن رَّحْمَتِنَآ أَخَاهُ هَٰرُونَ نَبِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nasi kwa rehema zetu tukamtunuku kakaye, Harun, awe Nabii.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱذْكُرْ فِى ٱلْكِتَٰبِ إِسْمَٰعِيلَ إِنَّهُۥ كَانَ صَادِقَ ٱلْوَعْدِ وَكَانَ رَسُولًا نَّبِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na mtaje katika Kitabu Ismail. Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi, na alikuwa Mtume, Nabii.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَكَانَ يَأْمُرُ أَهْلَهُۥ بِٱلصَّلَوٰةِ وَٱلزَّكَوٰةِ وَكَانَ عِندَ رَبِّهِۦ مَرْضِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na alikuwa akiwaamrisha ahali zake Swala na Zaka, na alikuwa mbele ya Mola wake Mlezi mwenye kuridhiwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱذْكُرْ فِى ٱلْكِتَٰبِ إِدْرِيسَ إِنَّهُۥ كَانَ صِدِّيقًا نَّبِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na mtaje katika Kitabu Idris. Hakika yeye alikuwa ni mkweli mno, Nabii.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَرَفَعْنَٰهُ مَكَانًا عَلِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tulimuinua mahali pa juu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أُو۟لَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ أَنْعَمَ ٱللَّهُ عَلَيْهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ مِن ذُرِّيَّةِ ءَادَمَ وَمِمَّنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ وَمِن ذُرِّيَّةِ إِبْرَٰهِيمَ وَإِسْرَٰٓءِيلَ وَمِمَّنْ هَدَيْنَا وَٱجْتَبَيْنَآ إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ءَايَٰتُ ٱلرَّحْمَٰنِ خَرُّوا۟ سُجَّدًا وَبُكِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hao ndio aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii katika uzao wa Adam, na katika uzao wa wale tuliowabeba pamoja na Nuhu, na katika uzao wa Ibrahim na Israili, na katika wale tuliowaongoa na tukawateua. Wanaposomewa Aya za Mwingi wa rehema, huanguka kusujudu na kulia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَخَلَفَ مِنۢ بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَٱتَّبَعُوا۟ ٱلشَّهَوَٰتِ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lakini wakaja baada yao wafuatizi walioipoteza Swala, na wakafuata matamanio. Basi watakujakuta malipo ya ubaya.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِلَّا مَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحًا فَأُو۟لَٰٓئِكَ يَدْخُلُونَ ٱلْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ شَيْـًٔا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Isipokuwa mwenye kutubu, akaamini, na akatenda mema. Hao basi, wataingia Bustanini wala hawatadhulumiwa chochote.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
جَنَّٰتِ عَدْنٍ ٱلَّتِى وَعَدَ ٱلرَّحْمَٰنُ عِبَادَهُۥ بِٱلْغَيْبِ إِنَّهُۥ كَانَ وَعْدُهُۥ مَأْتِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Bustani za milele ambazo aliwaahidi Rahmani (Mwingi wa rehema) waja wake katika ghaibu. Hakika Yeye ahadi yake hakuna shaka itafika.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا إِلَّا سَلَٰمًا وَلَهُمْ رِزْقُهُمْ فِيهَا بُكْرَةً وَعَشِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Humo hawatasikia upuuzi wowote, isipokuwa salama tu. Na watapata humo riziki zao asubuhi na jioni.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
تِلْكَ ٱلْجَنَّةُ ٱلَّتِى نُورِثُ مِنْ عِبَادِنَا مَن كَانَ تَقِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hiyo ndiyo Bustani tutakayowarithisha katika waja wetu wale waliokuwa wacha Mungu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا نَتَنَزَّلُ إِلَّا بِأَمْرِ رَبِّكَ لَهُۥ مَا بَيْنَ أَيْدِينَا وَمَا خَلْفَنَا وَمَا بَيْنَ ذَٰلِكَ وَمَا كَانَ رَبُّكَ نَسِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala hatuteremki isipokuwa kwa amri ya Mola wako Mlezi. Ni yake Yeye yaliyoko mbele yetu na yaliyoko nyuma yetu, na yaliyomo katikati ya hayo. Na Mola wako Mlezi si mwenye kusahau.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَٱعْبُدْهُ وَٱصْطَبِرْ لِعِبَٰدَتِهِۦ هَلْ تَعْلَمُ لَهُۥ سَمِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo kati yake. Basi muabudu Yeye tu, na usubiri katika kumuabudu. Je, unajua chochote kilicho sawa naye?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَيَقُولُ ٱلْإِنسَٰنُ أَءِذَا مَا مِتُّ لَسَوْفَ أُخْرَجُ حَيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na mwanadamu husema: Hivyo, nitakapokufa, ni kweli nitafufuliwa niwe hai tena?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَوَلَا يَذْكُرُ ٱلْإِنسَٰنُ أَنَّا خَلَقْنَٰهُ مِن قَبْلُ وَلَمْ يَكُ شَيْـًٔا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Je, hakumbuki mwanadamu ya kwamba hakika tulimuumba kabla, na wala hakuwa chochote?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَوَرَبِّكَ لَنَحْشُرَنَّهُمْ وَٱلشَّيَٰطِينَ ثُمَّ لَنُحْضِرَنَّهُمْ حَوْلَ جَهَنَّمَ جِثِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi ninaapa kwa Mola wako Mlezi! Kwa yakini tutawakusanya wao pamoja na mashetani. Kisha tutawahudhurisha kuizunguka Jahannamu huku wamepiga magoti!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ثُمَّ لَنَنزِعَنَّ مِن كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمْ أَشَدُّ عَلَى ٱلرَّحْمَٰنِ عِتِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kisha kwa yakini tutaondoa katika kila kundi wale miongoni mwao waliozidi kumuasi Arrahmani (Mwingi wa rehema).
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ثُمَّ لَنَحْنُ أَعْلَمُ بِٱلَّذِينَ هُمْ أَوْلَىٰ بِهَا صِلِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Tena hakika Sisi tunawajua vyema zaidi wanaostahiki kuunguzwa humo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَّقْضِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala hakuna yeyote katika nyinyi isipokuwa ataifikia. Hiyo ni hukumu ya Mola wako Mlezi ambayo lazima itimizwe.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ثُمَّ نُنَجِّى ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوا۟ وَّنَذَرُ ٱلظَّٰلِمِينَ فِيهَا جِثِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kisha tutawaokoa sawasawa wale waliomcha Mungu; na tutawaacha madhalimu humo huku wamepiga magoti.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ءَايَٰتُنَا بَيِّنَٰتٍ قَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَىُّ ٱلْفَرِيقَيْنِ خَيْرٌ مَّقَامًا وَأَحْسَنُ نَدِيًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale waliokufuru huwaambia wale walioamini: Ni lipi katika makundi mawili haya lenye cheo kizuri na lililo zuri zaidi barazani?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هُمْ أَحْسَنُ أَثَٰثًا وَرِءْيًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kaumu ngapi tuliziangamiza zilizokuwa na mapambo mazuri zaidi na wazuri zaidi katika muonekano!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قُلْ مَن كَانَ فِى ٱلضَّلَٰلَةِ فَلْيَمْدُدْ لَهُ ٱلرَّحْمَٰنُ مَدًّا حَتَّىٰٓ إِذَا رَأَوْا۟ مَا يُوعَدُونَ إِمَّا ٱلْعَذَابَ وَإِمَّا ٱلسَّاعَةَ فَسَيَعْلَمُونَ مَنْ هُوَ شَرٌّ مَّكَانًا وَأَضْعَفُ جُندًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sema: Yule aliye katika upotovu, basi Arrahmani (Mwingi wa rehema) na amuongezee (muda, mali na mengineyo) mpaka atakapoona yale waliyoahidiwa - ima ni adhabu au ni Saa, hapo ndipo watakapojua ni nani mwenye makao maovu zaidi na mwenye jeshi dhaifu zaidi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَيَزِيدُ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ٱهْتَدَوْا۟ هُدًى وَٱلْبَٰقِيَٰتُ ٱلصَّٰلِحَٰتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ مَّرَدًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Mwenyezi Mungu huwazidishia wale walioongoka uongofu. Na mema yenye kubakia ni bora katika malipo mbele ya Mola wako Mlezi na yana marejeo mema.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَفَرَءَيْتَ ٱلَّذِى كَفَرَ بِـَٔايَٰتِنَا وَقَالَ لَأُوتَيَنَّ مَالًا وَوَلَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Je, umemwona aliyezikufuru Ishara zetu na akasema: Kwa hakika mimi nitapewa mali na wana!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَطَّلَعَ ٱلْغَيْبَ أَمِ ٱتَّخَذَ عِندَ ٱلرَّحْمَٰنِ عَهْدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwani yeye amepata habari za ghaibu, au amechukua agano kwa Arrahmani (Mwingi wa rehema)?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَلَّا سَنَكْتُبُ مَا يَقُولُ وَنَمُدُّ لَهُۥ مِنَ ٱلْعَذَابِ مَدًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hasha! Tutaandika anayoyasema, na tutamuongezea sawasawa katika adhabu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَنَرِثُهُۥ مَا يَقُولُ وَيَأْتِينَا فَرْدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tutamrithi hayo anayoyasema, na atatujia mtupu peke yake!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ ءَالِهَةً لِّيَكُونُوا۟ لَهُمْ عِزًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na walichukua miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati iwape nguvu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَلَّا سَيَكْفُرُونَ بِعِبَادَتِهِمْ وَيَكُونُونَ عَلَيْهِمْ ضِدًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sivyo hivyo! Wataikataa hiyo ibada yao, na watakuwa ndio dhidi yao.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَلَمْ تَرَ أَنَّآ أَرْسَلْنَا ٱلشَّيَٰطِينَ عَلَى ٱلْكَٰفِرِينَ تَؤُزُّهُمْ أَزًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwani huoni ya kwamba tuliwatuma mashetani kwa makafiri wawachochee sawasawa?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَلَا تَعْجَلْ عَلَيْهِمْ إِنَّمَا نَعُدُّ لَهُمْ عَدًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi usiwafanyie haraka. Sisi tunawahesabia idadi ya siku zao.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ نَحْشُرُ ٱلْمُتَّقِينَ إِلَى ٱلرَّحْمَٰنِ وَفْدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku tutakayowakusanya wacha Mungu kuwapeleka kwa Arrahmani (Mwingi wa rehema) kuwa ni wageni wake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَنَسُوقُ ٱلْمُجْرِمِينَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ وِرْدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tukawaswaga wahalifu kwenda katika Jahannamu hali ya kuwa wana kiu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَّا يَمْلِكُونَ ٱلشَّفَٰعَةَ إِلَّا مَنِ ٱتَّخَذَ عِندَ ٱلرَّحْمَٰنِ عَهْدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hawatakuwa na mamlaka ya uombezi isipokuwa yule aliyechukua ahadi kwa Arrahmani (Mwingi wa rehema).
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَقَالُوا۟ ٱتَّخَذَ ٱلرَّحْمَٰنُ وَلَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na wao ati walisema kuwa Arrahmani (Mwingi wa rehema) alijifanyia mwana!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَّقَدْ جِئْتُمْ شَيْـًٔا إِدًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika mmeleta jambo la kuchusha mno!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
تَكَادُ ٱلسَّمَٰوَٰتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ ٱلْأَرْضُ وَتَخِرُّ ٱلْجِبَالُ هَدًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Zinakaribia mbingu kulipuka kwa hilo, na ardhi kupasuka, na milima kuanguka vipande vipande.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَن دَعَوْا۟ لِلرَّحْمَٰنِ وَلَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa kudai kwao kuwa Arrahmani (Mwingi wa rehema) ana mwana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا يَنۢبَغِى لِلرَّحْمَٰنِ أَن يَتَّخِذَ وَلَدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala Arrahmani (Mwingi wa rehema) hafailii kujichukulia mwana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِن كُلُّ مَن فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ إِلَّآ ءَاتِى ٱلرَّحْمَٰنِ عَبْدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakuna yeyote aliyemo mbinguni na ardhini isipokuwa atamjia Arrahmani (Mwingi wa rehema) kuwa ni mja wake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَّقَدْ أَحْصَىٰهُمْ وَعَدَّهُمْ عَدًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Yeye hakika amewadhibiti na amewahesabu sawasawa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَكُلُّهُمْ ءَاتِيهِ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ فَرْدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kila mmoja wao atamjia Siku ya Kiyama peke yake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ سَيَجْعَلُ لَهُمُ ٱلرَّحْمَٰنُ وُدًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika wale walioamini na wakatenda mema, Arrahmani (Mwingi wa rehema) atawafanyia mapenzi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَإِنَّمَا يَسَّرْنَٰهُ بِلِسَانِكَ لِتُبَشِّرَ بِهِ ٱلْمُتَّقِينَ وَتُنذِرَ بِهِۦ قَوْمًا لُّدًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika tumeifanya nyepesi (Qur'ani) kwa ulimi wako, ili uwabashirie kwayo wacha Mungu, na uwaonye kwayo kaumu wagumu mno.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَكَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّن قَرْنٍ هَلْ تُحِسُّ مِنْهُم مِّنْ أَحَدٍ أَوْ تَسْمَعُ لَهُمْ رِكْزًۢا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao. Je, unamuona hata mmoja katika wao au unasikia hata mnong'ono wao?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Al-Kahf
Sura Taa-Haa →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.