caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Kahf الكهف

Aya 110 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 69

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ٱلَّذِىٓ أَنزَلَ عَلَىٰ عَبْدِهِ ٱلْكِتَٰبَ وَلَمْ يَجْعَل لَّهُۥ عِوَجَا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye alimteremshia mja wake Kitabu, wala hakukifanya kuwa na upogo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَيِّمًا لِّيُنذِرَ بَأْسًا شَدِيدًا مِّن لَّدُنْهُ وَيُبَشِّرَ ٱلْمُؤْمِنِينَ ٱلَّذِينَ يَعْمَلُونَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا حَسَنًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKimenyooka sawa sawa, ili kionye adhabu kali kutoka kwake, na kiwabashirie Waumini watendao mema kwamba hakika wana ujira mzuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَّٰكِثِينَ فِيهِ أَبَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakae humo milele.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيُنذِرَ ٱلَّذِينَ قَالُوا۟ ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ وَلَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kiwaonye wasemao, "Mwenyezi Mungu alijifanyia mwana."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَّا لَهُم بِهِۦ مِنْ عِلْمٍ وَلَا لِـَٔابَآئِهِمْ كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَٰهِهِمْ إِن يَقُولُونَ إِلَّا كَذِبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWao hawana elimu yoyote ya jambo hili, wala baba zao. Ni neno kubwa hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi isipokuwa uongo tu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَعَلَّكَ بَٰخِعٌ نَّفْسَكَ عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِمْ إِن لَّمْ يُؤْمِنُوا۟ بِهَٰذَا ٱلْحَدِيثِ أَسَفًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuenda ukajihiliki nafsi yako kwa ajili yao, kuwasikitikia kwa kuwa hawayaamini mazungumzo haya!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا جَعَلْنَا مَا عَلَى ٱلْأَرْضِ زِينَةً لَّهَا لِنَبْلُوَهُمْ أَيُّهُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika tumevifanya vilivyoko juu ya ardhi kuwa ni pambo lake ili tuwafanyie mtihani, ni nani kati yao ndio wenye vitendo vizuri zaidi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّا لَجَٰعِلُونَ مَا عَلَيْهَا صَعِيدًا جُرُزًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Sisi tutavifanya vyote vilivyo juu ya ardhi kuwa kama nchi iliyopigwa na ukame.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ حَسِبْتَ أَنَّ أَصْحَٰبَ ٱلْكَهْفِ وَٱلرَّقِيمِ كَانُوا۟ مِنْ ءَايَٰتِنَا عَجَبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani unadhani ya kwamba wale watu wa Pangoni na Maandishi ndio walikuwa tu ajabu miongoni mwa ishara zetu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ أَوَى ٱلْفِتْيَةُ إِلَى ٱلْكَهْفِ فَقَالُوا۟ رَبَّنَآ ءَاتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterVijana hao walipokimbilia kwenye pango, na wakasema, "Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uongofu katika jambo letu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَضَرَبْنَا عَلَىٰٓ ءَاذَانِهِمْ فِى ٱلْكَهْفِ سِنِينَ عَدَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukayaziba masikio yao kuwalaza humo pangoni kwa muda wa miaka kadhaa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ بَعَثْنَٰهُمْ لِنَعْلَمَ أَىُّ ٱلْحِزْبَيْنِ أَحْصَىٰ لِمَا لَبِثُوٓا۟ أَمَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukawazindua ili tujue ni lipi katika makundi mawili yale ndilo lilihesabu sawa zaidi urefu wa muda waliokaa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

نَّحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ نَبَأَهُم بِٱلْحَقِّ إِنَّهُمْ فِتْيَةٌ ءَامَنُوا۟ بِرَبِّهِمْ وَزِدْنَٰهُمْ هُدًى

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSisi tunakusimulia habari zao kwa haki. Hakika wao walikuwa ni vijana waliomuamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidisha uongofu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَرَبَطْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ إِذْ قَامُوا۟ فَقَالُوا۟ رَبُّنَا رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ لَن نَّدْعُوَا۟ مِن دُونِهِۦٓ إِلَٰهًا لَّقَدْ قُلْنَآ إِذًا شَطَطًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukazitia nguvu nyoyo zao waliposimama na wakasema, "Mola wetu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi. Kamwe hatutamuomba mwingine badala yake kuwa ni Mungu. Hivyo, itakuwa tumesema jambo la kuvuka mpaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَٰٓؤُلَآءِ قَوْمُنَا ٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةً لَّوْلَا يَأْتُونَ عَلَيْهِم بِسُلْطَٰنٍۭ بَيِّنٍ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHawa kaumu yetu walijifanyia miungu mingine badala yake Yeye. Kwa nini basi hawawatolei uthibitisho ulio dhahiri? Na ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذِ ٱعْتَزَلْتُمُوهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ إِلَّا ٱللَّهَ فَأْوُۥٓا۟ إِلَى ٱلْكَهْفِ يَنشُرْ لَكُمْ رَبُّكُم مِّن رَّحْمَتِهِۦ وَيُهَيِّئْ لَكُم مِّنْ أَمْرِكُم مِّرْفَقًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mkijitenga nao na vile wanavyoviabudu badala ya Mwenyezi Mungu, basi kimbilieni pangoni, awafungulie Mola wenu Mlezi katika rehema zake, na awatengenezee ya kuwafaa katika mambo yenu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَرَى ٱلشَّمْسَ إِذَا طَلَعَت تَّزَٰوَرُ عَن كَهْفِهِمْ ذَاتَ ٱلْيَمِينِ وَإِذَا غَرَبَت تَّقْرِضُهُمْ ذَاتَ ٱلشِّمَالِ وَهُمْ فِى فَجْوَةٍ مِّنْهُ ذَٰلِكَ مِنْ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ مَن يَهْدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلْمُهْتَدِ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ وَلِيًّا مُّرْشِدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa unaliona jua linapochomoza, linainamia kuliani mwao kutoka hapo pangoni, na linapokuchwa, linawakwepa kushotoni, na wao wamo katika uwazi wa pango. Hizo ni katika ishara za Mwenyezi Mungu. Yule ambaye Mwenyezi Mungu anamwongoa, basi huyo ameongoka. Na yule ambaye anampoteza, basi hutampatia msimamizi wa kumwongoza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَحْسَبُهُمْ أَيْقَاظًا وَهُمْ رُقُودٌ وَنُقَلِّبُهُمْ ذَاتَ ٱلْيَمِينِ وَذَاتَ ٱلشِّمَالِ وَكَلْبُهُم بَٰسِطٌ ذِرَاعَيْهِ بِٱلْوَصِيدِ لَوِ ٱطَّلَعْتَ عَلَيْهِمْ لَوَلَّيْتَ مِنْهُمْ فِرَارًا وَلَمُلِئْتَ مِنْهُمْ رُعْبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNawe utawadhania wa macho, na hali wamelala. Nasi tunawageuza kulia na kushoto. Na mbwa wao amenyoosha miguu yake ya mbele kizingitini. Kama ungeliwatokea, hakuna shaka ungeligeuka kuwakimbia, huku umejaa hofu kubwa juu yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكَذَٰلِكَ بَعَثْنَٰهُمْ لِيَتَسَآءَلُوا۟ بَيْنَهُمْ قَالَ قَآئِلٌ مِّنْهُمْ كَمْ لَبِثْتُمْ قَالُوا۟ لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ قَالُوا۟ رَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثْتُمْ فَٱبْعَثُوٓا۟ أَحَدَكُم بِوَرِقِكُمْ هَٰذِهِۦٓ إِلَى ٱلْمَدِينَةِ فَلْيَنظُرْ أَيُّهَآ أَزْكَىٰ طَعَامًا فَلْيَأْتِكُم بِرِزْقٍ مِّنْهُ وَلْيَتَلَطَّفْ وَلَا يُشْعِرَنَّ بِكُمْ أَحَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa namna hiyo tuliwainua usingizini ili wapate kuulizana wao kwa wao. Alisema msemaji katika wao: Mmekaa muda gani? Wakasema: Tumekaa siku moja au sehemu ya siku. Wakasema: Mola wenu Mlezi ndiye anayejua zaidi muda mliokaa. Hebu mtumeni mmoja wenu na hizi fedha zenu aende mjini, akatazame chakula chake kipi kilicho bora kabisa awaletee cha kula. Naye afanye mambo hayo kwa busara, wala kamwe asiwataje kwa yeyote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّهُمْ إِن يَظْهَرُوا۟ عَلَيْكُمْ يَرْجُمُوكُمْ أَوْ يُعِيدُوكُمْ فِى مِلَّتِهِمْ وَلَن تُفْلِحُوٓا۟ إِذًا أَبَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani wao wakiwatambua, watawapiga mawe, au watawarudisha katika dini yao, na hapo kamwe hamtafanikiwa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكَذَٰلِكَ أَعْثَرْنَا عَلَيْهِمْ لِيَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ وَأَنَّ ٱلسَّاعَةَ لَا رَيْبَ فِيهَآ إِذْ يَتَنَٰزَعُونَ بَيْنَهُمْ أَمْرَهُمْ فَقَالُوا۟ ٱبْنُوا۟ عَلَيْهِم بُنْيَٰنًا رَّبُّهُمْ أَعْلَمُ بِهِمْ قَالَ ٱلَّذِينَ غَلَبُوا۟ عَلَىٰٓ أَمْرِهِمْ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيْهِم مَّسْجِدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa namna hivo ndivyo tulivyowajulisha kwa watu ili wapate kujua ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, na kwamba Saa haina shaka. Walipokuwa wakigombania jambo lao wao kwa wao, wakasema: Jengeni jengo juu yao. Mola wao Mlezi anawajua vyema. Wakasema wale walioshinda katika shauri yao: Bila ya shaka tutajenga msikiti juu yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَيَقُولُونَ ثَلَٰثَةٌ رَّابِعُهُمْ كَلْبُهُمْ وَيَقُولُونَ خَمْسَةٌ سَادِسُهُمْ كَلْبُهُمْ رَجْمًۢا بِٱلْغَيْبِ وَيَقُولُونَ سَبْعَةٌ وَثَامِنُهُمْ كَلْبُهُمْ قُل رَّبِّىٓ أَعْلَمُ بِعِدَّتِهِم مَّا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا قَلِيلٌ فَلَا تُمَارِ فِيهِمْ إِلَّا مِرَآءً ظَٰهِرًا وَلَا تَسْتَفْتِ فِيهِم مِّنْهُمْ أَحَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema: Walikuwa watatu, wa nne wao ni mbwa wao. Na wanasema: “Walikuwa watano, wa sita wao ni mbwa wao.ˮ Wanabahatisha ghaibu. Na wanasema: Walikuwa saba, na wa nane wao ni mbwa wao. Sema: “Mola wangu Mlezi ndiye anayejua sawa sawa hesabu yao. Hawawajui isipokuwa wachache tu.ˮ Basi usibishane juu yao isipokuwa kwa mabishano ya juu juu tu hivi. Wala usiulize habari zao kwa yeyote yule miongoni mwao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تَقُولَنَّ لِشَا۟ىْءٍ إِنِّى فَاعِلٌ ذَٰلِكَ غَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala kamwe usiseme kwa jambo lolote lile: Hakika nitalifanya hilo kesho.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ وَٱذْكُر رَّبَّكَ إِذَا نَسِيتَ وَقُلْ عَسَىٰٓ أَن يَهْدِيَنِ رَبِّى لِأَقْرَبَ مِنْ هَٰذَا رَشَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa Mwenyezi Mungu akipenda. Na mkumbuke Mola wako Mlezi pale unaposahau, na sema: huenda Mola wangu Mlezi ataniongoa kwenye uongozi ulio karibu zaidi kuliko huu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَبِثُوا۟ فِى كَهْفِهِمْ ثَلَٰثَ مِا۟ئَةٍ سِنِينَ وَٱزْدَادُوا۟ تِسْعًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walikaa katika pango lao hilo miaka mia tatu, na wakazidisha tisa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلِ ٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثُوا۟ لَهُۥ غَيْبُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ أَبْصِرْ بِهِۦ وَأَسْمِعْ مَا لَهُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَلِىٍّ وَلَا يُشْرِكُ فِى حُكْمِهِۦٓ أَحَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi muda waliokaa. Ni zake tu siri za mbingu na ardhi. Kuona vyema kulikoje kwake na kusikia kuzuri kulikoje! Hawana mlinzi yeyote isipokuwa Yeye, wala hamshirikishi yeyote katika hukumu yake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱتْلُ مَآ أُوحِىَ إِلَيْكَ مِن كِتَابِ رَبِّكَ لَا مُبَدِّلَ لِكَلِمَٰتِهِۦ وَلَن تَجِدَ مِن دُونِهِۦ مُلْتَحَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa soma yale uliyofunuliwa katika Kitabu cha Mola wako Mlezi. Hakuna yeyote awezaye kubadilisha maneno yake. Wala nawe hutapata makimbilio yoyote isipokuwa kwake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ ٱلَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِٱلْغَدَوٰةِ وَٱلْعَشِىِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُۥ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُۥ عَن ذِكْرِنَا وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ وَكَانَ أَمْرُهُۥ فُرُطًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka uso wake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la uhai wa dunia. Wala usimtii tuliyemghafilisha moyo wake asitukumbuke, na akafuata matamanio yake, na mambo yake yakawa ni kupita tu mipaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقُلِ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ فَمَن شَآءَ فَلْيُؤْمِن وَمَن شَآءَ فَلْيَكْفُرْ إِنَّآ أَعْتَدْنَا لِلظَّٰلِمِينَ نَارًا أَحَاطَ بِهِمْ سُرَادِقُهَا وَإِن يَسْتَغِيثُوا۟ يُغَاثُوا۟ بِمَآءٍ كَٱلْمُهْلِ يَشْوِى ٱلْوُجُوهَ بِئْسَ ٱلشَّرَابُ وَسَآءَتْ مُرْتَفَقًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa sema: Hii ni haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Basi atakaye, aamini. Na atakaye, akufuru. Hakika Sisi tumewaandalia madhalimu Moto ambao kuta zake zitawazingira. Na wakiomba msaada, watasaidiwa kwa kupewa maji yaliyo kama mafuta yaliyotibuka, yatakayowababua nyuso zao. Ni kinywaji kiovu mno kilichoje hicho, na ni mahali pabaya mno pa kupumzikia palipoje hapo!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجْرَ مَنْ أَحْسَنَ عَمَلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale walioamini na wakatenda mema, hakika Sisi hatupotezi ujira wa anayetenda mazuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أُو۟لَٰٓئِكَ لَهُمْ جَنَّٰتُ عَدْنٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهِمُ ٱلْأَنْهَٰرُ يُحَلَّوْنَ فِيهَا مِنْ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ وَيَلْبَسُونَ ثِيَابًا خُضْرًا مِّن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَّكِـِٔينَ فِيهَا عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ نِعْمَ ٱلثَّوَابُ وَحَسُنَتْ مُرْتَفَقًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao watapata Bustani za milele, zinazopita mito kwa chini yao. Humo watapambwa kwa mavazi ya mikononi ya dhahabu, na watavaa nguo za kijani za hariri na atilasi, huku wakiegemea humo juu ya makochi. Hayo ndiyo malipo bora zaidi! Na ndiyo matandiko mazuri mno ya kupumzikia!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱضْرِبْ لَهُم مَّثَلًا رَّجُلَيْنِ جَعَلْنَا لِأَحَدِهِمَا جَنَّتَيْنِ مِنْ أَعْنَٰبٍ وَحَفَفْنَٰهُمَا بِنَخْلٍ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمَا زَرْعًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wapigie mfano wa wanaume wawili: mmoja wao tulimpa vitalu viwili vya mizabibu, na tukavizungushia mitende, na kati yake tukatia mimea ya nafaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كِلْتَا ٱلْجَنَّتَيْنِ ءَاتَتْ أُكُلَهَا وَلَمْ تَظْلِم مِّنْهُ شَيْـًٔا وَفَجَّرْنَا خِلَٰلَهُمَا نَهَرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hivyo vitalu viwili vikatoa mazao yake, wala hapana kitu katika hayo kilichotindikia. Na ndani yake tukapasua mito.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكَانَ لَهُۥ ثَمَرٌ فَقَالَ لِصَٰحِبِهِۦ وَهُوَ يُحَاوِرُهُۥٓ أَنَا۠ أَكْثَرُ مِنكَ مَالًا وَأَعَزُّ نَفَرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye alikuwa na mazao mengi. Basi akamwambia mwenzake naye akibishana naye: Mimi nimekushinda wewe kwa mali na nguvu za watu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَدَخَلَ جَنَّتَهُۥ وَهُوَ ظَالِمٌ لِّنَفْسِهِۦ قَالَ مَآ أَظُنُّ أَن تَبِيدَ هَٰذِهِۦٓ أَبَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akaingia kitaluni kwake, huku anajidhulumu nafsi yake. Akasema: Sidhani kabisa kuwa haya yatawahi kuharibika milele.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَظُنُّ ٱلسَّاعَةَ قَآئِمَةً وَلَئِن رُّدِدتُّ إِلَىٰ رَبِّى لَأَجِدَنَّ خَيْرًا مِّنْهَا مُنقَلَبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala sidhani kuwa hiyo Saa (ya Kiyama) itatokea. Na ikiwa nitarudishwa kwa Mola wangu Mlezi, bila ya shaka nitapata marejeo bora zaidi kuliko haya.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ لَهُۥ صَاحِبُهُۥ وَهُوَ يُحَاوِرُهُۥٓ أَكَفَرْتَ بِٱلَّذِى خَلَقَكَ مِن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ سَوَّىٰكَ رَجُلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenzake akamwambia kwa kubishana naye: Je, unamkufuru aliyekuumba kutokana na udongo, tena kutokana na tone la manii, kisha akakufanya mwanamume aliye sawasawa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَّٰكِنَّا۠ هُوَ ٱللَّهُ رَبِّى وَلَآ أُشْرِكُ بِرَبِّىٓ أَحَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini Yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi. Wala simshirikishi Mola wangu Mlezi na yeyote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْلَآ إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَآءَ ٱللَّهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِٱللَّهِ إِن تَرَنِ أَنَا۠ أَقَلَّ مِنكَ مَالًا وَوَلَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa ulipoingia kitaluni kwako, ungelisema: Mashaallah (alitakalo Mwenyezi Mungu huwa)! Hakuna nguvu yoyote isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Ikiwa unaniona mimi nina mali kidogo zaidi na watoto kuliko wewe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَعَسَىٰ رَبِّىٓ أَن يُؤْتِيَنِ خَيْرًا مِّن جَنَّتِكَ وَيُرْسِلَ عَلَيْهَا حُسْبَانًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فَتُصْبِحَ صَعِيدًا زَلَقًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi huenda Mola wangu Mlezi akanipa kilicho bora kuliko kitalu chako, na akakitumia balaa kutoka mbinguni kwa hivyo kikageuka kuwa ardhi tupu inayoteleza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوْ يُصْبِحَ مَآؤُهَا غَوْرًا فَلَن تَسْتَطِيعَ لَهُۥ طَلَبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu maji yake yakazama (katika ardhi), basi usiweze kuyatafuta ukayapata.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأُحِيطَ بِثَمَرِهِۦ فَأَصْبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيْهِ عَلَىٰ مَآ أَنفَقَ فِيهَا وَهِىَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا وَيَقُولُ يَٰلَيْتَنِى لَمْ أُشْرِكْ بِرَبِّىٓ أَحَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi, yakateketezwa matunda yake, akabaki akipinduapindua viganja vyake, kwa vile alivyoyagharamia, huku miti yake imebwagika juu ya chanja zake. Akawa anasema: Laiti nisingelimshirikisha Mola wangu Mlezi na yeyote!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَمْ تَكُن لَّهُۥ فِئَةٌ يَنصُرُونَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَمَا كَانَ مُنتَصِرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala hakuwa na kikundi cha kumnusuru badala ya Mwenyezi Mungu, wala mwenyewe hakuweza kujinusuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هُنَالِكَ ٱلْوَلَٰيَةُ لِلَّهِ ٱلْحَقِّ هُوَ خَيْرٌ ثَوَابًا وَخَيْرٌ عُقْبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuko ulinzi ni wa Mwenyezi Mungu wa Haki tu. Yeye ndiye mbora zaidi wa malipo, na wa mwisho ulio bora zaidi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱضْرِبْ لَهُم مَّثَلَ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا كَمَآءٍ أَنزَلْنَٰهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ فَٱخْتَلَطَ بِهِۦ نَبَاتُ ٱلْأَرْضِ فَأَصْبَحَ هَشِيمًا تَذْرُوهُ ٱلرِّيَٰحُ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ مُّقْتَدِرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wapigie mfano wa uhai wa dunia ambao ni kama maji tunayoyateremsha kutoka mbinguni, yakachanganyika na mimea ya ardhi, kisha mimea hiyo ikawa vibuwa vinavyopeperushwa na upepo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلْمَالُ وَٱلْبَنُونَ زِينَةُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَٱلْبَٰقِيَٰتُ ٱلصَّٰلِحَٰتُ خَيْرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMali na wana ni pambo la uhai wa dunia. Na mema yanayobakia ni bora mbele ya Mola wako Mlezi kwa malipo, na bora kwa matumaini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَوْمَ نُسَيِّرُ ٱلْجِبَالَ وَتَرَى ٱلْأَرْضَ بَارِزَةً وَحَشَرْنَٰهُمْ فَلَمْ نُغَادِرْ مِنْهُمْ أَحَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku tutakapoiondoa milima na ukaiona ardhi iwazi, na tukawafufua, wala hatutamwacha hata mmoja miongoni mwao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَعُرِضُوا۟ عَلَىٰ رَبِّكَ صَفًّا لَّقَدْ جِئْتُمُونَا كَمَا خَلَقْنَٰكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍۭ بَلْ زَعَمْتُمْ أَلَّن نَّجْعَلَ لَكُم مَّوْعِدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakahudhurishwa mbele ya Mola wako Mlezi kwa safu (wakaambiwa): Mmetujia kama tulivyowaumba mara ya kwanza! Bali mlidai kwamba hatutawawekea miadi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَوُضِعَ ٱلْكِتَٰبُ فَتَرَى ٱلْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَٰوَيْلَتَنَا مَالِ هَٰذَا ٱلْكِتَٰبِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً إِلَّآ أَحْصَىٰهَا وَوَجَدُوا۟ مَا عَمِلُوا۟ حَاضِرًا وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kitawekwa mbele Kitabu. Basi utawaona wahalifu wanavyoogopa mno kwa sababu ya yale yaliyomo. Na watasema: "Ole wetu! Kitabu hiki kina nini! Hakikuacha dogo wala kubwa isipokuwa kililidhibiti vyema?" Na watayakuta yote waliyoyatenda yapo hadharani. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَٰٓئِكَةِ ٱسْجُدُوا۟ لِـَٔادَمَ فَسَجَدُوٓا۟ إِلَّآ إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ ٱلْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِۦٓ أَفَتَتَّخِذُونَهُۥ وَذُرِّيَّتَهُۥٓ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِى وَهُمْ لَكُمْ عَدُوٌّۢ بِئْسَ لِلظَّٰلِمِينَ بَدَلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tulipowaambia Malaika: Msujudieni Adam! Wakamsjudia isipokuwa Iblisi. Yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi. Je, mnamchukua yeye na dhuria yake kuwa vipenzi badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii ya madhalimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَّآ أَشْهَدتُّهُمْ خَلْقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَلَا خَلْقَ أَنفُسِهِمْ وَمَا كُنتُ مُتَّخِذَ ٱلْمُضِلِّينَ عَضُدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSikuwashuhudisha kuumbwa kwa mbingu na ardhi, wala kuumbwa kwa wao wenyewe. Wala sikuwafanya wapotezao kuwa ni wasaidizi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَوْمَ يَقُولُ نَادُوا۟ شُرَكَآءِىَ ٱلَّذِينَ زَعَمْتُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا۟ لَهُمْ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُم مَّوْبِقًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku atakaposema (Mwenyezi Mungu): Waiteni hao mliodai kuwa ni washirika wangu. Basi watawaita, na wao hawatawaitikia. Nasi tutaweka baina yao maangamio.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَرَءَا ٱلْمُجْرِمُونَ ٱلنَّارَ فَظَنُّوٓا۟ أَنَّهُم مُّوَاقِعُوهَا وَلَمْ يَجِدُوا۟ عَنْهَا مَصْرِفًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wahalifu watauona Moto na watajua ya kwamba wao lazima wataingia humo; wala hawatapata pa kuuepukia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ صَرَّفْنَا فِى هَٰذَا ٱلْقُرْءَانِ لِلنَّاسِ مِن كُلِّ مَثَلٍ وَكَانَ ٱلْإِنسَٰنُ أَكْثَرَ شَىْءٍ جَدَلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka tumewaelezea watu katika Qur-ani hii kila namna ya mfano. Lakini mwanadamu amezidi kuliko kila kitu kwa ubishi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا مَنَعَ ٱلنَّاسَ أَن يُؤْمِنُوٓا۟ إِذْ جَآءَهُمُ ٱلْهُدَىٰ وَيَسْتَغْفِرُوا۟ رَبَّهُمْ إِلَّآ أَن تَأْتِيَهُمْ سُنَّةُ ٱلْأَوَّلِينَ أَوْ يَأْتِيَهُمُ ٱلْعَذَابُ قُبُلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakikuwazuia watu kuamini ulipowajia uongofu, na kuomba maghfira kwa Mola wao Mlezi, isipokuwa iwafikie desturi ya wale wa mwanzo, au iwafikie adhabu jahara.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا نُرْسِلُ ٱلْمُرْسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ وَيُجَٰدِلُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِٱلْبَٰطِلِ لِيُدْحِضُوا۟ بِهِ ٱلْحَقَّ وَٱتَّخَذُوٓا۟ ءَايَٰتِى وَمَآ أُنذِرُوا۟ هُزُوًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hatuwatumi Mitume isipokuwa wawe wabashiri na waonyaji. Na wale waliokufuru wanabishana kwa batili, ili kwayo waivunje haki. Na walizifanya Ishara zangu na yale waliyoonywa kuwa ni mzaha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِۦ فَأَعْرَضَ عَنْهَا وَنَسِىَ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ إِنَّا جَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِىٓ ءَاذَانِهِمْ وَقْرًا وَإِن تَدْعُهُمْ إِلَى ٱلْهُدَىٰ فَلَن يَهْتَدُوٓا۟ إِذًا أَبَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Ishara za Mola wake Mlezi, naye akazipuuza na akasahau yaliyotangulizwa na mikono yake? Hakika Sisi tumeziba nyoyo zao ili wasifahamu, na uziwi uko kwenye masikio yao. Na ukiwaita kwenye uongofu, kamwe hawataweza kuongoka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَرَبُّكَ ٱلْغَفُورُ ذُو ٱلرَّحْمَةِ لَوْ يُؤَاخِذُهُم بِمَا كَسَبُوا۟ لَعَجَّلَ لَهُمُ ٱلْعَذَابَ بَل لَّهُم مَّوْعِدٌ لَّن يَجِدُوا۟ مِن دُونِهِۦ مَوْئِلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mola wako Mlezi ni Msamehevu, Mwenye rehema. Lau angeliwachukulia kwa mujibu wa yale waliyoyachuma, bila ya shaka angeliwafanyia haraka kuwaadhibu. Lakini wanayo miadi ambayo hawatapata makimbilio yoyote ya kuepukana nayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتِلْكَ ٱلْقُرَىٰٓ أَهْلَكْنَٰهُمْ لَمَّا ظَلَمُوا۟ وَجَعَلْنَا لِمَهْلِكِهِم مَّوْعِدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa miji hiyo tuliwaangamiza watu wake walipodhulumu. Na tukawawekea miadi ya maangamizo yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِفَتَىٰهُ لَآ أَبْرَحُ حَتَّىٰٓ أَبْلُغَ مَجْمَعَ ٱلْبَحْرَيْنِ أَوْ أَمْضِىَ حُقُبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pale Musa alipomwambia kijana wake, "Sitaacha kuendelea mpaka nifike zinapokutana bahari mbili, au nitaendelea kwa muda mrefu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّا بَلَغَا مَجْمَعَ بَيْنِهِمَا نَسِيَا حُوتَهُمَا فَٱتَّخَذَ سَبِيلَهُۥ فِى ٱلْبَحْرِ سَرَبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wawili hao walipofika zinapokutana hizo bahari mbili, walimsahau samaki wao, naye akashika njia yake akaponyokea baharini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّا جَاوَزَا قَالَ لِفَتَىٰهُ ءَاتِنَا غَدَآءَنَا لَقَدْ لَقِينَا مِن سَفَرِنَا هَٰذَا نَصَبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalipokwishapita, alimwambia kijana wake: Tupe chakula chetu cha mchana. Kwa hakika tumepata machovu kweli kwa hii safari yetu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ أَرَءَيْتَ إِذْ أَوَيْنَآ إِلَى ٱلصَّخْرَةِ فَإِنِّى نَسِيتُ ٱلْحُوتَ وَمَآ أَنسَىٰنِيهُ إِلَّا ٱلشَّيْطَٰنُ أَنْ أَذْكُرَهُۥ وَٱتَّخَذَ سَبِيلَهُۥ فِى ٱلْبَحْرِ عَجَبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema (kijana): Unaona! Pale tulipopumzika penye jabali, basi mimi nilimsahau yule samaki. Na hakuna aliyenisahaulisha kumkumbuka isipokuwa Shetani tu. Naye akashika njia yake baharini kwa ajabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ ذَٰلِكَ مَا كُنَّا نَبْغِ فَٱرْتَدَّا عَلَىٰٓ ءَاثَارِهِمَا قَصَصًا

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Musa) akasema: "Hayo ndiyo tuliyokuwa tunayataka." Basi wakarudi nyuma kwa kufuata njia waliyojia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَوَجَدَا عَبْدًا مِّنْ عِبَادِنَآ ءَاتَيْنَٰهُ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَعَلَّمْنَٰهُ مِن لَّدُنَّا عِلْمًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakamkuta mja katika waja wetu tuliyempa rehema kutoka kwetu, na tukamfunza mafunzo yaliyotoka kwetu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ لَهُۥ مُوسَىٰ هَلْ أَتَّبِعُكَ عَلَىٰٓ أَن تُعَلِّمَنِ مِمَّا عُلِّمْتَ رُشْدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMusa akamwambia: Nikufuate ili unifunze katika ule uongofu uliofunzwa wewe?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِىَ صَبْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Hakika wewe hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكَيْفَ تَصْبِرُ عَلَىٰ مَا لَمْ تُحِطْ بِهِۦ خُبْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa utawezaje kuvumilia yale usiyoyajua vilivyo undani wake?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ صَابِرًا وَلَآ أَعْصِى لَكَ أَمْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: In shaa Allah (Mwenyezi Mungu akitaka), utanikuta mvumilivu, wala sitaasi amri yako yoyote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ فَإِنِ ٱتَّبَعْتَنِى فَلَا تَسْـَٔلْنِى عَن شَىْءٍ حَتَّىٰٓ أُحْدِثَ لَكَ مِنْهُ ذِكْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Basi ukinifuata, usiniulize kitu mpaka mimi nianze kukutajia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَا رَكِبَا فِى ٱلسَّفِينَةِ خَرَقَهَا قَالَ أَخَرَقْتَهَا لِتُغْرِقَ أَهْلَهَا لَقَدْ جِئْتَ شَيْـًٔا إِمْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wawili hao wakatoka, hata walipoabiri jahazi (yule mtu), akalitoboa. (Musa) akasema: Unalitoboa ili uwazamishe watu wake? Hakika umefanya jambo baya mno.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ أَلَمْ أَقُلْ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِىَ صَبْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Je, sikusema kwamba wewe hakika hutaweza kuvumilia kuwa pamoja nami?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ لَا تُؤَاخِذْنِى بِمَا نَسِيتُ وَلَا تُرْهِقْنِى مِنْ أَمْرِى عُسْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Musa) akasema: Usinichukulie makosa kwa niliyosahau, wala usinipe uzito kwa jambo langu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَا لَقِيَا غُلَٰمًا فَقَتَلَهُۥ قَالَ أَقَتَلْتَ نَفْسًا زَكِيَّةًۢ بِغَيْرِ نَفْسٍ لَّقَدْ جِئْتَ شَيْـًٔا نُّكْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakatoka wawili hao mpaka wakamkuta kijana, akamuua. (Musa) akasema: Ala! Umemuua mtu asiye na kosa, na wala hakuua nafsi yoyote! Ama hakika umefanya jambo baya kabisa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ أَلَمْ أَقُل لَّكَ إِنَّكَ لَن تَسْتَطِيعَ مَعِىَ صَبْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Yule mtu) Akasema, "Je, sikukwambia kwamba hakika wewe hutaweza kusubiri kuwa pamoja nami?"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ إِن سَأَلْتُكَ عَن شَىْءٍۭ بَعْدَهَا فَلَا تُصَٰحِبْنِى قَدْ بَلَغْتَ مِن لَّدُنِّى عُذْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Musa) Akasema, "Nikikuuliza kuhusu kitu chochote baada ya haya, basi usifuatane nami. Kwani hakika umekwishapata udhuru kutoka kwangu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱنطَلَقَا حَتَّىٰٓ إِذَآ أَتَيَآ أَهْلَ قَرْيَةٍ ٱسْتَطْعَمَآ أَهْلَهَا فَأَبَوْا۟ أَن يُضَيِّفُوهُمَا فَوَجَدَا فِيهَا جِدَارًا يُرِيدُ أَن يَنقَضَّ فَأَقَامَهُۥ قَالَ لَوْ شِئْتَ لَتَّخَذْتَ عَلَيْهِ أَجْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakaondoka mpaka wakawafikia watu wa mji mmoja. Wakawaomba watu wake wawape chakula, nao wakakataa kuwakaribisha. Hapo wakakuta ukuta unataka kuanguka, (yule mja mwema) akausimamisha. (Musa) akasema, "Ungelitaka, ungelichukua ujira kwa haya."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ هَٰذَا فِرَاقُ بَيْنِى وَبَيْنِكَ سَأُنَبِّئُكَ بِتَأْوِيلِ مَا لَمْ تَسْتَطِع عَّلَيْهِ صَبْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Yule mtu) akasema: Huku ndiko kutengana baina yangu na wewe. Sasa nitakueleza maana ya yale ambayo hukuweza kuyastahamili.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمَّا ٱلسَّفِينَةُ فَكَانَتْ لِمَسَٰكِينَ يَعْمَلُونَ فِى ٱلْبَحْرِ فَأَرَدتُّ أَنْ أَعِيبَهَا وَكَانَ وَرَآءَهُم مَّلِكٌ يَأْخُذُ كُلَّ سَفِينَةٍ غَصْبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAma lile jahazi, hilo lilikuwa la masikini fulani wafanyao kazi baharini. Kwa hivyo, nilitaka kulitia dosari, kwani nyuma yao alikuwapo mfalme aliyekuwa akichukua kwa nguvu majahazi yote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَمَّا ٱلْغُلَٰمُ فَكَانَ أَبَوَاهُ مُؤْمِنَيْنِ فَخَشِينَآ أَن يُرْهِقَهُمَا طُغْيَٰنًا وَكُفْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ama yule kijana, wazazi wake walikuwa ni Waumini. Tukahofu aje kuwatia mashakani kwa kupindukia mipaka na ukafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَرَدْنَآ أَن يُبْدِلَهُمَا رَبُّهُمَا خَيْرًا مِّنْهُ زَكَوٰةً وَأَقْرَبَ رُحْمًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tulitaka Mola wao Mlezi awabadilishie aliye bora zaidi kuliko huyo kwa kutakasika, na aliye karibu zaidi kwa huruma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَمَّا ٱلْجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَٰمَيْنِ يَتِيمَيْنِ فِى ٱلْمَدِينَةِ وَكَانَ تَحْتَهُۥ كَنزٌ لَّهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَٰلِحًا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَن يَبْلُغَآ أَشُدَّهُمَا وَيَسْتَخْرِجَا كَنزَهُمَا رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ وَمَا فَعَلْتُهُۥ عَنْ أَمْرِى ذَٰلِكَ تَأْوِيلُ مَا لَمْ تَسْطِع عَّلَيْهِ صَبْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ama ukuta ule, huo ulikuwa ni wa vijana wawili mayatima kule mjini. Na chini yake ilikuwapo hazina yao; na baba yao alikuwa ni mtu mwema. Basi Mola wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima wao na wajitolee hazina yao wenyewe, hii ikiwa ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Wala mimi sikutenda hayo kwa amri yangu. Hiyo ndiyo tafsiri ya hayo ambayo wewe hukuweza kuyasubiria.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَسْـَٔلُونَكَ عَن ذِى ٱلْقَرْنَيْنِ قُلْ سَأَتْلُوا۟ عَلَيْكُم مِّنْهُ ذِكْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanakuuliza kuhusu Dhul-Qarnain. Waambie: nitawasomea baadhi ya hadithi yake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا مَكَّنَّا لَهُۥ فِى ٱلْأَرْضِ وَءَاتَيْنَٰهُ مِن كُلِّ شَىْءٍ سَبَبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Sisi tulimuimarisha katika ardhi na tukampa katika njia za kila kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَتْبَعَ سَبَبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi akaifuata njia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ مَغْرِبَ ٱلشَّمْسِ وَجَدَهَا تَغْرُبُ فِى عَيْنٍ حَمِئَةٍ وَوَجَدَ عِندَهَا قَوْمًا قُلْنَا يَٰذَا ٱلْقَرْنَيْنِ إِمَّآ أَن تُعَذِّبَ وَإِمَّآ أَن تَتَّخِذَ فِيهِمْ حُسْنًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMpaka alipofika machweo ya jua, akaliona linatua katika chemichemi yenye matope meusi. Na pale akawakuta kaumu fulani. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnain, ima uwaadhibu au uwafanyie uzuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ أَمَّا مَن ظَلَمَ فَسَوْفَ نُعَذِّبُهُۥ ثُمَّ يُرَدُّ إِلَىٰ رَبِّهِۦ فَيُعَذِّبُهُۥ عَذَابًا نُّكْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Ama aliyedhulumu, basi tutamuadhibu kisha atarudishwa kwa Mola wake Mlezi, naye atamuadhibu adhabu mbaya zaidi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَمَّا مَنْ ءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحًا فَلَهُۥ جَزَآءً ٱلْحُسْنَىٰ وَسَنَقُولُ لَهُۥ مِنْ أَمْرِنَا يُسْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ama yule mwenye kuamini na akatenda mema, basi huyo ana malipo mazuri, nasi tutamwambia lililo jepesi katika amri yetu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ أَتْبَعَ سَبَبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha akaifuata njia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ مَطْلِعَ ٱلشَّمْسِ وَجَدَهَا تَطْلُعُ عَلَىٰ قَوْمٍ لَّمْ نَجْعَل لَّهُم مِّن دُونِهَا سِتْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHata alipofika machomozeo ya jua, akaliona linawachomozea kaumu ambao hatukuwawekea pazia ya kuwakinga kutokana nalo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَٰلِكَ وَقَدْ أَحَطْنَا بِمَا لَدَيْهِ خُبْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterVivyo hivyo. Na Sisi tulizijua vilivyo habari zake zote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ أَتْبَعَ سَبَبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha akaifuata njia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ بَيْنَ ٱلسَّدَّيْنِ وَجَدَ مِن دُونِهِمَا قَوْمًا لَّا يَكَادُونَ يَفْقَهُونَ قَوْلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHata alipofika katikati ya milima miwili, alikuta nyuma yake kaumu ambao walikaribia kutofahamu neno lolote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ يَٰذَا ٱلْقَرْنَيْنِ إِنَّ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ فَهَلْ نَجْعَلُ لَكَ خَرْجًا عَلَىٰٓ أَن تَجْعَلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ سَدًّا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Ewe Dhul-Qarnain! Hakika Yaajuju na Maajuju wanafanya uharibifu katika ardhi. Basi je, tukupe ujira ili utie baina yetu na baina yao kizuizi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ مَا مَكَّنِّى فِيهِ رَبِّى خَيْرٌ فَأَعِينُونِى بِقُوَّةٍ أَجْعَلْ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُمْ رَدْمًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Yale ambayo Mola wangu Mlezi ameniimarisha ndani yake ndiyo bora zaidi. Lakini nisaidieni kwa nguvu. Nitaweka baina yenu na baina yao kizuizi imara.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ءَاتُونِى زُبَرَ ٱلْحَدِيدِ حَتَّىٰٓ إِذَا سَاوَىٰ بَيْنَ ٱلصَّدَفَيْنِ قَالَ ٱنفُخُوا۟ حَتَّىٰٓ إِذَا جَعَلَهُۥ نَارًا قَالَ ءَاتُونِىٓ أُفْرِغْ عَلَيْهِ قِطْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNileteeni vipande vya chuma. Hata alipoijaza sawasawa nafasi iliyo katikati ya milima miwili hiyo, akasema, "Pulizeni moto" mpaka alipokifanya kuwa moto, akasema, "Nileteeni shaba iliyoyeyuka niimimine juu ya chuma hicho."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَمَا ٱسْطَٰعُوٓا۟ أَن يَظْهَرُوهُ وَمَا ٱسْتَطَٰعُوا۟ لَهُۥ نَقْبًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi hawakuweza kukikwea, wala hawakuweza kukitoboa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ هَٰذَا رَحْمَةٌ مِّن رَّبِّى فَإِذَا جَآءَ وَعْدُ رَبِّى جَعَلَهُۥ دَكَّآءَ وَكَانَ وَعْدُ رَبِّى حَقًّا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema, "Hii ni rehema kutoka kwa Mola wangu Mlezi. Na itakapokuja ahadi ya Mola wangu Mlezi, atakivunjavunja. Na ahadi ya Mola wangu Mlezi ni ya kweli."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَرَكْنَا بَعْضَهُمْ يَوْمَئِذٍ يَمُوجُ فِى بَعْضٍ وَنُفِخَ فِى ٱلصُّورِ فَجَمَعْنَٰهُمْ جَمْعًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tutawaacha baadhi yao siku hiyo wachanganyike wao kwa wao, na litapulizwa baragumu, hapo tutawakusanya wote pamoja.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَعَرَضْنَا جَهَنَّمَ يَوْمَئِذٍ لِّلْكَٰفِرِينَ عَرْضًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku hiyo tutawadhihirishia wazi Jahannamu makafiri waione.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ كَانَتْ أَعْيُنُهُمْ فِى غِطَآءٍ عَن ذِكْرِى وَكَانُوا۟ لَا يَسْتَطِيعُونَ سَمْعًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale ambao macho yao yalikuwa paziani hawanikumbuki, na wakawa hawawezi kusikia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَحَسِبَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَن يَتَّخِذُوا۟ عِبَادِى مِن دُونِىٓ أَوْلِيَآءَ إِنَّآ أَعْتَدْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَٰفِرِينَ نُزُلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, wanadhani wale waliokufuru kwamba watawafanya waja wangu kuwa vipenzi wao badala yangu Mimi? Hakika Sisi tumeiandaa Jahannamu iwe ndipo pahali pa kuteremkia pa makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُم بِٱلْأَخْسَرِينَ أَعْمَٰلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Je, tuwatajieni wenye hasara mno katika vitendo vyao?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi wale ambao juhudi yao katika uhai wa dunia ilipotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya matendo mazuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أُو۟لَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمْ وَلِقَآئِهِۦ فَحَبِطَتْ أَعْمَٰلُهُمْ فَلَا نُقِيمُ لَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ وَزْنًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ni wale waliozikufuru Ishara za Mola wao Mlezi na kukutana naye. Kwa hivyo matendo yao yakapotea bure, na wala Siku ya Kiyama hatutawasimamishia mizani yoyote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ جَزَآؤُهُمْ جَهَنَّمُ بِمَا كَفَرُوا۟ وَٱتَّخَذُوٓا۟ ءَايَٰتِى وَرُسُلِى هُزُوًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ndiyo malipo yao, Jahannam, kwa walivyokufuru na wakafanyia stihizai Ishara zangu na Mitume wangu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ كَانَتْ لَهُمْ جَنَّٰتُ ٱلْفِرْدَوْسِ نُزُلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale walioamini na wakatenda mema, mashukio yao yatakuwa kwenye Bustani za Firdausi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

خَٰلِدِينَ فِيهَا لَا يَبْغُونَ عَنْهَا حِوَلًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatadumu humo; kamwe hawatataka kuondoka humo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُل لَّوْ كَانَ ٱلْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَٰتِ رَبِّى لَنَفِدَ ٱلْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَٰتُ رَبِّى وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِۦ مَدَدًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Lau kuwa bahari ingekuwa ndiyo wino kwa maneno ya Mola wangu Mlezi, basi bahari ingelimalizika kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu Mlezi, hata tungeliileta mfano wa hiyo kuongezea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ إِنَّمَآ أَنَا۠ بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰٓ إِلَىَّ أَنَّمَآ إِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَٰحِدٌ فَمَن كَانَ يَرْجُوا۟ لِقَآءَ رَبِّهِۦ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَٰلِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِۦٓ أَحَدًۢا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema, "Hakika mimi ni mwanadamu tu kama nyinyi. Ninaletewa ufunuo (wahyi) kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Kwa hivyo, mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi, basi na atende matendo mema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70