caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura As-Saaffaat الصافات

Aya 182 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 56

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ وَٱلصَّٰٓفَّٰتِ صَفًّا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNinaapa kwa wanaojipanga kwa safu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱلزَّٰجِرَٰتِ زَجْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa wenye kukataza mabaya.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱلتَّٰلِيَٰتِ ذِكْرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa wenye kusoma Ukumbusho.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ إِلَٰهَكُمْ لَوَٰحِدٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ ٱلْمَشَٰرِقِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yake, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنْيَا بِزِينَةٍ ٱلْكَوَاكِبِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَحِفْظًا مِّن كُلِّ شَيْطَٰنٍ مَّارِدٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kulinda na kila shetani muasi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى ٱلْمَلَإِ ٱلْأَعْلَىٰ وَيُقْذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

دُحُورًا وَلَهُمْ عَذَابٌ وَاصِبٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا مَنْ خَطِفَ ٱلْخَطْفَةَ فَأَتْبَعَهُۥ شِهَابٌ ثَاقِبٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa anayenyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinachong'ara.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَم مَّنْ خَلَقْنَآ إِنَّا خَلَقْنَٰهُم مِّن طِينٍ لَّازِبٍۭ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tuliowaumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unaonata.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بَلْ عَجِبْتَ وَيَسْخَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBali unastaajabu, na wao wanafanya masihara.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا ذُكِّرُوا۟ لَا يَذْكُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanapokumbushwa, hawakumbuki.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا رَأَوْا۟ ءَايَةً يَسْتَسْخِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanapoona Ishara, wanafanya masihara.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالُوٓا۟ إِنْ هَٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa husema: Haya si chochote isipokuwa ni uchawi tu ulio dhahiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAti tukishakufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوَءَابَآؤُنَا ٱلْأَوَّلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHata baba zetu wa zamani?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ نَعَمْ وَأَنتُمْ دَٰخِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Naam! Hali nanyi ni madhalili.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِنَّمَا هِىَ زَجْرَةٌ وَٰحِدَةٌ فَإِذَا هُمْ يَنظُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndipo wataona!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالُوا۟ يَٰوَيْلَنَا هَٰذَا يَوْمُ ٱلدِّينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَٰذَا يَوْمُ ٱلْفَصْلِ ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHii ndiyo Siku ya Hukumu mliyokuwa mkiikadhibisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱحْشُرُوا۟ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ وَأَزْوَٰجَهُمْ وَمَا كَانُوا۟ يَعْبُدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakusanyeni wale waliodhulumu, na wote walio mfano wao, na hao ambao wao walikuwa wakiwaabudu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مِن دُونِ ٱللَّهِ فَٱهْدُوهُمْ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلْجَحِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBadala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقِفُوهُمْ إِنَّهُم مَّسْـُٔولُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wasimamisheni. Hakika hao wataulizwa:

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا لَكُمْ لَا تَنَاصَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMna nini? Mbona hamsaidiani?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بَلْ هُمُ ٱلْيَوْمَ مُسْتَسْلِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBali hii leo, watasalimu amri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَآءَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWataelekeana wao kwa wao kuulizana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوٓا۟ إِنَّكُمْ كُنتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ ٱلْيَمِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ بَل لَّمْ تَكُونُوا۟ مُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيْكُم مِّن سُلْطَٰنٍۭ بَلْ كُنتُمْ قَوْمًا طَٰغِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَحَقَّ عَلَيْنَا قَوْلُ رَبِّنَآ إِنَّا لَذَآئِقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَغْوَيْنَٰكُمْ إِنَّا كُنَّا غَٰوِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِنَّهُمْ يَوْمَئِذٍ فِى ٱلْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِٱلْمُجْرِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHivyo ndivyo tutakavyowafanyia wahalifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّهُمْ كَانُوٓا۟ إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا ٱللَّهُ يَسْتَكْبِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWao walipokuwa wakiambiwa, "La ilaha illallaahu (Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu)", wanajivuna.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُوٓا۟ ءَالِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍۭ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بَلْ جَآءَ بِٱلْحَقِّ وَصَدَّقَ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBali huyu amekuja kwa haki, na amewasadikisha Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّكُمْ لَذَآئِقُوا۟ ٱلْعَذَابِ ٱلْأَلِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala hamlipwi isipokuwa hayo mliyokuwa mkiyafanya.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu walioteuliwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أُو۟لَٰٓئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَّعْلُومٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ndio watakaopata riziki maalumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَوَٰكِهُ وَهُم مُّكْرَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMatunda, nao wataheshimiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فِى جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKatika Bustani za neema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَٰبِلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWako juu ya viti mfano wa kitanda wameelekeana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يُطَافُ عَلَيْهِم بِكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍۭ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchemi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بَيْضَآءَ لَذَّةٍ لِّلشَّٰرِبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا فِيهَا غَوْلٌ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنزَفُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakina madhara, wala hakiwaleweshi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَعِندَهُمْ قَٰصِرَٰتُ ٱلطَّرْفِ عِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha, mazuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌ مَّكْنُونٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao wanawake kama mayai yaliyohifadhika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَآءَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakaelekeana kuulizana wenyewe kwa wenyewe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ قَآئِلٌ مِّنْهُمْ إِنِّى كَانَ لِى قَرِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nilikuwa na rafiki.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَقُولُ أَءِنَّكَ لَمِنَ ٱلْمُصَدِّقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAliyekuwa akiniambia: Hivyo wewe ni katika wanaosadiki.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَدِينُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAti tukishakufa tukawa udongo na mafupa, ndiyo tutalipwa na kufanyiwa hesabu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ هَلْ أَنتُم مُّطَّلِعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAtasema: Je, nyie mnawaona?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱطَّلَعَ فَرَءَاهُ فِى سَوَآءِ ٱلْجَحِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi atachungulia amwone katikati ya Jahannamu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ تَٱللَّهِ إِن كِدتَّ لَتُرْدِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAtasema: Wallahi! (Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu) Ulikaribia sana kunipoteza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْلَا نِعْمَةُ رَبِّى لَكُنتُ مِنَ ٱلْمُحْضَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa si neema ya Mola wangu Mlezi, bila ya shaka ningelikuwa miongoni mwa waliohudhurishwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَمَا نَحْنُ بِمَيِّتِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, sisi hatutakufa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا مَوْتَتَنَا ٱلْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa kifo chetu cha kwanza? Wala sisi hatutaadhibiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika huku bila ya shaka ndiko kufuzu kukubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِمِثْلِ هَٰذَا فَلْيَعْمَلِ ٱلْعَٰمِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa mfano wa haya na watende watendao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَذَٰلِكَ خَيْرٌ نُّزُلًا أَمْ شَجَرَةُ ٱلزَّقُّومِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, kukaribishwa hivi si ndiyo bora, au mti wa Zaqqum?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا جَعَلْنَٰهَا فِتْنَةً لِّلظَّٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Sisi tumeufanya huo kuwa ni mateso kwa waliodhulumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّهَا شَجَرَةٌ تَخْرُجُ فِىٓ أَصْلِ ٱلْجَحِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika huo ni mti unaotoka katikati ya Jahannamu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

طَلْعُهَا كَأَنَّهُۥ رُءُوسُ ٱلشَّيَٰطِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMashada ya matunda yake kama kwamba ni vichwa vya mashetani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِنَّهُمْ لَـَٔاكِلُونَ مِنْهَا فَمَالِـُٔونَ مِنْهَا ٱلْبُطُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi hakika bila ya shaka hao watayala hayo, na wajaze matumbo kwayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ إِنَّ لَهُمْ عَلَيْهَا لَشَوْبًا مِّنْ حَمِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha juu yake wanyweshwe mchanganyo wa maji ya moto yaliyochemka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ إِنَّ مَرْجِعَهُمْ لَإِلَى ٱلْجَحِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha hakika marejeo yao bila ya shaka yatakuwa Jahimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّهُمْ أَلْفَوْا۟ ءَابَآءَهُمْ ضَآلِّينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika waliwakuta baba zao wamepotea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَهُمْ عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِمْ يُهْرَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wao wakafanya haraka kufuata nyayo zao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ ضَلَّ قَبْلَهُمْ أَكْثَرُ ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka walikwisha potea kabla yao wengi wa watu wa zamani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا فِيهِم مُّنذِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Sisi hakika tuliwapelekea waonyaji.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلْمُنذَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi hebu angalia ulikuwaje mwisho wa walioonywa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ نَادَىٰنَا نُوحٌ فَلَنِعْمَ ٱلْمُجِيبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Nuhu alituita, na Sisi ni bora wa waitikiaji.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنَجَّيْنَٰهُ وَأَهْلَهُۥ مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tulimwokoa yeye na ahali zake kutokana na msiba mkubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَعَلْنَا ذُرِّيَّتَهُۥ هُمُ ٱلْبَاقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tuliwajaalia dhuria zake ndio wenye kubakia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukamwachia (sifa njema) kwa waliokuja baadaye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَلَٰمٌ عَلَىٰ نُوحٍ فِى ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIwe salama kwa Nuhu ulimwenguni kote!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika hivi ndivyo tunavyowalipa wanaofanya mema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika yeye ni katika waja wetu walioamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ أَغْرَقْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukawazamisha wale wengine.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ مِن شِيعَتِهِۦ لَإِبْرَٰهِيمَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Ibrahim alikuwa katika kundi lake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ جَآءَ رَبَّهُۥ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlipomjia Mola wake Mlezi kwa moyo mzima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِۦ مَاذَا تَعْبُدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlimwambia baba yake na watu wake: Mnaabudu nini?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَئِفْكًا ءَالِهَةً دُونَ ٱللَّهِ تُرِيدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa kuzua tu mnataka miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَمَا ظَنُّكُم بِرَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMnamdhania nini Mola Mlezi wa walimwengu wote?"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَنَظَرَ نَظْرَةً فِى ٱلنُّجُومِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha akapiga jicho kutazama nyota.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَقَالَ إِنِّى سَقِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Hakika mimi ni mgonjwa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَتَوَلَّوْا۟ عَنْهُ مُدْبِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNao wakamwacha, wakampa kisogo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَرَاغَ إِلَىٰٓ ءَالِهَتِهِمْ فَقَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi akaiendea miungu yao kwa siri, akaiambia: Mbona hamli?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا لَكُمْ لَا تَنطِقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMna nini hata hamsemi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَرَاغَ عَلَيْهِمْ ضَرْبًۢا بِٱلْيَمِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha akaigeukia kuipiga kwa mkono wa kulia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَقْبَلُوٓا۟ إِلَيْهِ يَزِفُّونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakamjia upesi upesi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ أَتَعْبُدُونَ مَا تَنْحِتُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Hivyo mnaviabudu vitu mnavyovichonga wenyewe?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱللَّهُ خَلَقَكُمْ وَمَا تَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hali Mwenyezi Mungu ndiye aliyekuumbeni nyinyi na hivyo mnavyovifanya!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ ٱبْنُوا۟ لَهُۥ بُنْيَٰنًا فَأَلْقُوهُ فِى ٱلْجَحِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: Mjengeeni jengo, na kisha mtupeni motoni humo!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَرَادُوا۟ بِهِۦ كَيْدًا فَجَعَلْنَٰهُمُ ٱلْأَسْفَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi walitaka kumfanyia vitimbi, lakini tukawafanya wao ndio wa chini zaidi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ إِنِّى ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّى سَيَهْدِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

رَبِّ هَبْ لِى مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEwe Mola wangu Mlezi! Nitunukie aliye miongoni mwa watenda mema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَبَشَّرْنَٰهُ بِغُلَٰمٍ حَلِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukambashiria mwana aliye mpole.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّا بَلَغَ مَعَهُ ٱلسَّعْىَ قَالَ يَٰبُنَىَّ إِنِّىٓ أَرَىٰ فِى ٱلْمَنَامِ أَنِّىٓ أَذْبَحُكَ فَٱنظُرْ مَاذَا تَرَىٰ قَالَ يَٰٓأَبَتِ ٱفْعَلْ مَا تُؤْمَرُ سَتَجِدُنِىٓ إِن شَآءَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلصَّٰبِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi alipofika makamo ya kwenda na kurudi pamoja naye, alimwambia: Ewe mwanangu! Hakika mimi nimeona usingizini kuwa ninakuchinja. Basi angalia wewe, waonaje? Akasema: Ewe baba yangu! Tenda unavyoamrishwa, utanikuta mimi, Insha Allah (Mwenyezi Mungu akipenda), katika wanaosubiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّآ أَسْلَمَا وَتَلَّهُۥ لِلْجَبِينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wote wawili walipojisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنَٰدَيْنَٰهُ أَن يَٰٓإِبْرَٰهِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTulimwita: Ewe Ibrahim!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَدْ صَدَّقْتَ ٱلرُّءْيَآ إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterUmekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyowalipa wanaotenda mema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ ٱلْبَلَٰٓؤُا۟ ٱلْمُبِينُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika haya ni majaribio yaliyo dhahiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَفَدَيْنَٰهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukamwachia (sifa njema) kwa watu waliokuja baadaye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَلَٰمٌ عَلَىٰٓ إِبْرَٰهِيمَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIwe salama kwa Ibrahim!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHivi ndivyo tunavyowalipa wanaofanya mema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika yeye ni katika waja wetu walioamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَبَشَّرْنَٰهُ بِإِسْحَٰقَ نَبِيًّا مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَبَٰرَكْنَا عَلَيْهِ وَعَلَىٰٓ إِسْحَٰقَ وَمِن ذُرِّيَّتِهِمَا مُحْسِنٌ وَظَالِمٌ لِّنَفْسِهِۦ مُبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuria zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ مَنَنَّا عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنَجَّيْنَٰهُمَا وَقَوْمَهُمَا مِنَ ٱلْكَرْبِ ٱلْعَظِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنَصَرْنَٰهُمْ فَكَانُوا۟ هُمُ ٱلْغَٰلِبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَءَاتَيْنَٰهُمَا ٱلْكِتَٰبَ ٱلْمُسْتَبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawapa wawili hao Kitabu kinachobainisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَهَدَيْنَٰهُمَا ٱلصِّرَٰطَ ٱلْمُسْتَقِيمَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawaongoa kwenye njia iliyonyooka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِمَا فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawaachia (sifa njema) katika watu waliokuja baadaye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَلَٰمٌ عَلَىٰ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIwe salama kwa Musa na Haruni!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika hivyo ndivyo tunavyowalipa walio wema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّهُمَا مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wawili hao ni katika waja wetu walioamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ إِلْيَاسَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِۦٓ أَلَا تَتَّقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlipowaambia watu wake: Hamumchi Mungu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَتَدْعُونَ بَعْلًا وَتَذَرُونَ أَحْسَنَ ٱلْخَٰلِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱللَّهَ رَبَّكُمْ وَرَبَّ ءَابَآئِكُمُ ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tumemwachia (sifa nzuri) kwa waliokuja baadaye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَلَٰمٌ عَلَىٰٓ إِلْ يَاسِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIwe salama kwa Ilyas.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika hivyo ndivyo tunavyowalipa walio wema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّهُۥ مِنْ عِبَادِنَا ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika yeye ni katika waja wetu walioamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ لُوطًا لَّمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ نَجَّيْنَٰهُ وَأَهْلَهُۥٓ أَجْمَعِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTulipomwokoa yeye na ahali zake wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا عَجُوزًا فِى ٱلْغَٰبِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa mwanamke mkongwe katika wale waliobakia nyuma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ دَمَّرْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha tukawaangamiza wale wengineo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّكُمْ لَتَمُرُّونَ عَلَيْهِم مُّصْبِحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَبِٱلَّيْلِ أَفَلَا تَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa usiku. Basi je, hamyatii akilini?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ أَبَقَ إِلَى ٱلْفُلْكِ ٱلْمَشْحُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlipokimbia akenda katika jahazi lililosheheni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ ٱلْمُدْحَضِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walioshindwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱلْتَقَمَهُ ٱلْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSamaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَوْلَآ أَنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلْمُسَبِّحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ingelikuwa hakuwa katika wanaomtakasa Mwenyezi Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَلَبِثَ فِى بَطْنِهِۦٓ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBila ya shaka angelikaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَنَبَذْنَٰهُ بِٱلْعَرَآءِ وَهُوَ سَقِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنۢبَتْنَا عَلَيْهِ شَجَرَةً مِّن يَقْطِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukauotesha juu yake mmea wa aina ya mung'unye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَرْسَلْنَٰهُ إِلَىٰ مِا۟ئَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَـَٔامَنُوا۟ فَمَتَّعْنَٰهُمْ إِلَىٰ حِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱسْتَفْتِهِمْ أَلِرَبِّكَ ٱلْبَنَاتُ وَلَهُمُ ٱلْبَنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ خَلَقْنَا ٱلْمَلَٰٓئِكَةَ إِنَٰثًا وَهُمْ شَٰهِدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَآ إِنَّهُم مِّنْ إِفْكِهِمْ لَيَقُولُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTazama, hakika ni kwa uzushi wao ndio wanasema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَدَ ٱللَّهُ وَإِنَّهُمْ لَكَٰذِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَصْطَفَى ٱلْبَنَاتِ عَلَى ٱلْبَنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAti amehiari watoto wa kike kuliko wanaume?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَلَا تَذَكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHamkumbuki?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ لَكُمْ سُلْطَٰنٌ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu mnayo hoja iliyo wazi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأْتُوا۟ بِكِتَٰبِكُمْ إِن كُنتُمْ صَٰدِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi leteni Kitabu chenu kama nyinyi ni wakweli.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَعَلُوا۟ بَيْنَهُۥ وَبَيْنَ ٱلْجِنَّةِ نَسَبًا وَلَقَدْ عَلِمَتِ ٱلْجِنَّةُ إِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wameweka mahusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwishajua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سُبْحَٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmetakasika Mwenyezi Mungu mbali na hayo wanayomsingizia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa waja wa Mwenyezi Mungu waliosafishwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi hakika nyinyi na mnaowaabudu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَآ أَنتُمْ عَلَيْهِ بِفَٰتِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHamwezi kuwapoteza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا مَنْ هُوَ صَالِ ٱلْجَحِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa yule atakayeingia Motoni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا مِنَّآ إِلَّا لَهُۥ مَقَامٌ مَّعْلُومٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّا لَنَحْنُ ٱلصَّآفُّونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّا لَنَحْنُ ٱلْمُسَبِّحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika sisi ndio wenye kutakasa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن كَانُوا۟ لَيَقُولُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walikuwapo waliokuwa wakisema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَوْ أَنَّ عِندَنَا ذِكْرًا مِّنَ ٱلْأَوَّلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTungelikuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَكُنَّا عِبَادَ ٱللَّهِ ٱلْمُخْلَصِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBila ya shaka tungelikuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye kumkusudia Yeye tu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَكَفَرُوا۟ بِهِۦ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini waliukufuru. Basi watakuja jua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ سَبَقَتْ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu waliotumwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّهُمْ لَهُمُ ٱلْمَنصُورُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYa kuwa wao bila ya shaka ndio watakaonusuriwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ ٱلْغَٰلِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwamba jeshi letu ndilo litakaloshinda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi waachilie mbali kwa muda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَبْصِرْهُمْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watazame, nao wataona.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, wanaiharakishia adhabu yetu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمْ فَسَآءَ صَبَاحُ ٱلْمُنذَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi itakaposhuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walioonywa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waache kwa muda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَبْصِرْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tazama, na wao wataona.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سُبْحَٰنَ رَبِّكَ رَبِّ ٱلْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmetakasika Mola wako Mlezi Mwenye utukufu mbali na yale wanayomzulia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَسَلَٰمٌ عَلَى ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Salamu juu ya Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70