caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Yaseen يس

Aya 83 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 41

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ يسٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYa Sin.[1]

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلْقُرْءَانِ ٱلْحَكِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Ninaapa) kwa Qur-ani yenye hekima!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّكَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wewe ni miongoni mwa waliotumwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJuu ya njia iliyonyooka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تَنزِيلَ ٱلْعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterUteremsho wa Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّآ أُنذِرَ ءَابَآؤُهُمْ فَهُمْ غَٰفِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa, basi wao wamekuwa wenye kughafilika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَقَدْ حَقَّ ٱلْقَوْلُ عَلَىٰٓ أَكْثَرِهِمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBila ya shaka kauli imekwisha thibiti juu ya wengi katika wao, kwa hivyo hawaamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا جَعَلْنَا فِىٓ أَعْنَٰقِهِمْ أَغْلَٰلًا فَهِىَ إِلَى ٱلْأَذْقَانِ فَهُم مُّقْمَحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTumeweka makongwa shingoni mwao, yakawafika videvuni. Kwa hivyo vichwa vyao viko juu tu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَعَلْنَا مِنۢ بَيْنِ أَيْدِيهِمْ سَدًّا وَمِنْ خَلْفِهِمْ سَدًّا فَأَغْشَيْنَٰهُمْ فَهُمْ لَا يُبْصِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTumeweka kizuizi mbele yao, na kizuizi nyuma yao. Na tumewafunika macho yao, kwa hivyo hawaoni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَسَوَآءٌ عَلَيْهِمْ ءَأَنذَرْتَهُمْ أَمْ لَمْ تُنذِرْهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi sawa sawa kwao ukiwaonya au usiwaonye, hawataamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّمَا تُنذِرُ مَنِ ٱتَّبَعَ ٱلذِّكْرَ وَخَشِىَ ٱلرَّحْمَٰنَ بِٱلْغَيْبِ فَبَشِّرْهُ بِمَغْفِرَةٍ وَأَجْرٍ كَرِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wewe unamwonya mwenye kufuata ukumbusho, na akamcha Arrahman (Mwingi wa rehema), kwa ghaibu. Basi mbashirie huyo msamaha na ujira mwema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا نَحْنُ نُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا۟ وَءَاثَٰرَهُمْ وَكُلَّ شَىْءٍ أَحْصَيْنَٰهُ فِىٓ إِمَامٍ مُّبِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Sisi tunawafufua wafu na tunayaandika wanayoyatanguliza, na wanayoyaacha nyuma. Na kila kitu tumekihifadhi katika daftari la asili lenye kubainisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱضْرِبْ لَهُم مَّثَلًا أَصْحَٰبَ ٱلْقَرْيَةِ إِذْ جَآءَهَا ٱلْمُرْسَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wapigie mfano wa wakazi wa mji walipojiwa na Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ أَرْسَلْنَآ إِلَيْهِمُ ٱثْنَيْنِ فَكَذَّبُوهُمَا فَعَزَّزْنَا بِثَالِثٍ فَقَالُوٓا۟ إِنَّآ إِلَيْكُم مُّرْسَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTulipowatumia wawili, wakawakanusha. Basi tukawazidishia nguvu kwa mwingine wa tatu. Wakasema: "Hakika sisi tumetumwa kwenu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ مَآ أَنتُمْ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا وَمَآ أَنزَلَ ٱلرَّحْمَٰنُ مِن شَىْءٍ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَكْذِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: "Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Na Mwingi wa Rehema hakuteremsha kitu. Nyinyi mnasema uongo tu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ رَبُّنَا يَعْلَمُ إِنَّآ إِلَيْكُمْ لَمُرْسَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: "Mola wetu Mlezi anajua kwamba hakika sisi tumetumwa kwenu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا عَلَيْنَآ إِلَّا ٱلْبَلَٰغُ ٱلْمُبِينُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوٓا۟ إِنَّا تَطَيَّرْنَا بِكُمْ لَئِن لَّمْ تَنتَهُوا۟ لَنَرْجُمَنَّكُمْ وَلَيَمَسَّنَّكُم مِّنَّا عَذَابٌ أَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: "Sisi hakika sisi tunaona mkosi kwenu. Ikiwa hamtaacha basi kwa yakini tutakupigeni mawe, na mtapata adhabu chungu kutoka kwetu."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ طَٰٓئِرُكُم مَّعَكُمْ أَئِن ذُكِّرْتُم بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWakasema: "Mkosi wenu mnao wenyewe! Je! Ni kwa kuwa mnakumbushwa? Ama nyinyi ni watu waliopindukia mipaka."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَآءَ مِنْ أَقْصَا ٱلْمَدِينَةِ رَجُلٌ يَسْعَىٰ قَالَ يَٰقَوْمِ ٱتَّبِعُوا۟ ٱلْمُرْسَلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akaja mtu mbio kutokea upande wa mbali wa mjini, akasema: "Enyi watu wangu! Wafuateni hawa waliotumwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱتَّبِعُوا۟ مَن لَّا يَسْـَٔلُكُمْ أَجْرًا وَهُم مُّهْتَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWafuateni ambao hawakutakini ujira, hali ya kuwa wenyewe wameongoka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا لِىَ لَآ أَعْبُدُ ٱلَّذِى فَطَرَنِى وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa nini nisimuabudu yule aliyeniumba na kwake nitarejeshwa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ءَأَتَّخِذُ مِن دُونِهِۦٓ ءَالِهَةً إِن يُرِدْنِ ٱلرَّحْمَٰنُ بِضُرٍّ لَّا تُغْنِ عَنِّى شَفَٰعَتُهُمْ شَيْـًٔا وَلَا يُنقِذُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, niishike miungu mingine badala yake? Arrahmani (Mwingi wa Rehema) akinitakia madhara uombezi wa hao hautanifaa kitu, wala hawataniokoa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنِّىٓ إِذًا لَّفِى ضَلَٰلٍ مُّبِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi hakika mimi hapo nitakuwa katika upotovu ulio dhahiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنِّىٓ ءَامَنتُ بِرَبِّكُمْ فَٱسْمَعُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika mimi nimemuamini Mola wenu Mlezi, basi nisikilizeni!"

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قِيلَ ٱدْخُلِ ٱلْجَنَّةَ قَالَ يَٰلَيْتَ قَوْمِى يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkaambiwa: "Ingia Peponi!" Akasema: "Laiti kuwa watu wangu wangelijua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بِمَا غَفَرَ لِى رَبِّى وَجَعَلَنِى مِنَ ٱلْمُكْرَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJinsi Mola wangu Mlezi alivyonisamehe, na akanifanya miongoni mwa walioheshimiwa."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَنزَلْنَا عَلَىٰ قَوْمِهِۦ مِنۢ بَعْدِهِۦ مِن جُندٍ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا كُنَّا مُنزِلِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hatukuwateremshia kaumu yake baada yake jeshi kutoka mbinguni, wala si wenye kuteremsha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً فَإِذَا هُمْ خَٰمِدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHaukuwa ila ukelele mmoja tu, na mara walizimwa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰحَسْرَةً عَلَى ٱلْعِبَادِ مَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNawasikitikia waja wangu. Hawajii Mtume ila wao humkejeli.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ يَرَوْا۟ كَمْ أَهْلَكْنَا قَبْلَهُم مِّنَ ٱلْقُرُونِ أَنَّهُمْ إِلَيْهِمْ لَا يَرْجِعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawaoni umma ngapi tulizoziangamiza kabla yao? Hakika hao hawarejei tena kwao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن كُلٌّ لَّمَّا جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hapana mmoja ila wote watakusanywa waletwe mbele yetu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَءَايَةٌ لَّهُمُ ٱلْأَرْضُ ٱلْمَيْتَةُ أَحْيَيْنَٰهَا وَأَخْرَجْنَا مِنْهَا حَبًّا فَمِنْهُ يَأْكُلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Ishara hiyo kwao ni ardhi iliyokufa, nasi tukaifufua, na tukatoa ndani yake nafaka, wakawa wanakula katika hizo!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَعَلْنَا فِيهَا جَنَّٰتٍ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَٰبٍ وَفَجَّرْنَا فِيهَا مِنَ ٱلْعُيُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukafanya ndani yake mabustani ya mitende na mizabibu, na tukatimbua chemichemi ndani yake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِيَأْكُلُوا۟ مِن ثَمَرِهِۦ وَمَا عَمِلَتْهُ أَيْدِيهِمْ أَفَلَا يَشْكُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli wale katika matunda yake, na hayo hayakufanywa na mikono yao! Basi je, hawashukuru?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سُبْحَٰنَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلْأَزْوَٰجَ كُلَّهَا مِمَّا تُنۢبِتُ ٱلْأَرْضُ وَمِنْ أَنفُسِهِمْ وَمِمَّا لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmetakasika yule aliyeumba dume na jike vyote katika vinavyomea katika ardhi na katika nafsi zao, na katika wasivyovijua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَءَايَةٌ لَّهُمُ ٱلَّيْلُ نَسْلَخُ مِنْهُ ٱلنَّهَارَ فَإِذَا هُم مُّظْلِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa usiku ni Ishara kwao. Tunauvua humo mchana, mara wao wanakuwa gizani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلشَّمْسُ تَجْرِى لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ ٱلْعَزِيزِ ٱلْعَلِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa jua linakwenda kwa kiwango chake. Hayo ni makadirio ya Mwenye nguvu, Mwenye kujua vyema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلْقَمَرَ قَدَّرْنَٰهُ مَنَازِلَ حَتَّىٰ عَادَ كَٱلْعُرْجُونِ ٱلْقَدِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mwezi tumeupimia vituo, mpaka unakuwa kama karara kongwe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا ٱلشَّمْسُ يَنۢبَغِى لَهَآ أَن تُدْرِكَ ٱلْقَمَرَ وَلَا ٱلَّيْلُ سَابِقُ ٱلنَّهَارِ وَكُلٌّ فِى فَلَكٍ يَسْبَحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHaliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na vyote vinaogelea katika njia zao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَءَايَةٌ لَّهُمْ أَنَّا حَمَلْنَا ذُرِّيَّتَهُمْ فِى ٱلْفُلْكِ ٱلْمَشْحُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni Ishara kwao kwamba Sisi tuliwapakia dhuria zao katika jahazi lililosheheni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَخَلَقْنَا لَهُم مِّن مِّثْلِهِۦ مَا يَرْكَبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawaumbia kutoka mfano wake wanavyovipanda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن نَّشَأْ نُغْرِقْهُمْ فَلَا صَرِيخَ لَهُمْ وَلَا هُمْ يُنقَذُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukitaka, tunawazamisha, wala hapana wa kuwasaidia, wala hawaokolewi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا رَحْمَةً مِّنَّا وَمَتَٰعًا إِلَىٰ حِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa kwa rehema zitokazo kwetu na starehe kwa muda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱتَّقُوا۟ مَا بَيْنَ أَيْدِيكُمْ وَمَا خَلْفَكُمْ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanapoambiwa: Jilindeni kutokana na yaliyoko mbele yenu na yaliyoko nyuma yenu, ili mpate kurehemewa...

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا تَأْتِيهِم مِّنْ ءَايَةٍ مِّنْ ءَايَٰتِ رَبِّهِمْ إِلَّا كَانُوا۟ عَنْهَا مُعْرِضِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa haiwafikii Ishara yoyote katika Ishara za Mola wao Mlezi isipokuwa wao huwa ni wenye kuipa mgongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ أَنفِقُوا۟ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ قَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَنُطْعِمُ مَن لَّوْ يَشَآءُ ٱللَّهُ أَطْعَمَهُۥٓ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا فِى ضَلَٰلٍ مُّبِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanapoambiwa: "Toeni katika aliyokupeni Mwenyezi Mungu", wale waliokufuru huwaambia wale walioamini: Je, tuwalishe wale ambao Mwenyezi Mungu angependa angeliwalisha mwenyewe? Nyinyi hammo isipokuwa katika upotovu ulio dhahiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَٰدِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi ni wakweli?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا يَنظُرُونَ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً تَأْخُذُهُمْ وَهُمْ يَخِصِّمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHawangojei isipokuwa ukelele mmoja tu utakaowachukua nao wamo kuzozana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَا يَسْتَطِيعُونَ تَوْصِيَةً وَلَآ إِلَىٰٓ أَهْلِهِمْ يَرْجِعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi hawataweza kuusia, wala kwa watu wao hawarejei.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنُفِخَ فِى ٱلصُّورِ فَإِذَا هُم مِّنَ ٱلْأَجْدَاثِ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يَنسِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa litapulizwa baragumu, mara watatoka makaburini wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ يَٰوَيْلَنَا مَنۢ بَعَثَنَا مِن مَّرْقَدِنَا هَٰذَا مَا وَعَدَ ٱلرَّحْمَٰنُ وَصَدَقَ ٱلْمُرْسَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema: Ole wetu! Ni nani aliyetufufua kwenye malazi yetu? Haya ndiyo aliyoyaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِن كَانَتْ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً فَإِذَا هُمْ جَمِيعٌ لَّدَيْنَا مُحْضَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHaitakuwa isipokuwa ukelele mmoja tu, mara wote watahudhurishwa mbele yetu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱلْيَوْمَ لَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْـًٔا وَلَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala hamtalipwa isipokuwa yale mliyokuwa mkiyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ أَصْحَٰبَ ٱلْجَنَّةِ ٱلْيَوْمَ فِى شُغُلٍ فَٰكِهُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika watu wa Bustani ya mbinguni leo wamo shughulini, wamefurahi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هُمْ وَأَزْوَٰجُهُمْ فِى ظِلَٰلٍ عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ مُتَّكِـُٔونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya viti vya kifahari.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَهُمْ فِيهَا فَٰكِهَةٌ وَلَهُم مَّا يَدَّعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatapata humo kila namna ya matunda na watapata kila watakachokitaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَلَٰمٌ قَوْلًا مِّن رَّبٍّ رَّحِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation Center"Salama!" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola Mlezi Mwenye kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱمْتَٰزُوا۟ ٱلْيَوْمَ أَيُّهَا ٱلْمُجْرِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa enyi wakosefu! Jitengeni leo!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ أَعْهَدْ إِلَيْكُمْ يَٰبَنِىٓ ءَادَمَ أَن لَّا تَعْبُدُوا۟ ٱلشَّيْطَٰنَ إِنَّهُۥ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, sikuagana nanyi, enyi wanadamu, kuwa msimuabudu Shetani? Hakika yeye ni adui dhahiri kwenu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنِ ٱعْبُدُونِى هَٰذَا صِرَٰطٌ مُّسْتَقِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo Njia iliyonyooka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ أَضَلَّ مِنكُمْ جِبِلًّا كَثِيرًا أَفَلَمْ تَكُونُوا۟ تَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka yeye amekwisha lipoteza kundi kubwa miongoni mwenu. Je, hamkuwa mkifikiri?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَٰذِهِۦ جَهَنَّمُ ٱلَّتِى كُنتُمْ تُوعَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHii basi ndiyo Jahannamu mliyokuwa mkiahidiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱصْلَوْهَا ٱلْيَوْمَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIngieni humo leo kwa vile mlivyokuwa mkikufuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلْيَوْمَ نَخْتِمُ عَلَىٰٓ أَفْوَٰهِهِمْ وَتُكَلِّمُنَآ أَيْدِيهِمْ وَتَشْهَدُ أَرْجُلُهُم بِمَا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLeo tunaviziba vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyokuwa wakiyachuma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْ نَشَآءُ لَطَمَسْنَا عَلَىٰٓ أَعْيُنِهِمْ فَٱسْتَبَقُوا۟ ٱلصِّرَٰطَ فَأَنَّىٰ يُبْصِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tungelipenda, tungeliyafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wangeionaje?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْ نَشَآءُ لَمَسَخْنَٰهُمْ عَلَىٰ مَكَانَتِهِمْ فَمَا ٱسْتَطَٰعُوا۟ مُضِيًّا وَلَا يَرْجِعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tungelitaka, tungewageuza sura hapo hapo walipo, basi wasingeweza kwenda wala kurudi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَن نُّعَمِّرْهُ نُنَكِّسْهُ فِى ٱلْخَلْقِ أَفَلَا يَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tunayemzeesha, tunamrudisha nyuma katika umbo. Basi je, hawazingatii?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا عَلَّمْنَٰهُ ٱلشِّعْرَ وَمَا يَنۢبَغِى لَهُۥٓ إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ وَقُرْءَانٌ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu isipokuwa ni ukumbusho na Qur-ani inayobainisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِّيُنذِرَ مَن كَانَ حَيًّا وَيَحِقَّ ٱلْقَوْلُ عَلَى ٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli imwonye aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّا خَلَقْنَا لَهُم مِّمَّا عَمِلَتْ أَيْدِينَآ أَنْعَٰمًا فَهُمْ لَهَا مَٰلِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawaoni kwamba tumewaumbia kutokana na iliyofanya mikono yetu wanyama wa mifugo, na wao wakawa wenye kuwamiliki.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَذَلَّلْنَٰهَا لَهُمْ فَمِنْهَا رَكُوبُهُمْ وَمِنْهَا يَأْكُلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Sisi tukawadhalilishia. Basi baadhi yao wako wanaowapanda, na baadhi yao wanawala.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَهُمْ فِيهَا مَنَٰفِعُ وَمَشَارِبُ أَفَلَا يَشْكُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je, hawashukuru?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱتَّخَذُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ ءَالِهَةً لَّعَلَّهُمْ يُنصَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu ili ati wapate kusaidiwa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَهُمْ وَهُمْ لَهُمْ جُندٌ مُّحْضَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio askari wao, watahudhurishwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَا يَحْزُنكَ قَوْلُهُمْ إِنَّا نَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi maneno yao yasikuhuzunishe. Hakika Sisi tunayajua wanayoyaweka siri na wanayoyadhihirisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوَلَمْ يَرَ ٱلْإِنسَٰنُ أَنَّا خَلَقْنَٰهُ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani mwanadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii? Kisha sasa yeye ndiyo amekuwa ndiye mgomvi wa dhahiri!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِىَ خَلْقَهُۥ قَالَ مَن يُحْىِ ٱلْعِظَٰمَ وَهِىَ رَمِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakayeihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ يُحْيِيهَا ٱلَّذِىٓ أَنشَأَهَآ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ataihuisha huyo huyo aliyeiumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kuumba.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلشَّجَرِ ٱلْأَخْضَرِ نَارًا فَإِذَآ أَنتُم مِّنْهُ تُوقِدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAliyekujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوَلَيْسَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ بِقَٰدِرٍ عَلَىٰٓ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُم بَلَىٰ وَهُوَ ٱلْخَلَّٰقُ ٱلْعَلِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani aliyeziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwani! Naye ndiye Muumbaji Mkuu, Mjuzi mno.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّمَآ أَمْرُهُۥٓ إِذَآ أَرَادَ شَيْـًٔا أَن يَقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika amri yake anapotaka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَسُبْحَٰنَ ٱلَّذِى بِيَدِهِۦ مَلَكُوتُ كُلِّ شَىْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake Yeye mtarejeshwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70