caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Saad ص

Aya 88 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 38

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ صٓ وَٱلْقُرْءَانِ ذِى ٱلذِّكْرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSwad. Ninaapa kwa Qur-ani yenye ukumbusho.[1]

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فِى عِزَّةٍ وَشِقَاقٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini waliokufuru wamo katika majivuno na upinzani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّن قَرْنٍ فَنَادَوا۟ وَّلَاتَ حِينَ مَنَاصٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMataifa mangapi tumeyaangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwishapita.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَعَجِبُوٓا۟ أَن جَآءَهُم مُّنذِرٌ مِّنْهُمْ وَقَالَ ٱلْكَٰفِرُونَ هَٰذَا سَٰحِرٌ كَذَّابٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walistaajabu kuwajia mwonyaji anayetokana nao wenyewe, na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo mno.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَجَعَلَ ٱلْـَٔالِهَةَ إِلَٰهًا وَٰحِدًا إِنَّ هَٰذَا لَشَىْءٌ عُجَابٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmewafanya miungu wote kuwa ni mungu mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱنطَلَقَ ٱلْمَلَأُ مِنْهُمْ أَنِ ٱمْشُوا۟ وَٱصْبِرُوا۟ عَلَىٰٓ ءَالِهَتِكُمْ إِنَّ هَٰذَا لَشَىْءٌ يُرَادُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu, kwani hili ni jambo lililopangwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا سَمِعْنَا بِهَٰذَا فِى ٱلْمِلَّةِ ٱلْـَٔاخِرَةِ إِنْ هَٰذَآ إِلَّا ٱخْتِلَٰقٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi tu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَءُنزِلَ عَلَيْهِ ٱلذِّكْرُ مِنۢ بَيْنِنَا بَلْ هُمْ فِى شَكٍّ مِّن ذِكْرِى بَل لَّمَّا يَذُوقُوا۟ عَذَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAti yeye tu ndiye aliyeteremshiwa mawaidha peke yake katika sisi? Lakini hao wana shaka na mawaidha yangu, bali hawajaionja adhabu yangu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ عِندَهُمْ خَزَآئِنُ رَحْمَةِ رَبِّكَ ٱلْعَزِيزِ ٱلْوَهَّابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu wanazo wao hazina za rehema za Mola wako Mlezi, Mwenye nguvu, Mpaji?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ لَهُم مُّلْكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَلْيَرْتَقُوا۟ فِى ٱلْأَسْبَٰبِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu wao wana ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo kati yavyo? Basi na wazipande njia za kwendea huko!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

جُندٌ مَّا هُنَالِكَ مَهْزُومٌ مِّنَ ٱلْأَحْزَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ni askari watakaoshindwa miongoni mwa makundi yatakayoshindwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَعَادٌ وَفِرْعَوْنُ ذُو ٱلْأَوْتَادِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalikanusha kabla yao kaumu ya Nuhu, na kina A'adi na Firauni mwenye majengo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَثَمُودُ وَقَوْمُ لُوطٍ وَأَصْحَٰبُ لْـَٔيْكَةِ أُو۟لَٰٓئِكَ ٱلْأَحْزَابُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Thamud na kaumu Luti na watu wa Machakani. Hayo ndiyo makundi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِن كُلٌّ إِلَّا كَذَّبَ ٱلرُّسُلَ فَحَقَّ عِقَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao wote waliwakadhibisha Mitume; basi wakastahiki adhabu yangu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا يَنظُرُ هَٰٓؤُلَآءِ إِلَّا صَيْحَةً وَٰحِدَةً مَّا لَهَا مِن فَوَاقٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hawa hawangojei ila ukelele mmoja tu usio wa kuchelewa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالُوا۟ رَبَّنَا عَجِّل لَّنَا قِطَّنَا قَبْلَ يَوْمِ ٱلْحِسَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walisema: ‘Mola wetu Mlezi! Tuletee upesi sehemu yetu ya adhabu kabla ya Siku ya Hesabu.’

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَٱذْكُرْ عَبْدَنَا دَاوُۥدَ ذَا ٱلْأَيْدِ إِنَّهُۥٓ أَوَّابٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSubiri kwa hayo wayasemayo, na umkumbuke mja wetu Daudi, mwenye nguvu. Hakika yeye alikuwa mwingi wa kutubia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا سَخَّرْنَا ٱلْجِبَالَ مَعَهُۥ يُسَبِّحْنَ بِٱلْعَشِىِّ وَٱلْإِشْرَاقِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika tuliidhalilisha milima pamoja naye ikisabihi jioni na asubuhi pamoja naye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلطَّيْرَ مَحْشُورَةً كُلٌّ لَّهُۥٓ أَوَّابٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pia ndege waliokusanywa makundi kwa makundi; wote walikuwa wanyenyekevu kwake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَشَدَدْنَا مُلْكَهُۥ وَءَاتَيْنَٰهُ ٱلْحِكْمَةَ وَفَصْلَ ٱلْخِطَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukautia nguvu ufalme wake, na tukampa hekima, na kukata hukumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَهَلْ أَتَىٰكَ نَبَؤُا۟ ٱلْخَصْمِ إِذْ تَسَوَّرُوا۟ ٱلْمِحْرَابَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa je, imekufikia habari ya wagombanao walipopindukia ukuta kuingia chumbani?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ دَخَلُوا۟ عَلَىٰ دَاوُۥدَ فَفَزِعَ مِنْهُمْ قَالُوا۟ لَا تَخَفْ خَصْمَانِ بَغَىٰ بَعْضُنَا عَلَىٰ بَعْضٍ فَٱحْكُم بَيْنَنَا بِٱلْحَقِّ وَلَا تُشْطِطْ وَٱهْدِنَآ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلصِّرَٰطِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalipomuingilia Daudi, naye akawaogopa. Wakasema: Usiogope! Sisi ni wagombanao wawili, mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe. Basi tuhukumu kwa haki, wala usipendelee. Na utuongoe kwenye njia iliyo sawa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ هَٰذَآ أَخِى لَهُۥ تِسْعٌ وَتِسْعُونَ نَعْجَةً وَلِىَ نَعْجَةٌ وَٰحِدَةٌ فَقَالَ أَكْفِلْنِيهَا وَعَزَّنِى فِى ٱلْخِطَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika huyu ndugu yangu ana kondoo wa kike tisini na tisa; na mimi ninaye kondoo mke mmoja. Akasema: Nipe huyo nikufugie! Na amenishinda kwa maneno.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ لَقَدْ ظَلَمَكَ بِسُؤَالِ نَعْجَتِكَ إِلَىٰ نِعَاجِهِۦ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ ٱلْخُلَطَآءِ لَيَبْغِى بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَقَلِيلٌ مَّا هُمْ وَظَنَّ دَاوُۥدُ أَنَّمَا فَتَنَّٰهُ فَٱسْتَغْفَرَ رَبَّهُۥ وَخَرَّ رَاكِعًا وَأَنَابَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Kweli amekudhulumu kwa kumtaka kondoo wako mmoja kuongezea kwenye kondoo wake. Na hakika washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipokuwa walioamini na wakatenda mema. Na hao ni wachache. Na Daudi akajua kuwa tumemfanyia mtihani. Basi akamwomba msamaha Mola wake Mlezi, na akaanguka kusujudu na kutubia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَغَفَرْنَا لَهُۥ ذَٰلِكَ وَإِنَّ لَهُۥ عِندَنَا لَزُلْفَىٰ وَحُسْنَ مَـَٔابٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukamsamehe kwa hayo. Naye kwa hakika anao mkaribisho mkubwa na marejeo mazuri kwetu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰدَاوُۥدُ إِنَّا جَعَلْنَٰكَ خَلِيفَةً فِى ٱلْأَرْضِ فَٱحْكُم بَيْنَ ٱلنَّاسِ بِٱلْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعِ ٱلْهَوَىٰ فَيُضِلَّكَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَضِلُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌۢ بِمَا نَسُوا۟ يَوْمَ ٱلْحِسَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEwe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio yakakupoteza ambali na Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika wanaoipotea Njia ya Mwenyezi Mungu wakaiacha, watapata adhabu kali kwa sababu ya kusahau kwao Siku ya Hisabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا خَلَقْنَا ٱلسَّمَآءَ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا بَٰطِلًا ذَٰلِكَ ظَنُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنَ ٱلنَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo kati yake bure. Hiyo ni dhana ya waliokufuru. Ole wao waliokufuru kwa Moto utakaowapata.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ نَجْعَلُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ كَٱلْمُفْسِدِينَ فِى ٱلْأَرْضِ أَمْ نَجْعَلُ ٱلْمُتَّقِينَ كَٱلْفُجَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, tuwafanye walioamini na wakatenda mema kama wafanyao uharibifu katika nchi? Au tuwafanye wacha Mungu kama waovu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كِتَٰبٌ أَنزَلْنَٰهُ إِلَيْكَ مُبَٰرَكٌ لِّيَدَّبَّرُوٓا۟ ءَايَٰتِهِۦ وَلِيَتَذَكَّرَ أُو۟لُوا۟ ٱلْأَلْبَٰبِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَوَهَبْنَا لِدَاوُۥدَ سُلَيْمَٰنَ نِعْمَ ٱلْعَبْدُ إِنَّهُۥٓ أَوَّابٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Daudi tukamtunukia Suleiman. Alikuwa mja mwema. Na hakika alikuwa mwingi wa kutubia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ عُرِضَ عَلَيْهِ بِٱلْعَشِىِّ ٱلصَّٰفِنَٰتُ ٱلْجِيَادُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlipopelekewa jioni farasi wasimamao kidete, tayari kutoka shoti.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَقَالَ إِنِّىٓ أَحْبَبْتُ حُبَّ ٱلْخَيْرِ عَن ذِكْرِ رَبِّى حَتَّىٰ تَوَارَتْ بِٱلْحِجَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi akasema: Navipenda vitu vizuri kwa kumkumbuka Mola wangu Mlezi. Kisha wakafichikana nyuma ya boma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

رُدُّوهَا عَلَىَّ فَطَفِقَ مَسْحًۢا بِٱلسُّوقِ وَٱلْأَعْنَاقِ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Akasema:) Nirudishieni hao! Basi akaanza kuwapapasa miguu na shingo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ فَتَنَّا سُلَيْمَٰنَ وَأَلْقَيْنَا عَلَىٰ كُرْسِيِّهِۦ جَسَدًا ثُمَّ أَنَابَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tulimtia mtihanini Suleiman, na tukauweka mwili juu ya kiti chake, kisha akarejea kwa kutubu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبِّ ٱغْفِرْ لِى وَهَبْ لِى مُلْكًا لَّا يَنۢبَغِى لِأَحَدٍ مِّنۢ بَعْدِىٓ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْوَهَّابُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usiomwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَسَخَّرْنَا لَهُ ٱلرِّيحَ تَجْرِى بِأَمْرِهِۦ رُخَآءً حَيْثُ أَصَابَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake, popote alipotaka kufika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلشَّيَٰطِينَ كُلَّ بَنَّآءٍ وَغَوَّاصٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukayafanya mashetani yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَءَاخَرِينَ مُقَرَّنِينَ فِى ٱلْأَصْفَادِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wengine wafungwao kwa minyororo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَٰذَا عَطَآؤُنَا فَٱمْنُنْ أَوْ أَمْسِكْ بِغَيْرِ حِسَابٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHiki ndicho kipawa chetu. Basi toa au zuia, bila ya hisabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ لَهُۥ عِندَنَا لَزُلْفَىٰ وَحُسْنَ مَـَٔابٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika yeye kwetu Sisi ana cheo cha kukaribishwa kwetu, na pahala pazuri pa kurejea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱذْكُرْ عَبْدَنَآ أَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُۥٓ أَنِّى مَسَّنِىَ ٱلشَّيْطَٰنُ بِنُصْبٍ وَعَذَابٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mkumbuke mja wetu Ayubu alipomwita Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika Shetani amenifikishia udhia na adhabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱرْكُضْ بِرِجْلِكَ هَٰذَا مُغْتَسَلٌۢ بَارِدٌ وَشَرَابٌ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Akaambiwa:) Piga-piga ardhi kwa mguu wako! Basi haya maji baridi ya kuogea na ya kunywa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَوَهَبْنَا لَهُۥٓ أَهْلَهُۥ وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنَّا وَذِكْرَىٰ لِأُو۟لِى ٱلْأَلْبَٰبِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukampa ahali zake na wengine kama wao pamoja nao, kuwa ni rehema itokayo kwetu, na iwe kumbusho kwa watu wenye akili.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَخُذْ بِيَدِكَ ضِغْثًا فَٱضْرِب بِّهِۦ وَلَا تَحْنَثْ إِنَّا وَجَدْنَٰهُ صَابِرًا نِّعْمَ ٱلْعَبْدُ إِنَّهُۥٓ أَوَّابٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa shika kicha cha vijiti tu mkononi mwako, kisha ndio upigie nacho, wala usivunje kiapo. Hakika tulimkuta mwenye subira, mbora wa waja, kwa hakika alikuwa mwingi wa kutubu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱذْكُرْ عِبَٰدَنَآ إِبْرَٰهِيمَ وَإِسْحَٰقَ وَيَعْقُوبَ أُو۟لِى ٱلْأَيْدِى وَٱلْأَبْصَٰرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakumbuke waja wetu, Ibrahim na Is-haqa na Yaa'qubu waliokuwa na nguvu na busara.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّآ أَخْلَصْنَٰهُم بِخَالِصَةٍ ذِكْرَى ٱلدَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSisi tumewahusisha wao kwa sifa ya ukumbusho wa Akhera.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّهُمْ عِندَنَا لَمِنَ ٱلْمُصْطَفَيْنَ ٱلْأَخْيَارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa walio bora.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱذْكُرْ إِسْمَٰعِيلَ وَٱلْيَسَعَ وَذَا ٱلْكِفْلِ وَكُلٌّ مِّنَ ٱلْأَخْيَارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mtaje Ismail na Alyasaa na Dhulkifli, na wote hao ni katika walio bora.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَٰذَا ذِكْرٌ وَإِنَّ لِلْمُتَّقِينَ لَحُسْنَ مَـَٔابٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuu ni ukumbusho. Na hakika wacha Mungu wana marudio mazuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

جَنَّٰتِ عَدْنٍ مُّفَتَّحَةً لَّهُمُ ٱلْأَبْوَٰبُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBustani za milele zitakazofunguliwa milango yao kwa ajili yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مُتَّكِـِٔينَ فِيهَا يَدْعُونَ فِيهَا بِفَٰكِهَةٍ كَثِيرَةٍ وَشَرَابٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHumo wataegemea matakia, wawe wanaagiza humo matunda mengi na vinywaji.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَعِندَهُمْ قَٰصِرَٰتُ ٱلطَّرْفِ أَتْرَابٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pamoja nao wake zao wenye kutuliza macho, hirimu moja.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَٰذَا مَا تُوعَدُونَ لِيَوْمِ ٱلْحِسَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHaya ndiyo mliyoahidiwa kwa Siku ya Hisabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ هَٰذَا لَرِزْقُنَا مَا لَهُۥ مِن نَّفَادٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika hii ndiyo riziki yetu isiyomalizika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَٰذَا وَإِنَّ لِلطَّٰغِينَ لَشَرَّ مَـَٔابٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNdiyo hivi! Na hakika wenye kuasi bila ya shaka watapata marudio maovu kabisa;

Tazama tafsiri zote za aya hii →

جَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا فَبِئْسَ ٱلْمِهَادُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNayo ni Jahannamu! Wataingia humo. Nacho hicho ni kitanda kiovu mno cha kulalia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَٰذَا فَلْيَذُوقُوهُ حَمِيمٌ وَغَسَّاقٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNdiyo hivi! Basi na wayaonje maji ya moto na ya usaha!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَءَاخَرُ مِن شَكْلِهِۦٓ أَزْوَٰجٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa adhabu nyenginezo za namna hii.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَٰذَا فَوْجٌ مُّقْتَحِمٌ مَّعَكُمْ لَا مَرْحَبًۢا بِهِمْ إِنَّهُمْ صَالُوا۟ ٱلنَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHili ndilo kundi litakalo ingia pamoja nanyi. Hapana makaribisho mema kwao. Hakika hao wanaingia Motoni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ بَلْ أَنتُمْ لَا مَرْحَبًۢا بِكُمْ أَنتُمْ قَدَّمْتُمُوهُ لَنَا فَبِئْسَ ٱلْقَرَارُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaseme: Lakini nyinyi! Hamna mapokezi mazuri! Nyinyi ndio mliotusababishia haya, napo ni pahala paovu kabisa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ رَبَّنَا مَن قَدَّمَ لَنَا هَٰذَا فَزِدْهُ عَذَابًا ضِعْفًا فِى ٱلنَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaseme: Mola wetu Mlezi aliyetusababishia haya, mzidishie adhabu mara mbili Motoni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالُوا۟ مَا لَنَا لَا نَرَىٰ رِجَالًا كُنَّا نَعُدُّهُم مِّنَ ٱلْأَشْرَارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema: Tuna nini hata hatuwaoni wale watu ambao tukiwahisabu ndio katika waovu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَتَّخَذْنَٰهُمْ سِخْرِيًّا أَمْ زَاغَتْ عَنْهُمُ ٱلْأَبْصَٰرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTulikosea tulipowafanyia masihara, au macho yetu tu hayawaoni?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ذَٰلِكَ لَحَقٌّ تَخَاصُمُ أَهْلِ ٱلنَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika hayo bila ya shaka ndiyo mahasimiano ya watu wa Motoni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ إِنَّمَآ أَنَا۠ مُنذِرٌ وَمَا مِنْ إِلَٰهٍ إِلَّا ٱللَّهُ ٱلْوَٰحِدُ ٱلْقَهَّارُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Hakika mimi ni mwonyaji tu; na hapana mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja, Mtenda nguvu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ٱلْعَزِيزُ ٱلْغَفَّٰرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ هُوَ نَبَؤٌا۟ عَظِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Hii ni habari kubwa kabisa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَنتُمْ عَنْهُ مُعْرِضُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbayo nyinyi mnaipuuza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا كَانَ لِىَ مِنْ عِلْمٍۭ بِٱلْمَلَإِ ٱلْأَعْلَىٰٓ إِذْ يَخْتَصِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSikuwa na elimu ya mambo ya viumbe wakuu watukufu walipokuwa wakishindana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِن يُوحَىٰٓ إِلَىَّ إِلَّآ أَنَّمَآ أَنَا۠ نَذِيرٌ مُّبِينٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHaikufunuliwa kwangu isipokuwa ya kwamba hakika mimi ni mwonyaji dhahiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَٰٓئِكَةِ إِنِّى خَٰلِقٌۢ بَشَرًا مِّن طِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMola wako Mlezi alipowaambia Malaika: Hakika Mimi nitaumba mtu kutokana na udongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِذَا سَوَّيْتُهُۥ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِى فَقَعُوا۟ لَهُۥ سَٰجِدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa nitakapomkamilisha na kumpulizia roho inayotokana nami, basi muangukieni kwa kumtii.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَسَجَدَ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi wakasujudu Malaika wote pamoja.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّآ إِبْلِيسَ ٱسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ ٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa Iblisi; alijivuna na akawa katika makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ يَٰٓإِبْلِيسُ مَا مَنَعَكَ أَن تَسْجُدَ لِمَا خَلَقْتُ بِيَدَىَّ أَسْتَكْبَرْتَ أَمْ كُنتَ مِنَ ٱلْعَالِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu akamwambia: Ewe Iblisi! Kipi kilichokuzuia kumtii yule niliyemuumba kwa mikono yangu? Je, umejiona mkubwa, au umekuwa katika wakuu kweli?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ أَنَا۠ خَيْرٌ مِّنْهُ خَلَقْتَنِى مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُۥ مِن طِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, na yeye umemuumba kwa udongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ فَٱخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe umelaaniwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنَّ عَلَيْكَ لَعْنَتِىٓ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلدِّينِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika laana yangu itakuwa juu yako mpaka Siku ya Malipo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ رَبِّ فَأَنظِرْنِىٓ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watakayofufuliwa viumbe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلْمُنظَرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu akasema: Basi umekwisha kuwa miongoni mwa waliopewa muhula.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْوَقْتِ ٱلْمَعْلُومِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMpaka siku ya wakati maalumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema (Iblisi): Naapa kwa utukufu wako, bila ya shaka nitawapoteza wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ ٱلْمُخْلَصِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa wale waja wako miongoni mwao waliohitariwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ فَٱلْحَقُّ وَٱلْحَقَّ أَقُولُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema: Haki! Na haki ninaisema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكَ وَمِمَّن تَبِعَكَ مِنْهُمْ أَجْمَعِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBila ya shaka nitaijaza Jahannamu kwa wewe na kwa hao wote wenye kukufuata miongoni mwao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ مَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلْمُتَكَلِّفِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema (Ewe Mtume): Sikuombeni ujira juu ya haya, wala mimi si katika wadanganyifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayakuwa haya ila ni mawaidha kwa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَتَعْلَمُنَّ نَبَأَهُۥ بَعْدَ حِينٍۭ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka mtajua habari zake baada ya muda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70