Mwanzo › Sura › Sura Az-Zukhruf
Sura Az-Zukhruf الزخرف
Aya 89 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 63
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ حمٓ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ha Mim.[1]
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلْكِتَٰبِ ٱلْمُبِينِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ninaapa kwa Kitabu kinachobainisha.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّا جَعَلْنَٰهُ قُرْءَٰنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Sisi tumeifanya Qur-ani kwa Kiarabu ili mfahamu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِنَّهُۥ فِىٓ أُمِّ ٱلْكِتَٰبِ لَدَيْنَا لَعَلِىٌّ حَكِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika hiyo imo katika Asili ya Maandiko yaliyoko kwetu, ni tukufu na yenye hekima.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَفَنَضْرِبُ عَنكُمُ ٱلذِّكْرَ صَفْحًا أَن كُنتُمْ قَوْمًا مُّسْرِفِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Je, tuache kuwakumbusha kabisa kwa kuwa nyinyi ni watu mliopita mipaka kwa ukafiri?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَكَمْ أَرْسَلْنَا مِن نَّبِىٍّ فِى ٱلْأَوَّلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Manabii wangapi tuliwatuma kwa watu wa zamani!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا يَأْتِيهِم مِّن نَّبِىٍّ إِلَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hawajii Nabii yeyote ila walikuwa wakimkejeli.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَأَهْلَكْنَآ أَشَدَّ مِنْهُم بَطْشًا وَمَضَىٰ مَثَلُ ٱلْأَوَّلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tuliwaangamiza waliokuwa na nguvu kushinda wao. Na mfano wa watu wa zamani umekwisha pita.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ خَلَقَهُنَّ ٱلْعَزِيزُ ٱلْعَلِيمُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ukiwauliza: 'Nani aliyeziumba mbingu na ardhi?' Bila ya shaka watasema: 'Kaziumba Mwenye nguvu, ajuaye zaidi.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلْأَرْضَ مَهْدًا وَجَعَلَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلًا لَّعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ambaye amewafanyieni ardhi kama tandiko, na akawafanyieni ndani yake njia mpate kuongoka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلَّذِى نَزَّلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءًۢ بِقَدَرٍ فَأَنشَرْنَا بِهِۦ بَلْدَةً مَّيْتًا كَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ambaye ndiye aliyeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi, na kwa hayo tukaifufua nchi iliyokufa. Na namna hivi ndivyo mtakavyotolewa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلَّذِى خَلَقَ ٱلْأَزْوَٰجَ كُلَّهَا وَجَعَلَ لَكُم مِّنَ ٱلْفُلْكِ وَٱلْأَنْعَٰمِ مَا تَرْكَبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ambaye ndiye aliyeumba katika kila kitu jike na dume, na akawafanyieni merikebu na wanyama mnaowapanda.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لِتَسْتَوُۥا۟ عَلَىٰ ظُهُورِهِۦ ثُمَّ تَذْكُرُوا۟ نِعْمَةَ رَبِّكُمْ إِذَا ٱسْتَوَيْتُمْ عَلَيْهِ وَتَقُولُوا۟ سُبْحَٰنَ ٱلَّذِى سَخَّرَ لَنَا هَٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُۥ مُقْرِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ili mkae vizuri migongoni mwao, kisha mkumbuke neema za Mola wenu Mlezi mnapokaa sawa sawa juu yao, na mseme: 'Ametakasika aliyemfanya huyu atutumikie, na tusingeliweza kufanya haya wenyewe.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا لَمُنقَلِبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika sisi tutarudi kwa Mola wetu Mlezi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَجَعَلُوا۟ لَهُۥ مِنْ عِبَادِهِۦ جُزْءًا إِنَّ ٱلْإِنسَٰنَ لَكَفُورٌ مُّبِينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na wanamfanyia katika waja wake fungu. Kwa hakika mwanadamu ni mtovu wa fadhila aliye dhahiri.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمِ ٱتَّخَذَ مِمَّا يَخْلُقُ بَنَاتٍ وَأَصْفَىٰكُم بِٱلْبَنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au amejichukulia watoto wanawake katika vile alivyoviumba, na akakuteulieni nyinyi watoto wanaume?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُم بِمَا ضَرَبَ لِلرَّحْمَٰنِ مَثَلًا ظَلَّ وَجْهُهُۥ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na anapobashiriwa mmoja wao kwa yale aliyompigia mfano Mwenyezi Mungu, uso wake husawijika na hujaa hasira.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَوَمَن يُنَشَّؤُا۟ فِى ٱلْحِلْيَةِ وَهُوَ فِى ٱلْخِصَامِ غَيْرُ مُبِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ati aliyelelewa katika mapambo na katika mabishano hawezi kusema kwa bayana?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَجَعَلُوا۟ ٱلْمَلَٰٓئِكَةَ ٱلَّذِينَ هُمْ عِبَٰدُ ٱلرَّحْمَٰنِ إِنَٰثًا أَشَهِدُوا۟ خَلْقَهُمْ سَتُكْتَبُ شَهَٰدَتُهُمْ وَيُسْـَٔلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake! Kwani wameshuhudia kuumbwa kwao? Ushahidi wao utaandikwa na wao watahojiwa!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَقَالُوا۟ لَوْ شَآءَ ٱلرَّحْمَٰنُ مَا عَبَدْنَٰهُم مَّا لَهُم بِذَٰلِكَ مِنْ عِلْمٍ إِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nao husema: 'Angelipenda Mwingi wa Rehema tusingeliwaabudu sisi.' Hawana ujuzi wowote wa hayo! Hawana ila kusema uongo tu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ ءَاتَيْنَٰهُمْ كِتَٰبًا مِّن قَبْلِهِۦ فَهُم بِهِۦ مُسْتَمْسِكُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwani tuliwapa Kitabu kabla ya hiki, na ikawa wao wanakishikilia hicho.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
بَلْ قَالُوٓا۟ إِنَّا وَجَدْنَآ ءَابَآءَنَا عَلَىٰٓ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِم مُّهْتَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Bali wanasema: 'Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini mahsusi, basi na sisi tunafuata nyayo zao.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَكَذَٰلِكَ مَآ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِى قَرْيَةٍ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتْرَفُوهَآ إِنَّا وَجَدْنَآ ءَابَآءَنَا عَلَىٰٓ أُمَّةٍ وَإِنَّا عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِم مُّقْتَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila watu wake waliodeka kwa starehe walisema: 'Hakika sisi tuliwakuta baba zetu wanashika dini mahsusi, na sisi tunafuata nyayo zao.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَٰلَ أَوَلَوْ جِئْتُكُم بِأَهْدَىٰ مِمَّا وَجَدتُّمْ عَلَيْهِ ءَابَآءَكُمْ قَالُوٓا۟ إِنَّا بِمَآ أُرْسِلْتُم بِهِۦ كَٰفِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Akasema (Mwonyaji): 'Hata nikiwaletea yenye uwongofu bora kuliko mliowakuta nao baba zenu?' Wakasema: 'Sisi tunayakataa tu hayo mliyotumwa nayo.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱنتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلْمُكَذِّبِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa hivyo, tukawalipizia. Basi angalia ulikuwaje mwisho wa waliokadhibisha!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِذْ قَالَ إِبْرَٰهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِۦٓ إِنَّنِى بَرَآءٌ مِّمَّا تَعْبُدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na pale Ibrahim alipomwambia baba yake na kaumu yake: 'Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayoyaabudu.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِلَّا ٱلَّذِى فَطَرَنِى فَإِنَّهُۥ سَيَهْدِينِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Isipokuwa yule aliyeniumba, kwani Yeye ataniongoa.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَجَعَلَهَا كَلِمَةًۢ بَاقِيَةً فِى عَقِبِهِۦ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
بَلْ مَتَّعْتُ هَٰٓؤُلَآءِ وَءَابَآءَهُمْ حَتَّىٰ جَآءَهُمُ ٱلْحَقُّ وَرَسُولٌ مُّبِينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka ikawafikia Haki na Mtume aliyebainisha.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَمَّا جَآءَهُمُ ٱلْحَقُّ قَالُوا۟ هَٰذَا سِحْرٌ وَإِنَّا بِهِۦ كَٰفِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ilipowafikia Haki wakasema: 'Huu ni uchawi, na sisi hakika tunaukataa.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَقَالُوا۟ لَوْلَا نُزِّلَ هَٰذَا ٱلْقُرْءَانُ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنَ ٱلْقَرْيَتَيْنِ عَظِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na walisema: 'Kwa nini Qur-ani hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii?'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَتَ رَبِّكَ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُم مَّعِيشَتَهُمْ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَٰتٍ لِّيَتَّخِذَ بَعْضُهُم بَعْضًا سُخْرِيًّا وَرَحْمَتُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwani wao ndio wanaogawa rehema za Mola wako Mlezi? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wengineo wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayoyakusanya.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَوْلَآ أَن يَكُونَ ٱلنَّاسُ أُمَّةً وَٰحِدَةً لَّجَعَلْنَا لِمَن يَكْفُرُ بِٱلرَّحْمَٰنِ لِبُيُوتِهِمْ سُقُفًا مِّن فِضَّةٍ وَمَعَارِجَ عَلَيْهَا يَظْهَرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na lau isingekuwa watu watakuwa kundi moja, tungeliwajaalia wanaomkufuru Rahmani nyumba zao kuwa na dari ya fedha, na ngazi zao pia wanazopandia
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلِبُيُوتِهِمْ أَبْوَٰبًا وَسُرُرًا عَلَيْهَا يَتَّكِـُٔونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na milango ya nyumba zao na vitanda wanavyoegemea juu yake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَزُخْرُفًا وَإِن كُلُّ ذَٰلِكَ لَمَّا مَتَٰعُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةُ عِندَ رَبِّكَ لِلْمُتَّقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na mapambo. Lakini hayo si chochote ila ni starehe ya maisha ya dunia tu, na Akhera iliyoko kwa Mola wako Mlezi ni ya wenye kumcha Mungu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَن يَعْشُ عَن ذِكْرِ ٱلرَّحْمَٰنِ نُقَيِّضْ لَهُۥ شَيْطَٰنًا فَهُوَ لَهُۥ قَرِينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Anayeyafanyia upofu maneno ya Rahmani tunamwekea Shetani kuwa ndiye rafiki yake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِنَّهُمْ لَيَصُدُّونَهُمْ عَنِ ٱلسَّبِيلِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika wao wanawazuilia Njia na wenyewe wanadhani kuwa wameongoka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَنَا قَالَ يَٰلَيْتَ بَيْنِى وَبَيْنَكَ بُعْدَ ٱلْمَشْرِقَيْنِ فَبِئْسَ ٱلْقَرِينُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hata atakapotujia atasema: 'Laiti ungelikuweko baina yangu na wewe kama umbali baina ya mashariki na magharibi. Rafiki mwovu mno wewe!'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَن يَنفَعَكُمُ ٱلْيَوْمَ إِذ ظَّلَمْتُمْ أَنَّكُمْ فِى ٱلْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa kuwa mlidhulumu, haitakufaeni kitu leo kwamba nyinyi mnashirikiana katika adhabu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَفَأَنتَ تُسْمِعُ ٱلصُّمَّ أَوْ تَهْدِى ٱلْعُمْىَ وَمَن كَانَ فِى ضَلَٰلٍ مُّبِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Je, unaweza kuwasikilizisha viziwi, au unaweza kuwaongoa vipofu na waliomo katika upotovu ulio wazi?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَإِمَّا نَذْهَبَنَّ بِكَ فَإِنَّا مِنْهُم مُّنتَقِمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hata tukikuondoa, Sisi tutalipiza kisasi chetu kwao.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَوْ نُرِيَنَّكَ ٱلَّذِى وَعَدْنَٰهُمْ فَإِنَّا عَلَيْهِم مُّقْتَدِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au tutakuonyesha tuliyowaahidi. Nasi bila ya shaka tuna uweza juu yao.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱسْتَمْسِكْ بِٱلَّذِىٓ أُوحِىَ إِلَيْكَ إِنَّكَ عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi wewe yashike yaliyofunuliwa kwako. Hakika wewe uko kwenye Njia iliyonyooka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِنَّهُۥ لَذِكْرٌ لَّكَ وَلِقَوْمِكَ وَسَوْفَ تُسْـَٔلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na mtakuja ulizwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَسْـَٔلْ مَنْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رُّسُلِنَآ أَجَعَلْنَا مِن دُونِ ٱلرَّحْمَٰنِ ءَالِهَةً يُعْبَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na waulize Mitume wetu tuliowatuma kabla yako: 'Je, tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rahmani?'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَإِي۟هِۦ فَقَالَ إِنِّى رَسُولُ رَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu aende kwa Firauni na waheshimiwa wake, na akasema: 'Hakika mimi ni Mtume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote!'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَلَمَّا جَآءَهُم بِـَٔايَٰتِنَآ إِذَا هُم مِّنْهَا يَضْحَكُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lakini alipowajia na Ishara zetu, wakaingia kuzicheka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا نُرِيهِم مِّنْ ءَايَةٍ إِلَّا هِىَ أَكْبَرُ مِنْ أُخْتِهَا وَأَخَذْنَٰهُم بِٱلْعَذَابِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa zaidi kuliko nyingineye. Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَقَالُوا۟ يَٰٓأَيُّهَ ٱلسَّاحِرُ ٱدْعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ إِنَّنَا لَمُهْتَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na wakasema: 'Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa ile ahadi aliyokuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُمُ ٱلْعَذَابَ إِذَا هُمْ يَنكُثُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi tulipowaondolea adhabu hiyo, mara wakaingia kuvunja ahadi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَنَادَىٰ فِرْعَوْنُ فِى قَوْمِهِۦ قَالَ يَٰقَوْمِ أَلَيْسَ لِى مُلْكُ مِصْرَ وَهَٰذِهِ ٱلْأَنْهَٰرُ تَجْرِى مِن تَحْتِىٓ أَفَلَا تُبْصِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Firauni alitangaza kwa watu wake akisema: 'Enyi watu wangu! Kwani mimi si ninao huu ufalme wa Misri, na hii mito inapita chini yangu. Je, hamwoni?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ أَنَا۠ خَيْرٌ مِّنْ هَٰذَا ٱلَّذِى هُوَ مَهِينٌ وَلَا يَكَادُ يُبِينُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au mimi si bora kuliko huyu aliye mnyonge, wala hawezi kusema waziwazi?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَلَوْلَآ أُلْقِىَ عَلَيْهِ أَسْوِرَةٌ مِّن ذَهَبٍ أَوْ جَآءَ مَعَهُ ٱلْمَلَٰٓئِكَةُ مُقْتَرِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi mbona hakuvikwa vikuku vya dhahabu au hawakuja Malaika pamoja naye wakamwandama?'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱسْتَخَفَّ قَوْمَهُۥ فَأَطَاعُوهُ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمًا فَٰسِقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi aliwachezea watu wake na wakamtii. Kwa hakika hao walikuwa watu wapotovu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَلَمَّآ ءَاسَفُونَا ٱنتَقَمْنَا مِنْهُمْ فَأَغْرَقْنَٰهُمْ أَجْمَعِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Walipotukasirisha, tuliwapatiliza tukawazamisha wote!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَجَعَلْنَٰهُمْ سَلَفًا وَمَثَلًا لِّلْـَٔاخِرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kisha tukawafanya kuwa watangulizi na mfano kwa wa baadaye.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَمَّا ضُرِبَ ٱبْنُ مَرْيَمَ مَثَلًا إِذَا قَوْمُكَ مِنْهُ يَصِدُّونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na alipopigiwa mfano Mwana wa Mariamu, watu wako waliupigia ukelele.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَقَالُوٓا۟ ءَأَٰلِهَتُنَا خَيْرٌ أَمْ هُوَ مَا ضَرَبُوهُ لَكَ إِلَّا جَدَلًۢا بَلْ هُمْ قَوْمٌ خَصِمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakasema: 'Miungu yetu kwani si bora kuliko huyu?' Hawakukupigia mfano huo ila kwa ubishi tu. Bali hao ni watu wagomvi!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنْ هُوَ إِلَّا عَبْدٌ أَنْعَمْنَا عَلَيْهِ وَجَعَلْنَٰهُ مَثَلًا لِّبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakuwa yeye (Isa) ila ni Mtumwa tuliyemneemesha na tukamfanya ni mfano kwa Wana wa Israili.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَوْ نَشَآءُ لَجَعَلْنَا مِنكُم مَّلَٰٓئِكَةً فِى ٱلْأَرْضِ يَخْلُفُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tungelipenda, tungeliwafanyia miongoni mwenu Malaika katika ardhi wakifuatana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِنَّهُۥ لَعِلْمٌ لِّلسَّاعَةِ فَلَا تَمْتَرُنَّ بِهَا وَٱتَّبِعُونِ هَٰذَا صِرَٰطٌ مُّسْتَقِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa hakika yeye ni alama ya Saa ya Kiyama. Basi usiitilie shaka, na nifuateni. Hii ndiyo Njia Iliyonyooka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَا يَصُدَّنَّكُمُ ٱلشَّيْطَٰنُ إِنَّهُۥ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala asiwazuilie Shetani. Hakika yeye ni adui yenu wa dhahiri.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَمَّا جَآءَ عِيسَىٰ بِٱلْبَيِّنَٰتِ قَالَ قَدْ جِئْتُكُم بِٱلْحِكْمَةِ وَلِأُبَيِّنَ لَكُم بَعْضَ ٱلَّذِى تَخْتَلِفُونَ فِيهِ فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na alipokuja Isa na ushahidi ulio wazi, alisema: 'Nimewajia na hekima na ili niwaeleze baadhi ya yale mliyokhitalifiana. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na mnitii mimi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ رَبِّى وَرَبُّكُمْ فَٱعْبُدُوهُ هَٰذَا صِرَٰطٌ مُّسْتَقِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na ni Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye tu. Hii ndiyo Njia Iliyonyooka.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱخْتَلَفَ ٱلْأَحْزَابُ مِنۢ بَيْنِهِمْ فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ مِنْ عَذَابِ يَوْمٍ أَلِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lakini makundi kwa makundi yao yalikhitalifiana wao kwa wao. Ole wao waliodhulumu kwa adhabu ya siku chungu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا ٱلسَّاعَةَ أَن تَأْتِيَهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Je, nini wanangojea ila Saa iwajie kwa ghafla na wala wao hawatambui?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱلْأَخِلَّآءُ يَوْمَئِذٍۭ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ إِلَّا ٱلْمُتَّقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku hiyo marafiki watakuwa ni maadui wao kwa wao, isipokuwa wacha Mungu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَٰعِبَادِ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمُ ٱلْيَوْمَ وَلَآ أَنتُمْ تَحْزَنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Enyi waja wangu! Hamtakuwa na khofu siku hiyo, wala hamtahuzunika.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ بِـَٔايَٰتِنَا وَكَانُوا۟ مُسْلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ambao waliziamini Ishara zangu na walikuwa Waislamu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱدْخُلُوا۟ ٱلْجَنَّةَ أَنتُمْ وَأَزْوَٰجُكُمْ تُحْبَرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ingieni Bustanini, nyinyi na wake zenu; mtafurahishwa humo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يُطَافُ عَلَيْهِم بِصِحَافٍ مِّن ذَهَبٍ وَأَكْوَابٍ وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ ٱلْأَنفُسُ وَتَلَذُّ ٱلْأَعْيُنُ وَأَنتُمْ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Watakuwa wanapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe, na vitakuwemo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَتِلْكَ ٱلْجَنَّةُ ٱلَّتِىٓ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hiyo ni Bustani ya mbinguni mliyorithishwa kwa mliyokuwa mkiyafanya.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَكُمْ فِيهَا فَٰكِهَةٌ كَثِيرَةٌ مِّنْهَا تَأْكُلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mnayo humo matunda mengi mtakayoyala.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ ٱلْمُجْرِمِينَ فِى عَذَابِ جَهَنَّمَ خَٰلِدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa hakika wakosefu watakaa katika adhabu ya Jahannamu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَا يُفَتَّرُ عَنْهُمْ وَهُمْ فِيهِ مُبْلِسُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hawatapumzishwa nayo, na humo watakata tamaa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا ظَلَمْنَٰهُمْ وَلَٰكِن كَانُوا۟ هُمُ ٱلظَّٰلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala Sisi hatukuwadhulumu, bali wao ndio waliokuwa madhalimu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَنَادَوْا۟ يَٰمَٰلِكُ لِيَقْضِ عَلَيْنَا رَبُّكَ قَالَ إِنَّكُم مَّٰكِثُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nao watapiga kelele waseme: 'Ewe Malik! Na atufishe Mola wako Mlezi!' Naye aseme: 'Hakika nyinyi mtakaa humo humo!'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَقَدْ جِئْنَٰكُم بِٱلْحَقِّ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَكُمْ لِلْحَقِّ كَٰرِهُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa yakini tulikuleteeni Haki, lakini wengi katika nyinyi mlikuwa mnaichukia Haki.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ أَبْرَمُوٓا۟ أَمْرًا فَإِنَّا مُبْرِمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au waliweza kupitisha amri yao? Bali ni Sisi ndio tunaopitisha.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْ يَحْسَبُونَ أَنَّا لَا نَسْمَعُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَىٰهُم بَلَىٰ وَرُسُلُنَا لَدَيْهِمْ يَكْتُبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au wanadhani kwamba hatusikii siri zao na minong'ono yao? Wapi! Na wajumbe wetu wapo karibu nao, wanayaandika.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قُلْ إِن كَانَ لِلرَّحْمَٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلْعَٰبِدِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sema: 'Ingelikuwa Rahmani (Mwingi wa Rehema) ana mwana, basi mimi ningelikuwa wa kwanza kumuabudu.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
سُبْحَٰنَ رَبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ رَبِّ ٱلْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ametakasika Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, Mola Mlezi wa A'rshi, na hayo wanayomsifia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا۟ وَيَلْعَبُوا۟ حَتَّىٰ يُلَٰقُوا۟ يَوْمَهُمُ ٱلَّذِى يُوعَدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi waache wapige porojo wakicheza mpaka wakutwe na hiyo siku yao waliyoahidiwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَهُوَ ٱلَّذِى فِى ٱلسَّمَآءِ إِلَٰهٌ وَفِى ٱلْأَرْضِ إِلَٰهٌ وَهُوَ ٱلْحَكِيمُ ٱلْعَلِيمُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Yeye ndiye Mungu mbinguni, na ndiye Mungu katika ardhi. Naye ndiye Mwenye hekima, Mwenye kujua mno.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَتَبَارَكَ ٱلَّذِى لَهُۥ مُلْكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَعِندَهُۥ عِلْمُ ٱلسَّاعَةِ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ametukuka Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo kati yake. Na uko kwake ujuzi wa Saa ya Kiyama, na kwake Yeye mtarudishwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَا يَمْلِكُ ٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِ ٱلشَّفَٰعَةَ إِلَّا مَن شَهِدَ بِٱلْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala hao mnaowaomba badala yake Yeye hawana uweza wa kumwombea mtu, isipokuwa anayeshuhudia kwa haki, na wao wanajua.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ ٱللَّهُ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ukiwauliza ni nani aliyewaumba. Bila ya shaka watasema ni Mwenyezi Mungu! Basi ni wapi wanakogeuziwa?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَقِيلِهِۦ يَٰرَبِّ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ قَوْمٌ لَّا يُؤْمِنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na usemi wake (Mtume) ni: ʻEwe Mola wangu Mlezi! Hakika hawa ni watu wasioamini.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱصْفَحْ عَنْهُمْ وَقُلْ سَلَٰمٌ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi wasamehe, na uwaambie maneno ya salama. Watakujajua.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Ash-Shura
Sura Ad-Dukhaan →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.