Mwanzo › Sura › Sura Ad-Dukhaan
Sura Ad-Dukhaan الدخان
Aya 59 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 64
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ حمٓ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ha Mim.[1]
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلْكِتَٰبِ ٱلْمُبِينِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ninaapa kwa Kitabu kinachobainisha.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّآ أَنزَلْنَٰهُ فِى لَيْلَةٍ مُّبَٰرَكَةٍ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Sisi tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hekima.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَمْرًا مِّنْ عِندِنَآ إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Jambo litokalo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
رَحْمَةً مِّن رَّبِّكَ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
رَبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَآ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yao, ikiwa nyinyi mna yakini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْىِۦ وَيُمِيتُ رَبُّكُمْ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلْأَوَّلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha- Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa mwanzo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
بَلْ هُمْ فِى شَكٍّ يَلْعَبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lakini wao wanacheza katika shaka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱرْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِى ٱلسَّمَآءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi ingoje siku ambayo mbingu zitakapoleta moshi ulio dhahiri.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَغْشَى ٱلنَّاسَ هَٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Utakaowafunika watu. Hii ni adhabu chungu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
رَّبَّنَا ٱكْشِفْ عَنَّا ٱلْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَنَّىٰ لَهُمُ ٱلذِّكْرَىٰ وَقَدْ جَآءَهُمْ رَسُولٌ مُّبِينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nini faida ya kukumbuka kwao? Na alikwisha wafikia Mtume mwenye kubainisha.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ثُمَّ تَوَلَّوْا۟ عَنْهُ وَقَالُوا۟ مُعَلَّمٌ مَّجْنُونٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na wao wakamgeuzia uso, na wakasema: 'Huyu amefunzwa, naye ni mwendawazimu.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّا كَاشِفُوا۟ ٱلْعَذَابِ قَلِيلًا إِنَّكُمْ عَآئِدُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika sisi tutaiondoa adhabu kidogo, lakini nyinyi kwa yakini mtarejea vile vile!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ نَبْطِشُ ٱلْبَطْشَةَ ٱلْكُبْرَىٰٓ إِنَّا مُنتَقِمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku tutakayoyashambulia mashambulio makubwa, bila ya shaka Sisi ni wenye kutesa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَقَدْ فَتَنَّا قَبْلَهُمْ قَوْمَ فِرْعَوْنَ وَجَآءَهُمْ رَسُولٌ كَرِيمٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hakika kabla ya hawa tuliwafanyia mtihani watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَنْ أَدُّوٓا۟ إِلَىَّ عِبَادَ ٱللَّهِ إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Akasema: 'Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume Muaminifu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَن لَّا تَعْلُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ إِنِّىٓ ءَاتِيكُم بِسُلْطَٰنٍ مُّبِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na msimfanyie kiburi Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitakuleteeni uthibitisho ulio wazi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِنِّى عُذْتُ بِرَبِّى وَرَبِّكُمْ أَن تَرْجُمُونِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nami najikinga kwa Mola wangu Mlezi na ndiye Mola wenu Mlezi pia, ili msinipige mawe.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَإِن لَّمْ تُؤْمِنُوا۟ لِى فَٱعْتَزِلُونِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنَّ هَٰٓؤُلَآءِ قَوْمٌ مُّجْرِمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ndipo akamwomba Mola wake Mlezi: 'Hakika watu hawa ni wakosefu.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَأَسْرِ بِعِبَادِى لَيْلًا إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mwenyezi Mungu akasema: 'Basi nenda na waja wangu usiku. Kwa yakini mtafuatwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱتْرُكِ ٱلْبَحْرَ رَهْوًا إِنَّهُمْ جُندٌ مُّغْرَقُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na iache bahari vivyo hivyo imeachana, hakika wao ni jeshi litakalozamishwa.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَمْ تَرَكُوا۟ مِن جَنَّٰتٍ وَعُيُونٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mabustani mangapi na chemchemi ngapi waliziacha!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَزُرُوعٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na mimea na vyeo vitukufu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَنَعْمَةٍ كَانُوا۟ فِيهَا فَٰكِهِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na neema walizokuwa wakijistareheshea!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَذَٰلِكَ وَأَوْرَثْنَٰهَا قَوْمًا ءَاخَرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ndio hivyo! Na tukawarithisha haya watu wengineo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ ٱلسَّمَآءُ وَٱلْأَرْضُ وَمَا كَانُوا۟ مُنظَرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi mbingu wala ardhi hazikuwalilia, wala hawakupewa muhula.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَقَدْ نَجَّيْنَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ مِنَ ٱلْعَذَابِ ٱلْمُهِينِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na bila ya shaka tuliwaokoa Wana wa Israili katika adhabu ya kuwadhalilisha,
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مِن فِرْعَوْنَ إِنَّهُۥ كَانَ عَالِيًا مِّنَ ٱلْمُسْرِفِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ya Firauni. Hakika yeye alikuwa jeuri katika wenye kupindukia mipaka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَقَدِ ٱخْتَرْنَٰهُمْ عَلَىٰ عِلْمٍ عَلَى ٱلْعَٰلَمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tuliwakhiari kwa ujuzi wetu kuliko walimwengu wengineo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَءَاتَيْنَٰهُم مِّنَ ٱلْـَٔايَٰتِ مَا فِيهِ بَلَٰٓؤٌا۟ مُّبِينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tukawapa katika ishara zenye majaribio yaliyo wazi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَيَقُولُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika hawa wanasema:
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنْ هِىَ إِلَّا مَوْتَتُنَا ٱلْأُولَىٰ وَمَا نَحْنُ بِمُنشَرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَأْتُوا۟ بِـَٔابَآئِنَآ إِن كُنتُمْ صَٰدِقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi warudisheni baba zetu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَهُمْ خَيْرٌ أَمْ قَوْمُ تُبَّعٍ وَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ أَهْلَكْنَٰهُمْ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ مُجْرِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Je, ni wao bora au watu wa Tubbaa' na waliokuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا خَلَقْنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَٰعِبِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake kwa mchezo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَا خَلَقْنَٰهُمَآ إِلَّا بِٱلْحَقِّ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hatukuviumba hivyo ila kwa Haki, lakini wengi wao hawajui.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ يَوْمَ ٱلْفَصْلِ مِيقَٰتُهُمْ أَجْمَعِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika siku ya Uamuzi ni wakati uliowekwa kwa wao wote.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ لَا يُغْنِى مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْـًٔا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِلَّا مَن رَّحِمَ ٱللَّهُ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Isipokuwa yule mbaye Mwenyezi Mungu atamrehemu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu mno.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ شَجَرَتَ ٱلزَّقُّومِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Mti wa Zaqqum
Tazama tafsiri zote za aya hii →
طَعَامُ ٱلْأَثِيمِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ni chakula cha mwenye dhambi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَٱلْمُهْلِ يَغْلِى فِى ٱلْبُطُونِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kama shaba iliyoyeyushwa, hutokota matumboni.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَغَلْىِ ٱلْحَمِيمِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kama kutokota kwa maji ya moto.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
خُذُوهُ فَٱعْتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلْجَحِيمِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center (Itasemwa): 'Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ثُمَّ صُبُّوا۟ فَوْقَ رَأْسِهِۦ مِنْ عَذَابِ ٱلْحَمِيمِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayochemka.'
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْكَرِيمُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ هَٰذَا مَا كُنتُم بِهِۦ تَمْتَرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika haya ndiyo mliyokuwa mkiyatilia shaka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى مَقَامٍ أَمِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika wacha Mungu watakuwa katika mahali pa amani.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فِى جَنَّٰتٍ وَعُيُونٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Katika mabustani na chemchemi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَلْبَسُونَ مِن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَقَٰبِلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakielekeana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَذَٰلِكَ وَزَوَّجْنَٰهُم بِحُورٍ عِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hivi ndivyo itakavyokuwa, na tutawaoza mahurilaini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَٰكِهَةٍ ءَامِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَا يَذُوقُونَ فِيهَا ٱلْمَوْتَ إِلَّا ٱلْمَوْتَةَ ٱلْأُولَىٰ وَوَقَىٰهُمْ عَذَابَ ٱلْجَحِيمِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda kutokana na adhabu ya Jahannamu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَضْلًا مِّن رَّبِّكَ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَإِنَّمَا يَسَّرْنَٰهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi tumeifanya nyepesi hii Qur-ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱرْتَقِبْ إِنَّهُم مُّرْتَقِبُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ngoja tu, na wao wangoje pia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Az-Zukhruf
Sura Al-Jaathiya →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.