قَالَ ءَامَنتُمْ لَهُۥ قَبْلَ أَنْ ءَاذَنَ لَكُمْ إِنَّهُۥ لَكَبِيرُكُمُ ٱلَّذِى عَلَّمَكُمُ ٱلسِّحْرَ فَلَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَٰفٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ فِى جُذُوعِ ٱلنَّخْلِ وَلَتَعْلَمُنَّ أَيُّنَآ أَشَدُّ عَذَابًا وَأَبْقَىٰ
Swahili Translation - Rowad Translation Center(Firauni) akasema: Oh! Mmemuamini kabla ya mimi kuwapa ruhusa? Hakika yeye ndiye mkubwa wenu aliyewafundisha uchawi huu. Basi kwa yakini nitawakatakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha. Na lazima nitawatundika misalabani katika vigogo vya mitende, na hapo kwa yakini mtajua ni nani katika sisi ndiye mkali zaidi wa kuadhibu na kuiendeleza zaidi adhabu yake.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani(Firauni) akasema: Oh! Mnamuamini kabla sijakupeni ruhusa? Hakika yeye ndiye mkubwa wenu aliye kufundisheni uchawi. Basi kwa yakini nitakukateni mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakutundikeni misalabani katika vigogo vya mitende, na hapo kwa yakini mtajua ni nani katika sisi aliye mkali wa kuadhibu na kuiendeleza adhabu yake.