وَلَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِۦٓ أَزْوَٰجًا مِّنْهُمْ زَهْرَةَ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا لِنَفْتِنَهُمْ فِيهِ وَرِزْقُ رَبِّكَ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala kamwe usivikodolee macho tulivyowastarehesha kwavyo baadhi ya watu miongoni mwao, kwa ajili ya mapambo ya duniani, ili tuwajaribu katika hivyo. Na riziki ya Mola wako Mlezi ni bora na yenye kudumu zaidi.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWala usivikodolee macho tulivyo wastareheshea baadhi ya watu miongoni mwao, kwa ajili ya mapambo ya duniani, ili tuwajaribu. Na riziki ya Mola wako Mlezi ni bora na inadumu zaidi.