وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَكُمْ أُمَّةً وَٰحِدَةً وَلَٰكِن يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهْدِى مَن يَشَآءُ وَلَتُسْـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu angelitaka, kwa yakini angeliwafanya kuwa umma mmoja. Lakini anampoteza amtakaye, na anamwongoa amtakaye. Na hakika mtaulizwa juu ya yale mliyokuwa mkiyatenda.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa Mwenyezi Mungu angeli taka, kwa yakini angeli kufanyeni umma mmoja. Lakini anamwachia kupotea anaye mtaka, na anamwongoa amtakaye. Na hakika mtaulizwa kwa yale mliyo kuwa mkiyafanya.