caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura An-Nahl, Aya 76

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 70 · 16:76

وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا رَّجُلَيْنِ أَحَدُهُمَآ أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَىْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَىٰ مَوْلَىٰهُ أَيْنَمَا يُوَجِّههُّ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ هَلْ يَسْتَوِى هُوَ وَمَن يَأْمُرُ بِٱلْعَدْلِ وَهُوَ عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa wanaume wawili. Mmoja wao ni bubu, hawezi chochote, naye ni mzigo kwa mlezi wake. Popote anapomuelekeza, haleti heri yoyote. Je, huyo anaweza kuwa sawa na yule anayeamrisha uadilifu, naye yuko kwenye njia iliyonyooka?
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa watu wawili. Mmoja wao ni bubu, hawezi chochote, naye ni mzigo kwa bwana wake. Popote anapo muelekeza haleti kheri. Je! Huyo anaweza kuwa sawa na yule anaye amrisha uadilifu,naye yuko juu ya Njia Iliyo Nyooka.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70